Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Sideeq; Nina uhakika Jokakuu atakujibu vizuri zaidi. Mimi kesho wakina Waryoba wakileta tu kipengele cha kupigia huu Muungano Kura, Sheikh wangu mimi nawatema Zenj. Huko kwenye mahesabu ya BOT wala sipo. Langu mimi ni kuwa kuishi na jirani tunalaumiana na kujuta ku-share nyumba kheri kila mtu atafute chumba kwingine.
 

asipokuelewa na hapa..
Sie vijana wa kijiweni tunaita "kajitoa ufahamu"
 

Nguruvi3.

Binafsi nakushangaa sana unasema wewe na mwisho unalalamika wewe.

labda nikupe kiduchu tu. Je unajua Znz hakuna hata mtu mtu mmoja anayekufa kwa njaa kwa kukosa chakula?

Je unajua Tanganyika kule Dodoma, Singida, mara , shinyanga na Arusha kuna watu wanakufa kwa njaa ktokana na maafa mbalimbali ikiwemo mafuriko, ukame na mengine.

sasa iweje Tanganyika hii iache wananchi wake wanakufa na njaa wao wakawafadhwili Znz. Je wana akili hawa?

Je unajua Znz wameshafanya jitihada nyingi sana kutaka kujivua huo Muungano lakin Nyerere alikuwa kipingamizi. Je unajua Siri ya Nyerere katika huo Muungano?

Lakin kubwa kwanini mumeuvua na kuukana utaifa wenu na kujivika joho la UTanzania na ukiitwa mtanganyika unaona kama mtu amekutusi?

lakin kwa muungwana ukiona inakuumiza BASI NI BORA UITUE NA SIO KUENDELEA KUBEBA HUKU UNALALAMA KWA MAUMIVU.

Lakn vipi ulipitia ile tovuti ya Joint Finance Commission na kuangalia ripoti zao ili tuzungumze zaidi kuhusu uchumi wenu. kama tayari sema tufungue darsa hapa kwa faida ya wengi kwani siku hizi zinazoongea ni FACTS na sio maneno ya mitaani.

Pole sana
 

jasusi na barubaru; jamani nawaombeni kuwa iacheni hii mada hasa ya watoto wa marehemu nyerere mimi naiona ni too intrusive kwenye private life ya a child. Jasusi nakusihi just stop the cycle of answering yaishe. Barubaru congratulations for your achievements
 

Hapo mkuu umegusa kitu kikubwa sana!

Sasa tuwahoji hawahawa wanaohubiri kuwa Shehe Hassan Bin Amir wamempa heshima kufatana na imani yao, iweje leo Nyerere anapotaka kupewa heshima na kanisa la imani yake wanaibuka na kupinga?

Labda hawajui mipaka ya imani yao! Wanataka kuwapangia wakatoliki mtu wakumpa heshima!
 
Ndugu yangu Jasusi

Mimi ningekuomba hiyo mada ya Mwalimu Nyerere na familia yake muiache,

Inatuondoa katika uwepo nakutufanya tutake kuongea kitu!

Tutulie kwenye lengo la uzi huu
 



Mkuu Nguruvi3,

Kuitwa Kaafir si neno la kukufanya ww usikitike napata tabu kulitafsiri neno hili kila mara lakini sitachoka kulitafsiri (Kaafir ni kiarabu na Kiswahili ni mpingaji na English ni Protestant ama non muslim) lakini kwanini tunatumia neno hilo,kwasababu mtu yoyote ambaye ni kinyume cha uislamu anakua ni non muslim bora nitumie term hiyo kuliko kutumia neno kaafir.Halafu wakristo walokuwepo mwanzo zanzibar walikua ni watu wastaarabu sana walikua hawana haja ya kututaka tusilimu na kutuwekea makanisa kila sehemu hawakua na haja hiyo lakini wanaokuja saivi dah we acha tuu.

Nafikiri utakua huna mashaka na neno hilo tena hata kama mtu atalitumia kwako.

Kuitwa machogo hata na sie si nawaona na nawasikia wengi wanatuita vichwa pasi mbona sisi hatujali tafuna tuu mkuu.


Kuhusu wazanzibar kufanya mradi kwamba tukitaka hela tunavuta kapu tuu sijaliona hilo unless unaushahidi kamili ndo uweze kuongea na kutishia kutoka kwenye muungano hatutishi yaani tuko serious tena sana na harakati hatukuzianza sisi nikupe mfano Karume Jnr alivyotaka kukata uhusiano na nyinyi kenda na maji Jumbe jela ya ndani Salmin Amour Commandoo wa udongo kapona chupuchupu sasa kwa akili ya kawaida nani anautaka muungano hata kama haumpi faida lakini anautaka kwa hali na mali na hakuna na wala hajatokea raisi watanganyika alotaka kuuvunja muungano.


Mkuu juzi ndo maana nikaweka mfano wa Scotland ukitizama budget ya UK nikubwa sana na ukitizama mchango wa Scotland ni mdogo sana kwa UK na bado wanataka kujitoa wanasema kua indepent ni bora kuliko kua na UK na bado mchango wao ni mdogo sana.Halafu inaendana na population ya watu kwa kuchangia katika mfuko wa muungano sasa unataka tuchangie 100 billion wakati population iko 1.1 million tena hakuna viwanda zanzibar hamna ukulima kama zimbabwe wenzetu ama south africa kikubwa kinachoingiza hela ni bandari kama visiwa vingi vinavyofanya duniani.

