Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Nadhani hapo juu umedadavuliwa vya kutosha katika sakata la Baraza la Mitihani kwamba limekua kama PAROKIA la Dini fulani, sasa kwa matokeo kama hayo yanayoendelea kutolewa na MOEVT, wewe ukiwa kama MKIRISTO na kwa mfano Baraza hilo lingelikua limesheheni Waislamu kama lilitapika Wakristo sasa; je kwa upande wako wewe ungejenga dhana gani? Na je kwa mfano ungelikua unalilalamikia Baraza hilo (ambalo lingekua limerundikiana Waislamu) kungekua kuna makosa?

Ingelikua upo makini katika kusoma hoja na majibu yanayotolewa usingelithubutu kuweka utumbo kama huu hapa![/QU

nyie waislam sikuzote huwa mnaonewa hakuna siku ambayo mmetendewa haki. kusoma wavivu mmekazania kwenye elim ahela mh! mtakuwa wamwisho kila siku.
 
Ungeweza kuniuliza vyuo nilivyoalikwa kuhadhiri bila hata ya kunitukana na kunikejeli.
Nami ningekujibu kiungwana na tungeendelea na mjadala. Kuanzia hapa usishangae ukioona nimekupuuza sikujibu kitu.
............

Asante sana kwa majibu mazuri, japo sipendezwi kwa tabia yako ya kiimla!

Majibu yako haya yamekuwa tofauti na majibu yako ya awali!

Lakini yanazaliwa maswali ndani ya majibu yako!

A) Mapokeo ya wahadhiriwa wa kuhadhiri kwako yaliuwaje?

B) Thibitisha uhalali wa maneno yako kuwa kitabu chako sasa ndicho chenye mamlaka ya historia ya uhuru wa nchi hii na si kile cha TANU
 
Mmm, naanza kuhisi kwamba kumbe wote tunatakiwa tuwe Wakristo cause ndio dini yenye nguvu, kwanini kila sehemu Waislam ni watu duni hivi? Je? mungu wao hana nguvu kama Mungu wa Wakristo? rejea maswali yalioulizwa kwa bwana mohamed said hapo juu, kwani Somalia nchi yenye waislam wengi lakini ni nchi duni isio hata na amani, nenda Nigeria kaskazini kule kwenye waislamu wengi, kote huko ni sehemu masikini kweli na duni hasa, niliona siku moja kwenye Emmanuel TV, TB Joshua anawapelekea misaada ya chakula na mavazi, hali za watu wale kwakweli ni za kutia huruma sana, yaani masikini wa kutupwa, kitu cha ajabu sana ambacho hua siwaelewi nyie waislamu hua ni hiki, utakuta mtu hana hata pesa ya kununulia Kandambili au Viatu, lakini huyo huyo anazo pesa za kununulia silaha za kuwaulia Wakristo, hapo hua sielewi kabisa, back to the topic, tusipo angalia tutakuja potosha Historia hivihiv, naona humu kuna watu wanaanza kuaminishwa kuwa Hospitali za Makanisa zimejengwa kwa msaada wa MOU, hivi MOU imesainiwa lini na hizo Hospitali zimejengwa lini, kwa kumbukumbu zangu, Bugando kwamfano, ukienda pale kwenye jengo lao utakuta imejengwa 1971, sijui hasa ujenzi uliianza lini lakini mwaka huo ndio hospitali ilianza kufanya kazi, waislamu mlikuwa wapi? KCMC, nimekua naisikia, KOlandoto Hospital ipo tokea miaka ya 60 huko, Peramiho kule Songea, tokea nikiwa mtoto mdogo kabisa, Ilembula Hospital kule Iringa (Sasa Njombe) ipo tokea miaka ya 70s, miaka yote hiyo watu wenye uwezo walikua wanaenda kutibiwa hospitali zilizokua zikiitwa za misheni.

Ukweli kinachowasumbua ndugu zangu waislam sio hayo madai, ni wivu tu tena wa kijinga, hakuna watu creative huko kwenu, angalia misaada mnayo itaka hata sasa, sio shule au hospitali, nyie mnadai mahakama ya kaadhi, hivi nyie mnajiona kuwa ni wafanya makosa sana au tusemeje? Pesa za kuendesha chuo cha Morogoro toka serikali mnapata, mbona chuo hakiendelei?, haya shule za Kiisalamu kama Jamuhuri Dodoma au ile ya Kinondoni, mnadai eti NECTA inawafelisha watoto, ngoja tuone kama ni kweli, haya na mitihani ya Mock ambayo waalimu husika ndio wanatunga na kusahihisha, matokeo yake huwa yakoje? Uvivu wa kufikiri nao sometimes ni msiba mkubwa kwenye jamii, Tafakarini!

mimi huu upuuzi huwa sisomagi nasoma comment tu huku napata coke bariid........unajua mbwa ukimjua jina hakupi shida.
 
