Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Ahsante sana ndugu yangu.
 
Yericko Nyerere,

Umefikia wapi kuhusu tape na vidio clip ya hotuba ya Nyerere ulisema umeambiwa ukachukue leo TBC.

Mkuu nimefika nimeziona hotuba nyingi, na ile muhimu tunayoisubiri nimeiona, jambo la ajabu kuna urasimu sana hapo TBC, mhusiika wa nyaraka hizo anasema zinauzwa!

Kanipiga kalenda niende kesho leo yupo bize!
 
Last edited by a moderator:

Babu...

Hebu Insha Allah pitia tena huo ukurasa hizo taarifa hazipo katika ukurasa wa 96
ulotaja.

Huenda umesoma vibaya.

Lakini nataka nikutahadharishe jambo moja.

Mwakigagile ana kitabu kingine na ninacho.
Kinaitwa ''Life in Tangnayika in the Fifitees.''
New Africa Press, Dar es Salaam, 2010.

Hiki kitabu kilipotoka tu rafiki zangu Marekani wakanitaarifu kuwa huyu mwandishi
huenda ameninakili katika kitabu.

Yaani kakopi.
Lipo neno la Kiingereza sitaki kulitumia kwa kuwa siamini katika hilo.

Hawa rafiki zangu kila wakisoma wanasema hii mbona kama Mohamed Said.

Mie nikawajibu kuwa katika Uislam elimu ni kitu cha bure huyu mwandishi hajafanya kosa
hata kama hakunitaja kuwa yale ni maandishi yangu.

Elimu ni kitu cha bure na huyu bwana kafanya kheri kusambaza elimu ni wa kupongezwa si
wa kutiwa misukosuko na kufedheheshwa.

Katika kitabu hiki nimo sana lakini yeye nadhani hajui.
Kuna Appendix kaweka vitu.

Huyo katika Appendix ni mimi lakini asingejua kwa kuwa jina langu halionekani.

Babu...
Ahsante kwa taarifa.
 

Mkuu nilidhani unajibu hoja hii

"mfano ukurasa wa 96, ameeLEzeA kabisa kuwa ABDU ALIKUWA KATIBU WAKATI NYERERE ANARUDI,

PIA MWANDISHI AMEONESHA KUWA ABDU ALIPENDELEA CHIEF MAKWAIA KUWA KIONGOZI WA TAA AMBAPO ALIKATAA, KABLA YA DR KYARUZI"

Badala yake unaanza ngano/simulizi?
 
aha! Kumbe tunakera? Nyani haoni nini vile?


mmechoka kwa hoja na mmelegea,mmeishiwa nguvu kabisa..!
Hazina pekee mliyobakiwa nayo ni kejeli,dharau na choko choko za kidini,mnataman ndugu moh said asitishe bakora zake za hoja ili mpate nafuu na kufuta machozi yenu lakini haisadii,
mmezid kujiaibisha,watu wengi wanawaona,wanawadharau na kuwashangaa..!

 
Yericko Nyerere,

Tulitegemea wewe ndo upo jikoni kabisa kutoa ushahidi aidha wa picha, sauti, videos na vitu vinginevyo kama ushahidi wa unayoyasema, kwasababu Mwalimu ni Mzee wako kabisa

Kisa cha Idd Fauz, tulitegemea wewe ndo ukisimulie kwa kiredu na mapana yake. Lakini unamtegea mzee Mohamed Said afanye hiyo kazi

Na bado tunategemea wewe ndo utupe mambo mingi zaidi kwenye historia ya Mwalimu.

kaka[MENTION]Do santos[/MENTION] naona upo kimya sana kaka yangu

Ritz asante sana kwa ile picha ya safari ya Mwalimu kwenda UN. Hakika ile ni kumbukumbu marwa sana

Nawasilisha
 
Last edited by a moderator:

Ritz,

Kumekucha,

Unanishushia picha moja moja kwa awamu kama
vidonge vya Muhimbili!

