Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Napendekeza tufanye mazungumzo na wewe nikuhoji kuhusu ulichoandika tuone utavumilia kwa muda gani kutetea hoja zako. Sidhani kama umeshakutana na maswali ninayouliza mimi.

Mzee Mwanakijiji,

Unamuuliza Mohamed Said atavumilia muda gani kutetea hoja zake.

Mohamed Said anakula na kulala JF bado masiku machache afikishe mwezi humu hakuna yeyote humu pamoja na wewe ambaye anaweza kukaa mwezi kwenye uzi kutetea hoja zake.

Mohamed Said anafundisha ndiyo tofauti yake na nyie.
 
Last edited by a moderator:

Ritz,

Huyu Mwanakijiji nimemwekea mambo yalotokea baina yangu
na CCM Dodoma kuhusu Abdulwahid Sykes, Waislam na historia
ya uhuru.

Nimemwekea na rejea.

Badala ya kuchukulia kutoka pale tukanogesha chembelecho Zomba
anakuja na viroja.

Kama hajiwezi si aungane na wenzake wanishambulie?
Angalau labda...
 

Bw Said miye sina sababu ya kukushambulia kwani huko si kujenga hoja. Ninachojaribu kuonesha ni jinsi hoja zako zilivyodhaifu, na jinsi maandishi yako yanavutia wenye hisia wasio tayari kutumia akili zao kufikiri. Kwa muda mrefu umepata uwanja huru wa kuuza histohisia yako na kwa vile hujawahi kukutana na maswali ya kimantiki na yenye msingi wa historia umeweza kuendelea kueneza hizi simulizi.

Hata hicho ulichoweka hapo juu kuhusu wewe na Kiwanuka nakubaliana zaidi na Kiwanuka kwani assessment yake ni ya kweli. Maandishi yako hayana historia yoyote zaidi ya kurusha majina ya watu mbalimbali ambayo hata tukikuuliza uzame kidogo huwezi zaidi ya kutuambia ulikunywa chai wapi, uliingia nyumba ya nani na ulifahamiana na nani. Yote hayo hayafanyi hoja zako kuwa kweli zinapomulikwa.

Mzee Said utawala wako wa simulizi zisizokoma na zenye kurudia yale yale na ambazo hazina msingi katika historia mbona umefikia kikomo. Utaweza kuwavutia wale ambao hawana uwezo wa kufikiria au kuhoji; wale ambao hawajui fallacies zilizojazana katika maandishi yako. In Shaa Allah watu watazidi kufahamu udhaifu wa hoja zako, na jinsi gani zimejengwa kutoka katika chuki, kisasi, wivu na zaidi ya yote hisia fulani ya uduni wa aina fulani. Inatokana na uchungu wa utotoni ambao ulisimuliwa na wazee wako kiasi kwamba ulishindwa kabisa kupima kipi ni cha kweli, kipi na wenyewe wanakisema kutoka katika machungu na kipi ni masimulizi tu ya kukutia moyo.

Kwa kweli katika uandishi wa kitabu chako cha Sykes ulichokifanya ni kumuonesha Nyerere kama kipenzi cha Waislamu na wasio Waislamu na hakuna lolote mle ndani ambapo umemuonesha Nyerere kama adui wa Waislamu. Unajaribu kulilazimisha hili baadaye lakini linashindwa kwa sababu kile tukitumia vipimo vingine utaona kuwa hoja zako hazisimami.
 
sawa; kwenye ukurasa wa ngapi wa kitabu cha kivukoni panaposema nyerere alisema amepigania uhuru peke yake; na ni ukurasa gani unasema nyerere alisema aandikwe yeye peke yake tu na si wengine. Unaweza ukaweka na nukuu yake.

kwaiyo kama hicho kitabu kama hakija analyse mambo hayo unayoyasema basi ni justification sasa ya kwamba ni kitabu kilichokamilika??
You cant be serious..
 

MM,

Kuna wakati historia hii ilikuwa haipo.
Sasa hali imebadilika sana.

