Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Nguruvi3,

Nikikusoma nafurahika mno kwa vitisho na umahiri wako. Unanikumbusha watu kama Nikita Khrushchev na Slobodan Moilosevic!ahaha!!

Hayo mambo ya kiTanga na Biography ni wewe ndie uliemuanzishia Sheikh Mohammed Said,nami ikanilazim nikunyoshee maneno.

Mbona nami family yangu ni wakulima wa asili kabla hata Wajarumani hawajakua na fikra za kutia maguu yao hapo Tanganyika, na tuna mashamba mpaka kesho yenye hekari nyingi tu kuanzia Daluni, Bwete,Mwele,Magoma,Maramba,Saadani,Ushongo na Mazinde. Bahati mbaya mimi binafsi ni mvivu ndo maana nimekimbilia kujificha huku nchi za watu kwa miaka tarkiban ishirini sasa,Allahmdulillahi.

Hiyo Barabara ya 10 unayoitaja,hapo kale ilikua ni mojawapo ya viunga vyetu vya minazi. Na leo hii tuna nyumba zetu pale mtaani peke yake sita. Nakupa challenge nenda kagonge mlango pale jirani na Msikiti mkubwa wa Al Jumaa, kwa Al Marhum Shariff Nuru(dada yao ni Aunt Mwananuru Shariff aliwahi kuwa Principal Secretary nafikiri Wizara ya Afya hapo enzi ya Rais Mwinyi),wale ni jamaa zetu wa karibu na watakufahamisha uzuri mimi ni nani. Au nenda kamuone Mayor wako pale Tanga akufungulie Archives/shajara na uwasome Wazee wetu kwa utuvu tangia enzi ya Mwarabu na Mjarumani.

Ukishindwa huko koote nenda pale Barabara ya 9,uliza kwa Kina Diwani,nao pia ni jamaa zetu nao watakufahamisha kwa uzuri.

Au muone Salum Shamte wa Mkonge,ambae ni hakika unamfahamu,yule ameoa kwetu kwa hiyo atakupa habri japo kiduchu.

Sasa wewe hiyo Barabara ya 10,nyumba yako/yenu ni ipi,jamaa zako ni nani,au wale kina Khara Wahindi walohamia Canada!?

Mindhal, unasema machozi yanakukurubia tuyaache na tuendelee na mnakasha Insha Allah.

Nakupenda saana Mzee wangu Nguruvi3,na kwa sasa najua wewe ni Uncle wangu from ma Mum's side hapa jamvini,basi nami naringa saana sasa!ahaha!!

Ahsanta.
 
Nanren,
Huyo mwandishi ame generalize ni sawa na kusema Tanzania wanakata viungo vya albino wakti mambo hayo anafanyika sehemu zisizo na ustaharabu na utamaduni wa kiislam.
Barubaru,


With all due respect,
embu soma hizo statements zako.. kuna ustarabu na utamaduni wa kiislamu tanzania???

 
Wickama,

..kama lijitu lina zali zake na Wamarekani na linatafutwa basi tusikubali kulipa hifadhi.

..zaidi, hawa jamaa wakianza kumtafuta mtu basi uwezekano mkubwa kuna kitu amekifanya, or he is about kukifanya.
 
Last edited by a moderator:
Ngoja nikubaliane na hoja yako kwa kuipanua zaidi.

Sehemu ambazo zimetamalaki uislam, watu wote ni wastaarabu, hamna crime, na hamna hata jela. Watu wote huko huwa wanaishi vizuri. Hakuna mauaji, ulevi wa madawa/pombe, uzinzi, ulawiti, kuoneana, domestic violence, FGM, hayo yote hayapo... Ila yatakuwepo tu sehemu ambazo hazina waislam. Hapa nimekubaliana nawe. Ngoja tuendelee na thread ya Yericko..
 

Narudia tena kukuambia JF siyo sehemu ya POROJO tupe majina ya hao viongozi wa dini ya Kiislam Misri waliotoa "fatwa" wanawake kukukeketwa.

Fatwa ya masuala ya Uislam Misri yanatolewa na Mufti of Egypt All Gomaa.

Wewe umeitoa wapi watu hawauitaji link za wakurdi wanaitaji majina ya hao viongozi uliowataja.

Cc.. gombesugu, Kadogoo, Ami, Barubaru,
 
Last edited by a moderator:
Mohamed,
Umeuliza swali zuri. Kipi kilichofanya Kikwete ampe marehemu Abdulwahid na Ally Sykes medali baada ya miaka 50 ya uhuru? Jibu lake linaweza kuwa VERY interesting. Lakini nadhani ni bora kila mtu aspeculate kivyake vyake.
Kaka Jasusi,
Hakuna haja ya speculation hapa. Hata Mwalimu alipewa medali hiyo siku hiyohiyo, mjane wake akaipokea kwa niaba yake. Ikumbukwe kuwa TANU haikuongozwa na mtu mwingine yeyote, mbali na Mwalimu, tangu inaundwa, inazinduliwa( tarehe 7.7.1954) hadi inakufa kifo cha kinyonga( nasikia kinyonga akizaa hufa muda huohuo!) tarehe 5.2.1977. Historia ya TANU ndio hiyo. Ile ya kufikirika ya Mzee wetu Mohamed inayoanzia Burma na TAA aendelee kuifundisha misikitini na huko anakojua yeye.
 

Mwanakijiji,

Haina neno ndugu yangu,tuko pamoja na niwie radhi kama nimekukera.

Hata hivyo bado kuna baadhi ya mambo napitia hapa jamvini na bado nina maswali kadhaa kwako binafsi Insha Allah.

