Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Spot on mkuu, mimi nilikuwa nimekaa kimya muda mrefu nikiangalia mtililiko wa mambo unavyo kwenda - kitu kinacho nishangaza ni kumshambullia Ndugu Moh kwa maneno ya kejeli na mengine yanayo onekana kutaka kumdhalilisha vile as if ni msaliti kwa kutujuza anayo yajuwa kuhusu historia ya kweli ya TAIFA letu - ili la watu kug'ang'ania kana kwamba historia ya kweli kuhusu taifa letu ilianzia mwaka 1954 huwa inanipa wakati mgumu sana mimi.

Watu wengi tuna kiu ya kujua historia ya kweli kuhusu Taifa letu bila ya kujali mtafiti/mwandishi ni wa DINI gani na waasisi wa kuanzisha harakati za kutukomboa walikuwa wa madhehebu gani, cha umuhimu hapa ni kujua UKWELI - hii dhana ya Islamphobia inatusadia nini? ndugu Moh anazungumzia historia ya Tanzania lakini watu wanataka ku-derail mada kwa kutumbukiza mambo ya Somalia/Tunisia mbona amzungumzii Saudi Arabia, IRAN na Uturuki kwani hizo si nchi za Kislaam - kwani Somalia wakati wa Said Barre ilikuwa na matatizo gani? Tunawezaje kujiaminia kwamba mambo yaliyo ikumba Somalia hayawezi kulikumba Taifa letu, kwani tunaishi kwenye kisiwa?


Mambo anayo zungumza humu Ndugu Moh yanapaswa kuwa fundisho kwa vizazi vijavyo kwamba haipendezi kujaribu kunyanyasa madhehebu ya dini nyingine, hivyo kulazimisha Serikali ambazo zitafuata kujirekebisha kwa kumaliza kero za waislaam kikamilifu; cha kushangaza hapo badala ya kumshukuru mwenzetu kwamba amejitolea kuwa mkweli nyinyi mnabeza beza, hivi kuna mtu amewahi kukaa chini na kujiuliza idadi ya waislaam ni wangapi Tanzania, hawana tofauti kubwa na Wakristo na sitashangaa kukuta wanatuzidi idadi - Mtu mwenye akili timamu anawezaje kupuuzia kundi hili kweli - and 4 howlong. Je ndugu Moh na wenzake wangeamua kukaa kimya lakini wakajipanga kufanya KWELI nchi hii itakuwa na amani kweli au mnafikili uwezo huo hawana???


Mimi na-copy makala zake na kuzipitia na kuwahoji watu wengine wa makamo, unakuta mambo mengi anayo zungumzia Moh yana ukweli - na kusema kweli anajua mambo mengi na ni msomi na mtafiti mahili, hajatulazimisha kukubaliana naye, kama mtu anaona anacho zungumza hakina mantiki basi fanya tafiti zako utuletee historia mbadala badala ya name calling na kumsingizia magonjwa ya akili ya kufikilika - mimi sijapenda tabia hii - we sema Moh ni mtu mvumilivu sana kutokana na malezi.

Watu mnakuwa irritated kupindukia - kisa, Moh kamsema Nyerere, kwa nini usimpuuzie kama utaki makala zake, wahachie watu wenye kiu ya kutaka kujua mengi kuhusu Taifa letu wamuhulize kwa heshima; lakini haya mambo ya kumtega tega na kubarisha mada kwa hila, tabia hii watu wegi inatukela sana.

Ahsante sana ndugu yangu.
 
Yericko Nyerere,

Umefikia wapi kuhusu tape na vidio clip ya hotuba ya Nyerere ulisema umeambiwa ukachukue leo TBC.

Mkuu nimefika nimeziona hotuba nyingi, na ile muhimu tunayoisubiri nimeiona, jambo la ajabu kuna urasimu sana hapo TBC, mhusiika wa nyaraka hizo anasema zinauzwa!

Kanipiga kalenda niende kesho leo yupo bize!
 
Last edited by a moderator:
Nadhani kitabu hiki,
Nyerere and Africa: End of an Era
by Godfrey Mwakikagile (Nov 19, 2006), kitabu hiki pia kwa kiasi kikubwa kimejibu kwa kiasi fulani hoja za Mzee MOHAMED SAID, UKIANGALIA Kwa mfano ukurasa wa 96, ameeLEzeA kabisa kuwa ABDU ALIKUWA KATIBU WAKATI NYERERE ANARUDI,


PIA MWANDISHI AMEONESHA KUWA ABDU ALIPENDELEA CHIEF MAKWAIA KUWA KIONGOZI WA TAA AMBAPO ALIKATAA, KABLA YA DR KYARUZI
KWA WASIO NA KITABI PITIA LINK
HII; Nyerere and Africa: End of an Era - Godfrey Mwakikagile - Google Books

Babu...