Mshume Kiyate ni maarufu sana.
Uliza.
 
Mzee Mwanakijiji,

Unamuuliza Mohamed Said atavumilia muda gani kutetea hoja zake.

Ritz, unatutania bana; Mohammed Said katetea hoja mahali popote humu? alichofanya ni kurudia rudia yale yale lakini akitakiwa azitetee hataki. Mbona anachofanya ni rahisi sana; kurudia kusema kile kile ulichokisema kwa sababu unakiamini - hata kama si kweli - mbona siyo kazi hivyo. Anaweza kufanya mwaka mzima. Lakini hatokuwa ametetea chochote; atakuwa amerudia rudia madai yake.

Kitu pekee ambacho ameonesha kushindwa kukifanya ni kuback up madai yake.

Kama hilo ndio unalojifunza well... can't help you buddy.
 
uwezo wenyewe wa kuhoji ni
huu unaouonyesha hapa JF?
Ujinga mtupu!
Eti utavumilia kiasi gani?
umeandaa maswali ya matusi,kejeli au....?
Kiasi cha kushindwa kuvumilia
Huna uwezo wa kufanya mahojiano na Mohamed Said
Huna hoja,huna maswali ya maana

Napendekeza tufanye mazungumzo na wewe nikuhoji kuhusu ulichoandika tuone utavumilia kwa muda gani kutetea hoja zako. Sidhani kama umeshakutana na maswali ninayouliza mimi.
 
Last edited by a moderator:
Sijibu kwa kuwa maswali yenu mengine yanachusha hayamtii mtu hamu ya kuandika.
Si kweli, wewe unachotaka ni kusema tu hutaki kutetea hoja zako, hutaki kujibu unachoulizwa. Hata hivyo ninaelewa sababu nini.
Umezoea kukalisha watu kitako na kuwasimulia huku wakisema tawire baba, wengine swadakta n.k.

Nikupe mfano mwingine wa maandiko yako maana mimi nimechoka kufikiri ninatumia kalamu yako mwenyewe kukufungua.
Mwanakijiji aliuliza swali kuwa je, wazulu walikuja Tanganyika wakiwa waislam? Jibu lako ni ndio.
Huo si ukweli! umepotosha.

Mzee Said, hapa hatupo kusikia unatumabia nini au unatutajia majina ya watu na picha zao. la hasha ustadhi! hapa ni hoja kwa hoja na wewe unajua hivyo lakini utakubali vipi mauzo ya kitabu toleo la 3 yadode?

Yaani utuambie kuwa Tanganyika imeundwa na Narung'ombe, Tandamti, mchikichini na kipata na makao makuu yake ni Gerezani nasi tuitikie tawire! real! Ibn Samtungo! Kwa jiografia hiyo kuna sababu za kulaumu NECTA kweli!
 
Ritz,
Hii picha ni baada ya TANU kuasisiwa. Waasisi wa TANU ni wale wazee 17 sio wazee wote waliokuwa TAA. Ndio maana nikamwomba mzee wetu Mohamed atuletee KATIBA ya mwisho ya TAA na ile ya KWANZA ya TANU. Amekataa ingawa anajua katiba ya TANU iliandikwaje.
 
Acha porojo 'babu'kama ni hivyo andika na wewekitabu cha historia ya uhuru wa tanganyikaumekalia hasadi na 'wivu wa kike'Siku zote ulikuwa wapi,hukuandika hicho unachokijua@mohamed said ameandika kitabu na kina miaka 15 sasa!kama 'ameongopa' andika chako kinachoelezea ukwelijibu zuri kwa Mohamed Said ilikuwa nanyi mtoe kitabusio kuandika ----- ktk mitandao
 
Last edited by a moderator:
hapo kwenye red wagala ndio mnaponichosha
umesema sio kweli,haya lete ukweli wewe
nyinyi ndo wapotoshaji na waongo
 
MM,

Kuna wakati historia hii ilikuwa haipo.
Sasa hali imebadilika sana.

historia isiyokuwepo siyo historia

Mshume Kiyate ni maarufu sana.
Uliza.

