Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

JokaKuu,

Huyu ni wewe au mtu kaiba password yako?

Wewe unajifunza Kizungu?

..kipindi hicho nilikuwa bwana mdogo sana.

..halafu vitabu vya watoto vya kujifunza kizungu kulikuwa hakuna, kwahiyo tukawa tunabanana kwenye africa events, africa now, etc
 
Nguruvi,
Mie sijasema maneno hayo.

Huenda kwa kusoma haraka
umechanganya mambo.
 
Tutasonga mbele na ukweli utabaki huru, historia huwa haipindishwi kwwhila na ghiriba ndugu yangu Mohamed Said, historia ipo inajiandika yenyewe bila mawaa
 
Na wala si lazima niandike ulichoandika. Nina hakika nikikuonyesha nilichoandika hutaweza kuuliza au kuhoji maana ni mambo yanayohusu maisha yako leo hii siyo simulizi.

Hivi unaweza kuhoji chochote kuhusu Limbic System na impact ya psychological trauma inayoyosababishwa na malezi mabaya! Kwanza tu nikisoma maandishi yako kwangi ni sehemu ya study. Unajua Grandiosity na inferiority complex zinavyofanya compliment each other.Unaweza kuchangia lolote kuhusu manic syndrome au schizophrenia.

Siyo lazima mtu aandike kisicho cha kweli ilimradi tu kaandika. Kuandika kwenye heshima ni kule kunakoleta fikra na mtazamo mpya. Kwanini niandike kuwa commonwealth ni mjumuiko wa mataifa yenye mfumokristo nikifahamu huo ni uongo mzuri tu?

Kwanini niudanganye umma kuwa Nigeria ndiyo nchi yenye waislam wengi duniani.
Kwanini niandike kitu nisichoweza kukitetea na pengine kunidhalilisha kama takwimu ulizotoa?

Umeanza ngano yako kuwaondoa wapiganaji kwa kutumia dini, ukabaki na waislam.
Nao umeanza kuwagawa kwa kutumia makabila Wazulu na wamanyema na sasa umezama kabisa katika Umanyema kama ambavyo nina nukuu za kutosha kuthibitisha hayo.

Kuwa maarufu hakuhitaji kuandika. Osale Otango, Osama, Budia, Ngweso au makundi kama Sandinista,Red brigade, Alqaeda au Hakhan si maaurfu eti kwasababu wameandika ni maarufu kwa sababu zao kama ulivyo maarufu kwa kufarakanisha Watanzania.Wewe ni maarufu kwa wasio na uwezo wa kuchambua maandishi yako.

Kwa watu wenye akil,i Mohamed Said, ni mchochezi, mzushi na muongo.
Umeandika ngano kwa kutumia majina bila kuwa na tafiti.
Kama moja ya tafiti ni hiyo ya takwimu nitaomba dunia ifute somo hilo.

Mohamed umaarufu wako uko wapi wakati unakimbia hoja lukuki.
Kututajia majina ya akina Tatu Said, Mwanameka n.k. haitusaidi kitu kwasababu majina tu hayatoshi kufanya unachosema kuwa kweli.

Kuwasingizia marehemu kwa maandishi ni kinyume cha maadili ya kiroho na Uislam.

Simama na tetea hoja zako. Umekimbia maswali na hoja za wanajamvi kama akina Mag3, Mwanakijiji, Platozoom n.k.
sasa umaarufu wako ni kuhusu nini. Lakini hapa hatupo kuonyesha umaarufu,tunatumia akili zetu kukueleza kuwa si kweli kuwa Sykes alianzisha AA na si kweli kuwa Sykes alimfundisha siasa Nyerere.

Tutakuwa hatuzitendi haki akili zetu tutakapokubali kuwa sheikh Chaurembo aliandika hotuba na Nyerere mwenye Master msomi na Mwalim aibebe kama ilivyo hadi UNO kuisoma. Real!

Kushindwa kwako kuthibitisha tuhuma kama za hotuba ya Nyerere kuhusu Sykes alipoaga ni ushahidi mzuri sana kuwa umejifungia chumbani, ukatumia majina ya watu na matukio kuandika tamthilia hii tamu.

Nakishukuru chuo kikuu cha DSM kutofikiria hadithi hii kama sehemu ya mtaala wa wanafunzi maana mwanafunzi anapaswa kupewa elimu na wala si chuki, udini na ukabila.

Ni tusi kumfundisha mwanafunzi kuwa bila Wazulu na Wamanyema uhuru wa Tanganyika ungekuwa mashakani.
Ni dhalili kumlisha mwanafunzi takwimu za kiwango chako tutegemee mwanafunzi huyo alisaidie taifa katika utafiti.

Kwa ufupi jitihada zako za kuandika ngano ili zijenge mazingira ya kufarakanisha watu sasa zi wazi.
Pengine tofauti baina yako na Ilunga ni namna ya kufikia hadhira.

