Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Ukiijuwa sababu ya kiongozi wa nchi katika Afrika yenye serikali isiyo na dini kupewa uwenye heri na kutaka kupewa utakatifu utakuwa umeshapata jawabu.
 
Acha uongo wewe, unajua kuwa mwaka 1985 Mzee Malecela alikuwa umbali gani na ikulu takatifu ya Tanzania?

Bora ungekaa kimya huna unachokijua ungekuwa mtoto wa Kambarage wala usingepinga, mmeomba jina mmpewa nenda kamuulize yupo hai wengine mkitajiwa mnasema marehemu huyu yupo hai.
 
HOTUBA kaandika Nyerere,hao kazi yao ilikuwa ku "rubberstamp"

Hii nyumba ya TANU,mbona inatatanisha ni ya akina sykes AU Cameroun ndio aliyeikabidhi,naona kuna utata ktk original owner
 

Ritz,

Hiyo safari yote ilitayarishwa na Idd Faizi Mofongo.
Idd Faiz ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kutafuta fedha za safari ya UNO.

Yeye ndiye alikuwa mweka hazina wa TANU na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Rashid Ali Meli kenda fungua safe ya Dar es Salaam Municipal Council akachota fedha
kumpa Idd Faiz atunishe mfuko wa safari ya Nyerere UNO.

Fikra ya safari hii ilikuwapo haya kabla Nyerere hajakutana na Abdu Sykes.

Historia hii leo inaitwa ''ngano.''

Nashutumiwa kwa ''uchochezi'' na ''uongo.''

Kwa wale wasiomfahamu Idd Faiz ni huyo aliyevaa koti, tarbush na kanzu.
Mmanyema na ndugu yake Idd Tosiri na Sheikh Mohamed Ramia.

Nyumba yake dhalili hadi leo ipo Magomeni Kondoa ambako anaishi binti yake
maarufu kwa jila na Biti Idd.

Juu ya kuwa alikabidhiwa hazina ya TANU kafa masikini.
Hakudokoa hata senti moja kuinufaisha nafsi yake.
 

Hiyo ndiyo ukisikia dhihaka ya kivukoni.
 
P,

Nakujibu kwa heshima zote mdogo wangu.
Umenikumbusha nilikotoka mimi miaka mingi nyuma.

Endelea kusoma kuwa na akili ya udadisi mengi utajua.

Ukiniita mdogo wako utakuwa umenipa cheo kikubwa sana.
Miye mtoto wako.
Huku "site"tunakoishi matatizo yanawapiga wote Waislam kwa Wakristo.
Kama ni kupata elimu yeyote mwenye jitihada ataipata na ukiona ameikosa ama mzembe au familia yake haimudu gharama.

Na naweza kukuapia kuwa wapo wengi nimewaona Waislam kwa Wakristo wakipata elimu na wapo niliowaona wakiikosa na ukiona aliyebaguliwa basi ni kwa sababu ya "hali" na si shari tena kwa uchache.

Mimi leo ukiniambia Ukristo wangu umenisaidia kupata elimu utakuwa umenitukana tusi kubwa sana. Kwa namna nilivyohangaika mimi na niliowaona, Baba na Mama wanajinyima ili niende shule. Wanaondoka Duniani napigana kiume na kozi kadhaa na kufaulu. Halafu leo tunaambiwa kuna mfumo Kristo.....Kichekesho kichungu.

Halikadhalika nimewaona walioingia kwenye biashara wakifaniikiwa na wengine wakifeli Wakristo kwa Waislam.

Hayo tuyaache: Wewe kama mtu unaesikilizwa na Waislam wengi unafanya jitihada gani kuhakikisha Waislam kule Kilwa, Kisiju, Korogwe, Kimanzichana n.k wanathamini shule? (Nimeona kwa macho yangu wengi wao wakiacha shule au wazazi wao wakiwaondoa shule au hata kutofuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni).

Usiseme waulizwe Waislam kwa sababu una sehemu ya mchango mkubwa tu kwa Waislam kujiona dhalili kama baadhi yao wanavyojiona leo.

Inshallah nitayasoma mapendekezo yako kesho, kwa sasa naenda ukumbini kumuoza mpwa wangu!
 