Ndio maarufu lakini ni umaarufu wa nini? Mtu yeyote anaweza kuwa maarufu lakini ukijiuliza utaona kuwa ni maarufu kwa nani? Unadhani ukienda Mbeya hata mjini u kiuliza Mshume Kiyate watu wanamjua. Kama ni maarufu miiongoni mwa Waislamu (kitu ambacho naamini unamaamisha) utasema umefanikiwa sana? Lakini umeangalia ni umaarufu gani unasema alikuwa nao?

Ngoja nitoe mfano kwenye maandishi yako mwenyewe. Unaanza simulizi lako kuhusu Mshume Kiyate kwa kusema hivi:


Sasa tufikirie kidogo: Huyu Nyerere mwenye chuki dhidi ya Waislamu na ambaye hakutaka wenzie walioshiri naye katika harakati za uhuru wajulikane anasimulia kisa hiki. Na anaye msimulia siyo Askofu wa Kikatoliki bali mmoja wa wazee wako - Ahmed Rashid Ali.

Unaendelea na kusema:

Baada ya Mwalimu Nyerere kumaliza kutoa msimamo wake wakawa sasa wamekaa wanapiga gumzo huku wakinywa vinywaji na Mwalimu alikuwa mtu hodari sana wa kustawisha baraza. Waliokuwa karibu na Nyerere wanamjua kwa sifa hii.

Haya ni maneno yako. Unachosema hapa ni kuwa hadi mwaka 1965 ambapo kisa hiki kinadaiwa kutokea Nyerere alikuwa na uhusiano mzuri tu na angalau mmoja wazee wako Ahmed Rashid Ali. Siyo uhusiano mzuri tu.. unasema walikuwa "wakinywa vinywaji" tena wapi.. nyumbai kwake. Dossa, mzee Rashid wako nyumbani kwa Mwalimu na kunywa naye chai; na hii ni mwaka 1965! Siyo maneno yangu haya ni ya kwako. Unaendelea tena:


Wanafunzi wako hapa kina Ritz nikiwauliza hapa mara moja Nyerere na Mshume Kiyate walifahamiana lini na wapi kwa haraka watasema "ofisini kwa Abdulwahid Sykes pale Kariakoo". Lakini ukweli ni kuwa hujui walifahamiana vipi na lini. Umeandika hisia zako kwa kusema "lakini huenda" ikawa mahali pale. Lakini hiyo ni hisia yako tu haina msingi wowote katika ukweli. Haya tuendelee


Unataka watu wenye akili timamu waamini kuwa Nyerere kaondoka nyumbani kwake kwenda Kariakoo kununua kitu sokoni bila kitu mfukoni. Siijui vizuri Dar-es-Salaam hasa eneo la "Majumba Sita" nitaulize nieleweshe tu uhusiano wake na ile "Majumba Sita" ya kule Kipawa. Hii Majumba Sita ya Magomeni ni ipi ili angalau niweze kufikiria umbali maana ile ya Kipawa ni mbali sana kuliko ya Magomeni. Sasa Nyerere anaondoka nyumbani kwake kwenda sokoni bila kitu mfukoni. Na haya ni maneno yake - uliyosimuliwa. Hadithi hadithi.. tuendelee

Akiwa njiani karibu na sehemu inayoitwa Mwembe Togwa (hapa kwa leo ni pale Fire makutano na Morogoro Road na Barabara ya Umoja wa Mataifa)Mwalimu alikutana na Mzee Mshume Kiyate.

Tukubaliane na weewe tu kuwa kati ya watu wote katika siku hiyo isiyo na jina Nyerere anautana na Mshume Kiyate. Sawa nasibu inaweza kutokea haya tuendelee.



Na wapo watu wanaamini hili simulizi; Mshume katoa karibu nusu ya gharama ya kujenga nyumba kampa Nyerere kwenda sokoni! koh koho koh... utamu njoo...


