Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Ritz linapokuja suala la kuwataja viongozi waliopigania uhuru wetu, huwezi kuwataja watu wote walioshiriki kwa ujua wao, mara nyingi hutajwa mtu aliyekua kiongozi wa harakati hizo. hii haina maana kuwa wengine walokuwa nae bega kwa bega wamesahaulika. ona jinsi anavyo enziwa Nelson Mandela kama mpigania uhuru A kusin, inamaana hakuwa na watu walio kuwa naye katika kusaka uhuru? mbona hawatajwi? Arafat wa palestina hutajwa yeye peke yake kama vile hakuwa na wapambanaji wengine. wapo na wengine wengi sana tu ambao hutajwa peke yao mf: Jomo kenyata, lumumba na wengine. angalia raisi kikwete anapokuwa katika ziara mbalimbali hutajwa yeye peke yake kuwa ndie kasema hiki na kile hata kama hotuba kaandaliwa na mwingine. hivyo suala la kwanini huyu kasahaulika ktkt historia sio la msingi.
 
Last edited by a moderator:

Hilo swali umelielekeza sipo.

Sisi Waislam tumeilalamikia serikali siku nyingi kuhusu dhulma.
Serikali imetupuuza.

Hapa nilipo nipo katika juhudi ya kueleza tulikotoka na nini kilipitika
hadi tumefika hapa.

Kitu cha kufanya ni kwa serikali ikatoka ilikojificha ikakubali ukweli
kuwa tuna tatizo.

Baada ya hapo tuzungumze na kusafiana nia.
 

Nikweli umesimulia, lakini hujawa msaada kwangu kwa mengi, msaada wako kwangu umekuwa ni 0.01% katika yale niyajuayo,

Ninaamimi katika simulizi za wazee wako wa kariakoo unaijua kwa 100% kabisa, lakini HISTORIA ya ukombozi wa nchi hii huijui, na unahitaji msaada mkubwa sana ikiwa mwili na akili yako bado vitakuwa na ushirikiano mzuri!

Karibu tujifunze histori ya nchi, sio ya wazee wako wale WALIOASI baada ya uhuru na wakakumbana na ghadhabu ya watanzania chini Mtakatifu Julius Nyerere!
 
Mohamed,
You and I know that a multiracial political party in those days and circumstances would not have gotten anywhere. UTP anyone? Usidharau moto ulioanzishwa na TANU bwana. Muulize Zuberi Mtemvu alipata kura ngapi 1959. Hamna cha kuspeculate hata kidogo.
 

Wala usihangaike kunikumbusha.
Hivi shida yote hiyo inikute kwa kutaka nini?

Nimekuelekeza nenda kwanza MNF niliwapa zote tena
miaka mingi sana iliyopita.
 
Ritz, mimi hata siku moja sikuwahi kusema wazee wetu walikuwa wadini. Kinyume chake nimekuwa natetea kuwa hawakuwa wadini ndio maana waliweza kufanya kazi across the board. Nimetolea mifano ya akina Sykes, Mshume, Rupia, Lugazia Kyaruzi, Kawawa, Chaurembo, Yufu Ngozi n.k. na mara zote nimesema wazee wetu tunawashukuru, sio tunawapongeza tu bali tunawashukuru sana!

Aliyeonyesha kuwa kulikuwa na udini ni Mohamed Said. Mohamed anasema miaka 1950 kulikuwa na radical moslems kwa maneno yake, waliotaka kumuondoa Nyerere katika uongozi wa chama kwasababu ya ukristu wake.
Tafadhali sana naomba uelewe ni Mohamed Said siyo maneno yangu.

Mohamed akaeleze kisa cha kuundwa kwa AMNUT na radicals.
Mohamed akasema kuwa bila Abdul Sykes Nyerere asingeweza kufanikiwa kwasababu kwa nyakati hizo mkristo hakukubalika. Hayo si maneno yangu ni ya Mohamed yakishadidia kuwa Mohamed aliona suala la udini kuanzia nyuma.

Hata pale ilipothibitika kuwa Kyaruzi na Mtamila waliwahi kuwa viongozi ndani ya jiji la Dar badio Mohamed ameshikilia kuwa Nyerere asingeweza kufanikiwa. Hii maana yake ni kuwa kulikuwa na udini kwa mtazamo wake

Kwa muktadha huo na ushahidi wa maneno ya Mohamed nasimama kusema kuwa Mohamed anajua udini ulikuwepo kuanzia zama hizo kwahiyo si haki kusema udini uliletwa na Nyerere.

Sijatuhumu wazee wetu, ninachofanya ni analysis ya maneno ya Mohamed na jinsi anavyo skew information.
Matokeo ya spinning ni kuwanyooshea kidole wale anaowatetea.

