Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

JokaKuu!
Ninachofahamu mimi kutoka kwako ni kuwa unajaribu kuwaonyesha wana ukumbi hasara za Muungano kwa Watanganyika na athari zake mbaya ikiwemo ukwamishaji wa "maendeleo" ya Mtanganyika kama vile Kusini.

Umetuonyesha huko nyuma pia kuwa upo mstari wa mbele katika kuwazindusha Watanganyika kuhusu hasara wanazozipata kutokana na Muungano.Ulitufahamisha vilevile kuwa Watanganyika wamechelewa katika kuzidai haki zao zinazohodhiwa na Muungano.

Unaweza kutuelezea ni sababu zipi unafikiria zilimchelewesha Mtanganyika kuzinduka katika kudai haki yake?
Ni matumaini yangu kuwa kuelewa kwa Mtanganyika wapi alijikwaa kutakuja kumsaidia sana mbeleni.
*Si lazima JokaKuu yoyote anaweza kujimwaga na kutupatia tathmini yake.

Sideeq; Nina uhakika Jokakuu atakujibu vizuri zaidi. Mimi kesho wakina Waryoba wakileta tu kipengele cha kupigia huu Muungano Kura, Sheikh wangu mimi nawatema Zenj. Huko kwenye mahesabu ya BOT wala sipo. Langu mimi ni kuwa kuishi na jirani tunalaumiana na kujuta ku-share nyumba kheri kila mtu atafute chumba kwingine.
 
Too late Mohamed, hoja iliyokuwepo mbele yetu ni kuwa Nyerere kwa ''udhalimu'' wake alimfukuza Sheikh Amir bila sababu. Ukaenda mbele na kumhusisha na EAMWS pale tulipouliza inawezekanaje Nyerere aamke asubuhi na kumchukia mtu aliyefanya naye kazi miaka mingi. Hakuna maelezo mengine zaidi ya kusema ukataili wa mwalimu dhidi ya wazee wako.

Leo unataka kueleza kisa baada ya kujulikana kuwa Sheikh alikuwa Msaliti.
Labda tuanzie na kwanini alikataa nafasi alizopewa na kwanini alijificha na kuendeleza siasa za pembeni.

Kuhusu Sheikh Amir kuwa Walii hilo halina tabu kama wapo walioamua kumpa hishma hiyo.
Lakini pia kuna jambo hapa, sasa kama alipewa hishma hiyo na wafuasi wake kwa taratibu za imani yao, Iweje basi wawepo watu wa kuhoji u-saint wa Nyerere anaotaka kupewa na watu wa imani yake?
Hakuna double standard kwa mtazamo wa haraka tu.

Mwisho, Sheikh kuitwa mnafiki na msaliti si tusi, kama lingekuwa tusi linalowaumiza basi msingezunguka duniani mkimsema Nyerere kuhusu viarago na pesa za vitoweo.

Kama lingekuwa linaumiza basi msingemvunjia hishma kwa kusema Laanatullah kila anapotajwa, wala asingeitwa habithi, baradhuli, mnafiki n.k.

Kwanini udhani kuwa sheik Amir anastahili hishma kuliko Nyerere wote wakiwa wanadamu, wazee na familia zao?

Hapa ndipo nasema kila siku lazima watu waangalie nyuma, pembeni na mbele.
Kurushia watu mawe ukiwa katika nyumba ya glasi si jambo jema.

Kila mzee wetu aliyepigania nchi hii na apewe heshima.
Tuache uchochezi usio na maarifa

Hii inaitwa fitna al maarifa kama anavyosema ndugu yangu Gombesugu.
Tuache haya tuangalie jamii inakwenda wapi, inahitaji nini, tufanye nini kwa pamoja na si kwa chuki na kubaguana.

asipokuelewa na hapa..
Sie vijana wa kijiweni tunaita "kajitoa ufahamu"
 
Unamkumbuka Dr Victor Umbrich!

Waambie wazanzibar ukweli kuwa muungano unafaida kwao.
Mbona ninaweka mambo hamjibu nukta kwa nukta mnajibu general?

Mathalan, hivi znz ilishawahi kuwa na bajeti ya ulinzi na usalama tangu mwakwa 1964?
Kama hapana nani analipa gharama hizo.
Hivi si kweli kuwa mapato na bajeti yana nakisi kubwa, je nani analipia nakisi hiyo?

