Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Nafurahi kuona mwamko wa watanzania kulinda hadhi za wanaukombozi wetu na kuulinda umoja wetu,

Safari ya kuzima maasi ya kiroho ni ndefu na inahitaji busara sana, mwitikio wa watu katika uzi huu ni dhahiri shahiri watanzania waaunga mkono juhudi za mashauriano ya kuzima uasi unaoongozwa kiroho na akina Mohamed Said na kundi lake,

Watanzania wenzangu, tujikite katika mashauruano, tusijadili watu, kwakuwa kufanya hivyo ni kupoteza shabaha ya mashauriano haya.

Tunataka watanzania wenzetu wote wasioijua historia ya uhuru na harakati zake basi watumiejukwaa hili kuijua, hata wale waliopotoshwa na maasiya kiroho ya Mohamed nao warejee kundini mwa umoja wa kitaifa.

Mzee Mohamed Said akiwa kama baba yangu mzazi sitamnyamazia pale anapolifarakanisha taifa kwa ngano zake hasa akitumia mwito wa kiroho.
 
Ritz, kilio changu,

..Al-Azhar ilianzishwa mwaka 972 kama chuo cha kidini.

..kwa miaka mingi waliendelea na utaratibu huo, na wameanza kufundisha degree za ki-secular miaka ya 1960.

..Chuo Kikuu kikongwe kabisa Oman kinaitwa Sultan Qaboos Univ na kimeanzishwa mwaka 1986.
 
Last edited by a moderator:
naona umekaa kiushabikishabiki humu,kwanini usiende jipumzisha kule chit-chat???

Ushabiki upi mbona unamtetea wewe na mtoto wa kwanza wa Julius Kambarage tuamini nani? Andrew Nyerere anasema ni habari hizi ni mpya kwake amemwambia Yericko ataje mama yake nani swali dogo tu. Jibu basi wewe unayetetea.
 
Hili neno inasemekana alilotumia Mohamed Said umelifanya kichaka cha kukosa kwako eneo la kuteteaa uozo wa uongozi wa Nyerere na uchoyo wake na kuwa kwake kibaraka.Pamoja na hivyo hili neno linatumika sana katika heshima ya uandishi ambayo bila shaka kwako imekuwa nongwa kwa vile hunayo.Hata katika mazungumzo mzee akiponwa hatumwambii kwa uwazi kilichomtokea lakini huwa ni kweli tunajua ameponwa.
Tuje upande mwengine kwenye haya maandiko.Hebu hesabu idadi ya inasemekana na idadi ya matukio yaliyowekewa tarehe zake mengine yaliyotokea ndani ya ikulu ni yepi mengi.Mbona huna takwimu mbadala wa kukanusha aliyoyasema Nyerere kwa padri ndani ya ikulu juu ya njama zake za kuukandamiza uislamu?.
Usitudanganye. Hata mimi ni muandishi ingawa sijachapisha kitu. Tulifunzwa kuwa neno "inasemekana" ni hearsay. Na kama wewe ni mwandishi makini utafuatilia chanzo cha kusemekana huko na uthibitishe na ndipo itakuwa fact. Kwa mfano nikipewa tip na third party lazima niifanyie kazi hiyo tip. Nikisema "inasemekana" ni kwamba sina uhakika na kinachosemekana na kama ni mtafiti basi hujakamilisha kazi yako mpaka hilo linalosemekana lithibishwe. Hapa naona umeshamhukumu Nyerere kuwa kiongozi mbovu, mchoyo na kibaraka kwa kuamini tu yale yaliyosemekana. Aliyoyasema Nyerere mbele ya mapadri ni matter of public record lakini kwa watu wenye ajenda sishangai mkikimbia kupindisha ukweli ili kukidhi agenda zenu za inasemekana.
 
Ami tazama juu alivyokujibu wewe na tazama hapa chizi siku mbili tatu nyuma alivyonijibu mimi:

Kaka,
Mimi si mwandishi. Na si kila mtu ana kipawa cha uandishi. Lakini hilo halininyimi haki yangu ya kufichua upotoshaji. Tungekuwa sote waandishi nani angekuwa na nafasi ya kumsoma na kumkosoa mwenzake?

