historia isiyokuwepo siyo historia
Ndio maarufu lakini ni umaarufu wa nini? Mtu yeyote anaweza kuwa maarufu lakini ukijiuliza utaona kuwa ni maarufu kwa nani? Unadhani ukienda Mbeya hata mjini u kiuliza Mshume Kiyate watu wanamjua. Kama ni maarufu miiongoni mwa Waislamu (kitu ambacho naamini unamaamisha) utasema umefanikiwa sana? Lakini umeangalia ni umaarufu gani unasema alikuwa nao?
Ngoja nitoe mfano kwenye
maandishi yako mwenyewe. Unaanza simulizi lako kuhusu Mshume Kiyate kwa kusema hivi:
Sasa tufikirie kidogo: Huyu Nyerere mwenye chuki dhidi ya Waislamu na ambaye hakutaka wenzie walioshiri naye katika harakati za uhuru wajulikane anasimulia kisa hiki. Na anaye msimulia siyo Askofu wa Kikatoliki bali mmoja wa wazee wako - Ahmed Rashid Ali.
Unaendelea na kusema:
Haya ni maneno yako. Unachosema hapa ni kuwa hadi mwaka 1965 ambapo kisa hiki kinadaiwa kutokea Nyerere alikuwa na uhusiano mzuri tu na angalau mmoja wazee wako Ahmed Rashid Ali. Siyo uhusiano mzuri tu.. unasema walikuwa "wakinywa vinywaji" tena wapi.. nyumbai kwake. Dossa, mzee Rashid wako nyumbani kwa Mwalimu na kunywa naye chai; na hii ni mwaka 1965! Siyo maneno yangu haya ni ya kwako. Unaendelea tena:
Wanafunzi wako hapa kina Ritz nikiwauliza hapa mara moja Nyerere na Mshume Kiyate walifahamiana lini na wapi kwa haraka watasema "ofisini kwa Abdulwahid Sykes pale Kariakoo". Lakini ukweli ni kuwa hujui walifahamiana vipi na lini. Umeandika hisia zako kwa kusema "lakini huenda" ikawa mahali pale. Lakini hiyo ni hisia yako tu haina msingi wowote katika ukweli. Haya tuendelee
Unataka watu wenye akili timamu waamini kuwa Nyerere kaondoka nyumbani kwake kwenda Kariakoo kununua kitu sokoni bila kitu mfukoni. Siijui vizuri Dar-es-Salaam hasa eneo la "Majumba Sita" nitaulize nieleweshe tu uhusiano wake na ile "Majumba Sita" ya kule Kipawa. Hii Majumba Sita ya Magomeni ni ipi ili angalau niweze kufikiria umbali maana ile ya Kipawa ni mbali sana kuliko ya Magomeni. Sasa Nyerere anaondoka nyumbani kwake kwenda sokoni bila kitu mfukoni. Na haya ni maneno yake - uliyosimuliwa. Hadithi hadithi.. tuendelee
Tukubaliane na weewe tu kuwa kati ya watu wote katika siku hiyo isiyo na jina Nyerere anautana na Mshume Kiyate. Sawa nasibu inaweza kutokea haya tuendelee.
Na wapo watu wanaamini hili simulizi; Mshume katoa karibu nusu ya gharama ya kujenga nyumba kampa Nyerere kwenda sokoni! koh koho koh... utamu njoo...
Pamoja na utamu wote wa simulizi hili na kwa kweli linagusa moyo tatizo ni kuwa Mama Maria Nyerere yupo hai. Yeye peke yake anaweza kuelezea kwa kirefu hili na kukupa ushahidi zaidi wa msaada wa Mshume. Hujawahi kumtafuta, hujawahi kumuuliza na hata kutaka kujua kumbukumbu alizonazo kuhusiana na hali ngumu ya maisha. Tunatakiwa tukubali tu...
