Mimi nimeongea na akina Suleiman Kitwara kule Kamunyonge,Musoma.
Vijana wake walikuwa marafiki.Mzee huyu alikuwa mtaratibu na mcha mungu sana.
Hebu angali picha za mwanzo au muulize Mohamed huyu ni nani.
Sisi tukiongea nao hatupigi pua tunapata maarifa na kukupasia wewe. Post iliyopita nilikupa kitu kuwa nitapitia kwa Mzee Erasto Mangenya(chifu)una mjua huyo. Halfu December nitapita kule kwa akina Akili Daniel.
Umeshawahi kumsikia Mzee Hemed Mkali, hao tukiongea nao. Familia ya Magogo Mputa kwangu ni nyumbani.
Sisi wengine hatuna sababu za kujifaragua na kupiga pua, haaata! hekima tu.
Ndio maana tukimpeleka kona mzee huwa hatoki ila kwa time out!
Kuonana na wazee wetu ni hidaya na namshukuru mwenyezi mungu. Hakika tuna mengi tukieleza mtashtuka
Nshapata ugali kwa ndezi aliyeungwa na ngogwe. Ritz mashallah unatoka mate.
Muheshimiwa Nguruvi3,
Nimefurahi saana kwa umahiri wako wa hao watu na mitaa/sehemu hizo! Nakukubali kwa u-
Al Watan wako!ahaha!! Nahisi sasa unaanza kuwa pamoja na
Sheikh Mohammed Said, na pia ni uzuri tumwache atupe darsa kwa utaratibu na huku sootetunamuuliza
maswali ya kina na kwa ustaarabu. Kidogodogo ndo mwendo lakini tutafika.
Hivi ni nani alikua
msomaji wa kwanza wa mashairi na tenzi kwenye
Radio Kichwele!? Tafadhalini naomba tujuzane wenzangu?
Huku kwenye nchi za wenzetu/"mataifa ya magharibi" wana utaratibu mzuri na wanathamini na kuwaenzi saana "wazee wao" na watu walotoa michango kwenye Historia/ ya nchi zao. Hakuna mchango ati mdogo saana au wa kipuuzi katika harakati za kupatikana uhuru wa nchi au mapambano ya nchi! Nashangaa sisi tumepoteza tamaduni hizi tulorithi toka kwa
mababu zetu!
Tafadhali jamaa na nyie kutoka mikoani,kipata fursa tusaidiane japo kiduchu kutaja baadhi ya majina
yalosahaulika. Nachelelea baadae tusijemlaumu
Sheikh Mohammed Said kuwa ati kapendelea mno
Wazee wake na vinyozi wa Kipata na Mkunguni!? Nashauri tukishamaliza mnakasha huu,nasisi soote kwa pamoja tukusanye makabrasha yetu humu na kuandika rasmi "
Marekebisho ya Historia ya Tanganyika kutoka JF".
Sheikh Mohammed,tafadhali kipata wasaa tena naomba udondoshe tena na kusherehesha kwa yale majina na mitaa ya enzi. Huwa nafarijika mno na najifunza mengi yalopita zama hizo kila ninapokusoma.
Naona ulianzia Gerezani na Kipata lakini naona sasa unateremkia
Mwembe Togwa na
Tuwe Tugawe. Nafikiri pale Swahili no.34 alikua akikaa
Shariff Abdalla Al Attas kwa miaka mingi ,halafu akahamia Lumumba Street na mara ya mwisho kabla ya kufariki nafikiri alikua akikaa pale kona ya Sikukuu na Twiga opposite na
Masjid Al Shadhily. Pale Msikitini ndio ilikua Al Qadiria kubwa ya kina Sheikh AbdulRahman Shamte,Sheikh Nurdin Hussein Al Shadhily na Sheikh Hashim Haji Abdallah. Kama wajua pia tupe nini asili ya
mtaa wa Mwazarau pale Magomeni Mapipa kuitwa jina lile? Na nini asili ya
Skuli/Shule ya Msingi Mzimuni magomeni kuitwa jina lile?
Nilicheka saana kile kisa cha yule jamaa wa kibondei
Martin Kayamba/Kwiyamba kumbe alikua ni mzandiki na mamluki wa wakoloni tu!?