Hawa ndio watu wanaobisha ilimradi wabishe tu. Ukweli wanaujuwa.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Ami
Ngoja Maalim Mohamed Said aje kukupa darsa kwenye hilo, ndio nyanja zake hizo.

Maalim Mohamed Said naomba tukumbushe kidogo kuhusu Bibi Tabu Bint Mzee.
Maalim,kakutana na vichwa humu,anapewa yeye darsa,anajuta kuijua JF maana huko kwote alikopitia alikuwa haulizwi hard hitting questions,humu kakutana na no nonsense approach ya akina Mwanakijiji basi MS anaona aibu kupandisha bendera nyeupe
 
Kwa kawaida inatamkwa darsa kwa ''sekne.''
Wewe umeweka ''alif'''

Kwa lugha ya Kiarabu ambako ndiko asili ya neno lenyewe unakuwa umelikosea.
Lakini sisi ukisema ''darasa'' yote sawa.

Maana ikiwa ''darasa'' unapoteza kabisa ile filosofi yenyewe ya neno ''darsa.''
Katika darsa huwa na adabu zake.

Hakuna kejeli hakuna tusi hapo.

Wanafunzi wamepiga goti wanasoma wameinamia vitabu wanamsikiliza maalim.
Na darsa ina adabu zake wanafunzi wanasomeshwa.

Ndiyo maana mimi napata shida kufanya mnakasha mtu akikejeli au akitukana.

Naweka hapa chini zawadi kwako.

View attachment 79724

Huyo ndiye Mshume Kiyate.

Rafiki kipenzi wa Nyerere kuanzia 1953 pale alipojulishwa kwake na Abdulwahid Sykes katika kundi lile la wafanyabiashara wa Karakoo Market.

Mzee Mshume ndiye alikuwa dalali mkubwa wa samaki pale sokoni biashara ambayo ilimtajirisha.

Abdulwahid alikuwa ndiye Market Master.

Mzee Mshume alikuwa mfadhili mkubwa wa TANU na alikuwa katika Baraza la Wazee wa TANU.

Nyerere alipolivunja baraza hili mwaka 1963 chini ya uenyekiti wa Mzee Idd Tulio wazee wale walisonononeka sana.
Kutokana na ustaarabu wa pwani ukifukuzwa hurejei wazee hawa wa baraza la TANU hawakurudi tena pale ofisi ya TANU yalipokuwa makao yao.

Taratibu mmoja baada ya mwingine wakafa na kuzikwa bila ya heshima yoyote ya chama au serikali.
Idd Tulio aligongwa na gari na kufa akazikwa na nduguze Waislam kimya, kimya, Mshume Kiyate aliugua kwa muda mrefu Muhimbili.

Kiongozi pekee aliyekwenda kumtembelea Mzee Mshume alikuwa Oscar Kambona na ilikuwa kumuaga maana alikuwa yuko njiani kutoroka nchini.

Hata siku ya maziko yake Mzee Mshume Mtaa wa Matumbi Dar es Salaam TANU wala serikali haikuonekana mazikoni.
Allah ana shani yake.

Pale yalipokuwa maziko yake nyumba ile ilikuwa karibu sana na mahali ambapo mwaka 1955 au 1956 Mzee Mshume alikutana na Nyerere (Cameron/Morogoro Road maarufu Mwembe Togwa sasa Faya au United Nations) akielekea sokoni wakajuliana hali na Mzee Mshume akatoa rundo la fedha kumpa Nyerere kisa ambacho nimekieleza huu ukumbini.

Kipindi hiki ni kipindi kigumu sana katika historia ya Waislam na chama cha TANU maana baada ya uhuru kupatikana zilianza kuingia fitna baina yao na Nyerere.

Hii ilipelekea kutolewa risala kwa Nyerere maarufu kwa jina ''Moto wa Waislam Ukiwaka'' risala iliyosomwa na Bilali Rehani Waikela kwa Nyerere katika ufungaji wa mkutano wa mwaka wa 1963 wa EAMWS. Inasemekana risala ile ilikuwa kalamu ya Sheikh Hassan bin Amir.