Pamoja na utamu wote wa simulizi hili na kwa kweli linagusa moyo tatizo ni kuwa Mama Maria Nyerere yupo hai. Yeye peke yake anaweza kuelezea kwa kirefu hili na kukupa ushahidi zaidi wa msaada wa Mshume. Hujawahi kumtafuta, hujawahi kumuuliza na hata kutaka kujua kumbukumbu alizonazo kuhusiana na hali ngumu ya maisha. Tunatakiwa tukubali tu...


Nyerere alikuwa na chuki na Waislamu; hadi hapa inaonekana kuwa hadi kupata uhuru hawakuwa na tatizo lolote. Na kwa vile unasema Ahmed Rashad Ali alisimuliwa kisa hiki na Baba wa Taifa mwaka 1965 akipata "vinywaji" na kina Dossa ni wazi kuwa hadi mwaka 1965 bado kulikuwepo na Waislamu wengi tu - miongoni in mzee wako Ahmed Rashad... walikuwa na nafasi nzito tu serikalini. Kukumbusha tu umetuambia kuwa Bw. Ali alikuwa Katibu Mkuu Msaidizi Idara ya Habari!

Lakini unaendelea na kusema:


Sasa hapa unaingiza ile kanuni yako; unawanukuu wale marehemu ambao huwezi kuwahoji. Marehemu Ditopile alikipata wapi kisa hiki. Tukumbuke kuwa kulikuwa na watu watatu tu ambao walikuwa wanafahamu kisa hiki. Mzee wako Rashad, Dossa Aziz na Lucy Lameck. Hivyo, Ditopile atakuwa amesimuliwa. Na nani?

Lakini pia unasahau kitu kimoja muhimu kwenye communication jinsi habari inavyobadilishwa kwa kadiri kinavyopitishwa kwa watu. Lucy Lameck alikuwa ni mtu pekee wa kukuhakikishia kisa hiki ili ulinganishe na ulichosikia toka kwa mzee wako. Lakini kwa miaka yote uliyoandika kitabu chako hukujaribu kwenda kuuliza toka kwa Lucy Lameck yeye anakumbuka vipi kisa hiki. Hukufanya hivyo Bana Said... yawezekana kwa sababu alikuwa Mkristu? au kwa vile ni mwanamke ushahidi wake hauaminiki sana? Tuendelee...


Magazeti yalisema nini na ni magazeti gani? Historia inadai uyataje matoleo na kile walichokisema angalau tujue jinsi gani waligeuza hicho kisa.


Lakini katika kuonesha jinsi ambavyo unaandika bila kufikiria sana unachosema unadai hivi (na bahati mbaya kina Ritz wataamini maskini)


Sasa hili linadai ukweli. Kweli kuna watu wanakusoma hapa na wanaamini kuwa Nyerere hakupiga picha yoyote kati ya 1955 na 1961 ambapo mzee Mshume hakuwemo ndani? Picha hii ni ya Nyerere na Machifu na ilichukuliwa 1961...



sasa simulizi lako ndivyo lilivyo. Lakini lote limeanza kwa simulizi la mtu mmoja tu ambaye peke yake umemuamini na sisi wengine wote tunatakiwa tuamini. Sina shaka hata kidogo Mshume Kiyate alikuwa na mchango wake lakini alikuwa na mchango kuliko Nyerere? Alifanya zaidi ya Nyerere? Ushahidi wako mwenyewe unaonesha Nyerere hakumsahau na hakutaka watu wasahau...

Inaitwa Spirit of TANU...

Leo unasema Nyerere alitaka watu wasahuliwe; yeye ambaye amekumbusha majina yao. Kwa ufupi, usingejua alichofanya Mshume kwa Nyerere kama Nyerere mwenyewe asingesimulia! Ungejuaje? Hata mzee wako Rashad asingeweza kujua. Kumbe ni Nyerere kamrudisha mzee Mshume kwenye historia. Siyo mzee Rashad, Siyo Kitwana Kondo, siyo Dossa Aziz. Wewe mwenyewe unaposimulia kisa hiki inabidi utoe shukrani kwa Nyerere kwa kuwa mwaminifu na muungwana wa kukiri.