Mimi nimeandika kuanzia mwaka 2011 katika minakasha kuhusu maneno ya Nyerere alivyokiri.
Hata katika uzi huu nimeandika hayo kama unanisoma vizuri.
Post iliyopita nimesema kuwa Nyerere amekiri katika kitabu chake ''we must run..'' kwa kuwataja wazee.

Mimi ni miongoni mwa watu waliokariri maneno ya Nyerere hata kabla kipande hakijawekwa.
Nimekuwa napinga dhana kuwa Nyerere aliwadharau wazee hawa na nimepinga dhana kuwa wazee walimdharau yeye.
Kwahiyo hapo unafanya spinning ku-discredit maandishi yangu lakini wasomaji wananielewa nasimamia nini.

Narudia, anayejenga dhana ya wazee hawa kuwa wadini ni Mohamed Said Abdallah Salum muyukwa Samtungo.
Siyo Nguruvi3 au Nyerere. Msome Mohamed vizuri.

Ama hili la kuita ngano, hilo ninabaki nalo kwasababu kila mtu ana mtazamo wake kuhusu maandishi ya Mohamed.
Wapo wanaomeza na wapo wanaofikiri. Inategemea mtu yupo upande gani wa mtazamo.

Lakini Ritz, hivi kama si ngano wewe ulijua kuwa shirika la dini la Maknol liliwahi kutoa ticket kwa Nyerere kusafiri kwenda UNO? Mbona hilo halisemwi na Mo? Hivi unajua kanisa lilishiriki vipi kuua EAMWS? unalo jibu wewe! maana Mo hana.

Ritz, Mo anasema Nyerere alikuja Dar 1952 ukweli si huo, je hiyo si ngano?
Ninabaki kusema kuwa Mohamed ameandika ngano hii kwa kutumia majina ya watu, nyakati na matukio ambayo ni ya kweli akiwa na lengo lake lililo nje ya ukweli uliokusudiwa bali aliokusudia ili kujenga mazingira anayotaka.
Kwa mintaarafu hiyo nasoama kitabu chake tofauti na wewe, kama unaona ni maandiko matakatifu hilo ni juu yako.
Mimi naona ngano! Nitty gritty!
 
Mbona na wewe unageuka kuwa copy and paste?
 

Jasusi,

Nilikusudia khasa ni hili.
Nyerere angeweza kuanzisha TANU Musoma?
 

Tukiziita "Ngano" za Sanderson Beck nadhani tutakuwa sahihi.
 
Mbona na wewe unageuka kuwa copy and paste?

Bila ya cut and paste mengi yasingepatikana humu ukumbini.

Hebu angalia hii:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] When Abdulwahid died the Ministry of Information issued a press release announcing that the President had attended the funeral of Abdulwahid Sykes.[1]

Surprisingly the press release gave few details of his government service, completely eclipsing his checkered political career.

It was an Englishman, Brendon Grimshaw, the editor of Tanganyika Standard, who published a fitting obituary to Abdulwahid describing him as: 'one of the architects of the independence movement and one of the men who helped launch President Nyerere on his political carrier...'

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] The obituary also paid glowing tribute to the family on its contribution to the political development of Tanganyika by mentioning that ‘much of the desire among Africans for a powerful political party in Tanzania came from the drive of the Sykes family'. [2]

It is said that this recognition of Abdulwahid as one of the founding fathers of the nation became a focus of attack from certain members of the TANU leadership.

They were overheard grumbling in the corridors of the TANU headquarters in Dar es Salaam that Ally and Abbas Sykes were trying to glorify their elder brother.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[1]See Press Release A/2746/68 IT/1.322 of 13 th October, 1968. East Africana, University of Dar es Salaam.
[2]Sunday News, 20 th October, 1968.
 

Kwa bahati mbaya sijauliza 'nyie wIslamu'.
Nimesema ninatatizwa sana na maelezo na mijadala ya 'wao' na 'sisi'.

Nimeanza kwa kusema Mzee Said, nikaendelea kwenye swali langu.
Lakini pia, wewe sio 'waislam' wewe ni Mzee Said ninayekuuliza swali hapa. Na ninataka kujua elimu yako na 'uhanaharakati' wako unawaweka wapi vijana wa Tanzania katika utu uzima na uzee wao.

Sijataka mawazo ya waislamu. Nikitaka nitapiga simu radio Iman au radio kheri.
Nimetaka mawazo yako kama mzee, mtanzania. Sio mwislam wala mwislam wa bara wala wa pwani.

Tafadhali sana.
Kama huwezi kujibu barazani kwasabau yoyoyte ile, nijibu hata kwa PM. Nitasema nimejibiwa, na nitashukuru.
 