Hebu Insha Allah pitia tena huo ukurasa hizo taarifa hazipo katika ukurasa wa 96
ulotaja.

Huenda umesoma vibaya.

Lakini nataka nikutahadharishe jambo moja.

Mwakigagile ana kitabu kingine na ninacho.
Kinaitwa ''Life in Tangnayika in the Fifitees.''
New Africa Press, Dar es Salaam, 2010.

Hiki kitabu kilipotoka tu rafiki zangu Marekani wakanitaarifu kuwa huyu mwandishi
huenda ameninakili katika kitabu.

Yaani kakopi.
Lipo neno la Kiingereza sitaki kulitumia kwa kuwa siamini katika hilo.

Hawa rafiki zangu kila wakisoma wanasema hii mbona kama Mohamed Said.

Mie nikawajibu kuwa katika Uislam elimu ni kitu cha bure huyu mwandishi hajafanya kosa
hata kama hakunitaja kuwa yale ni maandishi yangu.

Elimu ni kitu cha bure na huyu bwana kafanya kheri kusambaza elimu ni wa kupongezwa si
wa kutiwa misukosuko na kufedheheshwa.

Katika kitabu hiki nimo sana lakini yeye nadhani hajui.
Kuna Appendix kaweka vitu.

Huyo katika Appendix ni mimi lakini asingejua kwa kuwa jina langu halionekani.

Babu...
Ahsante kwa taarifa.
 
Babu...

Hebu Insha Allah pitia tena huo ukurasa hizo taarifa hazipo katika ukurasa wa 96
ulotaja.

Huenda umesoma vibaya.

Lakini nataka nikutahadharishe jambo moja.

Mwakigagile ana kitabu kingine na ninacho.
Kinaitwa ''Life in Tangnayika in the Fifitees.''
New Africa Press, Dar es Salaam, 2010.

Hiki kitabu kilipotoka tu rafiki zangu Marekani wakanitaarifu kuwa huyu mwandishi
huenda ameninakili katika kitabu.

Yaani kakopi.
Lipo neno la Kiingereza sitaki kulitumia kwa kuwa siamini katika hilo.

Hawa rafiki zangu kila wakisoma wanasema hii mbona kama Mohamed Said.

Mie nikawajibu kuwa katika Uislam elimu ni kitu cha bure huyu mwandishi hajafanya kosa
hata kama hakunitaja kuwa yale ni maandishi yangu.

Elimu ni kitu cha bure na huyu bwana kafanya kheri kusambaza elimu ni wa kupongezwa si
wa kutiwa misukosuko na kufedheheshwa.

Katika kitabu hiki nimo sana lakini yeye nadhani hajui.
Kuna Appendix kaweka vitu.

Huyo katika Appendix ni mimi lakini asingejua kwa kuwa jina langu halionekani.

Babu...
Ahsante kwa taarifa.

Mkuu nilidhani unajibu hoja hii

"mfano ukurasa wa 96, ameeLEzeA kabisa kuwa ABDU ALIKUWA KATIBU WAKATI NYERERE ANARUDI,

PIA MWANDISHI AMEONESHA KUWA ABDU ALIPENDELEA CHIEF MAKWAIA KUWA KIONGOZI WA TAA AMBAPO ALIKATAA, KABLA YA DR KYARUZI"

Badala yake unaanza ngano/simulizi?
 
aha! Kumbe tunakera? Nyani haoni nini vile?


mmechoka kwa hoja na mmelegea,mmeishiwa nguvu kabisa..!
Hazina pekee mliyobakiwa nayo ni kejeli,dharau na choko choko za kidini,mnataman ndugu moh said asitishe bakora zake za hoja ili mpate nafuu na kufuta machozi yenu lakini haisadii,
mmezid kujiaibisha,watu wengi wanawaona,wanawadharau na kuwashangaa..!

 
Yericko Nyerere,

Tulitegemea wewe ndo upo jikoni kabisa kutoa ushahidi aidha wa picha, sauti, videos na vitu vinginevyo kama ushahidi wa unayoyasema, kwasababu Mwalimu ni Mzee wako kabisa

Kisa cha Idd Fauz, tulitegemea wewe ndo ukisimulie kwa kiredu na mapana yake. Lakini unamtegea mzee Mohamed Said afanye hiyo kazi

Na bado tunategemea wewe ndo utupe mambo mingi zaidi kwenye historia ya Mwalimu.

kaka[MENTION]Do santos[/MENTION] naona upo kimya sana kaka yangu

Ritz asante sana kwa ile picha ya safari ya Mwalimu kwenda UN. Hakika ile ni kumbukumbu marwa sana

Nawasilisha
 
Last edited by a moderator:
bibiNyereretalk.jpg

Ritz,

Kumekucha,

Unanishushia picha moja moja kwa awamu kama
vidonge vya Muhimbili!