Anyway hiyo cc kwa Jasusi sijaipata. Link ya Mkuu Jokakuu nimeipitia kwa taarifa.
Barubaru alishaieleza tukaipitia siku nyingi, alichokuwa anaogopa ni kuweka hadharani kuwa Zanzibar inachangia billioni 24 katika muungano, hata kabla ya huduma nyingine za bure, znz inapewa bilioni 32 kupitia ofisi ya makamu wa Rais ! yaani inapewa nyingi kuliko inachoweka.

Ndio maana huwa nasema znz inachangia zero! sifuri! haina msaada ni tegemezi tu katika Tanganyika.

Mkuu Jokakuu amesema kuwa jitihada za kuwaamsha Watanganyika zinaendelea.
Mdomo wa wznz unawatokea puani sasa.

Muungano ukivunjika Tanganyika haina hasara Gombesugu.
EAC ilivunjika tukabaki uchi, leo sisi ni sehemu muhimu sana ya EAC, seuse znz, I mean Unguja!
Zile sababu za cold war hakuna tena!

Hebu tueleze Mtanganyika anafaidika nini na uwepo wa znz

Juzi Tanganyika wamejenga chuo znz kwa bilion 3.6 badala ya kujenga Mwanza au Mtwara
Leo znz haina hata eneo la kuchomea ngano(chakula si hii ya mzee), sasa unafikiri hao watu 350,000 wakirudi wataishi wapi kwa uchumi gani.

Muungano ukivunjika znz itakuwa mshindani, hivyo biashara kama ya utalii itakuwa na ushindani.
Saadan na Bagamoyo zikiendelezwa, Tanga ikawa bandari huru, znz itafanya nini!
Sasa hivi kuna kuonea haya kuwa ni sehemu yetu kwahiyo hakuna sababu za ushindani, nje ya hapo maumivu.

Gombesugu kwani umeshasikia tena zile kelele na midomo ya wzn kuhusu muungano baada ya kuambiwa let them go!
Mtanganyika ndiye mwenye muungano anaulipia, mzanz ni tegemezi tu hana msaada wa aina yoyote!

cc Jokakuu, Jasusi, Barubaru, Mag3,Mwanakijiji, Shariff Ritz, Akhyi wote na Makafir wa Tanganyika

Nguruvi3.

Binafsi nakushangaa sana unasema wewe na mwisho unalalamika wewe.

labda nikupe kiduchu tu. Je unajua Znz hakuna hata mtu mtu mmoja anayekufa kwa njaa kwa kukosa chakula?

Je unajua Tanganyika kule Dodoma, Singida, mara , shinyanga na Arusha kuna watu wanakufa kwa njaa ktokana na maafa mbalimbali ikiwemo mafuriko, ukame na mengine.

sasa iweje Tanganyika hii iache wananchi wake wanakufa na njaa wao wakawafadhwili Znz. Je wana akili hawa?

Je unajua Znz wameshafanya jitihada nyingi sana kutaka kujivua huo Muungano lakin Nyerere alikuwa kipingamizi. Je unajua Siri ya Nyerere katika huo Muungano?

Lakin kubwa kwanini mumeuvua na kuukana utaifa wenu na kujivika joho la UTanzania na ukiitwa mtanganyika unaona kama mtu amekutusi?

lakin kwa muungwana ukiona inakuumiza BASI NI BORA UITUE NA SIO KUENDELEA KUBEBA HUKU UNALALAMA KWA MAUMIVU.

Lakn vipi ulipitia ile tovuti ya Joint Finance Commission na kuangalia ripoti zao ili tuzungumze zaidi kuhusu uchumi wenu. kama tayari sema tufungue darsa hapa kwa faida ya wengi kwani siku hizi zinazoongea ni FACTS na sio maneno ya mitaani.

Pole sana
 
jasusi,

kwanza niliweka nia nikuwekee hapa ukukmbini watu wote kutoka tanzania waliopitia carleton university lakin nimepata ushauri toka kwa wengi nisiweke hapa lakin kama utapenda naweza nikaku pm wote uangalie kama huyo anna yupo.

