Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Ndugu yangu,

Kuna haja gani ya kutukana kiasi hicho?

Hoja zipo wazi anaetakiwa kuzijibu ni Mohamed Said, lakini ikiwa unaweza kuzijibu waweza kujibu hoja tu na sio kumjadili mleta hoja!


Ndio,wewe si unajifanya unazijua sana sheria za JF zaid ya watu wote humu?wewe si ndie kinara wa kukimbilia kwa mods na kuwareport watu wapigwe ban??

Haya sasa Kimbilia kwa Invisible kamwambie THE BIG SHOW kakutukana kakuita mpumbavu,na uombe nipwewe BAN then jibu atalpkupatia uje hapa utujulishe,,

Yericko,let me give you a piece of an advice,Dont Try to be A Hero...!!,we ni mweupe sana,na wala huna unalolijua na usipatwe na kiburi ukadhani watu wapo hapa kukusoma wewe,

Labda kuhusu hilo la kuacha hoja na kukujadili ni wewe mwenyewe umekaribisha kujadiliwa,

1.Uchochez wa Moh Said haujauonesha,zaid ya upumbavu tu ulioweka pale,,

2.Kuikimbila nasaba isiyo yako na kuja nayo hapa jukwaani bila haya,bila aibu,tukakuhoji uhalali huo umeutoa wapi??

Ukaja na majibu yako ya kichefu chefu eti ya kwamba hawa wote ni wazee wako,ya kwamba Nyerere,kingunge,warioba,butiku.Ally sykes n,k n,k,hawa wote ni wazee wako,,,


Tukakuuliza tena,sasa kama hao wote ni wazee wako ikawaje sasa ukachukua jina la mzee mmoja tuh Nyerere kuja nae jukwani kujiverify nae kwamba ni nasaba yako??


Kwa maana hata wanafamilia wa nyerere wanakanusha kukufaham,tukakuhoji sasa wewe ni yericko bin nani??


Yericko bin BUTIKU??,,kimyaaa,,


Yericko bin Ally sykes??,Kimyaaa,,


Yericko bin Kingunge ngombale mwiru??,,kimyaa,,

Umeng'ang'na yericko nyerere,yericko nyerere na haitoshi upo hapa 24/7 kumtetea kwa hoja zisizo na mashiko,,,

Yericko status haiwez patikana kwa style hiyo hata siku moja,

Kaa ukijua ya kwamba umejidhalilisha sana,na umeushusha sana utu wako,

Sisi tunakupa pole sana....
 

The Big Show bado hujamuelewa huyu jamaa "UBONDIA ANAUTAKA LAKINI ANAOGOPA MANUNDU" sasa sijui ataupataje ushindi!
 
The Big Show bado hujamuelewa huyu jamaa "UBONDIA ANAUTAKA LAKINI ANAOGOPA MANUNDU" sasa sijui ataupataje ushindi!


Atafute wa kupimana nae nguvu,Moh Said si size yake hata kidogo...

Yeye anaweza kule tunakotoa toa povu na makamanda wenzetu wa M4C na sio historia ya nchi hii,

Anajidhalilisha tuh....
 

Barubaru; kama sikuelewa vizuri maudhui ya ujumbe wako samahani ndugu yangu nilidhani kauli ilikuwa ya kati ikimhitaji Yericko kuwa na subira na ikimrai Gomgesugu kuona umuhimu wa kuyamaliza kindugu. Niwie radhi ndugu yangu kwa kutoelewa ulimaanisha nini. Pia samahani kwa usumbufu ulioambatana na kosa lenyewe.

Ama kuhusu Yericko na MS, naamini wana muda wa kuwatosha kuweka majadiliano haya kunakostahili. Kwa sasa naona kama yanapoteza dira. Ndio maana nimetoa rai rai kuwa kama tuhuma zipo basi zijibiwe na watu wazijue, lau kama mtuhumiwa hana la kujibu pia ijulikane. Kwa mwelekeo huu tulionao nadhani hatupo tena kwenye mada husika.

Kuhusu darsa kama ulivyosema pana fursa ya watoa mada kufungua thread husika ya kuelimisha umma juu ya mada hiyo na pia tukachangia na kujifunza.
 

Mkuu Mods hawafanyi kazi kwashinikizo la mtu bali husimamia sheria

Ukiona umeadhibiwa na Mods, jua wazi umevunja sheria za jf!


Ama kuhusu mimi kujadiliana Mohamed Said hilo kwangu halina tija, bali tija hasa ni kuona Watanzania kama wewe waliopotoshwa na Mohamed Said wanarudi kundi na kujua zaidi historia ya nchi yao takatifu!
 
Mbona amekueleza vizuri kama upumbavu ni tusi basi ban ianzie kwa invisible kapate kwanza glass 3 za maji upunguze jazba.
Haitoshi kumuita mtu mpumbavu bila kuonesha upumbavu huo kwa hoja, nyie mnamwita mpumbavu mtoa mada kwa ushabiki wenu tu, lakini hamuoneshi upumbavu huo uko wapi! soma tena haya mapovu ya jamaa yako na utuoneshe hoja iko wapi;
 
Hoja inayo jadiliwa hapa ni uchochezi wa maandiko ya Mohamed Said. Wewe unatokwa povu juu ya jina na nasaba ya Yericko Nyerere! na bado unataka tukuite wewe ni msomi na Great Thinker wa JF! unaonaje ukibaki msomaji tu na ukaendelea kufyonza ilm na sumu ya ustaadh Mohamed Said?
 
Tumeleta balua ya mechi tumeupenda mchezo wenu, msitambe tambe Temeke mje mtambe na Kaliakoo!
 