Hii Jangwani.

Unaziona kofia hizo na tarbush?

Hapo chini ya jukwaa yuko Rashid Sisso, Abbas Bakis na kundi
la Bantu Group.

Hawa ndiyo ''nascent'' TANU Intelligence.
Hao ndiyo walikuwa walinzi wa Nyerere na wahamasishaji.

Mkutano unaanza na nyimbo hii:

''Muheshimiwa nakupenda sana
Wallahi sina mwinginewe
Insha Allah Mungu yupo
Tanganyika tutajitawala.''

Huyo Bi Hawa Maftah, Bi. Tatu biti Mzee na kundi lao.
 
mkuu nilidhani unajibu hoja hii

"mfano ukurasa wa 96, ameelezea kabisa kuwa abdu alikuwa katibu wakati nyerere anarudi,

pia mwandishi ameonesha kuwa abdu alipendelea chief makwaia kuwa kiongozi wa taa ambapo alikataa, kabla ya dr kyaruzi"

badala yake unaanza ngano/simulizi?

yericko unatia huruma,umebakia kuwa debe tupu ulieishiwa hoja,
umekaa kusubiri back-up kwa ndugu zako lakini cha kustaajabu back-up hizo zinakuwa pumba kuliko ulchokisema wewe mwenyewe,unaishia kusononeka na kukimbilia kumdhihaki mkwasi wa maarifa ndugu moh said,tuliza akili upewe ilmu kijana,,
narudia tena kwa mara ya mwisho swali hili,,
"yericko nyerere una uhusiano gani na julius k nyerere?"
babu yako,baba yako,mjomba yako ama ni nani yako hasa??
Toa jibu kwa faida ya wafuatiliaji wa mjadala huu.
 
Mkuu nilidhani unajibu hoja hii

"mfano ukurasa wa 96, ameeLEzeA kabisa kuwa ABDU ALIKUWA KATIBU WAKATI NYERERE ANARUDI,

PIA MWANDISHI AMEONESHA KUWA ABDU ALIPENDELEA CHIEF MAKWAIA KUWA KIONGOZI WA TAA AMBAPO ALIKATAA, KABLA YA DR KYARUZI"

Badala yake unaanza ngano/simulizi?
Unarukaruka tu! umekataa kujibu maswali ya awali, ukaletewa swali la mwisho "umeipata wapi tafsiri ya neno muasisi uliyotuletea jamvini"? (tena baada ya kutushutumu humu jamvini kuwa hatujui maana yake) hujajibu unarukia kwingine!
 
Mkuu nilidhani unajibu hoja hii

"mfano ukurasa wa 96, ameeLEzeA kabisa kuwa ABDU ALIKUWA KATIBU WAKATI NYERERE ANARUDI,

PIA MWANDISHI AMEONESHA KUWA ABDU ALIPENDELEA CHIEF MAKWAIA KUWA KIONGOZI WA TAA AMBAPO ALIKATAA, KABLA YA DR KYARUZI"

Badala yake unaanza ngano/simulizi?

Yericko,

Kujibu hoja siyo kazi hata kidogo.

Lakini hebu soma nimesema nini katika hiyo post.
Hiyo taarifa haipo katika huo ukurasa wa 96.

Sasa wewe bila kusubiri Babu...ajibu ndugu yangu
unanishambulia.

Usomi hauendi hivyo tusubiri kwanza tusome Mwakigagile
kaandika nini kisha mimi nitazungumza.

Unajua fowadi mzuri akiwa katika kumi na nane hafanyi papara.
Anatulia na hivyo ndivyo anavyoweza kuziona nyavu.

Vinginevyo atapiga nje ya goli.

Tulia tumsubiri Babu...
 
Yericko Nyerere,

Tulitegemea wewe ndo upo jikoni kabisa kutoa ushahidi aidha wa picha, sauti, videos na vitu vinginevyo kama ushahidi wa unayoyasema, kwasababu Mwalimu ni Mzee wako kabisa

Kisa cha Idd Fauz, tulitegemea wewe ndo ukisimulie kwa kiredu na mapana yake. Lakini unamtegea mzee Mohamed Said afanye hiyo kazi

Na bado tunategemea wewe ndo utupe mambo mingi zaidi kwenye historia ya Mwalimu.

kakaDo santos naona upo kimya sana kaka yangu

Ritz asante sana kwa ile picha ya safari ya Mwalimu kwenda UN. Hakika ile ni kumbukumbu marwa sana

Nawasilisha
Kweli kabisa!...nilitegemea kuwa audio angeitoa kutoka kwenye maktaba ya familia! kumbe amepiga simu TBC! nani kati yetu asiyeweza kuwapigia TBC simu na kuwaomba audio ya hotuba ya Nyerere na kukumbana na anachokiita urasimu?!
 