Kama kuna
Mwanajamvi mwingine yeyote nae tafadhali pia atujuze habari za hawa wafuatao/sehemu hizo,na habari zao japo kiduchu za michango yao yoyote walojitolea kwenye harakati za kumng'oa mkoloni na hatimae kufanikisha uhuru:
Bint Sungura wa kona ya Congo na Rufiji,Mwinchande Kidato,Mtumwa Mkenge. Wale wa Korogwe vipi Mzee Mtanmbo wa Gonera nae? Na mtokao Chongoleani na Mikindani mpo? Buyuni Kuu,Ununio,Mkwaja na Saadani mpo!? Sheikh Mwinyikombo Bin Hassan wa Kisiju. Malenga Sheikh Mathias Mnyampala wa Dodoma. Rajab MwinyiKhamis Kiguu cha mbuzi. Chief Bategwa Rusimbi na Sheikh Khalfan Kiumbe wa Kigoma. Vipi wana wa Tongoni na Gombero mpo!? Sheikh Shame wa Mbuyu kutoka Kwale.
Bwana Jasusi tafadhali nawe kipata wasaa tudokeze habari za
Chief Burito wa
Butiama/Mwisenge na Mzee Makongoro wa Musoma mjini. Mwanza kwa kina Sheikh Mohammed Magongo na Idd Mtingwa!? Ramadahani Lofa na Miraj "Mzuri" Al Jahazmy wa Mlingotini. Ramadhani Mwinyipingu wa Jiwe la adabu. MwinyiKhamis wa Dodo,Maalim Mohammed Mwita,Sheikh Khamis Bin Akida Said Al Shirazy,Bwana Al Ruweihy wa Tungi,MwinyiBakari Mwinyimboni Al Amir,MwinyiShomari Mohammed Kimbau wa Mafia,Bwana Keis Bin Ali,Bwana Maalim Bin Salim Al Awadh,Bwana Abdallah Bin Jumaa Luga,Bwana Shaaban Al Madheheby,Sheikh Abdallah Kau wa Kibada. Maalim Pera Ridhwan wa Gombe kutoka Mnyanjani. Bila ya kumsahau Maalim/Sheikh Jumaa Bin Umar wa Bagamoyo.
Hivi hapo Tanzania zipo Archives za Serikali kuangalia kwa kina vitu kama hivi,au ndio vyoote vinapatikana kwenye maktaba za wazungu huku Europe na Amerika!?
Sheikh Mohammed Said,hivi ni kweli kuna kisa cha "
Sheikh mmoja" alofanza mijadala na majibizano makali mno kwenye
Dar Es Salaam City Legislative Council na kumshinda
Al noor Kassum ili kutetea na kuhakikisha city plan ya wakati huo inaidhinisha na kujenga
Mororgoro Road hapo ilipo leo
Uswahilini!? Niliwahi pia kusikia ati Sheikh huyo huyo ndiye alotetea na kumshawishi mfadhili kukubali hiyo
Anatouglo Hall iwepo/ijengwe pale Uswahilini ilipo leo!?
Nakumbuka kuna wakati
Sheikh Mohammed pia uliwahi kutaja "mandava" wa enzi zenu!aahaha!! Niruhusu na mimi nijaribu kutaja japo wachache kutoka mikoa mbalimbali ya
Tanganyika; Juma Kabati,Dongo la Maka,Sauti ya Chuma,Kunyamale,Hamis Subah, na Salum Machapati!ahahaha!!!
Nahisi ukiwatafuta nduguzo
Mpuya Rupia na
Abdallah Awadh sonara nao watakukumbusha wale
walosahaulika wengine wa Tungi,Kibada,Mjimwema,Jiwe la adabu,Mbwa Maji,Vijibweni na Tuangoma.
Tumalizie na kina
Mrisho Mkukuninga mpiga
zumari ya
Msanja na
Rashid Kishingo mpiga
Beni bati!aahaha!!
Nasikia pia kulikua na
Al Watan,
Al manzil na
Egyptian Club. Hivi ndio vilikua vyama vya starehe na mapumziko lakini sio
TA wala
TAA.
Ahsantani.
CC: Ritz,JokaKuu,Kadogoo,Mfumo,Boko Haram,Ami,The Big Show,Jasusi,Sheikh Mohammed Said.