Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
- Thread starter
-
- #13,001
Sina haja ya kuirudia. Nimeisoma nimeielewa na nikatoa hoja yangu baada ya kuisoma na kuilelewa. Kama unataka kuchangia kwenye hoja yangu basi unachotakiwa kufanya ni kuiwakilisha hoja yangu jamvini halafu uipinge hoja hiyo kwa hoja. Sasa unapotaka kupinga hoja ya mtu kisanii kwa kumwambia arudie tena kusoma haitakusaidia. Wewe chambua hoja yangu na elezea wapi nimekosea.
Mkuu hakuna hoja ya kuichambua wala kuifikirisha akili yangu.
Endelea kuitafsiri hivyo hii hotuba,
Mtu yeyote mwenye akili timamu akisoma hiyo hotuba ya Nyerere ataelewa kwamba huyu jamaa alikuwa mnafiki sana.
Haiingii akilini kumfahamu Abdul Sykes eti wakati amerudi kutoka Uingereza na baada ya kukaa pale Pugu kwa mda ndio aje Dar es Salaam kutaka kujua viongozi wa TAA ni kina nani. Alifahamishwa kuhusa TAA tangu yuko Makerere na akashauliwa kuacha kuanzisha chama kingine badala yake afungue tawi la TAA pale. Baada ya kurudi Makerere akachaguliwa kuwa Katibu wa TAA wa jimbo la Tabora. Aliwezaje kufungua tawi kule Makerere na baadaye kukubali kuwa Katibu wa TAA wa jimbo bila kumfahamu Abdul Skyes ambaye katika kipindi chote hicho alikuwa Katibu wa Chama?
Labda kama akili zake zilikuwa sio nzuri hivyo akakubali kuacha chama chake alichotaka kuanzisha na akajiunga na chama kingine bila kujua viongozi wa juu ni kina nani na nini malengo ya chama chao.
Zali la Mentali,
Wewe binadamu una fikra za hali ya juu sana hakuna mtu yeyote aliyegundua hicho kitu.
Wewe ni mtu muhimu sana kweye huu mnakasha karibu sana jamvini.
JF kuna vichwa bana siyo mchezo.
Hilo halipo huku bara tu. Ni tatizo katika jamii nyingi. Na ndio hasa sehemu ya huu mnakasha. Watu wanaacha kutafuta kiini cha tatizo, wanabaki kutafuta simple solutions. Mfumo wa kifisadi unamnyima kazi kijana wa kikristo/kiislam/asiye dini, badala ya watu kuangalia tatizo la ufisadi kwa ujumla wake, mwingine anaibuka anasema Yule kijana wa kiislam amenyimwa kwa sababu ya dini yake. Wakristo na waislam wa Lindi hawataki shule labda wanapendelea kuvua samaki zaidi, au wakristo na waislam na wapagan kwenye jamii za wafugaji wanakataa shule kwa kupenda zaidi ufugaji na uwindaji, halafu mtu anaibuka na kusema, waislam kwenye jamii hiyo wamebaguliwa na mfumo kristo Nafikiri hata huko Oman uliko, kuna watu wana mentality hiyo, ikitokea uprising because of social discontent, kuna watu hawatawia kuilaumu Marekani, badala ya kuangalia kiini cha matatizo ya wananchiNanren,
Moja ya tatizo nililolibaini huko Tanzania ni watu kujigeuza mbuni yaani kuficha kichwa chini yya majani wakti mwili wote upo nje akidhani kuwa haonekani.
Mohamed Said mara kadhaa amesema Nyerere hakuasisi TANU! Tukipinga hili mnasema tunamtetea Nyerere kwasababu ni mkristo mwenzetu, na tuna chuki na uislam. Na kila anayepingana nanyi, mnafikiri ni mkristo tuNanren,
Nimebainisha hapo Juu kuwa Kuna mazuri ya JKN na mabaya pia. Hakuna anayepinga kuwa JKN ni mmoja wa waasisi wa Tanu, Rais wa tanganyika na Tanzania pia.