Hapa ndio mzee Said unapokuwa huwatendei haki wasomaji wako; umetuwekea vichwa vya habari tu. Why don't you scan these documents and make them public for anyone to see?

MM,

Naweza kufanya hivyo lakini kwa wepesi hebu nenda Mwalimu Nyerere Foundation
niliwapa nyaraka zote nilizokuwanazo.

Kwa sasa itabidi nitulie nianze kuzisaka katika hazina yangu.
Kwani huniamini unadhani nime ''forge?''

Ondoa hofu hizo nyaraka zipo na nimezisoma zote.
 
Nanren, well said makuu.
Watu wengi wana miss point kwa kudhani kuwa wapo wanaopinga kwa ujumla hisia za Mohamed Said.
Nimeshawahi kusema na narudia, tunawashukuru sana wazee wote walioshiriki kuikomboa nchi hii tunayojaribu kuibomoa.

Nani anakataa uwepo wa Mshume Kiyate na mchango wake katika Uhuru kama ulivyo wa familia ya Sykes, Boman, Rupia, Nyerere, Kawawa, Kasella Bantu, Dr Kyaruzi, Lugazia, Dosa Azizi n.k.?

Nani anakataa kuwa gari alilopewa Nyerere lipo makumbusho na alipewa na Dosa?
Nani anakataa uwepo wa AA then TAA na mwisho TANU?

Nyerere mwenyewe kakiri ushiriki wa wazee wa Dar es Salaam, kasema kuhusu wazo la TANU lililopoanzia na jinsi alivyosirikiana na wenzake kuliendeleza gurudumu.
Nyerere aliandikiwa barua kuwa hakuna haja ya chama kingine wakati tayari kipo.
Sasa sisi kizazi hiki tutakataa kitu gain?

Tunachokataa ni jinsi hisia za Mohamed zilivyoandikwa strategically kuwaondoa baadhi ya washiriki, kuwatupia tuhuma walioshiriki, kuwadhalilisha baadhi ya washiriki na kuwakweza hata wasio husika.

Mifano, Mohamed amepindisha ukweli kuhusu ushiriki wa kanisa kwa kuficha ukweli kuwa safari ya UNO ilichangiwa na mashirika ya kikristo. Badala yake ametoa tuhuma nzito kuwa hakukuwa na ushiriki kwa hofu ya kuasi kanisa.

Mohamed, ameficha ukweli kuwa Nyerere aliwahi kuwepo Dar es Salaam kabla ya yeye kuzaliwa.
Alichokisema ni kuwa aliyemwingiza katika siasa ni Abdul Sykes.

Lengo kubwa ni kuonyesha kuwa Nyerere hakuijua siasa hadi alipokutana na Sykes.
Huu ni uzushi kwani alishakuwa katika siasa miaka mingi kuanzia Makerere.

Mohamed ameficha ukweli kuwa Clement Mtamila na Vedastus Kyaruzi na akina Lugazia walikuwa viongozi wa chama na wapigania uhuru.

Katika kupunguza thamani ya mchango wao, Mohamed ameingiza majina hata yasiyo na uhusika mkubwa just to mask the impact of true patriots.

Huwezi kuniaminisha kuwa Tatu Said alikuwa muhimu sana kuliko Kyaruzi au Yusuf Ngozi.
Ndio, kila mtu alikuwa muhimu lakini umuhimu huo una kiwango chake.

Haiwezekani aelezee kwa uchungu kifo cha Idd Faiz Mwafongo huku akisahau kuwa kifo cha aliyekuwa rais wa TAA Dr Kyaruzi hakikupewa uzito ule ule kama cha mweka hazina Mwafongo.

Lengo lilikuwa kuonyesha waislam walivyodhalilishwa huku akificha ukweli kuhusu upande wa pili.

Mohamed ametoa shutuma za Nyerere kumfukuza sheikh Amir.
Ameelezea hukumu ya Nyerere kwa sheikh bila kuweka mashtaka au tuhuma.

Leo tunajua kuwa Sheikh Amir na radical moslems walitaka kumuondoa Nyerere katika nafasi kwa sababu ya ukristu mara mbili achilia mbali kupanga mipango haramu dhidi ya serikali baada ya uhuru.