Angekuwa na Makuu Nyerere asingesimulia hili. Asingeheshimu mchango wa wazee hawa asingetaja miaka minne baadaye.

Mzee Said nikikuuliza ukiondoa hilo simulizi la Nyerere kumhusu rafiki yake ambalo leo linadumu na kunogesha mazungumzo yako ni kitu gani kingene ambacho mzee Mshume alikifanya na kupata umaarufu katika TANU. Mchango wake mwingine wa "hali na mali" ni upi? Sasa siulizi hili kwa sababu nadharau bali nataka kuonesha tu kuwa umaarufu wa Mshume umetokana na Nyerere na si vinginevyo. Kabla ya kukutana na Nyerere umesema alikuwa maarufu; kwenye mambo gani? kwenye siasa? au kwa kuwa mchuuza samaki?
 
hapo kwenye red wagala ndio mnaponichosha
umesema sio kweli,haya lete ukweli wewe
nyinyi ndo wapotoshaji na waongo
Nimesoma Ilm ya mnakasha, hutoi silaha zote kwa wakati mmoja!!
Soma vizuri na kwa fikra pana nilivyoandika halafu jiulize kwa sentesi yangu fupi je, sikujua kuwa ninapaswa kusema nini!
Zamani sisi tukitega ndege kwa karai na punje mbili za mahindi, ndege akiingia unavuta kamba!
sikuhizi mnatumia ipod! ok
 
Mzee wetu kawapaka vibaya UDINI wazee wake hawa akidhani anammaliza na kulipiza kisasi kwa Mwalimu. Anawagawa pia Waislam kwa kuwaita wengine ni "WAISLAM wa BAKWATA" kwa kuwa walimuunga mkono Mwalimu katika utawala wake na kupambana wazi na UDINI wa watu kama Sheikh Amir.
Mzee wetu Mohamed hatabadilika kwa kuwa alikwisha yaandika haya. Muhimu ni kuwa naye karibu tu asiendelee kuwavuruga vijana wadogo wa Kiislam ambao wana muda mrefu wa kuishi kuliko yeye. Mtu msomi wa kiwango chake hawezi kufikiria watu kugawana vyeo na madaraka kwa uwiano wa DINI, kugawana fursa za ELIMU kwa kuzingatia DINI, historia ya NCHI iandikwe kwa kuzingatia DINI za wahusika. Hatutaishia hapo tu.
Tuendelee kuijenga TANZANIA hii hivi tulivyo. Muislam anamuoa Mkristo au kinyume chake; Tunachaguana kwenye UONGOZI wa NCHI kwa sifa binafsi ya mtu sio dini yake.
 
huna unachokijua
sote tu watu wazima humu
ni ngumu kusema hujui
lakini tushakuelewa,
usijali tuendelee kuchota maarifa to kwa Mohamed Said
 
Last edited by a moderator:
umesahau kumwambia hata matonya (R.I.P) alikuwa omba omba maarufu sana hapa tanzania pengine kuliko hata baadhi ya viongozi waliopata kushika nyadhifa mbalimbali za kitaifa..
 

Mbona ueleweki wewe kila siku unaandika humu JF tatizo la Waislam ni Uislam wenyewe saizi unamlalamikia Mohamed Said.
 
Mbona ueleweki wewe kila siku unaandika humu JF tatizo la Waislam ni Uislam wenyewe saizi unamlalamikia Mohamed Said.
Ah! Ritz, hiyo post inajitosheleza. Isome tena. Yapo matatizo yanayochangiwa na UISLAM hasa upande wa ELIMU. Kwa kuna Muislam wa kiwango chenu cha elimu halioni hili huyo ni MDINI wa kutupwa. Ni mfiaDINI. Hatufai.
Labda nikuulize swali dogo Ritz: Uliwahi kupata kikwazo chochote cha ELIMU, MATIBABU, AJIRA, HUDUMA,..., kwa ajili ya DINI yako?
 


Leo unamjuwa mpaka Mshume, ungemjuwaje kama si Mohamed Said?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…