Kama umemsoma Mohamed Said vizuri, na umetusoma na sisi vizuri bila jicho la udini, utaona kuwa hatupingi hadithi za nani alimpa Nyerere baiskeli, au nani alikuwa anampokea kikapu pale sokoni. Hata akidai kuwa Nyerere alikuwa anaenda sokoni bila pesa, kama ni ndio ukweli, sisi ni nani hata tupinge? Tunachopinga ni kufichwa baadhi ya facts ili kumdunisha mmoja na kumkweza mwingine. Tunapinga hisia zinazoingizwa kwenye masimulizi na kufanywa kama sehemu ya ukweli. Mathalan anaposema the speech was farce, the TRUTH was muslims were no better than they were before independence bila kueleza hiyo TRUTH ameipataje. Kuna bandiko analirudi rudia eti The church declared islam as its enemy wakati hiyo declaration is his own imagination. Anaposema watu walifungwa kwa uislam wao wakati actually walifungwa kwa kukaidi sheria za wakati huo (ikiwa ni pamoja na wasio waislam), huoni kuwa ni hisia tu ambazo zina lengo la kugawa wananchi? Mpaka amefikia hatua ya kutuma vijana na masheikh kuzunguka misikitini kuwaambia waislam wasichague Chadema ili wamchague muislam Kikwete? Hayo bwana Barubaru ndio tunayoyapingaSasa unapotolewa ushahidi kuthibitisha yeye ni mmoja wa waasisi na sio kinara katika uasisi tena kwa kupewa ushahidi madh'buti unakataa sijui unataka nini. Ikumbukwe kuwa Nyerere hakuwa na uenyeji Dar na hata tunapoambiwa nyumba alipofikia baada ya kuacha ualimu pugu alipewa kwa ufadhwili tu wa watu mnabisha.
nafikiri Nanren inabidi mfunguke hata kwa ushahidi wa mazingira tu. Nyerere hakuwa na pesa wala uenyeji wa Dar jiulizeni alikuwa anaishije ishije dar? hapo utaona kulikuwa na watu waliojitolea kumfadhwili. sasa anapotokea mtu kuachambua hao wafadhwili ambao wamesahaulika katika historia usipinge bali ingzeni katika historia yenu na sio kuficha kichwa mkidhani kuwa hamuonekani. Namshukuru Al Akhiy Mohamed Said kutujuza mengi ambayo tulikuwa hatuyajui pamoja na kuisoma historia ya nchi hiyo lakin hatufahamishwi na kufundishwa.
NimekusomaNafikiri nitakuwa nimekujibu lakin kama utahitaji ziada basi Bismillah
Nafyonza Ilm tu hapa.
Duuuuh ndugu wewe unaelekea kokote upepo unakovuma ilimradi hauathiri udini wako,
jisimamie ndugu yangu,
Nikusaidie kitu.Enzi za Nyerere professional hazikuwa zinazingatiwa bali mambo yote Chama kimeshika hatamu za uongozi. Kila pahala siasa inatawala.Lakin kumbuka nimekulia Tz na kuzunguka karibu nchi nzima wila zote za Tz Bara najua mengi. Kumbuka kuwa unaposema Mbeya mtu yoyote huko atakwambia wanatoka wanyakyusa lakin kumbuka kuna makabila mengi sana wakiwemo wapangwa, wasafwa na wengine.Unaposema Mara watu wote watakwambiia wanatoka wakurya, lakin kuna makabila mengi sana kule wakiwemo wang'oreme, waikizu, wazanani na wengine wengi tu.Kwa bahati najua sana utendaji na uwezo wa Nyirabu na hata warioba kwani kwa namna moja au nyingine niliwahi kufanya nao kazi hivyo ninachozungumza nalinganisha na uwezo wao kikazi na utendaji wao. wapo wengi lakin naona tuishie hapa kwani ni upendleo wa dhwahir.
BarubaruWC,
warabu wanasema hivi " Ujinga usio na khasara ni bora sana Kuliko Ilmu isiyo na Faida".
Unajuwa katika sehemu zilizofata na kutamalaki mila na desturi za Uislam ndizo sehemu zilizostaharabika sana hakuna mauaji ya vikongwe, watu kutembea na magovi, kukeketa, kuchuna ngozi na kunyofoa viungo vya albino na hata mateso kwa akina mama. Kwani Utamaduni wa kiislam unahimiza sana Utu na kuthamini hilo.
