Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Yericko,
Najua unasema hivyo kwa kuwa kuna mengi hujasikia kuhusu siasa
iliyokuwapo pale sokoni na nguvu iliyojikita TANU kutokana na watu
hawa.

Nyerere alikuwa haruhusiwi kula ovyo na ndiyo maana Shariff Attas
alikuwa kivuli chake wakenda kula pamoja.

Wakati ule Special Branch waliweka kambi nje ya ofisi ya Abdu...

Yericko wajukuu wa Shariff Attas wako Dar watafute wana mengi ambayo
iko siku utakapotaka kuandika historia ya baba yako yatakufaa.
 

Yericko,
Hebu tufahamishe publisher wa kitabu chetu.
 
Hehee heeehee dah!

Mkuu Mohamed Said unanilazimisha sasa nizame kukijadili kisa hicho kwakutumia facts za kisomi na sio vingine,

Hebu twende taratibu,

Kwa kusema

"Nyerere alikuwa haruhusiwi kula ovyo na ndiyo maana Shariff Attas alikuwa kivuli chake wakenda kula pamoja".

Unamaana yakuwa Sharif Atass alikuwa mlinzi wa Mwalimu Nyerere??

Kama jibu ni ndio,

Kisa hicho hapo awali ulikitaja kuwa ni miaka ya 1950 na amini kuwa kipindi hicho Nyerere hakuwapo Dar na hakuwa kiongozi wa TAA hapa Dar je alimlindaje?

Kama ulinzi wa Sharif Atass kwa Nyerere ulianza baada ya Nyerere kuacha kazi ama kuchaguliwa kuwa rais wa TAA 1953, Je ulikoma baada ya Nyerere kuwa Rais wa Tanganyika?


Ngano za kutunga huwa ngumu sana kama unaowatungia ni mabingwa wa ngano pia!
 
Hapo ndipo mnapokosea sana. Kisa cha Shariff Attas kimewekwa ili tupate mazingatio, kuwa Nyerere alikuwa na tabia ya kuwasahau wahisani wake. Wewe upo kwenye kupeana vitu. Kuwa makini kuelewa maudhui Sio kusoma Kama hadithi simulizi.

Huyo dogo Yericko uwezo wake wa kuelewa mambo ni mdogo sana
 

Yericko;
usiturudishe nyuma! historia ya Tanganyika sasa iko wazi na kila mwenye akili na ustaarabu hawezi kukubali kudanganywa tena na hisohistoria bandia za kumtukuza na kumsifia Nyerere tu ati katuletea uhuru! nikiwa shuleni msingi waalimu wa siasa na propaganda walituimbisha oo Nyerere,,,ameleta!!!! Kawawa,,,ameleta!!! na Jumbe,,, ameleta!!! uhuru wa Tanzania!!! angalia uongo huo!!! lini Nyerere, Kawawa na Jumbe wameleta uhuru wa TZ? la kuchekesha Jumbe alipochafua hali ya hewa mwaka 1984 na kulazimishwa kujiuzulu, wimbo huo wa kudai alileta uhuru wa TZ nao ukasimama!

Yericko;
Huu si wakati tena wa kuimbishwa zidumu fikra sahihi za Mwalimu! Wazee waliopigania uhuru wote wanajulikana! siasa za majitaka hazina nafasi karne hii ya 21! unaweza kudanganya umma kipindi fulani, lakini kuendelea kudanganya umma huo daima ni muhali!

Mohamed Said;

Nakuomba uendelee kutupa darsa kwani haki imesha dhihiri na wasiotaka haki wendezao! bado tunahitaji darsa lako adhimu la historia ya kweli ya Tanganyika na Zanzibar! nahakika una mengi ya kutujuza mbali na Tanganyika pia tuna hamu ya kujua mengi kuhusu Zanzibar na harakati zao za kupigania uhuru! Yericko na washirika wake wameshindwa kuthibitisha madai yao ya kukuhusisha wewe na uchochezi sasa wamebaki kurudia rudia na kuimba wimbo na ngonjera zisizokuwa na mwanzo wala mwisho! yaani hata ngonjera na mashairi yao hayakidhi masharti muhimu ya mizani na kimo!

Matusi na kejeli za baadhi ya wadau wachache yasikutishe! mpuuze yoyote anaekuja na kejeli au matusi kama unavyompuuza kubwa lao! hapa kuna umma unahamu na ghamu ya kuchota ilmu ili wende na kurudi tena! mahali tulipofika si haba tunamshukuru Mola! kaza kamba isikatike Mzee Mohamed!
 