Hapa lengo ni kuonyesha kuwa baada ya uhuru Nyerere aliwachukia waislam kwa kuanzia na mufti wao.
Mohamed amesahau kuwa udini anaousema upo kumbe ulianza kwa waislam hata kabla ya uhuru

Mohamed ametoa tuhuma za ushiriki wa kanisa katika kuua EAMWS.
Ameombwa ushahidi kwa bahati mbaya sana hana, ametuletea maandishi ya Sivalon.

Kumbuka huyu ndiye mtu aliyefanya research! Tulitegemea atumie maandishi ya Sivalon kutafuta ukweli, hakufanya hivyo kwa sababu lengo lilikuwa tuhuma dhidi ya kanisa na kuonyesha uhalifu wa kanisa hata kama si kweli au hakuna ukweli alio nao.

Orodha ya mambo ni mengi sana haya ni kwa uchache tu kwa mifano, ili watu watambue kwanini watu wengi hawakubaliani na uchochezi na hisia za Mohamed.Hakuna anayetaka historia ya kweli ipindishwe, lakini basi isiandikwe kwa kupindisha ukweli ili kukidhi chuki, hisia na hasira za mtu mmoja

Muhimu sana ni kuwa kwavile Mohamed anatuhuma na mashtaka dhidi ya watu na taasisi, basi anayo dhima ya kuthibitisha tuhuma zake. Utetezi wa kutaka watu waandike vitabu au kukata vipande vya maandiko yake ni wa kiwango dhifu sana cha uandishi.

Lakini pia anapohitaji heshima lazima awe tayari kutoa heshima.

Nguruvi3,

Wewe unaponda maandishi ya Mohamed Said na kuyaita ngano yako kwako sijui tuyaitaje.

Unasema udini ulikuwepo toka kabla ya uhuru sijui umeipata wapi wewe na Nyerere sijui tumuamini nani.

Pitia tena hotuba ya Nyerere anavyowaelezea wazee wa Dar es Salaam wakati wa TANU na harakati za kupigania uhuru.

Nyerere mwenyewe anakiri fadhira za Wazee wa Dar es Salaam kuna kipindi anasema alikuwa Mkiristu peke yake lakini wanamtendea wema wewe leo unasema walikuwa wadini.

Angalia hizo picha wazee walivyokuwa na mahaba na Nyerere.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nilidhani unajibu hoja hii

"mfano ukurasa wa 96, ameeLEzeA kabisa kuwa ABDU ALIKUWA KATIBU WAKATI NYERERE ANARUDI,

PIA MWANDISHI AMEONESHA KUWA ABDU ALIPENDELEA CHIEF MAKWAIA KUWA KIONGOZI WA TAA AMBAPO ALIKATAA, KABLA YA DR KYARUZI"

Badala yake unaanza ngano/simulizi?

Bila ya kukusimulia ungenijuaje?

Hebu soma hii kutoka katika kitabu changu:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] In 1954, risking his job as Market Master, little did Abdulwahid realise that a time would come when the history of the struggle would be written and his name would not be associated with that important period in the history of Tanganyika as a nation.

One can also speculate what would have been the role of Nyerere in the politics of Tanganyika if Chief Kidaha had accepted TAA's proposal to become president of the Association in 1951; or what would have been the future of Tanganyika if Abdulwahid and the TAA inner circle had accepted Ivor Bayldon's proposal to form a multiracial political party.

This was an obvious ploy contrived by the government to co-opt the nationalists and hence compromise their stand for majority rule.

What the government was seeking was to incorporate the TAA leadership with the traditional authorities in the Legislative Council and form what could be wrongly perceived as true representative body of authority with the Governor at the top.

This would have nipped in the bud the struggle for majority rule for the Africans of Tanganyika.

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] With such an hypothetical set up, would Nyerere had been able to form a political party of his own, either within the framework of the TAA or from any other base? Would his party build its power base first from the peasantry in his home area in Musoma, or could he have ventured to build his base from Dar es Salaam with the same Muslim support he was able to get in TANU through his acquaintance with the townsmen? [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
He is on a mission(jihad)
Halafu wanatokea watu kama Mag3 wanataka kutia mchanga kitumbua chake, hata usingizi hawezi kuupata! Kitu ambacho yeye Mohamed Said na "cheerleader" wake (nimeona wakiitana waje kuokoa jahazi) wanashindwa kukitambua ni jinsi huu uzi unavyozidi kumuumbua na kumwacha uchi...sasa yeye mzee wa watu badala ya kuchutama anazidi tu kujifunua, duh! Tofauti na Mwanakijiji na wenine, mimi naziita hizi simulizi zake kwa jina lake, ngano...sifichi msimamo wangu.