Tupo hapa kuwaonyesha wanajamvi mbinu zako za kujenga mazingira ya kusema watu fulani wanaonewa huku ukijua ukweli kuwa uonevu ni zao la kujionea.Unashinda kuwapigia watu hadithi badala ya kuwaambia wapeleke watoto shule, wawasaidie homework, kuwajengea kujiamini na kwamba sky is the llimit. Wewe unawafanya wajiskie dhalili, watu wa kiwango duni na kwamba wakibadili majina yao basi maisha yatanyooka wakiwa vitandani.

Kibaya zaidi ni jinsi unavyowafanya vijana hasa wa kiislam kuamini kuwa mafanikio yao yanaambatana na majina na wala si jithad. Kwamba jihad iwe kutafuta nani kafanya nini na wala si wao wanafanya nini katika maisha yao.

Unafanya hivyo ukijua wao hawatahoji kuwa wewe ni zao la mfumo kristo na kwamba ni ALUMNI wa st Joseph Catholic school. Unawadanganya waandamane kwenda kumuwekea dhamana Ponda na wala si kwenda maktaba.

Mohamed, sifa ya uislam ni ukweli na haki. Maandiko yako yanaacha maswali mengi kuliko majibu na ni vema ukasema historia uandikayo ni ya wazee wako wa Narung'ombe wala si Tanganyika. Ukitaja Tanganyika umetualika na hapo hakuna favor or fear, just facts on the table.
 
Nguruvi,
Wapi nimemtaja Chaurembo na hotuba?

Hotuba ya muago si sote tunaisuburi?
Iweje mzigo unitwishe mimi?

Mengine hayanishughulishi nakuachia
mwenyewe.
 
Mzee Mohamed Said umekwama kwa hoja mpaka ukaamua kujikomba kwa Jasusi kiasi hiki! aibu! haya tunasubiri kuona kama kweli mkuu Jasusi atakubali kufugika kama walivyofugwa vijakazi wako wanaojaza kurasa humu kwa maneno ya kinafiki kila siku!
 
Mkuu Nguruvi3, usitegemee kupata majibu ya maana kutoka kwa huyu mzushi, sana sana atawatuma watwana wake waje hapa na sifa kemu kemu za kumsifia yeye ati ni bingwa wa historia! Sasa ameamua kumurubuni mkuu Jasusi kwa vimaneno vya kitoto akidhani Jasusi atapunguza maswali magumu kwake! Ukweli uko wazi na yeye anajua kuwa hakuna jipya aliloliweka hapa zaidi ya uzushi na uzandiki!
 
Nguruvi,
Wapi nimemtaja Chaurembo na hotuba?

Hotuba ya muago si sote tunaisuburi?
Iweje mzigo unitwishe mimi?

Mengine hayanishughulishi nakuachia
mwenyewe.

Mohamed Said,

Ganda la mua la jana chungu kaona kivuno.
 
Jasusi,

Niko kwenye tab.

Nikirudi Insha Allah kwenye mpakato nitakupa kisa cha ile Mercedes.

Chini wanakwenda watu.

Jasusi,

Bwana Abdu alikuwa na dada yake wa kupanga Bi Sakina Arab.

Nikisema wa kupanga ni kuwa hakuwa dada wa damu lakini wazee
wetu walikuwa na mama, wajomba na watoto wa kupanga.

Hii ni hulka imeenea sana kwa Wamanyema na nadhani waliwaambukiza
na Wazulu.

Inawezekana kwa kuwa walikuwa watu ''wa kuja'' hawana ndugu hii ikawa
njia moja ya kuunga udugu na wenyeji.

Bi Sakina kwa umaarufu akijulikana kama Mwalimu Sakina kwa kuwa
alikuwa mwalimu akifundisha Al Jamiatul Islamiyya School pale
New Street.

Hii shule ipo hadi leo lakini sijui inaitwa Lumumba.

Mwalimu Sakina alikuwa na kaka yake akiitwa Mustafa rafiki ya baba
yangu na walisoma wote Al Jamiatul Islamiyya.

Hawa walikuwa Wanubi.

Huyu Mwalimu Sakina aliolewa na Shariff Attas ambae alikuwa chini
ya Market Master pale Kariakoo kwa ufupi alikuwa kaifanya kazi chini
ya Abdu Sykes.

Shariff Attas ni katika watu wa mwanzo kujuana na Nyerere pale sokoni
Kariakoo.

Ndiyo katika moja ya hoja hapa nikasema Nyerere akifika pale sokoni wala hana
haja ya kushika kikapu yeye mwenyewe kwani wana TANU wanakipokea nje ya soko pale
Mkunguni na yeye anakwenda ofisini kwa Abdu Sykes kikapu kinamfuata ndani ya ofisi
kishatakata.

