Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
- Thread starter
-
- #14,001
Mtu yeyote anayemuona Nyerere kaleta Uhuru wakati katunyang'anya uhuru wetu Watanganyika na Wazanzibari tulioupigania kwa damu yetu kwa kuwaruhusu wakoloni waendelee kutonyonya chini ya ukoloni mambo leo huyo ni MPUMBAVU.
Naaaam! naaaam!
Ndugu yangu Mohamed Said,
Kama kuna mtu atasema kuwa amejifunza historia ya uhuru wa Tanganyika kupitia Ngano zako juu ya akina Shariff Attas, Mshume Kiyate na wengine waliokuwa wakicheka na Mwalimu Nyerere huyo ni MPUMBAVU na kamwe hata erevuka!
Tunapozungumzia historia ya nchi huwa tunasimamia yale yenye mafaa kwa taifa tu,
Hivi leo uzungumze historia ya Uhuru wa China halafu halafu ukaanza kumuchambua/kumuelezea Wen Fang Lee swahiba wa Mao Tse Tong,
Kisa cha kumzungumzia Wen Fang Lee nikuwa alimuazima kalamu Mao Tse Tong walipokuwa chuoni, hivyo walikuwa maswahiba wakubwa!
Je mwandishi huyu wa historia atakuwa amefuzu viwango vyakuandika historia ya nchi au atakuwa mbabaisha na mchochezi???
Mohamed Said tunapozungumzia nchi tunamaana ya hadhi na masanifu ya hadidu zake zitamalaki vizazi na vizazi!
Hakuna duniani pote ambapo wanamapinduzi hawakufanya upuuzi wa kitoto ama wakikubwa,
Kama visa hivyo havikuathiri harakati za ukombozi yanini kuvifanya viwe vya kitaifa ilihali ni vyakipuuzi (vyakiuungwana wa kiafrika)
Sio kila upuuzi uliofanywa na wanaukombozi basi nilazima uandikwe,
Utakuwa unajipunja mwenyewe hadhi ya kuwa mwandishi wa kimataifa hasa izingatiwa unaangazia kuitwa mwandishi wa historia ya Uhuru wetu!
Mwalimu Nyerere aliwanyang'anya Uhuru wenu chini ya Mkoloni muingereza mkristu??
Kweli dunia hadaha, Ulimwengu Shujaa!
Mkuu changamoto kama hiyo uliyoileta kuna watu hawaikubali kwani hawataki kusikia negative side za Nyerere.Wanasahau alikuwa binadamu na kuna mazuri na mabaya aliyotenda.Tumpeni credit kwa mazuri yake na kwa mabaya tuyajadili ili iwe fundisho kwa vizazi vyetu.
Hivi wanajamvi kuna yeyote mwenye kuujua mkasa uliomfika Chifu Kidaha Makwaia mpaka Nyerere mara tu baada ya uhuru akamzuia Tunduru kwa muda mrefu.Naomba atujuze maana kwenye record za Waingereza inaonyesha Chifu Kidaha alifanikiwa kumweka karibu Nyerere na Gavana wa Tanganyika kabla ya uhuru.
ahsante
Uthman,
Katika maajabu ya historia ya uhuru wa Tanganyika ni kisa cha Abdu Sykes, Chief Kidaha na Nyerere.
Abdu katika ya 1950 - 1952 alihangaika sana kutaka kumwingiza Chief Kidaha katika TAA aje kuwa rais
kisha waunde TANU.
Bahati mbaya Chief Kidaha hakupenda kujiumga na TAA kwa kuwa alikuwa na maslahi zaidi kati serikali
ya kikoloni na ile nafasi yake kama Member wa Legislative Council (Legco).
Bi. Mwamvua mke wa Abdu Sykes anasema kila Chief Kidaha akija Dar es Salaam kuhudhuria baraza akitokea
Shinyanga Abdu alikuwa akitafuta siku maalum akimualika nyumbani kwa ajili ya chakula cha usiku.
Katika mazungumzo yao mama yetu anasema ilikuwa ni Abdu kujaribu kumshawishi Chief Kidaha kuingia TAA
wamchague kuwa rais na kisha waunde TANU.
Alipotokea Nyerere mwaka 1952 yeye hakusita hata chembe kukubaliana na rai ya Abdu.
Alichaguliwa rais wa TAA April 1953 na July 1954 TANU ikaundwa.
Swali la kutafakari ni hili.
Chief Kidaha alijionaje Nyerere alipokuja kuchukua uongozi wa nchi na akatoa amri Chief Kidaha akamatwe na
akafungwe Tunduru?
Hakuna wasiwasi kuwa alimkumbuka Abdu Sykes.