Jasusi,

Nilikusudia khasa ni hili.
Nyerere angeweza kuanzisha TANU Musoma?
Kwa Musoma hapana. Nitakupa sababu zake. Nyerere alikuwa nationalist. Labda enzi hizo tumwite territorial. Aliiangalia Tanganyika si kwa macho ya Umusoma, au Gerezani kama unavyofanya. Na nahisi hiyo ndiyo tofauti kubwa kati yako na Nyerere kwa sababu yeye aliiona Tanzania kwa umoja wake wakati wewe uliiangalia zaidi kupitia macho ya Gerezani.Hata ukiangalia juhudi alizofanya akiwa Makerere alijikita zaidi kushirikiana na wenzake kutafuta chombo cha kuikomboa Tanganyika. Sasa, kama Musoma ingekuwa ndiyo makao makuu ya Tanganyika, then that would have been another issue. Sijui umenielewa?
 
Tukiziita "Ngano" za Sanderson Beck nadhani tutakuwa sahihi.

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] When Abdulwahid died the Ministry of Information issued a press release announcing that the President had attended the funeral of Abdulwahid Sykes.[1]

Surprisingly the press release gave few details of his government service, completely eclipsing his checkered political career. It was an Englishman, Brendon Grimshaw, the editor of Tanganyika Standard, who published a fitting obituary to Abdulwahid describing him as: ‘one of the architects of the independence movement and one of the men who helped launch President Nyerere on his political carrier...'
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] The obituary also paid glowing tribute to the family on its contribution to the political development of Tanganyika by mentioning that ‘much of the desire among Africans for a powerful political party in Tanzania came from the drive of the Sykes family'. [2]

It is said that this recognition of Abdulwahid as one of the founding fathers of the nation became a focus of attack from certain members of the TANU leadership.

They were overheard grumbling in the corridors of the TANU headquarters in Dar es Salaam that Ally and Abbas Sykes were trying to glorify their elder brother.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[1]See Press Release A/2746/68 IT/1.322 of 13 th October, 1968. East Africana, University
of Dar es Salaam.


[2]Sunday News, 20 th October, 1968.
 

Sana nimekuelewa.

Je bila ya ''inner circle'' ya TAA na viongozi wa Dar es Salaam angeweza kupata
watu wa kumuunga mkono?

Nani angelimjulisha wa Sheikh Hassan bin Amir?
 
Jasusi, Nilikusudia khasa ni hili.
Nyerere angeweza kuanzisha TANU Musoma?
Exactly! Angekuwa mdini angefanya exactly that. Lakini tukiacha hii dhihaka yako kwa watu wa Musoma (niliwahi kukuonya kuhusu dhihaka kama hizi!), na mimi nikuulize, ilikuwaje wazee wako wa Dar es Salaam wampe usukani mtu wa Musoma? Kwami akina Abdulwahid Sykes, Dossa Aziz, Abdallah Salum muyukwa Samtungo hawakuwepo? Hivi hata kwa akili ya kawaida hujui kuwa Dar es Salaam ilikuwa ndiyo maao makuu ya utawala wa kikoloni? Nafikiri swala zuri zaidi ni hili, je, kwa kiwango gani TANU ingefanikiwa kama haingeungwa mkono na watu si wa Musoma tu bali Kilimajaro, Mwanza, Bukoba, Mbeya, Rungwe, Iringa na sehemu zote za Tanganyika? Je unajua kwamba katika muda mfupi zaidi ya asilimia 60% ya wanachama wa mwanzo wa TANU walitoka mikoa ya Ziwa?

Hilo moja lakini la pili, unayo habari kuwa kabla ya uhuru (1961) wengi wa wazee wako waliokuwa wanachama wa TANU walijiengua na kujiunga AMNUT? Unajua kuwa kama ingekuwa ni mapenzi na maamuzi ya wazee wako tusingepata uhuru tarehe 9 Desemba 1961? Unaona unavyojaribu kupotosha mambo kwa makusudio ya kupanda, kupalilia na kujenga chuki za kidini kwa sababu tu baba zako wa Gerezani walidhani uhuru ukipatikana basi kila moja atakuwa na wadhifa kama wa Raisi wa nchi. Tazama unavyomjenga Abdulwahid Sykes...kamfundisha Nyerere kuvaa, kamfundisha kuongea kiswahili, kamfundisha siasa, kampa uenyekiti wa TANU, kamwandikia hata hotuba...duh, yaani hata kama ni matusi, aibu huna?
 
mfa maji siku zote haishi kutapa tapa,eti yericko nae anatamba sasa kumtambia moh said aende kwake kujifunza historia?historia gani sasa,umeambiwa andika basi kitabu umekosa cha kujibu,,
yaan yericko kadir muda unavozid kwenda ndivo unavozid kuonekana kwako kuwa wewe si lolote si chochote,hufaham lolote na ni kama debe tupu unaetegemea back up zisizo na tija,

ona sasa umeamua kumvisha kambarage julius utakatifu..!what a shame...!
Kambarage utakatifu autolee wapi??si huyu huyu kambarage aliezusha ya kwamba idd amini ni nduli mla nyama za watu?au mwingine si huyu??
Mmeishiwa nguvu kabisa..
 
