Ritz,
Wazee wetu hawakunyanyaswa na Nyerere kama walivyofanyiwa wazee wake Mohamed. Yeye kaandika kitabu kusimulia manyanyaso ya wazee wake. Labda Nyerere angewanyanyasa wazee wetu na sisi tungeandika. Lakini kumbuka usemi "avumaye baharini na wengine wamo." Mohamed anataka kutuaminisha kuwa wazee wake walikuwa "vital" katika harakati za uhuru akisahau kuwa na wengine wamo.
Jasusi,
Katika wazee wako hapo Musoma mnae mtu kama Kleist
na mwanae Abdulwahid.
Watu wanaoweza kukupa historia yao ya harakati kuanzia
Wajerumani walipotia mguu Tanganyika hadi walipoingia
Waingereza?
Hapo Musoma mna Askofu aliyekuwa ndani ya TAA kisha
TANU kama Mufti Sheikh Hassan bin Amir.
Hapo Musoma mnao mfano wa Sheikh Mohamed Yusuf
Badi na mwanafunzi wake Yusuf Chembera wa Lindi
waloasisi TANU na kupambana na fitna za Kanisa Katoliki
lilokuwa linawatisha Wakristo wasijiunge na harakati za
kudai uhuru?
Sitaki nionekane nasimanga lakini ngoja nikuambie neno
langu la mwisho...
Hatungeweza sisi kuona historia hii ya wazee wetu inatupwa
nasi tukakaa kimya.
Hivi unajua kuwa siku ya Nyerere Day ndiyo Waislam nasi
huwaadhimisha mashujaa wetu?
Najua fika.
Hukuwa unajua.
Huu ndiyo ukweli.
Hivi ndivyo mambo yalivyo.