Uthman,
Hivi ndivyo visa na mikasa katika historia ya TANU.
shukran MS nipo hapa tangu mwanzo wa mnakasha huu kuchota ilm ni vizuri na ni kheri kutuletea huo mkasa kujifunza popote tu
Naaaam! naaaam!
Ndugu yangu Mohamed Said,
Kama kuna mtu atasema kuwa amejifunza historia ya uhuru wa Tanganyika kupitia Ngano zako juu ya akina Shariff Attas, Mshume Kiyate na wengine waliokuwa wakicheka na Mwalimu Nyerere huyo ni MPUMBAVU na kamwe hata erevuka!
Tunapozungumzia historia ya nchi huwa tunasimamia yale yenye mafaa kwa taifa tu,
Hivi leo uzungumze historia ya Uhuru wa China halafu halafu ukaanza kumuchambua/kumuelezea Wen Fang Lee swahiba wa Mao Tse Tong,
Kisa cha kumzungumzia Wen Fang Lee nikuwa alimuazima kalamu Mao Tse Tong walipokuwa chuoni, hivyo walikuwa maswahiba wakubwa!
Je mwandishi huyu wa historia atakuwa amefuzu viwango vyakuandika historia ya nchi au atakuwa mbabaisha na mchochezi???
Mohamed Said tunapozungumzia nchi tunamaana ya hadhi na masanifu ya hadidu zake zitamalaki vizazi na vizazi!
Hakuna duniani pote ambapo wanamapinduzi hawakufanya upuuzi wa kitoto ama wakikubwa,
Kama visa hivyo havikuathiri harakati za ukombozi yanini kuvifanya viwe vya kitaifa ilihali ni vyakipuuzi (vyakiuungwana wa kiafrika)
Sio kila upuuzi uliofanywa na wanaukombozi basi nilazima uandikwe,
Utakuwa unajipunja mwenyewe hadhi ya kuwa mwandishi wa kimataifa hasa izingatiwa unaangazia kuitwa mwandishi wa historia ya Uhuru wetu!
Naaaam! naaaam!
Ndugu yangu Mohamed Said,
Kama kuna mtu atasema kuwa amejifunza historia ya uhuru wa Tanganyika kupitia Ngano zako juu ya akina Shariff Attas, Mshume Kiyate na wengine waliokuwa wakicheka na Mwalimu Nyerere huyo ni MPUMBAVU na kamwe hata erevuka!
Tunapozungumzia historia ya nchi huwa tunasimamia yale yenye mafaa kwa taifa tu,
'"Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.Hizi ni dharau na kejeli dhidi ya Wazee wetu wazalendo hebu msome Nyerere anavyowaelezea wazee wetu
Endelea kumsoma tena hapa chini
Walikuwa na beberu la mbuzi. Wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama. Beberu akachinjwa, huku anaambiwa, "Twining (Twainingi) umekwisha!" (Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo). Ndipo nikaambiwa: Tambuka! Nikavuka lile shimo. Hapo nikaambiwa na wazee: Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!Sio kila upuuzi uliofanywa na wanaukombozi basi nilazima uandikwe,
Utakuwa unajipunja mwenyewe hadhi ya kuwa mwandishi wa kimataifa hasa izingatiwa unaangazia kuitwa mwandishi wa historia ya Uhuru wetu!
Mzee Mo,Wickama,
Ikiwa umeridhia na BAKWATA hilo hakuna wa kukuzuia.
Binadamu lazima tughitilafiane hatuwezi kukubaliana kwa
kila jambo.
Ila ngoja nikupe kitu huenda hukijui.
Wale wote walioleta fitna ya kuvunja umoja wa Waislam
wote wamekufa dhalili chini ya unyayo.
Kuna waliotubia hadharani.
Kuna waliosafiri hadi Zanzibar kumshika miguu Sheikh
Hassan bin Amir na kutaka radhi.
Wapo wengine miili yao ilitahayar muda tu baada ya
kukata roho.
Wapo waliosalitiwa na hao waliowasaidia kuivunja EAMWS.
Lakini kubwa kuna aliyeomba dua Allah amuweke hai ashuhudie
wote waliotia fitna wakidhalilika na Allah alimkubalia dua yake.
Katika kundi lile la fitna alipokufa wa mwisho haukupita muda na
yeye akafa.
Huyu ni Shariff Adnan mmoja wa wanafunzi wa Sheikh Hassan bin
Amir.
Isalia,
Katika vitu ambavyo vilinipa tabu katika kuandika kitabu cha Abdu Sykes ilikuwa lipi niliseme
lipi niliache.