Hii Jangwani.

Unaziona kofia hizo na tarbush?

Hapo chini ya jukwaa yuko Rashid Sisso, Abbas Bakis na kundi
la Bantu Group.

Hawa ndiyo ''nascent'' TANU Intelligence.
Hao ndiyo walikuwa walinzi wa Nyerere na wahamasishaji.

Mkutano unaanza na nyimbo hii:

''Muheshimiwa nakupenda sana
Wallahi sina mwinginewe
Insha Allah Mungu yupo
Tanganyika tutajitawala.''

Huyo Bi Hawa Maftah, Bi. Tatu biti Mzee na kundi lao.
 

yericko unatia huruma,umebakia kuwa debe tupu ulieishiwa hoja,
umekaa kusubiri back-up kwa ndugu zako lakini cha kustaajabu back-up hizo zinakuwa pumba kuliko ulchokisema wewe mwenyewe,unaishia kusononeka na kukimbilia kumdhihaki mkwasi wa maarifa ndugu moh said,tuliza akili upewe ilmu kijana,,
narudia tena kwa mara ya mwisho swali hili,,
"yericko nyerere una uhusiano gani na julius k nyerere?"
babu yako,baba yako,mjomba yako ama ni nani yako hasa??
Toa jibu kwa faida ya wafuatiliaji wa mjadala huu.
 
Unarukaruka tu! umekataa kujibu maswali ya awali, ukaletewa swali la mwisho "umeipata wapi tafsiri ya neno muasisi uliyotuletea jamvini"? (tena baada ya kutushutumu humu jamvini kuwa hatujui maana yake) hujajibu unarukia kwingine!
 

Yericko,

Kujibu hoja siyo kazi hata kidogo.

Lakini hebu soma nimesema nini katika hiyo post.
Hiyo taarifa haipo katika huo ukurasa wa 96.

Sasa wewe bila kusubiri Babu...ajibu ndugu yangu
unanishambulia.

Usomi hauendi hivyo tusubiri kwanza tusome Mwakigagile
kaandika nini kisha mimi nitazungumza.

Unajua fowadi mzuri akiwa katika kumi na nane hafanyi papara.
Anatulia na hivyo ndivyo anavyoweza kuziona nyavu.

Vinginevyo atapiga nje ya goli.

Tulia tumsubiri Babu...
 
Kweli kabisa!...nilitegemea kuwa audio angeitoa kutoka kwenye maktaba ya familia! kumbe amepiga simu TBC! nani kati yetu asiyeweza kuwapigia TBC simu na kuwaomba audio ya hotuba ya Nyerere na kukumbana na anachokiita urasimu?!
 
Hapa ndio mzee Said unapokuwa huwatendei haki wasomaji wako; umetuwekea vichwa vya habari tu. Why don't you scan these documents and make them public for anyone to see?

MM,

Naweza kufanya hivyo lakini kwa wepesi hebu nenda Mwalimu Nyerere Foundation
niliwapa nyaraka zote nilizokuwanazo.

Kwa sasa itabidi nitulie nianze kuzisaka katika hazina yangu.
Kwani huniamini unadhani nime ''forge?''

Ondoa hofu hizo nyaraka zipo na nimezisoma zote.
 

Nguruvi3,

Wewe unaponda maandishi ya Mohamed Said na kuyaita ngano yako kwako sijui tuyaitaje.

Unasema udini ulikuwepo toka kabla ya uhuru sijui umeipata wapi wewe na Nyerere sijui tumuamini nani.

Pitia tena hotuba ya Nyerere anavyowaelezea wazee wa Dar es Salaam wakati wa TANU na harakati za kupigania uhuru.

Nyerere mwenyewe anakiri fadhira za Wazee wa Dar es Salaam kuna kipindi anasema alikuwa Mkiristu peke yake lakini wanamtendea wema wewe leo unasema walikuwa wadini.