Lakin unapoandika kitu hakikisha kuwa una yakini nacho kama mimi ninavyoyakinisha. kumbuka kuwa enzi hizo ili mtu aende chuo kikuu ilimpasa kwanza amalize form four na kisha aende form six na kisha apite jkt. au apitie adult chances ambazo nina hakika yeye hajapita huko.sa

sasa hebu dadavua kidogo kuwa je aifanikiwa kupata maksi za kutosha kwenda form six. Je alisoma skuli gani na jkt alipitia wapi kama huu msema kweli?

nitakuongezea moja hapo yule mtoto wake uliyesema alikwenda airforce china. Je unajua kuwa alikuwa form four akaenda kusomea kozi ya urubani ambazo colifications zake zilihitaji form six. Na wote aliokuwa nao walikuwa form six yeye pekee ndio alikuwa form four? Na alikuja baada e alishindwa masomo hayo. Je nae alipitishwa kinamna hiyo au ... Je nalo hili unalikataa?

kwa kuwa najua mengi sana kwa sababu nilikuwa karibu na familia hiyo nilipokuwa tz. Napenda kukwambia nyerere alipenda sana vijana wake wasome lakin ...

Nilichokubainishia hapa alipenda watoto wa wengine wapite njia sahihi yeye wake walipita njia za mkato japo wengi hawakufanikiwa kufika. Ndio maana tunasema hakuwa mwadilifu.

Kuhusu phd yangu isikutie khofu kwani nimeipata kihalali kabisa toka mtendeni skuli dar, tambaza, ilboru, jkt ruvu, udsm(tz). Carleton univ(can), na sofia univ (jpn).tafuta tu jina la dr hamza yousuf al-naamaniy

tuendelee na mnakasha kwani tutaingilia siri za ndani za familia hii ambazo si vizuri kuzianika hapa.

Pole sana

jasusi na barubaru; jamani nawaombeni kuwa iacheni hii mada hasa ya watoto wa marehemu nyerere mimi naiona ni too intrusive kwenye private life ya a child. Jasusi nakusihi just stop the cycle of answering yaishe. Barubaru congratulations for your achievements
 
Too late Mohamed, hoja iliyokuwepo mbele yetu ni kuwa Nyerere kwa ''udhalimu'' wake alimfukuza Sheikh Amir bila sababu. Ukaenda mbele na kumhusisha na EAMWS pale tulipouliza inawezekanaje Nyerere aamke asubuhi na kumchukia mtu aliyefanya naye kazi miaka mingi. Hakuna maelezo mengine zaidi ya kusema ukataili wa mwalimu dhidi ya wazee wako.

Leo unataka kueleza kisa baada ya kujulikana kuwa Sheikh alikuwa Msaliti.
Labda tuanzie na kwanini alikataa nafasi alizopewa na kwanini alijificha na kuendeleza siasa za pembeni.

Kuhusu Sheikh Amir kuwa Walii hilo halina tabu kama wapo walioamua kumpa hishma hiyo.
Lakini pia kuna jambo hapa, sasa kama alipewa hishma hiyo na wafuasi wake kwa taratibu za imani yao, Iweje basi wawepo watu wa kuhoji u-saint wa Nyerere anaotaka kupewa na watu wa imani yake?
Hakuna double standard kwa mtazamo wa haraka tu.

Mwisho, Sheikh kuitwa mnafiki na msaliti si tusi, kama lingekuwa tusi linalowaumiza basi msingezunguka duniani mkimsema Nyerere kuhusu viarago na pesa za vitoweo.

Kama lingekuwa linaumiza basi msingemvunjia hishma kwa kusema Laanatullah kila anapotajwa, wala asingeitwa habithi, baradhuli, mnafiki n.k.

Kwanini udhani kuwa sheik Amir anastahili hishma kuliko Nyerere wote wakiwa wanadamu, wazee na familia zao?

Hapa ndipo nasema kila siku lazima watu waangalie nyuma, pembeni na mbele.
Kurushia watu mawe ukiwa katika nyumba ya glasi si jambo jema.

Kila mzee wetu aliyepigania nchi hii na apewe heshima.
Tuache uchochezi usio na maarifa

Hii inaitwa fitna al maarifa kama anavyosema ndugu yangu Gombesugu.
Tuache haya tuangalie jamii inakwenda wapi, inahitaji nini, tufanye nini kwa pamoja na si kwa chuki na kubaguana.

Hapo mkuu umegusa kitu kikubwa sana!

Sasa tuwahoji hawahawa wanaohubiri kuwa Shehe Hassan Bin Amir wamempa heshima kufatana na imani yao, iweje leo Nyerere anapotaka kupewa heshima na kanisa la imani yake wanaibuka na kupinga?

