Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Sie tuna kigoda cha mwalimu. Tunawaalika maprofesseri. mnakaribishwa
 
Amiin Rabilaalmiin..
 
Last edited by a moderator:
Jee, alimpuuza chaguo lake Mzee Mkapa baada ya kuuza mashirika yote ya umma likiwemo NBC? au alifurahia kazi nzuri aliyofanya Rais wake?
Mwl, mpaka anaingia kabulini, hakuacha kuililia Nbc bank.
Mkapa alimgeuka Nyerere na hakuacha kukemea.
 

Mkuu SoA naomba uiweke hapa mkuu tafadhali.
 
Mzee Ms,
Kabati la fedha hufunguliwa katika mahitaji ya tanu tu?
Je? na akitaka kuagiza mzigo mpya wa mafuta inakuwaje?
Au kisima kilikuwa kikitoa mafuta muda wote bila kujazwa tena?
 

MS,
Umeitaja BBC na makala yako nikamkumbuka Bwana mmoja akiitwa Athumani Matata au (somebody matata) huyu nadhani alifanya kazi na BBC au Radio Tanzania kwa lugha ya Kiingereza. Unazo habari za huyu bwana mahali alipo?
 

Barubaru:
Nakuhakikishia hawawezi kuandika kitabu hawa! wanahofia kije kuwa kichekesho!
 
WML Walifukuzwa nchini au ilikuwaje wakafunga ofisi?
Mohamed, watu wana kiu. Tafadhali tulizungumze hili.
 
Mkuu JokaKuu hili ndilo nalisema kila siku. Nashukuru labda lugha yako itaeleweka.
Watu wamefunga macho kuhusu matatizo halisi, wamejificha nyuma ya udini, so sad! Hapa Mzee na wazee wenzake wa WARSHA wanabeba dhima ya kuupumbaza umma kikamilifu.

Leo watu wakifikiri watatunga nini kuhusu udini, pesa za Radar walizoelezwa zitanunua vitabu zinatafunwa kwa utimilifu.
Watu wapo nyuma ya pazia bovu na chafu la udini. So sad!
 
Mohamed, hawa WML walipewa kibali na nani, walikuwa wanashughulikia nini, walikuwa wanajamii gani wanayoihudumia?
Je, walifukuzwa au waliondoka wenyewe?
 
Barubaru, mbona unapata taabu kuuelewa huu mnakasha unahusu nini, kinchogomba si Mohamed kuandika historia ya wazee wake, hapana, ni namna anavyowahadaa wananchi kwa madai ya kipuuzi yasiyo na ukweli wowote...hata hivyo naomba kwa niaba ya hao wengine usiowataja nikutake uzingatie mambo matatu muhimu;

  1. Hicho kitabu, tofauti na ngano za Mohamed Said, kitachambua michango ya Watanganyika wote bila kutanguliza makabila yao, dini zao, eneo wala rangi zao...hakutakuwepo na cha sisi na wao.
  2. Hicho kitabu kitaongelea michango ya Watanganyika zaidi ya milioni nane kutoka kila kona ya nchi na hakitajikita katika watu wa Dar es Salaam tu ambao walikuwa hawafiki laki moja na nusu.
  3. Hicho kitabu kikiandikwa kwa staili hii hii alotumia Mohamed Said, nakuhakikishia kitapata upinzani kama huu huu unaoushudia hapa hata kama mwandishi atadai na yeye kafanya utafiti wa miaka 50.
gombesugu, maadamu umeamua na wewe kuingia kwenye mkumbo huo huo wa kuwatazama waliokuwa Watanganyika katika misingi ya wao na sisi katika harakati za uhuru, naomba nikukumbushe jambo moja muhimu...huko unakoita mikoani ndiko walipoishi zaidi ya asilimia 98% ya wananchi milioni nane. Kwa idadi ya wakazi wa Dar es Salaam wakati huo, unaweza kuwataja hadi vichanga, hutaweza kufikia idadi ya wakazi wa kadistrict kamoja tu ka Mwanza. Heri mfungue thread mahsusi mtajiane majina yote yale tangia Arab Street, Kichwele, Ring Street, Main Avenue hadi mtaa wa Unter Den Akazien.