Na katika kuchangia jamani michango ninayoiona ni ya SMT na si ya Tanganyika kama ni tanganyika iko wapi ya SMT je Tanganyika inachangia ngapi katika mfuko wa SMT yetu sisi 24 yenu ngapi utanambia Tanzania bara ndio Tanganyika jee Budget ya SMT iko ngapi munajichanya tuu kama tuliwaita ni wizi ama wanyang'anyi basi naona inaanza kuthibitika.

Hatuhitaji kuzuiwa ngoja muungano ukatike tuu utajua na hata watakao baki mukitaka mutawaondosha wenyewe sisi ni wakarimu sana mukitaka mutakaa mukitaka mutaondoka mulikuwepo mwanzo hatutakufukuzeni saivi
 
Mwenye access na radio heri 104.1 Mohamed Said, yupo hewani anaelezea maisha ya Ally Sykes.
 
Last edited by a moderator:
Mwenye access na radio heri 104.1 Mohamed Said, yupo hewani anaelezea maisha ya Ally Sykes.
 
Last edited by a moderator:


Mkuu

Unasubiri kesho sisi tumeanza tangu ulipoa sisiwa endelea kusubiri tuu watakupa
 
Timothy Peter Thomas, nitakujibu japo kwa ufupi kwani naamini kama umeufuatilia huu mjadala toka mwanzo wake, majibu mengi ya maswali yako yapo humu humu. Hata hivyo kwa kukusaidia;

Field Marshal John Okello ndiye aliyeyaongoza mapinduzi ule usiku wa tarehe 12 January 1963, mapinduzi yaliyomfungasha virago Sultani Sayyid Jamshid bin Abdullah Al Said, kiongozi mkuu wa serikali ya Zanzibar. Okello ndiye alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Mpinduzi na hata baada ya kumtangaza Karume kama Raisi kupitia chama cha ASP, alibaki kama msemaji mkuu wa serikali. Baada ya wiki moja tu vitendo vya Okello vilianza kumfadhaisha sana Karume pamoja na viongozi wengine wa serikali lakini ikawawia vigumu kuchukua hatua kwani Okello alikuwa na wafuasi waliokuwa tayari kumlinda kwa gharama yoyote ile. Kujaribu kumweka kando akiwa bado kwenye ardhi ya Zanzibar kungeweza kusababisha machafuko makubwa ambayo pengine yangeuangusha serikali ya Karume.

Mpango ulisukwa na kuna wakati Karume alitaka hata msaada wa Jomo Kenyatta, Raisi wa Kenya, amkamate Okello alipozuru Kenya katikati ya mwezi wa pili lakini mpango huu haukufanikiwa. Baadaye Okello na Karume walisafiri pamoja kuja Dar es Salaam kwa mwaliko wa Mwalimu Julius Nyerere ambaye pia wakati huo hakuwa anafurahishwa na vitendo vya kikatili alivyoendesha Okello. Bila kujua Okello alikubali huo mwaliko lakini baada ya kufika Dar es Salaam alizuiliwa na hakuweza kurejea Zanzibar. Kilichofuata ni namna ya kuwatuliza wafuasi wake ambao walianza kuonesha wasi wasi kwa yaliyompata hivyo ilibidi mbinu isukwe jinsi ya kupooza mambo.




Kazi ya propaganda ya kufuta nyayo za Okello zilianzia hapo na kazi hiyo alikabidhiwa Abdulrahman Babu ambaye tarehe 23 Machi 1964, alianza rasmi kazi hiyo. Babu alidai redioni kuwa Field Marshal John Okello siyo tu hakuongoza mapinduzi ya Zanzibar bali alikuwa ni moja tu katika watu waliofanikisha mapinduzi. Hizi zilikuwa ni jitihada katika kupambana na umaarufu wa Okello kama kiongozi mkuu wa mapinduzi na kuwashawishi wafuasi wake kwa kuwaahidi waliokuwa wapiganaji wake ajira ndani jeshi la wananchi lililokuwa linaundwa. Walifanya jitihada sana kufanikisha hili lakini hawakuweza kufuta vielelezo vyote kama picha zake na sauti yake, hizi zipo mpaka leo.
 
Last edited by a moderator:
Asante sana mkuu Mag3 kwa ufafanuzi murua!

Bila shaka ndugu yetu Timothy Peter Thomas ameelewa!
 

Asante kwa maelezo murua kabisa ndugu yangu Mag3. Nipo hapa tangu siku ya kwanza kabisa ya mnakasha huu, jina la Okelo halijapata nafasi kabisa. Umenisaidia kujua pa kuanzia, barikiwa sana kaka.. Ningefurahi sana kama ungepata nafasi ya kuyajibu maswali yote kwenye swalh langu msingi, kipengele hadi kipengele..
 
Last edited by a moderator:

Timothy; Tulihangaika na hii mada sana kama wiki mbili tuu nyuma. Jaribu kupitia threads za nyuma utaikuta. Go kama 40 pgs back. Kwa kuongezea alichokupa Mag3 kuna hii video ya siku husika;


https://www.youtube.com/watch?v=-sMDkCSC_5g
 
na iwe hivyo mkuu, babu yangu kule lushoto alitembea kwa miguu umbali mrefu, toka mlalo hadi Tanga mjini katika harakati za kudai uhuru leo useme wazee wako wa new street ndo waliotuletea uhuru........!!!!!

Zumbemkuu,
Ikiwa babu yetu alifanya juhudi hizo hilo ni jambo zuri na yeye anastahili sifa
kama wanazopata wote waliopigania uhuru.
 

Ukisha kuwa kiongozi wa umma hakuna cha Private life tena! ndio maana aliyekuwa Rais wa Marekani Clinton habari zake za kumpapasa papasa Dada Lewinsky ziliwekwa hadharani na dunia nzima tukapashwa! mwangalie Beliskoni wa Italy!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…