Barubaru
Egypt wanakeketa wanawake. Mara kadhaa, viongozi wa juu wa kiislam nchini humo wamekuwa wakisisitiza kuwa mwanamke wa kiislam ni lazima akeketwe. Hapa Tanzania (unapojisifia kuwa umetembea na kuzijua sehemu nyingi) warangi na Wamanyema ("Alhamdullilah I have never seen a christian Manyema"-by Moh Said) wote wana hiyo culture, na asilimia kubwa ya makabila hayo ni muslims. Kuhusu ustaarabu wa tamaduni za kiislam kuwa zinajali na kuthamini utu, na kuzuia mateso ya kina mama.... Ngoja tusiingie huko... Maana at times huwa nashindwa kujua ni wakati gani muislam huwa ni "muislam" na wakati gani anakuwa sio "muislam", kwa mfano ni wakati gani Sheikh Yahaya anahesabiwa kuwa ni muislam na wakati gani anakuwa sio...
Cha muhimu ujue kuwa mambo anayofanya anayejiita muislam katika maisha ya kawaida (mnayohusisha na ustaarabu) kama vile kutumia maji chooni, kutahiri, kusaidia wasiojiweza, huwa pia yanafanywa na watu ambao hawaujui huo uislam. Na ujambazi, ujangili, uzinzi, uasherati na kuuza madawa ya kulevya na kutumia pombe and other vices, vinafanywa na watu wa aina zote hata wale wanaohesabika kuwa ni waislam...
Asante kushukuru Wickama;
Kwa kweli nimesoma jinsi mambo ya Tanga yalivyo basi hadi nimesikia uchungu. Nimeishi Tanga maisha yangu ya utoto na ujana na kukulia miongoni mwa Waislamu. Nimesoma na Waislamu toka darasa la kwanza hadi sekondari. Sasa siyo kusoma tu hivi hivi lakini kuwa na urafiki wa karibu kiasi cha kwenda nao kwenye Maulidi ya Mtume, na utotoni hata kupiga nyimbo za daku - na unajua bana hakuna wanakofanya vizuri kama Tanga (sijui siku hizi). Ni Tanga ambako miye sikujua wapo Waislamu ambao walikuwa hawajaendelea; nimekua nikiwaona wanafanya biashara, wana maduka, wana mabasi (na hapa sizungumzii Waarabu tu - kina Mabrouk) la hasha nawazungumzia hawa weusi tii wenzetu. Tulipokuwa shule tukisoma pamoja niliwaona uwezo wao darasani; mtu mmoja darasani alikuwa best wangu na tulikuwa tukishandana sana aliitwa Saleh Khalfan (alikuwa ni mswalihina hadi mtu unaona wivu); baba yake Mzee Khalfan akiishi pale Majani Mapana karibu na duka la Chako ni Chako. Binti aliyekuwa anatutesa wote, mpole kwelikweli - Mwanahawa Salim alikuwa ni Binti wa Kiislamu; mwingine ambaye alikuwa anatuzingua darasa aliitwa Mpaji Juma akiishi pale kijijini cha Mwamboni (sijui kama bado kipo). Dada zangu wamesoma ile shule ya Jumuiya (pale karibu na stendi). Mwenyewe nikaenda kusoma Pangani. Kote huku - nisamehe kwa kutembelea kumbukumbu za zamani - niliishi nikiamini kabisa kuwa sisi sote tulikuwa tunashindana vizuri darasani na wenye kipaji walikuwa na kipaji - sikufikiria kabisa suala hili la dini. Na kweli niliwaona vijana wa Kiislamu wakipasua darasani vizuri tu na wengi wameenda mbali leo hii. Na niliwaona watoto wa Kikristu wakiharibu darasani na leo maisha yao yako duni vile vile.