Kwetu wengine tutabaki tukitanguliza Utaifa (Utanganyika) kwanza na kuwatukuza wazee wetu bila kuangalia tofauti zao kama za wenye mji na watu wa kuja au watu wa pwani na watu wa bara.

Baada ya hayo machache naomba turudi tupate maelezo kutoka kwa mwalimu mtoa darsa Mohamed Said, je ilikuwaje katika unaoitwa MfumoKristo shirika la World Muslim League (WML) likaweza kuruhusiwa kufungua ofisi nchini hadi expatriate wake Mburundi akapewa Uraia na pasi ya Tanzania!
 
Wanajamvi, kwa vile naona kuna "interest" ya kuandika kitabu cha kusaidiana na vilivyopo, mchango ni huu hapa. Mzee MS utatusaidia kujua kama ni sahihi kiasi gani, lakini ni published articles. Nimenakili sehemu chache sababu ya kukosa muda;

1. source : Arthur Kirby; Tanganyika Triumph: African Affairs, Vol. 61, No. 243 (Apr., 1962), pp. 114-125

“………This accords with the sentiment recently expressed by Mr. Kahama, the Ministerf or Home Affairs, when he said that the people of Tanganyika would like to light a candle and put it on the top of Mount Kilimanjaro.” (MS, kauli hii alitoa nani? Kahama au Nyerere?)

“………Sir Donald Cameron, determined that there should be provision for the ' proper ventilation and discussion' of legislation measures before enactment. He established a Legislative Council with unofiicial representation open to all races. There were no African members until 1948, and even then only four because so few could debate in English.” (yaelekea matatizo ya kiingereza yameanza zamani, Is this correct?)


2. Lord Twining: The Last Nine Years in TanganyikaAuthor(s): African Affairs, Vol. 58, No. 230 (Jan., 1959), pp. 15-24

“…..TANU or the Tanganyikan African National Union was a result of outside influences, advices and pressure. I have never actually quarreled with it, except over some parts of its platform which are completely unacceptable.”

“……. the party policy was racial- it was pure racialism, and the platform was that we should declare that Tanganyika was primarily an African territory and that we should introduce universal suffrage.”

“……Peoples said to me, " Why do you not come to terms with Mr Nyerere ? " Well, I saw him on several occasions and talked to him. I always found him quite a reasonable man, and I even nominated him to Legislative Council. But he expected that when he blew his trumpet, the walls of Jericho would tumble down, and of course they did not so he resigned from the Legislative Council.”

At least matatizo ya Julius kutopendwa hayakuanza leo!!!!
 
Barubaru:
Nakuhakikishia hawawezi kuandika kitabu hawa! wanahofia kije kuwa kichekesho!
Usidharau usichokijua. Hivi kweli leo Mag3 na Nguruvi waunganishe nguvu zao waandikie kitabu patakalika kweli hapa jamvini?
 
Usidharau usichokijua. Hivi kweli leo Mag3 na Nguruvi waunganishe nguvu zao waandikie kitabu patakalika kweli hapa jamvini?

Jasusi,

Hata Shigongo kila siku anaandika vitabu waambie hao jamaa zako waandike kitapata soko sana Kanisani na kwenye vigango lakini siyo kwa Watanzania.

Hao waandishi wako kuna mmoja yeye anasema wazi kabisa kuwataja hao wazee wenu wa Kariakoo kwake ni matusi makubwa.

Bahati nzuri kitabu chenu kitakuwa kimejaa wasomi watupu hakuna mmoja hata mwenye akili za madrasa, mnywa gahawa, washinda vibarazani, kina mwanameka.

Jasusi, jikusanyeni wote muandike hapo kweli humu jamvini hapatakalika lakini kwa Watanzania ndiyo itakuwa mtihani na kituko kusoma hizo ngano.
 
Mzee Ms,
Kabati la fedha hufunguliwa katika mahitaji ya tanu tu?
Je? na akitaka kuagiza mzigo mpya wa mafuta inakuwaje?
Au kisima kilikuwa kikitoa mafuta muda wote bila kujazwa tena?

Mgashi,
Ili maswali yako kwangu yapangike vizuri nadhani tungelianza na rangi ya
kabati lenyewe, kisha tuje kwa seremala wake, kisha mpiga vanish nk. nk.