Kadogoo,
Nakushukuru kwa dua zako na maneno ya kunitia moyo.

In Sha Allah darsa itaendelea.
 

Hivi huyu Nyerere aliyeuza uhuru wetu kwa kugeuzwa kibaraka wa Wamarekani, Waingereza na Kanisa Katoliki ndiye mnayemsifia kiasi hiki bila haya? Huyu ambaye aliendeleza ukoloni wa Watanganyika na baadaye Wazanzibari kwa kuruhusu wakoloni waendelee kutunyonya baada ya wao kushindwa kuendelea kufanya hivyo kutokana na mapambano ya Watanganyika na Wazanzibari dhidi ya wakoloni?

Upande wa Kanisa Katoliki nan chi za magharibi kumtumia Nyerere kuendeleza Mfumo Kristo nimeshauelezea. Sasa angalieni jinsi Nyerere alivyokuwa anatumiwa kama Condom na mataifa ya magharibi kwa ajili ya kutunyang'anya uhuru wetu uliopatikana kwa jasho kwa kufuatilia makala hii Justifying the role of imperialism in Africa - World Socialist Web Site

Huyu Nyerere HAFAI hata kupewa kumbukumbu kwa kuupa jina mtaa ulioko Manzese kwa Mfuga Mbwa.
 
Suala la historia ya Zanzibar ni mtambuka sana unahitaji kuisoma historia kwa utulivu sana,

Ukikurupuka utaibuka na histohisia za akina Mohamed Said ambao wanadai Mapinduzi yale Matukufu yalikuwa ni dhidi ya uislamu na sio dhidi ya ukoloni wa sultan!
 

Yericko;

we kiboko! mwenzetu ulialikwa Pentagon! Jee, ulipiga picha na wenyeji wako? naomba tubandikie picha ulizopiga huko kama unazo tafadhali!
 

MS;

Hapo umewashika pabaya! patamu hapo! endelea Mzee!
 

Shukran kwa kuiweka hiyo link,mimi nilishawahi kuiona.

Kama nilivyowahi kueleza katika mojawapo ya bayana zangu za awali hapa jamvini,yakuwa hili suala la Palestine,Non Alignment Movement na masuala ya Polisario ni baadhi ya vitu vichache mno nilivyokua nakubaliana na Nyerere. Japo sina hakika na motives zake,khususan kutokana na historia yake na vitimbi vyake kwa yale mengine alokua akifanza.

Kwa mfano kushiriki kwake kikamilifu katika mauaji ya kinyama/massacre ya Matabeleland. Sio WaTanzania wengi wanaofahamu yakuwa Nyerere alishiriki kikamilifu katika mauaji yale ya kikatili na kumuunga mkono kupita kiasi Robert Mugabe dhidi ya Joshua Nkomo na Wanachi wengine wa Zimbabwe. Nyerere/Tanzania ilipeleka Wanajeshi 350 kushiriki katika mauaji yale machafu dhidi ya raia wengi wasio na hatia wakiwemo wanawake,vikongwe na watoto.

Tukirejea katika suala la Palestine;ni aghalab kumkuta well learned Christian/Catholic hasa anaejua kwa kina masuala ya Medieval History,Anthrolopolgy,Contemporary History,Current Affairs,halafu awe anawakubali au kushirikiana na Israel kwa karibu mno. Nyerere alikua ni mahiri katika hayo majambo na pia alikua ni Mkristo/Mkatoliki mtiifu mno.

Mayahudi na Vatican,hawa ni maadui wa asili. Lakini uadui wao ulikithiri khasa katika ile Slave Trade. Vatican inafahamu fika yakuwa Mayahudi ndo watu pekee wanaojua siri zao za ndani. Na ndo hao hao Mayahudi wanaowachafua kila siku kwa kutumia kupitia mainstream media wanazohodhi.

Ndo maana katika ule mkutano wa JFK na Nyerere,hao Wakatoliki wawili walikumbushana pia "wajibu wao" wa kupambana na Jewish Lobby kwa kila njia.

Tunajua kabisa yakuwa JFK hakuwa mtu mwenye historia ya sympathy,empathy au hata mawasiliano mazuri na Civil Right Movements. Tafauti kabisa na Bobby Kennedy. Mara nyingi akina Tom Mboya walikua close na Senator Richard Nixon kuliko JFK. Lakini utaona ghafla baada ya Tanganyika kupata uhuru,na maagizo maalum kutoka Vatican kwenda kwa JFK ndipo utakuta ile connection ya Nyerere pale ilipokolea mno.