Labda hawajui mipaka ya imani yao! Wanataka kuwapangia wakatoliki mtu wakumpa heshima!
 
Ndugu yangu Jasusi

Mimi ningekuomba hiyo mada ya Mwalimu Nyerere na familia yake muiache,

Inatuondoa katika uwepo nakutufanya tutake kuongea kitu!

Tutulie kwenye lengo la uzi huu
 
Sheikh Farid, ahlan wahsalan muungwana.
Sina chuki na wzn kwasababu nikiwachukia lazima nianzie katika familia yetu.
Ninachofanya ni kujibu yale ambayo wznz wamekuwa wanasema miaka nenda rudi.
Wakatuita Makafir ndiyo maana tukakubali na ndio maana ya hiyo cc, kwamba ukitoka bara ''hilo chogo la kuja,kaafir huyo'' Wakatuita wanyonyanyaji, wakasema sisi wezi tunawaibia na kila aina ya fitna.

Leo Watanganyika wanaweka kila kitu mubashir mnaona ni chuki au matusi. Chuki kaanza nani?
Pili, muungano wa Nyerere ulikuwa wa Pan Afrika na ukichagizwa na nguvu ya pamoja kudhibiti madhara ya cold war pia.

Nia ilikuwa kuendelea kwa pamoja tukijisahihisha hadi kuridhiana.
Wznz wakageuza kuwa ni mradi, kila wakitaka jambo tishio tunavunja muungano.
Sasa hivi Watanganyika wanasema wala hamna haja ya kusema ondokeni tu! hata kuaga msiage mtume twitter mkishateremka Malindi.

Sasa yanazuka madai ya kugawana. Kwamba watu wagawane kisichokuwepo. Wewe una sh 24 mwenzako 1498 halafu unataka mgawane sawa. Hata hizo 24 hukuziweka katika mchango. Unadai nini kama si upungufu wa fikra.
Hatutazuia begi la mznz, lakini hakuna atakayeondoka na kingine! njia nyeupeee

Kuhusu utegemezi, ah ndugu yangu si tumeweka kila mnachotegemea?
Jana tu mumeomba mkatupe ngano bara maana hamna eneo, huo si uetegemezi.
Unaposoma bure wakati mwenzako analipa mkopo, huo si utegemezi

Nadhani ujibu kwa nukta moja hadi nyingine ukionyesha wapi si utegemezi, vinginevyo Yericko kasema mtoto aliyebebwa ana viwembe sasa ni wakati tumtue atembee mwenyewe.

Mkuu Nguruvi3,

Kuitwa Kaafir si neno la kukufanya ww usikitike napata tabu kulitafsiri neno hili kila mara lakini sitachoka kulitafsiri (Kaafir ni kiarabu na Kiswahili ni mpingaji na English ni Protestant ama non muslim) lakini kwanini tunatumia neno hilo,kwasababu mtu yoyote ambaye ni kinyume cha uislamu anakua ni non muslim bora nitumie term hiyo kuliko kutumia neno kaafir.Halafu wakristo walokuwepo mwanzo zanzibar walikua ni watu wastaarabu sana walikua hawana haja ya kututaka tusilimu na kutuwekea makanisa kila sehemu hawakua na haja hiyo lakini wanaokuja saivi dah we acha tuu.

Nafikiri utakua huna mashaka na neno hilo tena hata kama mtu atalitumia kwako.

Kuitwa machogo hata na sie si nawaona na nawasikia wengi wanatuita vichwa pasi mbona sisi hatujali tafuna tuu mkuu.

Kuhusu wazanzibar kufanya mradi kwamba tukitaka hela tunavuta kapu tuu sijaliona hilo unless unaushahidi kamili ndo uweze kuongea na kutishia kutoka kwenye muungano hatutishi yaani tuko serious tena sana na harakati hatukuzianza sisi nikupe mfano Karume Jnr alivyotaka kukata uhusiano na nyinyi kenda na maji Jumbe jela ya ndani Salmin Amour Commandoo wa udongo kapona chupuchupu sasa kwa akili ya kawaida nani anautaka muungano hata kama haumpi faida lakini anautaka kwa hali na mali na hakuna na wala hajatokea raisi watanganyika alotaka kuuvunja muungano.