Ndugu yangu Gwalihenzi

Ni jambo la kushangaza sana ikiwa hawa ndugu zetu wanajiita ni Great Thinker

Badala yakujibu hoja wao wanashambulia watu,

Lakini ndio hivyo tutafika tu na historia itabaki huru bila kuchafuliwa!
 

Wanaukumbi, huyu Yericko Nyerere, kaongea mengi sana lakini ni uongo tu mimi siwezi kukaa kimya bila kudadavua bayana zake JF inasoma kwingi.
2.Kitabu hicho mimi nakikosoa kuwa kinamapungufu mengi,

Mifano ya mapungufu hayo ni kama,

A) Malima kuanzisha Namba za mitihani (get exact dates when the Ministry started this) utakuta ina -predate Malima kuwa pale ministry (this is easy)
Wanaukumbi haya maandishi aliyoandika Yericko hayamo kabisa kwenye kitabu cha Mohamed Said, kwa faida ya wanaukumbi hawaambie ni ukurasa wa ngapi kuna hiyo habari ya Kigoma Malima...ninacho-quote ni maneno yake baadae wasije kusema nafanya spinning.
B) Madai mengine katika maandishi ya Mohamed Said juu ya elimu nchini nikuwa hata hatua ya Mwalimu Nyerere kutaifisha shule za kidini ili kila mtanzania asome (analysis yake) analaumu kuwa hatua hiyo haimkumsaidia mtoto wa kiislamu
Wanaukumbi huu nu muendelezo wa uongo na uzushi haya maneno hayamo kwenye kitabu cha Mohamed Said, kwa faida ya wanaukumbi wafaamishe ni ukurasa wa ngapi hayo maneno yapo.
Wanaukumbi hebu hapa chini tumsome Nyerere mwenyewe halafu tutafakari kidogo kweli mtu ulikuwa kiongozi wa TAA Tabora lakini humjui Katibu wa Taifa jina lake, kwani wakati Nyerere anaondoka kwenda kusoma aliwaacha kina nani viongozi wa TAA.
Wanaukumbi mpaka hapo nadhani mmeona uongo wa Yericko Nyerere, naendelea kudadavua bayana zake.
 
Wanaukumbi watu wana haki ya kuhoji kutokana na maneno ya Yericko, yeye anajinasibisha na Juius Kambarage hebu hapo chini msomeni Yericko.
Mimi Mwalimu Nyerere kama Baba yangu mzazi, nakufahamisha tangu sasa kuwa Chifu Marealle alikuwa mfadhiri wa Mwalimu Nyerere (kiuchumi)

Wanaukumbi sijaongeza kitu wala kupunguza kitu hayo ni maneno ya Yericko mwenyewe mtaamua wenyewe, mimi nadadavua tu hizi bayana.
 
Yericko Nyerere,

Usikimbie njoo twende sawa leo mimi na wewe tu. bado kuna bayana zako nyingi zinaitaji majibu.
 
Last edited by a moderator:
Yericko Nyerere,

Nakusubiri kama umeshindwa kujibu waambie wenzako wakusaidie kuna mipini nimekuandalia hii naifanya kwa kumuenzi ndugu yetu gombesugu,
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu Gwalihenzi

Ni jambo la kushangaza sana ikiwa hawa ndugu zetu wanajiita ni Great Thinker

Badala yakujibu hoja wao wanashambulia watu,

Lakini ndio hivyo tutafika tu na historia itabaki huru bila kuchafuliwa!

Yericko; Shukran
Naona tunarudi main stream kwenye mada. Nipo kwenye hawa wanaoitwa Wamakonde wa Kipumbwi walioipindua serikali ya sultan zenj kwa msaada wa Julius Nyerere. Hofu yangu ni kuwa likiachwa kama lilivyo, mabwana hawa (Wamakonde)wataonekana kama wahuni tuu waliovamia nchi ya watu na kuiondoa serikali yao madarakani kumbe wao walikuwa askari tuu. Hii haitakuwa haki ukizingatia mchango wao katika kuleta historia mpya Zenj. Kwa kiwango cha chini kabisa inatakiwa kutowaonyesha aina yoyote ya dharau kutokana na nasaba zao.

Sasa, kwa vile sio kila "Makonde aliyeshiriki Kipumbwi" ataandika "kitabu" cha kuinasua nafsi yake na tuhuma au dharau zinazolundikwa juu yao, na ikizingatiwa kuwa wamiliki wa mapinduzi haya kikubwa ni ASP (hawajawahi kukana mapinduzi haya na bado wanayaenzi) na inaelekea Nyerere alijitolea kuwapa msaada wa kujikwamua na dhiki yao (yeye na Karume walijua kwa nini wasaidiane kwenye hili) hapa nina maswali yatakayohitaji majibu;

(i) Hivi, ASP waliomba au walilazimishwa msaada na Julius Nyerere kuhusu mapinduzi haya? Hii ni muhimu kujua nani mwenye dhamana nayo.

(ii)Nani aliyejenga sababu za mapinduzi haya huko Zenj na kwanini? Iwekwe wazi pia na ushahidi tunauomba

(iii)SMZ wanawachukulia vipi washiriki/askari waliweka maisha yao hatarini kwenye mapinduzi haya?

(iv) Kuna yeyote anayesema haikuwa halali wao ASP kupinduwa ile serikali ya sultan? atoe msimamo wake na sababu ili utafutwe msaada hata wa SMZ tujibiwe

(v)jee nasaba ya askari aliyeshiriki kupinduwa ina umuhimu? (km, askari wangekuwa ni wagunya/wacomoro ingeleta ahueni?)

Hii naiona ni muhimu kwa vile moja kati ya dondoo zako za tuhuma umeeleza kuwa Mzee MS hayuko bayana juu ya Mapindizi haya

cc Mohammed Said
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…