Angalia hizo picha wazee walivyokuwa na mahaba na Nyerere.
 
Last edited by a moderator:

Bila ya kukusimulia ungenijuaje?

Hebu soma hii kutoka katika kitabu changu:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] In 1954, risking his job as Market Master, little did Abdulwahid realise that a time would come when the history of the struggle would be written and his name would not be associated with that important period in the history of Tanganyika as a nation.

One can also speculate what would have been the role of Nyerere in the politics of Tanganyika if Chief Kidaha had accepted TAA's proposal to become president of the Association in 1951; or what would have been the future of Tanganyika if Abdulwahid and the TAA inner circle had accepted Ivor Bayldon's proposal to form a multiracial political party.

This was an obvious ploy contrived by the government to co-opt the nationalists and hence compromise their stand for majority rule.

What the government was seeking was to incorporate the TAA leadership with the traditional authorities in the Legislative Council and form what could be wrongly perceived as true representative body of authority with the Governor at the top.

This would have nipped in the bud the struggle for majority rule for the Africans of Tanganyika.

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] With such an hypothetical set up, would Nyerere had been able to form a political party of his own, either within the framework of the TAA or from any other base? Would his party build its power base first from the peasantry in his home area in Musoma, or could he have ventured to build his base from Dar es Salaam with the same Muslim support he was able to get in TANU through his acquaintance with the townsmen? [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
He is on a mission(jihad)
Halafu wanatokea watu kama Mag3 wanataka kutia mchanga kitumbua chake, hata usingizi hawezi kuupata! Kitu ambacho yeye Mohamed Said na "cheerleader" wake (nimeona wakiitana waje kuokoa jahazi) wanashindwa kukitambua ni jinsi huu uzi unavyozidi kumuumbua na kumwacha uchi...sasa yeye mzee wa watu badala ya kuchutama anazidi tu kujifunua, duh! Tofauti na Mwanakijiji na wenine, mimi naziita hizi simulizi zake kwa jina lake, ngano...sifichi msimamo wangu.

Narudia maswali yangu na sasa nimeongeza la nane;

  1. Abdulwahid Sykes aliingia kwenye uongozi wa AA mwaka gani kwa mara ya kwanza na kwa wadhifa gani?
  2. Je mwaka 1946, Mwalimu Nyerere alipohudhuria mkutano wa AA Dar es Salaam kama katibu wa tawi la Tabora, Abdulwahid alikuwa na nafasi gani ndani ya AA?
  3. Je, Abdulwahid Sykes alihudhuria huo mkutano uliofanyika mwaka 1946 Dar es Salaam na kwa wadhifa upi ndani ya AA?
  4. Je, Abdulwahid Sykes kama alihudhuria, kwa nini idaiwe ni mwaka saba baadaye, 1953, ndio kakutana na Nyerere kwa mara ya kwanza?
  5. Je, kama mwaka 1946, Abdulwahid Sykes hakuwa na sifa wala wadhifa wa kuhudhuria huo mkutano wa AA, nani kati yake na kaka yake Mwalimu Nyerere alitangulia kwenye siasa?
  6. Je si kweli kuwa Dr. Kyaruzi, aliyefahamiana na Mwalimu Nyerere toka Makerere, ndiye aliongoza mapinduzi ndani ya AA mwaka 1950 na yeye kuchaguliwa Raisi wa kwanza wa TAA?
  7. Mkutano wa kwanza wa kuizindua AA mwaka 1929, ulifanyika nyumbani kwa nani na chini ya uongozi wa nani?
  8. Kwa nini hasa AA ilianzishwa mwaka 1929...je hiyo AA iliihusu Tanganyika peke yake? Ni wakati gani ilibidi ibadilike na kuitwa TAA na kwa sababu gani?
Nitatoa hapa nukuu kidogo kutoka kitabu cha Sanderson Beck, "Tanganyika and the British 1918-1950".