Mohamed Said,

Asante kwa majibu mazuri.
Kama una mda naomba uendelee kunielimisha machache kutokana na maswali ninayokuuliza. Naamini wapo na wengine watalaokuwa wanaelimika.
Inawezekana kweli hao wazee wetu (naamini ni wazee wa watanzania wote), walibaguliwa katika historia ya uhuru kwa sababu ya dini yao. Hata hivyo upo uwezekano sio kwa sababu ya dini pia, nikidhani kuwa pengine wapo hata wengine ambao hawakuwa waislamu ambao 'wamefunikwa'.
Naamini pia wewe kama muislamu una fahari kuwaenzi wazee wako waislamu. Swali langu dogo ni je, wewe kama mwanahistoria, huoni umuhimu wa kuandika pia historia ya hawa wazee, bila kuattach dini zao? Namaanisha kwamba ukatumia resources ulizojaaliwa kuwa nazo, na uwezo wako wa kuandika, na ukawaelimisha Watanzania historia ya uhuru, pengine bila ya kutaja sana dini? Nauliza hivi kwa sababu, kwa mtu ambaye ni radical kidogo, akisikiliza, au akisoma maandiko yako, anaona kama unaandika kwa ajili ya waislamu. Tutegemee kutoka kwako maandiko mengine ambayo yatataja wapigania uhuru bila kujali dini zao?

Umeniuliza swali zuri sana.

Hakika wapo Wakristo ambao walikuwa kwenye vile vita vya ukombozi wa Tanganyika.
Mimi nimewataja katika kitabu changu ingawa wamefunikwa (kutumia msamiati wako) katika historia rasmi huwaoni.

Wapo wale madaktari watano: Dk. Luciano Tsere, Dk. Michael Lugazia, Dk. Joseph Mutahangarwa, Dk. Wilbard Mwanjisi na Dk. Vedasto Kyaruzi. Hawa walifanya kazi kubwa katika TAA baada tu ya kumaliza masomo yao Makerere na baadhi kuja Dar es Salaam kuanza kazi.

Hawa walimtangulia Nyerere katika TAA New Street lakini hawatajwi.

Lady Judith Listowel katika kitabu chake ''The Making of Tanganyika'' (1965) kawapa jina kawaita ''Makerere Intellectuals.''

Historia rasmi ya TANU imewatoa hawa katika orodha ya wapigania uhuru huwaoni popote.

Lakini ifahamike kitu kimoja kuwa harakati za uhuru zilihodhiwa mahali pakubwa sana Waislam na mengi yalitendeka pale New Street ofisi ya TANU.

Mimi katika kitabu changu hawa wote nimewataja lakini kwa kuwa hakukuwa na kubwa la kusema na wakati wao ni ule wa awali kabla ya 1950 nimewaeleza kwa njia ya kupita tu.

TAA iliwaka moto kuanzia 1950 wakati wa uongozi wa Dk. Vedasto Kyaruzi na Abdulwahid Sykes kama nilivyoeleza katika kitabu changu.

Napenda kuhitimisha kwa kukufahamisha kuwa ni bahati mbaya sana kuwa wengi wanachomwa na ukweli kuwa Waislam ndiyo walipigania uhuru wa Tanganyika.

Huu ni ukweli wa historia na ni lazima usemwe kama vile huwezi kupinga kuwa ni Wakikuyu ndiyo walionyanyua silaha kupambana na Waingereza Kenya.

Kama kuna mtu anaweza kuja kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika na akadhani ataweza kuuficha ukweli huu wa mchango wa Waislam atashindwa kama alivyoshindwa Nyerere.

Leo kitabu cha historia ya TANU cha Kivukoni kimekufa. Hakuna mtu yeyote anaekiweka maanani.
Kwa nini?

Kwa sababu waliuogopa ukweli.