Mkuu juzi ndo maana nikaweka mfano wa Scotland ukitizama budget ya UK nikubwa sana na ukitizama mchango wa Scotland ni mdogo sana kwa UK na bado wanataka kujitoa wanasema kua indepent ni bora kuliko kua na UK na bado mchango wao ni mdogo sana.Halafu inaendana na population ya watu kwa kuchangia katika mfuko wa muungano sasa unataka tuchangie 100 billion wakati population iko 1.1 million tena hakuna viwanda zanzibar hamna ukulima kama zimbabwe wenzetu ama south africa kikubwa kinachoingiza hela ni bandari kama visiwa vingi vinavyofanya duniani.

Na katika kuchangia jamani michango ninayoiona ni ya SMT na si ya Tanganyika kama ni tanganyika iko wapi ya SMT je Tanganyika inachangia ngapi katika mfuko wa SMT yetu sisi 24 yenu ngapi utanambia Tanzania bara ndio Tanganyika jee Budget ya SMT iko ngapi munajichanya tuu kama tuliwaita ni wizi ama wanyang'anyi basi naona inaanza kuthibitika.

Hatuhitaji kuzuiwa ngoja muungano ukatike tuu utajua na hata watakao baki mukitaka mutawaondosha wenyewe sisi ni wakarimu sana mukitaka mutakaa mukitaka mutaondoka mulikuwepo mwanzo hatutakufukuzeni saivi
 
Mwenye access na radio heri 104.1 Mohamed Said, yupo hewani anaelezea maisha ya Ally Sykes.
 
Last edited by a moderator:
Mwenye access na radio heri 104.1 Mohamed Said, yupo hewani anaelezea maisha ya Ally Sykes.
 
Last edited by a moderator:
Sideeq; Nina uhakika Jokakuu atakujibu vizuri zaidi. Mimi kesho wakina Waryoba wakileta tu kipengele cha kupigia huu Muungano Kura, Sheikh wangu mimi nawatema Zenj. Huko kwenye mahesabu ya BOT wala sipo. Langu mimi ni kuwa kuishi na jirani tunalaumiana na kujuta ku-share nyumba kheri kila mtu atafute chumba kwingine.

Mkuu

Unasubiri kesho sisi tumeanza tangu ulipoa sisiwa endelea kusubiri tuu watakupa
 
Wana Baraza na Ndugu zangu katika Mnakasha huu..
Sina shaka kuwa jina la field marshal John Okelo si geni masikioni penu. Historia inayofundishwa darasani haimtaji kabisa mtu huyu. Nilitaka nami kumpuuza tu, lakini nimepitia pahala pameandikwa jambo zito na la kutisha likimwelezea Okelo pamoja na Baba wa Taifa. Tafadhalini sana, kwa wale wanaoweza kutupa historia ya huyu bwana na kugusa yafuatayo watusaidie ili niweze kukileta kwenu hiki kinachoniduwaza hapa..
1. Huyu John Okelo alikuwa ni nani?
2. Alihusikaje na siasa za Zanzibar?
3. Alipata wapi suport ktk utendaji wake?
4. Alifaidika vipi na mapinduzi aliyoyasimamia?
5. Alikuwa raia wa wapi?
6. Alikwenda wapi baada ya mapinduzi?
7. Yu hai hata sasa au alikwishatangulia mbele ya hak?
8. Kwanini historia rasmi ktk maskuli haimtambui kama inavyomtambua Karume na wengine?
9. Kwanini John Okelo hajawekwa kama msingi wa mapinduzi ya zanzibar?
Kwenu wana jamvi.
C.C Mohamed Said, Yericko Nyerere, Ritz, Gombesugu, Jokakuu, Mag3, Bigshow na wote humu..
Timothy Peter Thomas, nitakujibu japo kwa ufupi kwani naamini kama umeufuatilia huu mjadala toka mwanzo wake, majibu mengi ya maswali yako yapo humu humu. Hata hivyo kwa kukusaidia;

Field Marshal John Okello ndiye aliyeyaongoza mapinduzi ule usiku wa tarehe 12 January 1963, mapinduzi yaliyomfungasha virago Sultani Sayyid Jamshid bin Abdullah Al Said, kiongozi mkuu wa serikali ya Zanzibar. Okello ndiye alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Mpinduzi na hata baada ya kumtangaza Karume kama Raisi kupitia chama cha ASP, alibaki kama msemaji mkuu wa serikali. Baada ya wiki moja tu vitendo vya Okello vilianza kumfadhaisha sana Karume pamoja na viongozi wengine wa serikali lakini ikawawia vigumu kuchukua hatua kwani Okello alikuwa na wafuasi waliokuwa tayari kumlinda kwa gharama yoyote ile. Kujaribu kumweka kando akiwa bado kwenye ardhi ya Zanzibar kungeweza kusababisha machafuko makubwa ambayo pengine yangeuangusha serikali ya Karume.