Nyerere alikuwa na chuki na Waislamu; hadi hapa inaonekana kuwa hadi kupata uhuru hawakuwa na tatizo lolote. Na kwa vile unasema Ahmed Rashad Ali alisimuliwa kisa hiki na Baba wa Taifa mwaka 1965 akipata "vinywaji" na kina Dossa ni wazi kuwa hadi mwaka 1965 bado kulikuwepo na Waislamu wengi tu - miongoni in mzee wako Ahmed Rashad... walikuwa na nafasi nzito tu serikalini. Kukumbusha tu umetuambia kuwa Bw. Ali alikuwa Katibu Mkuu Msaidizi Idara ya Habari!
Lakini unaendelea na kusema:
Sasa hapa unaingiza ile kanuni yako; unawanukuu wale marehemu ambao huwezi kuwahoji. Marehemu Ditopile alikipata wapi kisa hiki. Tukumbuke kuwa kulikuwa na watu watatu tu ambao walikuwa wanafahamu kisa hiki. Mzee wako Rashad, Dossa Aziz na Lucy Lameck. Hivyo, Ditopile atakuwa amesimuliwa. Na nani?
Lakini pia unasahau kitu kimoja muhimu kwenye communication jinsi habari inavyobadilishwa kwa kadiri kinavyopitishwa kwa watu. Lucy Lameck alikuwa ni mtu pekee wa kukuhakikishia kisa hiki ili ulinganishe na ulichosikia toka kwa mzee wako. Lakini kwa miaka yote uliyoandika kitabu chako hukujaribu kwenda kuuliza toka kwa Lucy Lameck yeye anakumbuka vipi kisa hiki. Hukufanya hivyo Bana Said... yawezekana kwa sababu alikuwa Mkristu? au kwa vile ni mwanamke ushahidi wake hauaminiki sana? Tuendelee...
Magazeti yalisema nini na ni magazeti gani? Historia inadai uyataje matoleo na kile walichokisema angalau tujue jinsi gani waligeuza hicho kisa.
Lakini katika kuonesha jinsi ambavyo unaandika bila kufikiria sana unachosema unadai hivi (na bahati mbaya kina Ritz wataamini maskini)
Sasa hili linadai ukweli. Kweli kuna watu wanakusoma hapa na wanaamini kuwa Nyerere hakupiga picha yoyote kati ya 1955 na 1961 ambapo mzee Mshume hakuwemo ndani? Picha hii ni ya Nyerere na Machifu na ilichukuliwa 1961...
sasa simulizi lako ndivyo lilivyo. Lakini lote limeanza kwa simulizi la mtu mmoja tu ambaye peke yake umemuamini na sisi wengine wote tunatakiwa tuamini. Sina shaka hata kidogo Mshume Kiyate alikuwa na mchango wake lakini alikuwa na mchango kuliko Nyerere? Alifanya zaidi ya Nyerere? Ushahidi wako mwenyewe unaonesha Nyerere hakumsahau na hakutaka watu wasahau...
Inaitwa Spirit of TANU...
Leo unasema Nyerere alitaka watu wasahuliwe; yeye ambaye amekumbusha majina yao. Kwa ufupi, usingejua alichofanya Mshume kwa Nyerere kama Nyerere mwenyewe asingesimulia! Ungejuaje? Hata mzee wako Rashad asingeweza kujua. Kumbe ni Nyerere kamrudisha mzee Mshume kwenye historia. Siyo mzee Rashad, Siyo Kitwana Kondo, siyo Dossa Aziz. Wewe mwenyewe unaposimulia kisa hiki inabidi utoe shukrani kwa Nyerere kwa kuwa mwaminifu na muungwana wa kukiri.
Angekuwa na Makuu Nyerere asingesimulia hili. Asingeheshimu mchango wa wazee hawa asingetaja miaka minne baadaye.
Mzee Said nikikuuliza ukiondoa hilo simulizi la Nyerere kumhusu rafiki yake ambalo leo linadumu na kunogesha mazungumzo yako ni kitu gani kingene ambacho mzee Mshume alikifanya na kupata umaarufu katika TANU. Mchango wake mwingine wa "hali na mali" ni upi? Sasa siulizi hili kwa sababu nadharau bali nataka kuonesha tu kuwa umaarufu wa Mshume umetokana na Nyerere na si vinginevyo. Kabla ya kukutana na Nyerere umesema alikuwa maarufu; kwenye mambo gani? kwenye siasa? au kwa kuwa mchuuza samaki?