Mimi sikuogopa kusema ukweli kuwa Sheikh Hassan bin Amir ndiye aliyeongoza kampeni Nyerere akubalike kwa Waislam lau nilijua ninalosema ni jambo zito na huenda likaniweka matatani.

Mimi sikuogopa kusema kuwa kama sifa ya kuasisi TANU itakwenda kwa mtu mmoja tu basi tuanze na Abdulwahid Sykes si Nyerere.

Umeniluza kuwa naandika kwa ajili ya Waislam.
Kuwa naandika kwa Waislam khasa hilo ndilo lilikuwa kusudio langu.

Dhamira yangu ilikuwa kuadhimisha historia ya wazee wangu na kuonesha mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa nchi yetu.

Hao Wamarekani na wengine walikuja kuingia na kutaka kujua historia hii baada ya kuona kuwa kitabu changu kilikuwa na ukweli ambao ulifichwa kwa muda mrefu.
 
Kwa mara nyingine asante sana Dr kwa majibu mazuri. Japo mimi ni 'mtu wa sayansi' na kuna wakati nimekuwa napuuzia historia, hakika kwa kiasi fulani nimehamasika sasa kutafuta na kusoma historia za vitu fulani vinavyonihusu. Hata hivyo kwa kiasi fulani napatwa na woga kuwa inawezekana historia nyingi nitakazosoma zitakuwa 'zimechakachuliwa' pengine kwa maslahi ya watu binafsi.

Naomba nikuulize swali moja (pengine litakuwa la mwisho, lakini usijali kama utaona nimehamasika kuuliza mengine);
Kwa maoni yako unaona waislamu walidhulumiwa na wakoloni (wakristo), na pengine na watanzania wenzao ambao nao (au wengi wao), ni wakristo... hiyo ilitokea katika historia ingawa ninahisi (kutokana na kauli zako), kuwa unaamini kuna vitu vinaendea hadi sasa...

Swali; Je, unawachukia wakristo (kwa umoja wao au kwa makundi fulani)?
 
Swali zuri sana mdau, nasubiri jibu la mwanazuoni
 
OMBI

Tufanye juhudi kuwakomboa wale wote walio nyumakielimu Tanzania. Wako
wengi, kwa dini na makabila, lakini wote niWatanzania. Walio nyuma
wasiseme kuna uonevu, bali waondoe kilichowakwamisha.Hatuwezi
kulinganisha utamaduni wa elimu wa watu wa Kilwa,Mafia, Rufiji na
Pangani, na watu wa Moshi, Kyela, au mkoani Kagera. Tuwe wakweli.
Mwenyezi Mungu hapendiwaongo. Kwanini shule za binafsi hazina pia
waislamu wengi? Nani anawazuia waislamu kujenga shuleTanzania? Je,
kama kweli unataka mtoto wako apate elimu safi, naamekosa nafasi ya
shule ya serikali, utampeleka wapi? Pale Kinondoni Muslim? Tuseme
ukweli….

Naamini tunao uwezo wa kuyatatua matatizo yetu yakihistoria na
kitamaduni na si kukaa chini kupanga vurugu kwa madaiya kuonewa.
Waislamu wa Saudi Arabia hawajasoma licha ya utajiriwao. Je, hao nao
waziri wao wa elimu na baraza la mitihani ni yaTanzania? Mbona
waislamu wa Uturuki, Tunisia, Misri, Senegal na AfrikaMagharibi yote
wana elimu?

Tutafute chanzo cha kweli cha tatizo, halafu wotetushirikiane
kulitatua; wote kabisa.
 
Hicho ndicho Mohamed Said na wenzake hawataki kukisikia kabisa, bali wao ni wimbo wa dhuluma tu, tena wakimdhihaki Mzee Nyerere!
 
OMBI

Tufanye juhudi kuwakomboa wale wote walio nyumakielimu Tanzania. Wako
wengi, kwa dini na makabila, lakini wote niWatanzania. Walio nyuma
wasiseme kuna uonevu, bali waondoe kilichowakwamisha.Hatuwezi
kulinganisha utamaduni wa elimu wa watu wa Kilwa,Mafia, Rufiji na
Pangani, na watu wa Moshi, Kyela, au mkoani Kagera. Tuwe wakweli.
Mwenyezi Mungu hapendiwaongo. Kwanini shule za binafsi hazina pia
waislamu wengi? Nani anawazuia waislamu kujenga shuleTanzania? Je,
kama kweli unataka mtoto wako apate elimu safi, naamekosa nafasi ya
shule ya serikali, utampeleka wapi? Pale Kinondoni Muslim? Tuseme
ukweli….