Sana nimekuelewa.

Je bila ya ''inner circle'' ya TAA na viongozi wa Dar es Salaam angeweza kupata
watu wa kumuunga mkono?

Nani angelimjulisha wa Sheikh Hassan bin Amir?
Hakuna anayebisha juu ya "inner circle." Hata kabla hujaandika kitabu chako nilishasoma kitabu cha Judith Listowell nilipokuwa Aga Khan 1967. Ndio maana nilithamini sana uhusiano wangu na mzee Abdulwahid kwa sababu huyu nilishamsoma mchango wake. Wewe, kitabu chako, ambacho pia nimekisoma, kingekuwa na maana zaidi kwa kila Mtanzania, kama ungeelezea tu mchango wa wazee wa Gerezani bila kuingiza mambo ya udini na bila kushusha au kubeza mchango wa Mwalimu Nyerere. Nadhani wote tulio upande huu wanakubaliana na mimi kwa hilo. Lakini kwa zoezi hili unatugawa, ninyi waislamu, na sisi wakristo. Hivi utajisikiaje nikikwambia kuwa baba yangu mdogo, Suleiman Mukama, alikuwa ni muislamu, mfuasi wa Zuberi Mtemvu na mpaka anaenda kaburini hakutaka kusikia habari za TANU na Nyerere? Lakini akija nyumbani, tunaweka siasa pembeni tunaweka mbele damu yetu. Hii ndiyo Tanzania niliyokulia.
 
ungekuwa unaijua historia ya nchi hii
wala usingepata tabu ya kuandika utumbo humu jamvini
Wala usingehangaika kutafuta hotuba ya 1985 leo hii
Huna unachokijua zaidi ya kuleta uongo hapa jamvini
Kwa kweli umejifunza mengi kwa Mohamed Said
ukiangalia maandishi yako hilo lipo wazi
Huna chochote cha maana ulichoeleza kuhusu historia ya tanganyika
Umeshindwa wewe na wenzio kutuelezea hiyo historia ya 'kweli' ya tanganyika
badala yake mna kejeli na kuleta dharau juu ya kitabu cha Mohamed Said
USISAHAU KUANGALIA HAPO CHINI KWENYE RED


 
Last edited by a moderator:

satelite,

Ni kweli unachosema huwezi kuwataja wote lakini kuna wale muhimu lazima watajwe wewe nikikuuliza hebu nitajie wanachama 20 wa mwanzo wa TANU huwajuhi. Lakini wa Chadema au CUF unawajua.

ANC ya kina Mandela wapingania uhuru wao mbona wanajulikana na wameandikwa kwenye historia ya yao.

Walioanzisha ANC ni watu watatu ni John Dude, Pixley ka Isaka Seme, Sol Plaatie, mwaka 1912 wakati Nelson Mandela kazaliwa mwaka 1918 historia ipo wazi Mandela kaingia ANC na vijana wenzake wakati ule kina Olive Tambo.

Bahati mbaya kwetu kila kitu kafanya Nyerere wote tunaambiwa walikuwa wasaidizi wake.
 
Last edited by a moderator:

Mohamed,
Tatizo si nani aliyechangia uhuru wa Tanzania. Tumekusoma na tumekuelewa. Tatizo ni pale unapotaka kuunganisha kuwa nyuma kwa Waislamu katika elimu na Nyerere. Tumekubaliana sote kwamba wakati tunapata uhuru wakristo walikuwa mbele katika elimu kuliko Waislamu. Hilo halina ubishi. Pia tumeona, ingawa si katika maandishi yako, kwamba Mwalimu Nyerere alitambua tatizo hilo na kuchukua hatua kwa kutaifisha shule za wamisheni ili watanzania wote wasome bila kubaguliwa dini zao. Lakini hilo sijaona popote una acknowledge. Unaendelea zaidi kuwa kwa kupiga EAMWS marufuku Nyerere alirudisha nyuma elimu ya waislamu. Kwa hiyo tatizo si nani alichangia juhudi za uhuru. Tatizo ni hizi propaganda zako kuwa leo waislamu wako nyuma kwa sababu ya Nyerere. Hapo ndipo tunapopingana. We seem to be barking at the wrong tree. Nyerere has been dead 14 years now. Has been out of power almost 30 years. Je, mbali na Kikwete kupromote mahakimu waislamu wasio na elimu ya kutosha, kumechukuliwa hatua gani kuwasaidia Waislamu wajiendeleze katika elimu? What is the end game?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…