Mpango ulisukwa na kuna wakati Karume alitaka hata msaada wa Jomo Kenyatta, Raisi wa Kenya, amkamate Okello alipozuru Kenya katikati ya mwezi wa pili lakini mpango huu haukufanikiwa. Baadaye Okello na Karume walisafiri pamoja kuja Dar es Salaam kwa mwaliko wa Mwalimu Julius Nyerere ambaye pia wakati huo hakuwa anafurahishwa na vitendo vya kikatili alivyoendesha Okello. Bila kujua Okello alikubali huo mwaliko lakini baada ya kufika Dar es Salaam alizuiliwa na hakuweza kurejea Zanzibar. Kilichofuata ni namna ya kuwatuliza wafuasi wake ambao walianza kuonesha wasi wasi kwa yaliyompata hivyo ilibidi mbinu isukwe jinsi ya kupooza mambo.

images

Kazi ya propaganda ya kufuta nyayo za Okello zilianzia hapo na kazi hiyo alikabidhiwa Abdulrahman Babu ambaye tarehe 23 Machi 1964, alianza rasmi kazi hiyo. Babu alidai redioni kuwa Field Marshal John Okello siyo tu hakuongoza mapinduzi ya Zanzibar bali alikuwa ni moja tu katika watu waliofanikisha mapinduzi. Hizi zilikuwa ni jitihada katika kupambana na umaarufu wa Okello kama kiongozi mkuu wa mapinduzi na kuwashawishi wafuasi wake kwa kuwaahidi waliokuwa wapiganaji wake ajira ndani jeshi la wananchi lililokuwa linaundwa. Walifanya jitihada sana kufanikisha hili lakini hawakuweza kufuta vielelezo vyote kama picha zake na sauti yake, hizi zipo mpaka leo.
 
Last edited by a moderator:
Asante sana mkuu Mag3 kwa ufafanuzi murua!

Bila shaka ndugu yetu Timothy Peter Thomas ameelewa!
 
Asante kwa maelezo murua kabisa ndugu yangu Mag3. Nipo hapa tangu siku ya kwanza kabisa ya mnakasha huu, jina la Okelo halijapata nafasi kabisa. Umenisaidia kujua pa kuanzia, barikiwa sana kaka.. Ningefurahi sana kama ungepata nafasi ya kuyajibu maswali yote kwenye swalh langu msingi, kipengele hadi kipengele..
 
Timothy; Tulihangaika na hii mada sana kama wiki mbili tuu nyuma. Jaribu kupitia threads za nyuma utaikuta. Go kama 40 pgs back. Kwa kuongezea alichokupa Mag3 kuna hii video ya siku husika;

https://www.youtube.com/watch?v=-sMDkCSC_5g
 
na iwe hivyo mkuu, babu yangu kule lushoto alitembea kwa miguu umbali mrefu, toka mlalo hadi Tanga mjini katika harakati za kudai uhuru leo useme wazee wako wa new street ndo waliotuletea uhuru........!!!!!

Zumbemkuu,
Ikiwa babu yetu alifanya juhudi hizo hilo ni jambo zuri na yeye anastahili sifa
kama wanazopata wote waliopigania uhuru.
 
jasusi na barubaru; jamani nawaombeni kuwa iacheni hii mada hasa ya watoto wa marehemu nyerere mimi naiona ni too intrusive kwenye private life ya a child. Jasusi nakusihi just stop the cycle of answering yaishe. Barubaru congratulations for your achievements

Ukisha kuwa kiongozi wa umma hakuna cha Private life tena! ndio maana aliyekuwa Rais wa Marekani Clinton habari zake za kumpapasa papasa Dada Lewinsky ziliwekwa hadharani na dunia nzima tukapashwa! mwangalie Beliskoni wa Italy!

Back
Top Bottom