Na hili ni kweli siyo hapo Tanga tu; nimebahatika nami kupita sehemu kubwa ya nchi yetu. Ni mikoa mitano tu ambayo sikujaliwa kufika kabisa; Mtwara, Lindi, Rukwa (Katavi), Kigoma na Pemba. Sehemu nyingine zote nimefika; nimefika Mwera, Boza, Muheza, Maramba, Dunga, Ileje, Ndala, Unguja, Kisarawe n.k ni sehemu nyingi. Nimekuja kuelewa kitu kimoja ambacho Mohammed Said na wengine wenye kuamini histohia hii hawajajaribu basi kuangalia - maendeleo Tanzania yameenda kimaeneo zaidi (geographical). Kwamba kuna maeneo ambayo yamefanikiwa sana kutokana na historia yake bila kujali makabila yaliyomo ndani yake. Leo hii huwezi kushangaa kuwakuta Wahaya Waislamu waliosoma sana; huwezi kushangaa kukuta Wachagga Waislamu ambao ni wasomi vile vile n.k
Lakini cha kushangaza sana; utaona kuwa wanaodai kuwa Waislamu wamedhulumiwa hawawezi kuelezea mafanikio ya Waarabu Waislamu, au Wahindi Waislamu, au hata Wahindu wa Tanzania. Mfumo Kristu ambao unapendelea Wakristu unaweza vipi kuachilia Waislamu wa makundi mengine wakafanikiwa? Wanatolea mfano hapa wa kuvunjwa kwa EAMWS kama mfano mmoja wa jinsi Uislamu ulivyopigwa vita; lakini hawahawa hawawi wa kweli kusema kuwa Aga Khan (muasisi na mfadhili mkuu wa EAMWS) aliendelea kuwekeza Tanzania na mahusiano yake na utawala wa Nyerere hayakuingia mawaa hata chembe.
Kwangu mimi kurahisisha tu kudai kuwa haya yote ni kwa sababu Waislamu/Uislamu unapigwa vita.
Hilo halipo huku bara tu. Ni tatizo katika jamii nyingi. Na ndio hasa sehemu ya huu mnakasha. Watu wanaacha kutafuta kiini cha tatizo, wanabaki kutafuta simple solutions. Mfumo wa kifisadi unamnyima kazi kijana wa kikristo/kiislam/asiye dini, badala ya watu kuangalia tatizo la ufisadi kwa ujumla wake, mwingine anaibuka anasema Yule kijana wa kiislam amenyimwa kwa sababu ya dini yake. Wakristo na waislam wa Lindi hawataki shule labda wanapendelea kuvua samaki zaidi, au wakristo na waislam na wapagan kwenye jamii za wafugaji wanakataa shule kwa kupenda zaidi ufugaji na uwindaji, halafu mtu anaibuka na kusema, waislam kwenye jamii hiyo wamebaguliwa na mfumo kristo… Nafikiri hata huko Oman uliko, kuna watu wana mentality hiyo, ikitokea uprising because of social discontent, kuna watu hawatawia kuilaumu Marekani, badala ya kuangalia kiini cha matatizo ya wananchi…
Mohamed Said mara kadhaa amesema Nyerere hakuasisi TANU! Tukipinga hili mnasema tunamtetea Nyerere kwasababu ni mkristo mwenzetu, na tuna chuki na uislam. Na kila anayepingana nanyi, mnafikiri ni mkristo tu
Na sisi hatukatai kuwa kulikuwa na waasisi wengine. Walikuwepo lakini Nyerere alikuwa ndio kinara. Au unataka kinara awe Abdul ambaye hakuwa na uongozi wowote ndani ya TANU kuanzia 1954???
Kama umemsoma Mohamed Said vizuri, na umetusoma na sisi vizuri bila jicho la udini, utaona kuwa hatupingi hadithi za nani alimpa Nyerere baiskeli, au nani alikuwa anampokea kikapu pale sokoni. Hata akidai kuwa Nyerere alikuwa anaenda sokoni bila pesa, kama ni ndio ukweli, sisi ni nani hata tupinge? Tunachopinga ni kufichwa baadhi ya facts ili kumdunisha mmoja na kumkweza mwingine. Tunapinga hisia zinazoingizwa kwenye masimulizi na kufanywa kama sehemu ya ukweli. Mathalan anaposema "the speech was farce, the TRUTH was muslims were no better than they were before independence" bila kueleza hiyo TRUTH ameipataje. Kuna bandiko analirudi rudia eti "The church declared islam as its enemy" wakati hiyo declaration is his own imagination. Anaposema watu walifungwa kwa uislam wao wakati actually walifungwa kwa kukaidi sheria za wakati huo (ikiwa ni pamoja na wasio waislam), huoni kuwa ni hisia tu ambazo zina lengo la kugawa wananchi? Mpaka amefikia hatua ya kutuma vijana na masheikh kuzunguka misikitini kuwaambia waislam wasichague Chadema ili wamchague muislam Kikwete? Hayo bwana Barubaru ndio tunayoyapinga
Nimekusoma
Nilikuuliza lile suala la your treatment as Zanzibari arab by your Oman hosts. Je wanakuona ni mwarabu kama wao, au na wewe wanakuita mwarabu pori? (Najaribu kulinganisha na wanaoitwa wangazija pori kule Comoro)
Itapendeza sana kama mtajadiri mambo hayo "objectively"bila kutafuta visingizio vya mfumo kristo!Nilipo Blue.