Lazim kwanza ukubali kuwa mimi binafsi na wewe tuna mitizamo tafauti mpaka hapa tulipofikia kwenye huu mnakasha, na kwa sababu zetu kadhaa. Na labda pia tafauti ya kuelewa vitu kadhaa au pia ku-over look vitu vingine vingi tu. Kwa hiyo huku tukiendelea na mnakasha ni vizuri kuheshimiana tafauti zetu nyingi mno.

Badala ya kutaka kwa ulazim na kwa haraka haraka kukubali hayo mapungufu ya kitabu cha Sheikh Mohammed,nijaalie muda kiduchu tuangalie atakapoishia na soote kwa pamoja, ndo tukate shauri la kujua nani mkweli na nani ni mrongo/alokosea. Halafu ndipo pia tutarejea tena kujua huko kukosea, je kunahalalisha na kutosheleza malengo ya hii mada kama ilivyoletwa hapa jamvini na Yericko Nyerere!?

Kwa kifupi,haya yoote tusumbukayo hapa jamvini,lakini la muhimu zaidi ni kuthibitisha shutuma dhidi ya Sheikh mohammed Said. Na pia tuangalie,je hata kama hizo shutuma dhidi yake tukizithibitisha,alizifanya kwa makusudio au ni tafran na dhahama tu za kiuandishi zilimzidi kimo,lakini moyoni mwake alikua na bado anayo makusudio mema kwa Watanzania wenzie na nchi yake!?

Ahsanta.
 
Nafyonza Ilm tu hapa.
Fyonza tu wewe kama ndege kwenye mauwa
Spike,
Upo kama vile haupo.....................
Huyu kijana uwepo wake ni wa kiaina.Safari ya mwanzo alifyonzaa weee.Aliposhiba akaingia ukumbini kupigana mieleka.Jamaa wakaanza kulalamika kama kawaida yao.Nusura wamuitie polisi jinsi alivyowabwaga mmoja mmoja.
 

Acha uvivu.
Hizo links nimekupa, zisome zote kwa undani. Umeiona hiyo ya Muslim brotherhood?
Kama hutaki acha.
Sheikh mkuu wa Egypt mwaka 1995 akiwa anapingana na mambo ya mkutano wa Beijing, alitangaza (Nilimsikiliza kwenye BBC) akisema kuwa ni wajibu kwa mwanamke wa kiislam kukeketwa.
Kama huamini haya nisemayo, basi acha. Ngoja Barubaru (akiamua kusema ukweli this time) akwambie, labda ndio utaamini.
 
Mimi siumi maneno, mimi nasema nachoamini.Kwa hiyo wewe Unachotaka kuniambia Wamarekani wanawavamia hizi nchi simply kwasababu ni waislamu?????
marekani waliivamia iraqi kwa kudai saddam alikuwa na silaha za maangamizi! matokeo yake wamepeleka makampuni yao ya mafuta ili wanufaike na mafuta ya iraqi! baada ya kumnyonga saddam wamegawa silaha kwa makundi ya kidini leo wairaqi wanachinjana wenyewe kwa wenyewe! huko afganistani alivamia ili kumkamata osama lakini wanadai wamemtupa baharini baada ya kumsalia sala ya maiti! leo wamarekani bado wako afganistani hatujui ni kwa malengo gani! baada ya hapo wameivamia libya kwa kusaidia uasi ili wanufaike na mafuta yao na baada ya gaddafi kuuwawa leo libya haina usalama kwa sababu ya uvamizi wa nchi za kikristo! sasa jiulize kwanini marekani haivamii nchi kama korea kaskazini au zimbabwe au venezuela? kwa mujibu wa bush junior alitangaza vita vya msalaba wakati anaivamia afganistani na iraqi ronald regan wakati anaondoka madarakani aliitangaza dini ya kiislamu kuwa ni adui aliyebakia baada ya ukomunisti! sasa mundus sijui unataka ufahamishwe vipi ili utambue hali halisi!
 
MUNDUGUS; hapa kwetu tuna sheria ya ugaidi lakini sheria hii inawahusu waislamu tu! ndio maana tundu lisu kashangaa lwakatware kahusishwa na ugaidi wakati sheria hii inawahusu waislamu tu!
 

Ritz,

Ni kweli,nahisi haya mambo ya technology na kurahisishwa kwa source of information inaharibu saana baadhi ya watu. Ghafula mtu waeza kujiona unajua mambo mengi, kumbe ni ile jamaa zangu Wahindi wa Kimamba wanaita "machele punga"!ahaha!!

Lakini haina neno na tuendelee na mnakasha.
 

Naona bado unazunguka kwenye kichuguu kama nguchiro tupe ushahidi wa hao viongozi na majina yao hizi links sijawaona viongozi wakuu wa dini kutoka Misri wakiruhusu ukeketeji, usichanganye mila za watu na Uislam.
 
Kadogoo,

..wewe una kengeza la UDINI.

..kama sheria ya Ugaidi inawahusu Waislamu, kama unavyodai, kwanini basi Lwakatare na Ludovick wanashtakiwa kwa sheria hiyo wakati wao ni Wakristo??

..umejaribu kupotosha utetezi wa Tundu Lissu kwa Lwakatare.
 
Last edited by a moderator:

ulimsikia akisema hivyo?
 

gombesugu,

"Fatwa" hutolewa na Maulamaa wenye Ilm siyo Bejing, ha haa haha.

Chele Punga...
 
Last edited by a moderator:
Kuna wakati binadamu huwa tunapitwa na jambo fulani...Unaweza kunisaidia/kunikumbusha labda ni waislam wangapi hapa Tanzania wameshafikishwa mahakamani au wameshashtakiwa kwa kutumia hii sheria ya Ugaidi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…