Narudia maswali yangu na sasa nimeongeza la nane;

  1. Abdulwahid Sykes aliingia kwenye uongozi wa AA mwaka gani kwa mara ya kwanza na kwa wadhifa gani?
  2. Je mwaka 1946, Mwalimu Nyerere alipohudhuria mkutano wa AA Dar es Salaam kama katibu wa tawi la Tabora, Abdulwahid alikuwa na nafasi gani ndani ya AA?
  3. Je, Abdulwahid Sykes alihudhuria huo mkutano uliofanyika mwaka 1946 Dar es Salaam na kwa wadhifa upi ndani ya AA?
  4. Je, Abdulwahid Sykes kama alihudhuria, kwa nini idaiwe ni mwaka saba baadaye, 1953, ndio kakutana na Nyerere kwa mara ya kwanza?
  5. Je, kama mwaka 1946, Abdulwahid Sykes hakuwa na sifa wala wadhifa wa kuhudhuria huo mkutano wa AA, nani kati yake na kaka yake Mwalimu Nyerere alitangulia kwenye siasa?
  6. Je si kweli kuwa Dr. Kyaruzi, aliyefahamiana na Mwalimu Nyerere toka Makerere, ndiye aliongoza mapinduzi ndani ya AA mwaka 1950 na yeye kuchaguliwa Raisi wa kwanza wa TAA?
  7. Mkutano wa kwanza wa kuizindua AA mwaka 1929, ulifanyika nyumbani kwa nani na chini ya uongozi wa nani?
  8. Kwa nini hasa AA ilianzishwa mwaka 1929...je hiyo AA iliihusu Tanganyika peke yake? Ni wakati gani ilibidi ibadilike na kuitwa TAA na kwa sababu gani?
Nitatoa hapa nukuu kidogo kutoka kitabu cha Sanderson Beck, "Tanganyika and the British 1918-1950".
After the armistice of November 11, 1918 and the 1919 Peace Conference, German East Africa was turned over to the British and became known as Tanganyika. Horace Byatt had been in charge of German East Africa since 1917, and on January 31, 1919 he became Civil Administrator. In 1919 the Indians refused to vote for two members of the Legislative Council because many fewer Europeans were allowed to elect eleven. The League of Nations came into existence in January 1920, but the B mandates did not take effect until July 1922. The Administrator Byatt became the Governor and Commander-in-Chief. In 1920 the judiciary was revised by the Courts Ordinance, and the departments of Agriculture, Forest, Education, and Land Survey were created. Between 1920 and 1922 the British provided Tanganyika with £408,000 in grants-in-aid, and Governor Byatt tried to increase revenue by promoting African cash crops. On March 22, 1921 the Belgians ceded Ujiji District and the parts of Ufipa and Biharamulo they had held. The Belgian mandate of Rwanda-Urundi was fixed in December 1923.

In 1922 Martin Kayamba and other educated Africans formed the Tanganyika Territory African Civil Servants Association. They started libraries and bought newspapers. Education lagged behind what the Germans had, and in 1924 Tanganyika had only 72 schools in rural areas. Conflict in the Chagga and Haya regions led coffee growers to form associations to compete with the chiefs, who were educated and became a privileged group. In 1924 other educated Haya organized the Bukoba Buhaya Union and demanded equal opportunity in education and a share of coffee profits. Major C. St. J. Orde Browne was appointed Special Labour Commissioner to investigate labor problems. The Phelps-Stokes Commission visited in 1924, and the Government encouraged mission schools; but in 1925 Africans were not allowed to be in the same schools as Indians lest they get political ideas. A school in Tabora was restricted to the sons of chiefs and headmen.

Governor Donald Cameron (1925-31) did not approve an Advisory Council. In 1925 the Chagga asked the Governor to let them export coffee through the Kilimanjaro Native Planters' Association because Indian merchants had combined to keep their prices down. In 1926 the Masters and Servants Ordinance required paying wages in cash and reporting any serious injury to an employee. The first Legislative Council met on December 7, 1926 with fourteen officials and five Europeans and two Indians as unofficials. In 1927 Cameron opposed the federation plan of the Hilton Young Commission; but Tanganyika adopted the customs tariff used in Kenya and Uganda, and the three territories agreed to free trade across their borders. The African Education Ordinance provided for grants-in-aid to begin January 1, 1928, and the Government's budget for education increased to £80,000 a year. This was less than the Medical Department, which the East Africa Commission considered just as understaffed as the Education and Agricultural departments.