Historia ya TANU na Waislam ina mengi sana.
Mzee Mshume wanaukumbi msingemjua kama nisingemtaja humu ukumbini.

zomba,

Bila Mohamed Said tungeyajua haya kusoma hujui hata picha uoni.
 
Last edited by a moderator:
Ami tazama juu alivyokujibu wewe na tazama hapa chizi siku mbili tatu nyuma alivyonijibu mimi:

Hawa ndio watu wanaobisha ilimradi wabishe tu. Ukweli wanaujuwa.

Hata kuambia umechakachua watu wanabisha mpaka wanapoteza kumbukumbu wengine mpaka wanawakana baba zao wazazi.
 
Last edited by a moderator:
Mohamed Said,

..unaweza kutuletea risala "moto wa Waislamu ukiwaka" aliyoisoma Bilal Rehani Waikela mbele ya Mwalimu Nyerere?

..je, ni kweli Bilal Waikela, aliposoma risala hiyo, alimnyooshea bakora Raisi Mwalimu Juliasi Nyerere?

..je, hudhani kwamba risala hiyo ilikuwa ya vitisho, na kuijaribu mamlaka ya Raisi na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania??

cc: Ritz, Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, zomba, Jasusi, Mag3
 
Last edited by a moderator:
Maalim,kakutana na vichwa humu,anapewa yeye darsa,anajuta kuijua JF maana huko kwote alikopitia alikuwa haulizwi hard hitting questions,humu kakutana na no nonsense approach ya akina Mwanakijiji basi MS anaona aibu kupandisha bendera nyeupe

Naona umeamua kujifariji na kujiliwaza.

Vipi picha zimeisha unapozitoa.

www.juliusnyerere.info
 
Mohamed Said,

..unaweza kutuletea risala "moto wa Waislamu ukiwaka" aliyoisoma Bilal Rehani Waikela mbele ya Mwalimu Nyerere?

..je, ni kweli Bilal Waikela, aliposoma risala hiyo, alimnyooshea bakora Raisi Mwalimu Juliasi Nyerere?

..je, hudhani kwamba risala hiyo ilikuwa ya vitisho, na kuijaribu mamlaka ya Raisi na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania??

cc: Ritz, Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, zomba, Jasusi, Mag3
Mkuu hujui kuwa kwahisani ya shehe Mohame hiyo ni "inasemekana" tu?
 
Last edited by a moderator:
Ritz, Katika vitu ambavyo vinanipa shida ni kukosa faragha. Hakuna nitakapokwenda Tanzania nisijulikane. Hata nikiingia msikiti wa pembezoni nikajificha nyuma. Ikisha sala watu weshanizunguka na kama ni Sala ya Ijumaa Imam atatangaza kuwa nimo msikitini. Nashukuru tena nashukuru.
hujui kwa sababu gani? unawafundisha ughaidi Mood.
 
sio wazanaki tu bali makabila yote ya mkoa wa mara hata wanawake nao wanaoa.

nilijifunza haya maajab nilipokuwa huko wakti nipo mwanza.

Tusubiri jibu la Yericko
Acha uwongo mwingine wewe. Mwanza siyo Mara. Ni Wakurya peke yao walio na hii mila ya mwanamke kuoa mwanamke mwingine. Na wala hujui historia yake. Si kwamba huyo mwanamke anaolewa na huyo mama ila mama anamlipia mahari ili watoto atakaozaa wawe wa kwake. Na lengo lake lilikuwa ni kudumisha ukoo kwa mfano kama mama hakuzaa watoto. Usidanganye hapa na kujifanya mjuzi kama ulivyofanya kwenye ule mjadala wa makabila ya Kenya na Uganda.
 
Ami tazama juu alivyokujibu wewe na tazama hapa chizi siku mbili tatu nyuma alivyonijibu mimi:

Hawa ndio watu wanaobisha ilimradi wabishe tu. Ukweli wanaujuwa.

Sasa hapo unataka maelezo? Mimi ni muandishi in the sense that I have a degree in journalism and I have worked in the media profession. Mimi si mwandishi in the sense that I have not published anything worthwhile. Context. Mukhtadha.
Unalo jengine?
 
Back
Top Bottom