Katika moja ambalo nililiacha kulisema ni hili la kafara walofanya wanaharakati wa TANU pale
Soko la Kariakoo kumhami Abdu Sykes dhidi ya Afisa wa Kiingereza aliyekuwa akimuamdama
kwa sababu ya uongozi wake katika TANU.
Shariff Attas anasema kuwa iko siku huyo afisa Mzungu alimvamia Abdu ofisini kwake na akakuta
Abdu ana kadi za TANU.
Abdu Sykes alikuwa akiuza kadi zile za TANU pale sokoni nyingene akiwawa jamaa kuzisambaza na
kuwaita wananchi kujiunga na chama.
Shariff Attas anasema siku ile kulikuwa na raha ya pekee kati ya Muingereza na Abdu.
Abdu alikuwa na ulimi mzuri wa kuzungumza Kiingereza na lile zogo kati ya Abdu na Mzungu lilifanyika
mbele ya watu wakiwasikiliza wakiparurana.
Yule Mzungu alihisi kafedheheka kwa hiyo alitunga uongo kuwa ofisi ile inatumiwa dhidi ya serikali na ikawa
Abdu sasa anatakiwa ajibu shtaka lile akishindwa afukuzwe kazi.
Soko liliwaka moto wanaharakati pale sokoni hawa akina Shariff Attas, Mshume Kiyate, Shariff Mbaya Mtu na
wengine wakawa sasa wanakwenda mbio kutafuta vipi wamsaidie Abdu dhidi ya njama za Waingereza.
Ndipo ikaamuliwa lifnywe kafara zito la kumzika kondoo mzima pwani huku kavishwa sanda na macho katobolewa.
Yalioyompata Mzungu yule naogopa hata kusema...
Abdu alibaki kazini.
Sasa Nyerere alipoanza kuandamwa na serikali ndipo ikaamuliwa ifanyike kafara kama ile ya Abdu Twining akomeshwe.
Isalia,
Historia ya uhuru ina mengi sana.
Sasa hawa wenyewe ukizungumza nao katika mambo haya kule kuamini kwao kwa ''silaha'' hizi na hisia zao zilikuwa juu
kiasi wewe msikizaji unaogopa kulichimba zaidi.
Ndiyo maana lile kafara na Nyerere ambalo mwenyewe alilieleza katika hotuba yake ya muago na hili kafara la Abdu Sykes sikutaja katika kitabu changu.
Yericko,
Pole sana.
Hao CIA wengine tumejuananao katika anga za kisomi na wametusikiza
katika mikutano ya kimataifa tukiwapa majibu ya dhulma zao.
Pentagon sijaalikwa lakini nimepita nje na nimeiona.
Ground Zero nimefika...
Wewe unataharuki leo na mambo hayo.
Mimi nimehadhir kwenye vyuo vyao kwa mwaliko wao.
Hivi una kipi wewe katika dunia hii ya wasomi uandike kitu
cha kuwastua Waamerika!
Au huwajui?
Al Akhiy Mohd said.
Kweli wewe ni bahr ya ilmu kwani tunajifunza mengi kutoka Kwako na Allah atakubarik kwa darsa lako hili.
Nimefurahi sana kiswa hichi kwani niliwahi kuhadithiwa na rafiki wa baba yangu Al marhum Ali Mpina (watoto zake akina Zarara, Nuru) wa mkunguni na livingstone.
hakika alivyonihadithia ni sawa kabisa na ulivyokieleza hichi kisa ya Abdu.
Allah akubarik sana Mohamed Said uzidi kutupa darsa hili kubwa na lenye manufaa kwetu kujua ukweli halisai wa historia hizi.
nafikiri tu anatakiwa ajue waamerika hawana rafiki wa kudumu na wala adui wa kudumu. yeye anatumiwa kama muwa tu ukiisha utamu unatupwa nje.
Tumpe pole.
Hapana!
Sijawakebehi, nimehoji uhalali wa kisa hicho na umenilazimisha nihoji kwakutumia mantiki ya hadithi yako!
Sasa kama kuhoji kisa ni kukebehi basi hatuna haja yakuganda hapa mzee wangu!
Mzee Mo,
Huo ni uongo mtupu, Ndo maana hata radio iman watangazaji wake huwaongopea watu kuwa mrema wamempiga dua.
Kumbe mtu anamaladhi yake yanamsumbua wanakaa kuwadanganya watu kumbe mtu anakisukali.
Mbona sasa hivi ametoka shavu inamaana dua imeisha nguvu? Mzee mo, kunatofauti gani ya habari yako ya kuhusu hao jamaa na watu wa radio imani na mrema? Ila tambua kila mtu atakufa kwa kifo alicho pangiwa na mola wake.
Mohamed Said usidanganye umma kweupe hivi,
Hii ni jf, ukidanganya jiandae kutetea uongo wako!