Kwa wale wajuba msotaka kusikia,jaribuni kupitia Barack Obama - The Story,JFK Biography by Prof. Michael O'Brien na nyaraka/sources nyingine mbalimbali na mtabainisha mengi.

Nilipitia baadhi ya Threads hapa JF,nikakuta malumbano fulani ya kidini na jinsi "jamaa fulani" anavyojaribu kuonyesha "mantiki" na kupambanua "hoja" zake ili kuhalalalisha yakuwa Tanzania ni bora iwe na mahusiano na Israel ati ili Wakristo waokoke na kupata misaada toka kwa "ndugu zao"! Ilinilazim kucheka.

Kwa kifupi,Rais ali Hassan Mwinyi alifanza mengi mno mazuri lakini nae katika yale machache ambayo sikubalianai nae ni hili suala la kurejesha uhusiano wetu kwa karibu mno na Israel. Niliwahi kumuuliza Bwana Jabir(alikua Private Secretary/Special Advisor wa Mwinyi) kuhusu habari hii ,akanijibu ati "ililazim" kufanza hivyo maana walishinikizwa!? Sina hakika maana hakunambia nami sikuona haja ya kumuuliza na nani au kwanini!?

Niliwahi kukutana na baadhi ya jamaa "Waandamizi" walioongozana na ujumbe wa Baloz Ali Idd pale Tel Aviv wakti fulani. Jinsi nilivyowasikia mazungumzo yao nilipatwa na butwaa...ni watu ambao hata nilianza kushuku viwango vyao vya elimu na uelewa wao wa mambo ya kimataifa. Wifey wangu ni Austrian Jew na tulikua pamoja. Aliwahi kuniuliza hivi kwanini hawa watu wanafuatana na Viongozi wakubwa kama hivi,tena kwenye misafara ya kimataifa kama hii lakini inaelekea kuna vitu hawavijui kabisa!? Wallahi nilitahayari pasi kiasi!

Kwa kifupi walichachafywa mno na "vijana waduchu waduchu" kutoka Israel Ministry of Foreign Affairs,mpaka ikaonekana kuwa hao jamaa ni kuwa walifanza tu ile trip bila hata ya maandalizi ya kutosha au kujua walifata nini pale!? Japo sipo hapo nyumbani kitambo,lakini nahisi Tanzania tunaeleka pabaya!!?

Ahsanta.
 

Ni kweli elimu siyo certificate ndio maana tunasema ingawa Nyerere alisoma lakini certificate yake haikumsaidia pale alipoamua kuwapendelea Wakatoliki waziwazi dhidi ya dini na madhehebu mengine ya Kikristo na pale alipokubali kutumika kama Condom na wakoloni ili kuuza uhuru wa Watanganyika na baadaye Wazanzibari.

Kuhusu kusahau yaliyopita ili tugange yajayo, huo msemo ni sahihi tu kama utafahamu wapi tulipopita? Huwezi kujua njia unayotakiwa kupita kama hujui hapo ulipo ulitokea wapi. Ndio maana kazi za watu kama Mzee Said ni kazi za msingi sana sana kwa ajili ya maendeleo yetu ya mbeleni. Jua kwanza ulitokea wapi na wapi ulijikwaa. Ndipo utaweza kujua njia gani unatakiwa uende ili upate mafanikio yanayotarajiwa.
 
Yagawe utakavyo lakini moja ni kigano vingi ni vigano au ngano!

Sideeq,

Salaam

Huyu jamaa kila kukicha heshi kujinasib na Kiswahili na Uswahili,lakini anazidi kujinyambua na kujinanga kwa wale wenye kujua.

Tafadhali asikushughulishe.

Shukran.
 

Yericko,
Kibri kimefunika hata hiyo elimu kiduchu ulokuwanayo.

Ndiyo maana umefikishwa mahali umetukanisha hadi wazazi wako.

Punguza ujuvi utajifunza mengi katika maisha ya awali ya baba yako
kutoka kwangu.
 
Nimekuja ukumbini kufyonza Ilm siyo kufyonza matusi, Mzee Mohamed Said tunakuomba chonde chonde usiondoke ukumbini endelea kutudarasisha kuhusu historia yetu tanganyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…