Al akhiy Gombesugu umegusa saaaaaana saaana kama nawaona hawa baadhwi ya masheikh uliowataja. naona umesaha vitongoji vngine Muhimu kama Ndumi na darini kisiwani kwani huko ndio chimbuko na bahri kubwa ya ilmu kwa wengi.
Mimi nashauri tuweke uzi maalum tuichambue TANGA ilivyokuwa kabla ya uhuru na baada ya uhuru kwanini Tanga imedidimia kiuchumi wakti kila kitu wanacho kuanzia bandari na hali ya hewa safi kuona dhulma walizofanyiwa.Upande wangu nitachambua sana kiuchumi kwani nina data nyingi sana za huko na wapi waliwakona na kuwadhulumu.
Nimefurahi sana uchambuzi wako na Allah akubariki sana.
maa salaam
Wanajamvi leo tumeingia page # 649,Mzee wetu Mohamed Said anaelekea kukubali makosa ya kitabu chake namwona hatu lugha anayoitumia si ile ya mwanzo ana weka tahadhari kubwa kabla hajachangia hoja si kama kule mwanzo.
Napenda kuwapongeza Mag3 Nguruvi3 Mzee Mwanakijiji Jasusi platozoom WildCard Wickama .......Kazi mliyoifanya si haba Mzee wetu Moh kajivunza mambo mengi hakujua Nyerere alishaingia Dar kabla ya mwaka 1950.Hakuwa anajua Nyerere alikuwa kiongozi wa AA mwaka 1945 huko Tabora.Hakupenda wasomaji wake wafahamu Rais wa kwanza wa AA alikuwa Cecil Matola angetokea Gerezani angeandika page 10 kumwelezea uhodari wake,usomi wake ......Mzee wetu kwa maksudi alitaka kutudanganya kwamba Abdul Sykes ndiye aliyemtambulisha Nyerere katika siasa za Dar hakujua Nyerere alionana na Dossa Aziz mwaka 1945 bila shaka Abdul Sykes wakati huo hakuwa na ushawishi wowote na kama alikuwa nao basi ulikuwa hauvuki Gerezani.
Nasema tena nawashukuru sana kazi mliyoifanya ni kubwa na mnastahili nishani ya uraia wema uliotukuka.Uchambuzi na hoja mbali mbali hakika ni funzo kubwa kwa anayetaka kujifunza.
Naona sasa unataka kulazimisha Bao.
Pole sana
Nitaelezea kwa ufupi jinsi kanisa la Tanganyika lilivyoshiriki harakati za ukombozi wa Tanganyika na madhila liliyokumbana nayo.
Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini. Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?.
Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kassi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa.
Nilipo Blue.
Al akhiy Gombesugu umegusa saaaaaana saaana kama nawaona hawa baadhwi ya masheikh uliowataja. naona umesaha vitongoji vngine Muhimu kama Ndumi na darini kisiwani kwani huko ndio chimbuko na bahri kubwa ya ilmu kwa wengi.
Mimi nashauri tuweke uzi maalum tuichambue TANGA ilivyokuwa kabla ya uhuru na baada ya uhuru kwanini Tanga imedidimia kiuchumi wakti kila kitu wanacho kuanzia bandari na hali ya hewa safi kuona dhulma walizofanyiwa.Upande wangu nitachambua sana kiuchumi kwani nina data nyingi sana za huko na wapi waliwakona na kuwadhulumu.
Nimefurahi sana uchambuzi wako na Allah akubariki sana.
maa salaam
Mzee MS, nina hoja ndogo. Nijuze specifically why you went and what you did kule Iran. Na kwa asseessment yako uli-achieve nini na ni kwanini unadhani ni muhimu kwa watu kama wewe kwenda kule Please.