Nakuuliza katika safari hii na mafao mengine je Shirika la Maryknoll Sister wanatajwa?

Je Edgar Arestde Maranta anatajwa?

Je Shehe Iss Bin Amir anatajwa?

Je mfadhiri namba moja wa baba wa taifa na aliyekuwa akimlpa mshahara kabisa wa shilingi 600 huku akiwa kaacha kazi akiwa Musoma Padre Art Wille anatajwa popote?

Nakufahamisha kuwa katika moja ya vibwagizo vya Mwalimu mwaka 1985 alitamka wazi kuwa Padre Wille ni BOSS wake halali! Hilo alilisema akikumbuka mbali sana hasa mazngira yake yakukatiwa tiketi ya kwenda na kurudi UNO

Kasisi Wille alikuwa ni mmoja ya wanajopo la wa Maryknoll Sister wakiwa sambamba kabisa na Pandre Maranta wakiunga mkono juhudi za ukombozi zilizokuwa zikiongozwa na Mwalimu Nyerere!
 

Jee, umepata kusikia kisa cha NECTA?
 
HOTUBA kaandika Nyerere,hao kazi yao ilikuwa ku "rubberstamp"

Hii nyumba ya TANU,mbona inatatanisha ni ya akina sykes AU Cameroun ndio aliyeikabidhi,naona kuna utata ktk original owner

Son,

Mimi nimeeleza yote ninayojua kuhusu nyumba hiyo.
Sina zaidi cha kuongeza.

Ikiwa nyie wenzetu mna habari zaidi Insha Allah ileteni
hapa jamvini tuisikie.

Lakini njuiavyo mimi ilijengwa kati 1929 - 1933 na Abdu
anasema yeye kashuhudia kwa jicho lake nyumba hiyo
ikijengwa kwa kujitolea siku za Jumapili yeye akifatana
na baba yake pale New Street na Kariakoo.
 

1) Jee, hao unaowataja wako kwenye hiyo picha?

2) Father Kit Cunningham mbona umemsahau?
 
Alikuja nayo Nyerere kutoka Butiama.

wewe zomba hujawahi kuwa "clown" inaonekana wewe wa kwanza ukooni kulikabili darasa la maana lakini huachi asilia you write garbage 24/7 Hiyo Bells haikusaidia kitu-wewe kaa kibarazani uendelee kukusanya kodi
 
Last edited by a moderator:

Hapa ndio panapomfunga jela Mohamed Said
 
Last edited by a moderator:
wewe zomba hujawahi kuwa "clown" inaonekana wewe wa kwanza ukooni kulikabili darasa la maana lakini huachi asilia you write garbage 24/7 Hiyo Bells haikusaidia kitu-wewe kaa kibarazani uendelee kukusanya kodi

Nyumba ya tatu kutoka Nyumba hiyo ilipozaliwa TANU ndio nilipozaliwa na kukulia mimi.
 
Nyumba ya tatu kutoka Nyumba hiyo ilipozaliwa TANU ndio nilipozaliwa na kukulia mimi.

na hakika ulikuwa less then average student,mpaka mfumo wa Nyerere wa kutaka mcatch up kielimu ukakusaidia-leo umesahau-unatukana
 
"Nyerere's second visit to the United States was sponsored by Maryknoll. Instrumental in arranging it were Fr. William Collins, Fr. Al Nevins and Fr. John Considine. Maryknoll paid for his passage from Europe to America and back. His air line ticket from Tanganyika to Europe and back was bought by money raised in Tanganyika from a number of sources including Fr. Richard Walsh W.F. The purpose of this trip was to enable Nyerere to appear before the Fourth Committee of the U.N. on December 20, 1956. Maryknoll also arranged a lecture tour for Nyerere to visit various universities to acquaint himself with the American educational system and to seek scholarships for Tanganyikans. He also made an appearance on television with Eleanor Roosevelt on the Mike Wallace show"
 

Yericko,

Taarifa nzuri na zinajazia historia ya uhuru wa Tanganyika.

Kuna fedha katika vyanzo hivyo alipokea Idd Faiz kama mweka
hazina wa TANU?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…