Naamini tunao uwezo wa kuyatatua matatizo yetu yakihistoria na
kitamaduni na si kukaa chini kupanga vurugu kwa madaiya kuonewa.
Waislamu wa Saudi Arabia hawajasoma licha ya utajiriwao. Je, hao nao
waziri wao wa elimu na baraza la mitihani ni yaTanzania? Mbona
waislamu wa Uturuki, Tunisia, Misri, Senegal na AfrikaMagharibi yote
wana elimu?

Tutafute chanzo cha kweli cha tatizo, halafu wotetushirikiane
kulitatua; wote kabisa.

Ahsante sana kwa fikra nzuri.
Nakuwekea hapa chanzo cha matatizo haya yanayotukabili hivi sasa ili ujue kwa nini Waislam leo wanatahadharisha serikali kuhusu dhulma dhidi yao:

Tarehe 5 Novemba, 1985 kabla hajastaafu urais, Nyerere aliwahutubia wazee wa Dar es Salaam. Hotuba hii ilijaa simanzi, Nyerere akikumbuka jinsi Waislam walivyompokea Dar es Salaam kwa mapenzi makubwa ingawa yeye alikuwa Mkristo. Wazee hawa wengi wao walikuwa wanachama wa zamani wa TANU waliomuunga mkono Nyerere wakati wa kudai uhuru. Nyerere aliusifia mchango wa Waislam katika kipindi kile kigumu cha kudai uhuru. Nyerere alisema kuwa upogo katika elimu uliorithiwa na serikali yake kutoka kwa Waingereza baina ya Waislam na Wakristo yeye ameuondosha katika kipindi cha utawala wake:
''Waislam wametupa nafasi kupitia sera yetu ya elimu, kurekebisha upogo. Sasa nipo katika hali ya kufarahisha kwa kuwa wakati mwingine sielewi kama Mbunge mpya, Waziri, au Katibu Mkuu katika wizara zetu za serikali, ni Muislam au Mkristo au hana dini labda pale jina lake la kwanza linapotoa utambulisho. Na hata hivyo hiyo siyo njia ya kuaminika kutoa utambulisho wa dini kwa kuwa tuna Wakristo wenye majina ya Kiislam, na Waislam wenye majina ya Kikristo. Kuvumiliana huku nyie ndiyo sababu; nilichofanya mimi ni kuzungumzia maadili haya kwa niaba yenu.''

Hotuba hii ilikuwa ya ulaghai. Ukweli ni kuwa miongo mitatu baada ya uhuru Waislam hawajanufaika chochote wako katika hali ile ile aliyowaacha wakoloni au mbaya zaidi. Sivalon amefichua kuwa Kanisa limeweza kujenga himaya yake ambayo inahodhi asilimia 75% za viti katika Bunge la Tanzania. Kati ya viti hivyo 75% vipo mikononi mwa Wakatoliki na vilivyobaki vimegawika kati ya Waislam na Wakristo wa madhehebu nyingine.[1] Baada ya kupatikana uhuru, Kanisa lilipohisi wasiwasi, limeweza kwa urahisi kabisa kuwazuia na kuwadhibiti Waislam. Serikali imeweza kutumia nguvu iliyokuwanayo katika kudhibiti siasa kuzuia harakati za Waislam kudai fursa sawa na Wakristo katika kugawana madaraka katika serikali. Kanisa limehakikisha kuwa kupinduliwa kwa ukoloni si kizingiti kwa Ukristo, ingawa ingetegemewa kuwa Kanisa lingedhirika kwa kuanguka kwa ukoloni. Katika miaka yake zaidi ya mia moja, Kanisa lilikuwa limestarehe kama muokozi wa nafsi na watu wenyewe. Kanisa lilikuwa salama na halikupambana na msukosuko wowote kutoka kwa serikali kwa kuwa lilikuwa Kanisa ndilo lilishika hatamu ya serikali.

(Kutoka ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...'')
 
asante sana kwa majibu mazuri, japo sipendezwi kwa tabia yako ya kiimla!

Majibu yako haya yamekuwa tofauti na majibu yako ya awali!

Lakini yanazaliwa maswali ndani ya majibu yako!

A) mapokeo ya wahadhiriwa wa kuhadhiri kwako yaliuwaje?