Jamaa wakanijia juu kwa matusi.

Turudi kwenye Mercedes ya Bwana Abdu.

Sasa baada ya Abdu kufariki na kuanua tanga watu wakamuona Mwalimu Sakina katoka na
funguo za Mrecedes anawasha gari anaondoka.

Kuulizwa akajibu akasema yeye anachukua gari ya kaka yake akaombolezenayo kifo cha kaka
yake.

Hiki ndicho kisa cha ile Mercedes.
Mwalimu Sakina alikuwa anaogopewa kwa kukimwaga kimombo!

Ogopa sana.
Usimuone kavaa baibui lake ukamchokoza kwa Kiingereza utakaa kitako.

Shariff Attas ana kisa chake na Nyerere...
Unataka kukisikia?
 
The Prime Minister is the head of government in England. But the Queen is the head of the British Kingdom. The QUEEN is the head of the Church of England.

Jasusi unazidi kujikoroga narudia tena hakuna kitu kama hicho usitake kusema uongo. Kudhibitisha uongo wako na usivyo na haya nakudondoshea misumari hii.

Elizabeth II (Elizabeth Alexandra Mary; born 21 April 1926[SUP][note 1][/SUP]) is the constitutional monarch of 16 sovereign states, known as the Commonwealth realms, and their territories and dependencies, and head of the 54-member Commonwealth of Nations. She is Supreme Governor of the Church of England and, in some of her realms, carries the title of Defender of the Faith as part of her full title.


Sasa tutizame huyo Supreme Governor of the Church of England ni nani?

The Supreme Governor of the Church of England is a title held by the British monarch that signifies titular leadership over the Church of England.[SUP][1][/SUP] Although the monarch's authority over the Church of England is largely ceremonial, the position is still very relevant to the church and is mostly observed in a symbolic capacity. The Supreme Governor formally appoints high-ranking members of the church on the advice of the Prime Minister of the United Kingdom, who is in turn advised by church leaders.[SUP][1][/SUP]


Labda Jasusi tukuulize kwanini hii position ni Ceremonial? Jibu lake utalipata hapa:

To placate critics the Oath of Supremacy, which nobles were required to swear, gave the monarch's title as Supreme Governor rather than Supreme Head of the church. This wording avoided the charge that the monarchy was claiming divinity or usurping Jesus Christ, whom the Bible identifies as head of the church.[SUP][5][/SUP]

Hivyo narudi Archbishop of Cantebury is the head of the Church of England. The Queen of England is a constitutional monarch for 16 sovereign states. Pengine hujui what is a constitutional monarch. Wajuzi wanaitafsiri kama hivi:

Constitutional monarchy (or limited monarchy)[SUP][citation needed][/SUP] is a form of government in which a monarch acts as head of state within the guidelines of a constitution, whether it be a written, uncodified, or blended constitution. This form of government differs from absolute monarchy in which an absolute monarch serves as the source of power in the state and is not legally bound by any constitution and has the powers to regulate his or her respective government.
 

Son...
Huna cha kuzungumza kwa ile ''excerpt'' niliyokuwekea ya Sheikh Kassim?
 
Nguruvi,
Hotuba ya muago si sote tunaisuburi?
Iweje mzigo unitwishe mimi?

Mengine hayanishughulishi nakuachia
mwenyewe.
Hotuba kaiweka hapa Jokakuu umedai video! wewe ndiye umeleta hoja (mashtaka) kuwa Nyerere alisema hamtambui Sykes wakati anaaga wazee wa Dar es Salaam. Je, hukusema maneno hayo?
 
Hotuba kaiweka hapa Jokakuu umedai video! wewe ndiye umeleta hoja (mashtaka) kuwa Nyerere alisema hamtambui Sykes wakati anaaga wazee wa Dar es Salaam. Je, hukusema maneno hayo?

Nguruvi,

Hakika nimesema.
Bwana Yericko Nyerere akaweka maneno ya hotuba.

Nikasema ilwekwe clip.
Akasema Yericko itawekwa...

Bado tunasubiri.
 
Mohamed Said,

Ebu tupe habari za vyama vya wafanyakazi vilivyojiunga na TANU.
 
Nguruvi,

Hakika nimesema.
Bwana Yericko Nyerere akaweka maneno ya hotuba.

Nikasema ilwekwe clip.
Akasema Yericko itawekwa...

Bado tunasubiri.

Ikiwekwa clip ya sauti, itaombwa ya Video. Labda Mzee Mohammed Said niulize wakati unaandika kwenye
Kitabu chako kwamba Nyerere alisema hakumtambua Sykes uliyapata kwa: Kusikiliza Redio, Kutizama TV,
ulisoma kwenye gazeti, Wazee wako walikwambia au si kati ya hayo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…