Ninchotaka kusema hapa ni kwamba Watanganyika Weusi walibaguliwa kwa rangi yao na si dini na hivyo mwamko ukawa ni kudai usawa na haki. Huu mwamko kama mnavyoona ulichelewa sana kuanza Dar es Salaam...sasa kama huu mwamko ndio udaiwe kuwa msingi wa harakati za uhuru, basi ni miaka mingi kabla ya kuzaliwa AA ya Cecil Matola akishirikiana na wazee wa Mohamed ambao kwa muono wake ni Manyema na Wazulu, wa Gerezani na Waislaam. Lakini kama tunaongelea chama kilichoasisiwa rasmi kudai uhuru na kutambulika kama chama cha siasa, ni TANU iliyozaliwa tarehe 7, Julai 1954 ikiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere.

Kwa nini nasema hivi? Yako madai ya kipuuzi yanayoletwa na Mohamed Said kwamba AA ndiyo msingi wa kupatikana kwa uhuru nchini. Kwa nini tusianzia mwaka 1922? mwaka 1923? mwaka 1925? au mwaka 1927? Mbona tayari vyama vya kupigania maslahi ya Watanganyika vilikuwepo sehamu nyingi tu ya Tanzania hata kabla ya AA. Je ni kwa sababu mababu zake Mohamed Said walishiriki kuanzisha AA mwaka 1929 ndio wawe vinara wa harakati hizo? Mimi namtaka Mohamed Said ajibu hayo maswali yangu kwanza ili wanajamvi waweze kutambua uwongo, ghilba, chuki, uchochezi...vilivyotawala maandishi yake.

Turudi kidogo nyuma wakati wa Mjerumani...Wazulu na Manyema wanaingiaje hapa? Hebu someni hii;

Na hii pia;


Je yawezekana miaka hiyo ya nyuma hataji Mohamed Said kwa sababu mababu zake walikuwa upande wa Mkoloni Mjerumani? Jamani tumetoka mbali, tusizikubali hizi ngano za kichochezi anazoleta Mohamed katika mission yake ya kupandikiza chuki za kidini, ili iweje? Kutusambaratisha?
 
fatilien history msipelekwe pelekwe abdulwahid sykes mwaka 1948 alikua katbu wa chama cha wafanyakaz bandarin wakat huo nyerere dsm anaickia tu nyerere kaletwa kwa abdul na kasela bantu kwa kimemo pia hcho chama cha taa kimeanzshwa na baba yke abdulwahd sykes nyumban kwao jiulize taa imeanzshwa mwaka 1929 Nyerere kaingia mwaka 1953
 

La hasha mkuu wangu wala sijadhani umeforge; nina maana ulichosema hapo juu ni kana kwamba nakala za hizo documents ndio umetuwekea kumbe ni vichwa vya habari tu. Kama wewe unazo na zinaweza kupatikana kutoka kwako itakuwa vizuri tu na rahisi zaidi... jitihadi utupatie tunatanguliza shukrani.

Unayo hotuba ya Nyerere kuaga mwaka 1985?
 

Nikweli ninayo mengi sana, lakini hata hayo niliyokkupeni yana mafaa pia ndugu!
 
Last edited by a moderator:
Hate is taught, Love comes naturally.

Mzee Said, ninatatizwa sana na mitazamo hasi, mitazamo ya 'wao' na 'sisi'.

What kind of future do you see in Tanzania?
Hilo ni swali langu moja na nitaendelea kukuuliza swali hilo kila nipatapo nafasi, likiwa na sehemu tofauti tofauti.

Wakati unanijibu, uwe unajiuliza, what difference have you made to the youth of this nation that inspire the future you want to see. Nitakuwa nakukumbusha hili.

You must be the change you wish to see in the world.
—Gandhi

I’d rather live with a good question than a bad answer.
—Aryeh Frimer
 
Nani hapa anayejiabisha? Yule anayechomekezea maneno yake na kubadilisha uwongo kuwa ukweli? Acha ushabiki na upofu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…