Unaonaje?
 
Mag3;6109922]Barubaru, mbona unapata taabu kuuelewa huu mnakasha unahusu nini, kinchogomba si Mohamed kuandika historia ya wazee wake, hapana, ni namna anavyowahadaa wananchi kwa madai ya kipuuzi yasiyo na ukweli wowote...
Mag3, kwahakika wengi sana wamesema na wamerudia kuwa Mohamed akaiamua kutaja majina ya wajukuu, vilembwe na vining'inia toka miaka waarabu wanaingia Mzizima, wala hakuna atakaye nyanyua mdomo.

Tatizo linakuja pale ambapo, kwanza atatumia majina hayo kama Tanganyika, pili atayatumia kupandia ngazi kwa kudhalilisha michango ya wengine na muhimu kupotosha kama si kuficha ukweli au kudanganya.

Sijui Baru baru angependa kila mmoja aandike kitabu kuhusu maana na makusudio ya commonwealth.
Hivi kweli inahitaji kitabu hiyo. Lazima aelewe kuwa kama ameandika kitu, basi maandishi hayo yapo kwa credit, discredit, criticized and a the subject to critical thinking and analysis.
Hizi habari za kila mtu kuandika kitabu ni dalili za kukwepa hoja muhimu sana.

Kila mmoja ameonyesha mchango wake ingawa kwa bahati mbaya sana Mohamed hapendi kueleza ukweli.
Hivi sasa kuna hoja ya WML na Sheikh Rukara ambayo ameikabidhi kwa wizara ya mambo ya ndani.

Hoja hii ni muhimu sana kwasababu inafafana na madai yake kuwa sheikh Amir alifukuzwa kwa fihi, husda na inda na hakuwa na kosa.

Kwa kiongozi makini kama Nyerere Rukara aliyekuwa mfanyakazi wa WML asingeruhusiwa kufanya harakati za kidini.
Na watu hawaelewi kuwa huyu bwana ameoa na anamiliki vitu visivyoruhusiswa kwa mtu mwenye work permit.

Na wala hakuwa na work permit, alijulikana kama Mtanzania akiwa na hati zote hadi pale alipoteuliwa kuwa seneta.
Alijihusisha sana na makundi ya kisiasa wakati wa machafuko na ndiyo maana amerudishwa kula keki ya taifa Burundi.

Hapa ndipo tunasema Sheikh Amir kama alivyo Maliki na Rukara hawakuishi nchini kwa kufuata misingi na taratibu za kisheri.Taratibu zilizowawezesha wao kuishi na kufanya uharamia ni zile zile anazolalamikia Mohamed chini ya mfumokristo.

Lakini pia kuhusu WML hapa kuna funzo linalokataa kabisa maandishi na dhana nzima ya Mohamed kuandika kuhusu wazee wake.

Kilichomkuta sheikh Amir ni sawa na kile cha Maliki na Rukara.
Tunafaham kuwa Rukar alipata kibali cha kuishi na kufanya atakayo katika mfumo kristo

Tumeona WML wakiingia na kufungasha virago kwa hiyari yao.
Sasa wapi unatoka ushahidi kuwa wakrito wanapewa upendeleo na taasisi zao kusajiliwa tofauti na waisla.

Mo kaandika kuwa wakristo wanaruhusiwa kuwa na uhusiano na world church council, world vision na Vatican.
Waislam wamekataliwa. Sasa WML au Africa Muslim agency ni ya watu wa aina gani?
Hili nalo linahitaji kitabu kweli!

Kila tunapojaribu kuweka rekodi clear tunaambiwa tunapinga.
Tunaambiwa tuandike vitabu.

Mag3, Gombesugu baada ya kujificha ficha katika kivuli cha dini hakika ametoka kiukweli.
Sidhani kama kuna atakayepinga majina ya wazee wake. Lakini basi wazee wake si Tanganyika
 
Hili la WML linaitaji majibu ya kina ili kuweka mambo sawa hapa,naomba lisipuuzwe
Ritz hauna hata majibu ya hili?!
 

Aaah, tusimulie basi juu ya WML.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…