In 1929 the Native Courts Ordinance removed the supervision of the High Court from the native courts and placed them under the Provincial Administration. The African chiefs were authorized to maintain order and collect taxes, and they could use a portion of the taxes and fines for administration. That year Tanganyika began grants-in-aid to Indian schools. The unofficial members of the Legislative Council were increased, but still no Africans were appointed. Cameron reorganized the 22 districts into eleven provinces. He appointed Charles Dundas as secretary for native affairs, and he was succeeded by Philip Mitchell. Governor Cameron opened up the Iringa area and other places for settlement, and he allowed Germans to return. In 1929 the Tanganyika African Association (TAA) was formed as a national improvement organization, and they formed nine branches. In 1930 the Tanganyika Sisal Growers' Association was formed to try to reduce wages.

The depression of the early 1930s caused Tanganyika's major exports of sisal and coffee to fall sharply. Sisal had been selling for £32 a ton, but by 1931 the price was only £12 a ton. In 1931 Tanganyika had 8,200 Europeans but 25,000 Indians. That year a Parliament committee in London listened to influential Africans object to enlarging the political power of white settlers. Governor Stewart Symes (1931-34) tried to increase agricultural production, especially by Africans. Prices began to rise in 1933, and in 1935 the sisal exported was worth £1,000,000. Cotton revived, and tea and sugar were successfully produced. In 1936 the Bukoba Buhaya Union protested the chiefs' new coffee rules. When riots resulted, the British jailed the leaders. Erica Fiah founded the Tanganyika African Welfare and Commercial Association, and in 1937 he founded the Swahili newspaper, Kwetu.

By the end of the 1930s gold had become a major export. In 1938 the Governor agreed to contribute £100,000 to Makerere College in Uganda to train professionals. After World War II began in September 1939, Tanganyika exhausted its reserves by giving £200,000 to Britain. Because the territory had 3,205 Germans compared to 4,054 British residents, the enemy aliens were interned during the war. German leaders, confident of victory, instructed the settlers not to resist. About 87,000 Africans in Tanganyika were conscripted for service in the war. In 1940 all incomes over £350 a year were taxed, and the next year all those over £200 were taxed.

During the first five years after World War II Tanganyika developed its economy, and their trade tripled in three years. The TAA continued to agitate for more opportunities for Africans. Two Africans were appointed to the Legislative Council in 1945, and two more were added in 1948; but the Europeans had seven unofficial members and the Asians three. At a conference at Dar es Salaam in 1946 they called for the election of Africans to representative councils and self-government. The United Nations Trusteeship Council urged Britain to develop Tanganyika toward independence, and its first mission visited the colony in 1948. When Edward Twinning became governor in 1949, he appointed a committee to investigate constitutional development.

Ninchotaka kusema hapa ni kwamba Watanganyika Weusi walibaguliwa kwa rangi yao na si dini na hivyo mwamko ukawa ni kudai usawa na haki. Huu mwamko kama mnavyoona ulichelewa sana kuanza Dar es Salaam...sasa kama huu mwamko ndio udaiwe kuwa msingi wa harakati za uhuru, basi ni miaka mingi kabla ya kuzaliwa AA ya Cecil Matola akishirikiana na wazee wa Mohamed ambao kwa muono wake ni Manyema na Wazulu, wa Gerezani na Waislaam. Lakini kama tunaongelea chama kilichoasisiwa rasmi kudai uhuru na kutambulika kama chama cha siasa, ni TANU iliyozaliwa tarehe 7, Julai 1954 ikiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere.

Kwa nini nasema hivi? Yako madai ya kipuuzi yanayoletwa na Mohamed Said kwamba AA ndiyo msingi wa kupatikana kwa uhuru nchini. Kwa nini tusianzia mwaka 1922? mwaka 1923? mwaka 1925? au mwaka 1927? Mbona tayari vyama vya kupigania maslahi ya Watanganyika vilikuwepo sehamu nyingi tu ya Tanzania hata kabla ya AA. Je ni kwa sababu mababu zake Mohamed Said walishiriki kuanzisha AA mwaka 1929 ndio wawe vinara wa harakati hizo? Mimi namtaka Mohamed Said ajibu hayo maswali yangu kwanza ili wanajamvi waweze kutambua uwongo, ghilba, chuki, uchochezi...vilivyotawala maandishi yake.

Turudi kidogo nyuma wakati wa Mjerumani...Wazulu na Manyema wanaingiaje hapa? Hebu someni hii;
In 1889 Hermann Wissmann as Imperial Commissioner, recruited 600 Sudanese from Cairo, 50 Somalis from Aden, and 350 Zulus from Mozambique. Wissmann established his headquarters at Bagamoyo only six miles from Abushiri's camp at Sanganzeru. He repudiated the armistice the Germans had made with Abushiri and routed his forces in May. Wissmann built a fort at Mpwapwa. Abushiri retreated inland and recruited 5,000 Maviti from the Yao and other tribes. They marched on Bagamoyo in October, but Abushiri was defeated again and fled. He was caught and hanged at Pangani on December 15. Wissmann then regained Kilwa, Lindi, and Mikindani...

