Swali zuri sana mdau, nasubiri jibu la mwanazuoni
Hapana siwezi kumchukia mtu tu kwa kuwa dini zetu ni tofauti.
Siwachukii Wakristo.
Kwa hili wala sina haja ya kusema sana.
Pitia nyuzi zangu zote.
Nawataja Wakristo kwa utambulisho tu.
Uislam haufunzi chuki.
Waislam tumefunzwa kukaa kwa hisani na wasio Waislam.
Unajua ni nani aliyempokea Nyerere Dar es Salaam?
Abdulwahid Sykes.
Unajua ni nani alimfanyia kampeni Nyerere asipate upinzani katika
TANU kutoka Waislam kama Schneider Abdillah Plantan,
Sheikh Suleiman Takadir, Mashado Ramadhani Plantan, Saleh Muhsin na
wengine wengi?
Mufti Sheikh Hassan bin Amir.
Unajua ni akina nani walipambana na Kanisa Katoliki Jimbo la Kusini ili
liwaachie Wakristo wajiunge na TANU?
Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Suleiman Masudi Mnonji, Shariffa biti Mzee, Salum Mpunga, Yusuf Chembera.
Unajua nani aliongoza kampeni dhidi ya Sheikh Suleiman Takadir alipompinga
Nyerere kwa Ukristo wake 1958 katika Halmashauri Kuu ya TANU?
Idd Tulio.
Unajua nani alimpeleka Nyerere kwa Sheikh Mohamed Ramia Bagamoyo,
Idd Faiz Mafongo na Idd Tosiri.
Unajua rafiki zake Nyerere wakubwa wakati wa kudai uhuru vijana wenzake walikuwa
akina nani?
Abdu na Ally Sykes na Dossa Aziz.
Unajua wazee gani walimhakikishia maisha yake Nyerere wakati wa 1954 - 1961?
Mshume Kiyate, Mwinjuma Mwinyikambi, Mohamed Jumbe Tambaza, Said Chamwenyewe.
Unajua shoga wa Mama Maria Nyerere Dar es Salaam walikuwa akina mama gani?
Tatu Biti Mzee, Mwamvua Biti Masha, Hawa biti Maftah, Titi Mohamed, Mwalimu Sakina
Biti Arab.
Imekuwaje leo.
Kimepita nini leo.
Mimi Mohamed Said
Mjukuu wa Salum Abdallah
Mmoja wa wanachama wa AA na Al Jamiatul Islamiyya
Leo anatoka mtu ananiuliza kama nawachukia Wakristo.
Nini kimempelekea yeye kuhisi kuwa kuna chuki baina yangu
na Wakristo?
Wakati June 1953 katika mkutano wa siri wa TAA Tabora babu yangu
kampa fedha Germano Pacha aje Dar es Salaam katika mkutano wa kuasisi
TANU amuwakilishe.
Na Germano Pacha alikuwa Mkatoliki wa Kipalapala.