Kusema Abdul alimshawishi Chifu Kidaha ajiunge na TAA ili aje awe rais wa TANU (chama chakufikirika enzi hizo), ni UONGO
Wanajamvi,
Abdul Sykes akiwa BONDIA wa kivita ndie aliyeongoza mapinduzi yakuong'oa utawala wa wazee katika TAA na kuwa katibu wa kimabavu,
Kisha kuwa rais wa mpito baada ya rais wakuchaguliwa Dr Kyaruzi kupelekwa uhamishoni Shinyanga Kahama,
Huyo huyo 1953 akaingia vitani kugombea urais wa TAA na Julius Nyerere na akapigwa chini,
Sasa jiulize nawe msomaji, je ngano za Mohamed Said kuwa Abdul Sykes alikuwa ni mtu mwenye huruma kwa maana ya ku create jambo kisha kutafuta mtu wakukisimamia,
Hii ni udharirishaji kuwa Nyerere alipofika Dar akapewa dili la kuwa rais na Abdul Syke,
Hata hotuba tu ya muago ya Nyerere hapo juu inapingana na uongo wa Mohamed Said!
Mwalimu anasema wazi kuwa alikuwa na malengo ya kisiasa (political vision) tangu angali mdogo shuleni Tabora
Mohamed Said nilikwambia uongo ni kazi sana hasa ukiwa unategemea wasikiliza waliopevuka na werevu!
"Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.
Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu nikawa ninakuja Dar es Salaam, kwa mguu; kila Jumamosi. Baadaye wazee wakanipa baiskeli nikawa ninakuja mjini kukutana na wenzangu; kufanya mikutano.
Hivyo ndivyo tulivyofanya. Wazee wakaniamini upesi sana. Tukawa na uhusiano mkubwa sana. Wadogo wenzangu wengine walikuwa Abdul Sykes, Abass Sykes (mdogo wake), Dosa Aziz waliokuwa wengi ni wazee.
Katika kuhutubia mikutano yangu, nilikuwa nikisema: Wazee na Ndugu zangu! Wazee hasa ndio walikuwa na mikutano ya awali ya TAA na TANU. Walikuwa na msimamo wa hali ya juu kabisa! Hawakuyumba hata kidogo! Vijana walikuwa na mashaka. Wengine walikuwa na vikazi vyao, waliogopa kuvipoteza.
Nalo jambo lenyewe ni la hatari la kuzungumzia uhuru! Unaweza ukakosa kazi; na wapo waliopoteza kazi; wengine wakaacha kazi. Akina Rashid (Kawawa) waliona watoke kwenye shughuli hizo tuje tuungane katika chama.
Wazee wa Dar es Salaam, na baadaye wa nchi nzima, wakatuunga mkono, na kila nilipokwenda, watu wa kwanza walionielewa, walikuwa wazee.
Walikuwa na beberu la mbuzi. Wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama. Beberu akachinjwa, huku anaambiwa, Twining (Twainingi) umekwisha! (Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo). Ndipo nikaambiwa: Tambuka! Nikavuka lile shimo. Hapo nikaambiwa na wazee: Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!
Barubaru,
Salaam.
Sina hakika huyu unaemzungumzia wewe. Nimjuaye mimi ni Bwana Islam jamaa zao kina Prof. Abdilrahman Babu. Mara ya mwisho nakumbuka akikaa pale Maweni Str. Upanga na alikua na Madrassa. Hiyo ya duka ni kweli,lakini nikumbukavyo duka lake lilikua ubavuni pa Al Masjid Maamur pale Malik Road Upanga.
Ni mtu mwenye bashasha mno. Nakumbuka kuna siku nilkwenda kwake kumfuata Sahib yangu mwanae Eddy Islam. Nilipobisha hodi akanifungulia yeye Sheikh Islam mwenyewe. Nikamwamkua,na nikamuuliza je Sheikh Eddy nimemkuta!?
Japo akinifahamu uzuri,lakini akanijibu;kumradhi Bwana mdogo labda umepotea njia maana huyo "Sheikh wako" Eddy hakai humu. Maana humu ndani kuna Sheikh mmoja tu,na ndie mimi.
Nami sikumwacha,nikamjibu kama Sheikh Mathias Mnyampala ali-qualify kuitwa Sheikh basi namimi kwanini nisimwite ndugu yangu Eddy Sheikh!?ahaha!! Wallahi,alicheka mno...akanambia wewe ulikua mtulivu lakini sasa umekua Maluuni saana!ahaha!!
Pale Ally Khan,kama uliwahi kuishi pia palikua na yule Mzee mstaarabu mno wa Kihaya...Mzee Bulengero,lakini alifariki kitambo maskini.