B) thibitisha uhalali wa maneno yako kuwa kitabu chako sasa ndicho chenye mamlaka ya historia ya uhuru wa nchi hii na si kile cha tanu

kwani amekulazimisha ukisome??toa hoja wapi kuna upotoshaji kwenye maandiko yake??
Hapa mchochezi na mwenye choko choko unaonekana ni wewe,,hueleweki hasa unataka nini,au unaenjoy kuona huu mjadala upo unaendelea,unachangiwa na wengi,muanzilishaji ni wewe n,k.,hueleweki ni hasa unataka,unatuchosha yericko,,

what the hell are you talking about??actions are by their intentions,so whats your intention mr??
 
Swali zuri sana mdau, nasubiri jibu la mwanazuoni

Hapana siwezi kumchukia mtu tu kwa kuwa dini zetu ni tofauti.
Siwachukii Wakristo.

Kwa hili wala sina haja ya kusema sana.
Pitia nyuzi zangu zote.

Nawataja Wakristo kwa utambulisho tu.

Uislam haufunzi chuki.
Waislam tumefunzwa kukaa kwa hisani na wasio Waislam.

Unajua ni nani aliyempokea Nyerere Dar es Salaam?
Abdulwahid Sykes.

Unajua ni nani alimfanyia kampeni Nyerere asipate upinzani katika
TANU kutoka Waislam kama Schneider Abdillah Plantan,
Sheikh Suleiman Takadir, Mashado Ramadhani Plantan, Saleh Muhsin na
wengine wengi?
Mufti Sheikh Hassan bin Amir.

Unajua ni akina nani walipambana na Kanisa Katoliki Jimbo la Kusini ili
liwaachie Wakristo wajiunge na TANU?
Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Suleiman Masudi Mnonji, Shariffa biti Mzee, Salum Mpunga, Yusuf Chembera.

Unajua nani aliongoza kampeni dhidi ya Sheikh Suleiman Takadir alipompinga
Nyerere kwa Ukristo wake 1958 katika Halmashauri Kuu ya TANU?
Idd Tulio.

Unajua nani alimpeleka Nyerere kwa Sheikh Mohamed Ramia Bagamoyo,
Idd Faiz Mafongo na Idd Tosiri.

Unajua rafiki zake Nyerere wakubwa wakati wa kudai uhuru vijana wenzake walikuwa
akina nani?
Abdu na Ally Sykes na Dossa Aziz.

Unajua wazee gani walimhakikishia maisha yake Nyerere wakati wa 1954 - 1961?
Mshume Kiyate, Mwinjuma Mwinyikambi, Mohamed Jumbe Tambaza, Said Chamwenyewe.

Unajua shoga wa Mama Maria Nyerere Dar es Salaam walikuwa akina mama gani?
Tatu Biti Mzee, Mwamvua Biti Masha, Hawa biti Maftah, Titi Mohamed, Mwalimu Sakina
Biti Arab.

Imekuwaje leo.
Kimepita nini leo.

Mimi Mohamed Said
Mjukuu wa Salum Abdallah
Mmoja wa wanachama wa AA na Al Jamiatul Islamiyya
Leo anatoka mtu ananiuliza kama nawachukia Wakristo.
Nini kimempelekea yeye kuhisi kuwa kuna chuki baina yangu
na Wakristo?

Wakati June 1953 katika mkutano wa siri wa TAA Tabora babu yangu
kampa fedha Germano Pacha aje Dar es Salaam katika mkutano wa kuasisi
TANU amuwakilishe.

Na Germano Pacha alikuwa Mkatoliki wa Kipalapala.
 
Ahsante sana kwa fikra nzuri.
Nakuwekea hapa chanzo cha matatizo haya yanayotukabili hivi sasa ili ujue kwa nini Waislam leo wanatahadharisha serikali kuhusu dhulma dhidi yao:

Tarehe 5 Novemba, 1985 kabla hajastaafu urais, Nyerere aliwahutubia wazee wa Dar es Salaam. Hotuba hii ilijaa simanzi, Nyerere akikumbuka jinsi Waislam walivyompokea Dar es Salaam kwa mapenzi makubwa ingawa yeye alikuwa Mkristo. Wazee hawa wengi wao walikuwa wanachama wa zamani wa TANU waliomuunga mkono Nyerere wakati wa kudai uhuru. Nyerere aliusifia mchango wa Waislam katika kipindi kile kigumu cha kudai uhuru. Nyerere alisema kuwa upogo katika elimu uliorithiwa na serikali yake kutoka kwa Waingereza baina ya Waislam na Wakristo yeye ameuondosha katika kipindi cha utawala wake:
''Waislam wametupa nafasi kupitia sera yetu ya elimu, kurekebisha upogo. Sasa nipo katika hali ya kufarahisha kwa kuwa wakati mwingine sielewi kama Mbunge mpya, Waziri, au Katibu Mkuu katika wizara zetu za serikali, ni Muislam au Mkristo au hana dini labda pale jina lake la kwanza linapotoa utambulisho. Na hata hivyo hiyo siyo njia ya kuaminika kutoa utambulisho wa dini kwa kuwa tuna Wakristo wenye majina ya Kiislam, na Waislam wenye majina ya Kikristo. Kuvumiliana huku nyie ndiyo sababu; nilichofanya mimi ni kuzungumzia maadili haya kwa niaba yenu.''

Hotuba hii ilikuwa ya ulaghai. Ukweli ni kuwa miongo mitatu baada ya uhuru Waislam hawajanufaika chochote wako katika hali ile ile aliyowaacha wakoloni au mbaya zaidi. Sivalon amefichua kuwa Kanisa limeweza kujenga himaya yake ambayo inahodhi asilimia 75% za viti katika Bunge la Tanzania. Kati ya viti hivyo 75% vipo mikononi mwa Wakatoliki na vilivyobaki vimegawika kati ya Waislam na Wakristo wa madhehebu nyingine.[1] Baada ya kupatikana uhuru, Kanisa lilipohisi wasiwasi, limeweza kwa urahisi kabisa kuwazuia na kuwadhibiti Waislam. Serikali imeweza kutumia nguvu iliyokuwanayo katika kudhibiti siasa kuzuia harakati za Waislam kudai fursa sawa na Wakristo katika kugawana madaraka katika serikali. Kanisa limehakikisha kuwa kupinduliwa kwa ukoloni si kizingiti kwa Ukristo, ingawa ingetegemewa kuwa Kanisa lingedhirika kwa kuanguka kwa ukoloni. Katika miaka yake zaidi ya mia moja, Kanisa lilikuwa limestarehe kama muokozi wa nafsi na watu wenyewe. Kanisa lilikuwa salama na halikupambana na msukosuko wowote kutoka kwa serikali kwa kuwa lilikuwa Kanisa ndilo lilishika hatamu ya serikali.

(Kutoka ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...'')
Ndiyo shukrani ya kutaifisha shule ili na wenyewe wasome...shule zisingetaifishwa sijui angepakwa vipi matope baba wa watu. Hivi huo upogo wa Elimu , Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete bado wanauendeleza?
 
Ndiyo shukrani ya kutaifisha shule ili na wenyewe wasome...shule zisingetaifishwa sijui angepakwa vipi matope baba wa watu. Hivi huo upogo wa Elimu , Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete bado wanauendeleza?

Baada ya kueleza hayo yote ni muhimu sasa kuangalia jinsi ukereketwa wa Kikristo unavyofanya kazi katika serikali na jinsi kazi hiyo inavyoathiri Uislam. Wizara ya Elimu inachukuliwa kama mfano kwa sababu ya umuhimu wake katika jamii. Katika wizara hii, inaweza kuonekana kwa uwazi kabisa jinsi Ukristo unavyofanya kazi na jinsi udini ulivyoshamiri katika kugawa nafasi muhimu kati ya Waislam na Wakristo.

Ilikuwa katika wizara hii katika historia ya Tanzania ndipo kwa mara ya kwanza waziri Muislam alipochaguliwa kuongoza wizara, Kanisa likaingilia kati waziwazi kumpiga waziri vita na kuhoji nafasi nyingine za juu ambazo zilipewa Waislam. Serikali haikuweza kupingana na Kanisa na waziri huyo, marehemu Profesa Kighoma Ali Malima aliondoshwa katika wizara hiyo.

Mwaka 1987 Profesa Malima aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu akiwa Muislam wa kwanza kushika nafasi hiyo. Mawaziri wanane waliopita walikuwa Wakristo. Kulikuwa na malalamiko kutoka kwa Waislam kuwa wizara hiyo imegeuzwa jimbo la Wakristo, hasa pale padri alipoteuliwa na Julius Nyerere kuongoza wizara hiyo.