Na hii pia;

...German administrators often used Swahilis and Arabs as akidas (agents). In 1905 the southern region of German East Africa rebelled. For the next two years the Rufiji people working in the communal cotton fields were not paid, and they began the Maji Maji war that was led by Kinjikitili Ngwale. He was a prophet for the African deity Bokoro and sprinkled people with special water (maji) to make them immune to German bullets. In July at Kibata in the Matumbi hills the Africans refused to do compulsory labor, and they besieged the local akida in his house. On July 28 they cut the telegraph line between Kilwa and Dar es Salaam. Three separate forces led by Germans attacked before the villagers at Kibata surrendered.

Je yawezekana miaka hiyo ya nyuma hataji Mohamed Said kwa sababu mababu zake walikuwa upande wa Mkoloni Mjerumani? Jamani tumetoka mbali, tusizikubali hizi ngano za kichochezi anazoleta Mohamed katika mission yake ya kupandikiza chuki za kidini, ili iweje? Kutusambaratisha?
 
fatilien history msipelekwe pelekwe abdulwahid sykes mwaka 1948 alikua katbu wa chama cha wafanyakaz bandarin wakat huo nyerere dsm anaickia tu nyerere kaletwa kwa abdul na kasela bantu kwa kimemo pia hcho chama cha taa kimeanzshwa na baba yke abdulwahd sykes nyumban kwao jiulize taa imeanzshwa mwaka 1929 Nyerere kaingia mwaka 1953
 
MM,

Naweza kufanya hivyo lakini kwa wepesi hebu nenda Mwalimu Nyerere Foundation
niliwapa nyaraka zote nilizokuwanazo.

Kwa sasa itabidi nitulie nianze kuzisaka katika hazina yangu.
Kwani huniamini unadhani nime ''forge?''

Ondoa hofu hizo nyaraka zipo na nimezisoma zote.

La hasha mkuu wangu wala sijadhani umeforge; nina maana ulichosema hapo juu ni kana kwamba nakala za hizo documents ndio umetuwekea kumbe ni vichwa vya habari tu. Kama wewe unazo na zinaweza kupatikana kutoka kwako itakuwa vizuri tu na rahisi zaidi... jitihadi utupatie tunatanguliza shukrani.

Unayo hotuba ya Nyerere kuaga mwaka 1985?
 
Yericko Nyerere,

Tulitegemea wewe ndo upo jikoni kabisa kutoa ushahidi aidha wa picha, sauti, videos na vitu vinginevyo kama ushahidi wa unayoyasema, kwasababu Mwalimu ni Mzee wako kabisa

Kisa cha Idd Fauz, tulitegemea wewe ndo ukisimulie kwa kiredu na mapana yake. Lakini unamtegea mzee Mohamed Said afanye hiyo kazi

Na bado tunategemea wewe ndo utupe mambo mingi zaidi kwenye historia ya Mwalimu.

kaka[MENTION]Do santos[/MENTION] naona upo kimya sana kaka yangu

Ritz asante sana kwa ile picha ya safari ya Mwalimu kwenda UN. Hakika ile ni kumbukumbu marwa sana

Nawasilisha

Nikweli ninayo mengi sana, lakini hata hayo niliyokkupeni yana mafaa pia ndugu!
 
Last edited by a moderator:
Hate is taught, Love comes naturally.

Mzee Said, ninatatizwa sana na mitazamo hasi, mitazamo ya 'wao' na 'sisi'.

What kind of future do you see in Tanzania?
Hilo ni swali langu moja na nitaendelea kukuuliza swali hilo kila nipatapo nafasi, likiwa na sehemu tofauti tofauti.

Wakati unanijibu, uwe unajiuliza, what difference have you made to the youth of this nation that inspire the future you want to see. Nitakuwa nakukumbusha hili.

You must be the change you wish to see in the world.
—Gandhi

I’d rather live with a good question than a bad answer.
—Aryeh Frimer
 
mmechoka kwa hoja na mmelegea,mmeishiwa nguvu kabisa..!
Hazina pekee mliyobakiwa nayo ni kejeli,dharau na choko choko za kidini,mnataman ndugu moh said asitishe bakora zake za hoja ili mpate nafuu na kufuta machozi yenu lakini haisadii,
mmezid kujiaibisha,watu wengi wanawaona,wanawadharau na kuwashangaa..!

Nani hapa anayejiabisha? Yule anayechomekezea maneno yake na kubadilisha uwongo kuwa ukweli? Acha ushabiki na upofu.
 
Back
Top Bottom