Profesa Malima aliposhika wizara hiyo aliona upo umuhimu wa kufanya marekebisho kadhaa ili kurejesha imani ya Waislam katika wizara hiyo. Kulikuwa na tuhuma kuwa Wizara ya Elimu ilikuwa ikiwabagua vijana wa Kiislam kupata nafasi katika vyuo vya elimu ya juu na ilikuwa ikizuia kupanda vyeo kwa Waislam.

Profesa Malima alipoona dhulma ile iliyokuwapo katika wizara ile dhidi ya Waislam, Profesa Malima aliwateua Waislam wanne kushika nafasi katika kurugenzi mbalimbali na akaandika taarifa ya siri kwa Rais Ali Hassan Mwinyi [1]kumtaarifu udini [1] alioukuta katika wizara ile. Katika taarifa ile kwa rais,[1]

Profesa Malima alieleza kuhusu kudumazwa kwa Waislam katika mgao wa elimu. Taarifa hii ilivuja kwa vyombo vya habari[1] na kwa Wakristo wengine. Katika watu walioipata taarifa hii ni Rais Mstaafu Julius Nyerere wakati ule akiwa Mwenyekiti wa chama tawala CCM.
Kuwekwa kando kwa Waislam kupo wazi kiasi ya kuwa mtafiti haihitaji hata kufanya utafiti wa kina unaopewa nguvu na takwimu.

Mtafiti yeyote wa sayansi ya jamii hatoweza kushindwa kuona ukweli huu kwa macho tu. Hali hii inaonekana katika kila nyanja ya maisha. Utafiti wa kwanza katika tatizo hili la Waislam kudhulumiwa katika ugawaji wa madaraka ulifanywa na vijana wa Kiislam katika jumuiya yao iliyokuwa ikijulikana kama Warsha ya Waandishi wa Kiislam, kwa ufupi ikijulikana kama Warsha.

Kanisa kwa mara ya pili tokea mwaka 1963 ilipata wasiwasi kuhusu mabadiliko ambayo yalikuwa yanafanyika katika Wizara ya Elimu. Lakini katika miaka ya 1980, hali ya mambo yalikuwa yamebadilika sana. Waislam walikuwa wamejizatiti nje ya mfumo wa siasa kiasi ya kuwa hapakuweza kupatika kibaraka katika Waislam ambae angekuwa tayari kutumika kulihami Kanisa. Hali ya uhasama wa wazi kati ya Waislam na serikali ilikuwa imejitokeza wazi kabisa.

Hata hivyo mawakala wa kanisa katika serikali walimshutumu Profesa Malima kwa kuwa Muislam mwenye ësiasa kalií. Profesa Malima akatakiwa ahojiwe mbele ya Kamati Kuu ya CCM kwa kuingiza hisia za kidini ambazo zimesababisha uadui baina ya waumini wa dini hizi mbili. Suala hili likajadiliwa Dodoma chini ya uenyekiti wa Julius Nyerere.

Lakini badala ya kujadili suala la dhulma kwa Waislam na kulitafutia ufumbuzi, yule anaedhulumiwa ndiye aliyewekwa kizimbani badala ya dhalim anaedhulumu; msukumo wa mjadala ukawa katika uteuzi wa wakurugenzi wanne Waislam aliofanya Profesa Malima katika Wizara ya Elimu. Profesa Malima alionekana amekiuka mwenendo na taratibu zulizodumu katika wizara ile kwa kipindi kirefu ya kuwa ni Wakristo pekee wenye haki ya kushika nafasi za juu katika wizara za serikali.

Kwa ajili hii profesa Malima akavuliwa madaraka kama Waziri wa Elimu. Rais Mwinyi alikuwa hana uwezo wa kuhimili nguvu ya Kanisa. Nchi inayodai kuwa ni ya kisekula ilikuwa imeshindwa kwa mara nyingine kuwapa Waislam haki yao waliyohakikishiwa na katiba ya Tanzania.

(Kutoka ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...'')
 
Porojo za wazee wa Gerezani bado zinaendelea, duh...! Hakuna adui wa maendeleo kama porojo...kama kawaida kuna watu porojo ni jadi yao! Wanakula porojo, wanavaa porojo na wanalala porojo, kwao porojo na ukweli ni kitu kimoja.
 
Back
Top Bottom