DULLAH MSAVIVOR,Vema sana BaruBaru..
hawa hawataki tuh kuskia huu ukweli kwa kuwa unasemwa na muislam,pia unaonekana kama vile unawatetea waislam na uislam,kitu ambacho ni kweli,
uislam uachwe kama ulivyo,waislam waache kama walivyo.,waangalie je,kilichoelezwa kipo ama hakipo?kina uhalisia ama hakina?kwa maana kila kitu wametafuniwa hapo,wao wamekaa kukashifu uislam na waislam,watu wa ajabu sana hao..
uislam ulikuepo tokea zama hizo,hapa iangaliwe hii historia inayofichuliwa kisha ipimwe uhalisia wake,sisi tushajitosheleza tayari kwa uhalisia wa historia hii inayoelezwa na Mohamed Said..
..tatizo siyo kama unavyoliona wewe.
..tatizo ni Mohamed Said kuandika historia akiongozwa na hisia za udini.
..yeye kila jambo lilolotokea wakati wa harakati za uhuru na baadaye analihusisha na udini, tena Uislamu vs Ukristo.
..Yako matatizo ya kisiasa yalitokea wakati wa awamu ya Mwalimu Nyerere, na rungu la usalama wa taifa lilipopita halikuangalia dini ya mtu. Watu wengi, taasisi na jumuiya zilizoonekana ni tishio kwa utawala wa Mwalimu, na siyo dini yake, zilishughulikiwa na vyombo vya usalama.
..vyama vya wafanyakazi vilivyokuwa na mchango mkubwa ktk harakati za uhuru vilivunjwa na kuanzishwa jumuiya wa wafanyakazi ya Tanu na baadaye CCM. Wanaharakati wa uhuru kama Balozi Christopher Kassanga Tumbo waliwekwa kizuizini -- nakumbuka Kassanga Tumbo alikuja kutolewa kizuizini na Raisi Mwinyi. Utawala wa Machifu ulifutwa na wapo machifu waliopelekwa uhamishoni. Zaidi, jumuiya ya Waislamu Afrika Mashariki ilivunjwa kwa tuhuma za kujihusisha na siasa.
..Mohamed Said ana mahusiano kindugu na baadhi ya Mashekhe walioshughulikiwa na vyombo vya usalama wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere. Sasa uchambuzi wake wa historia na matukio yaliyotokea uanaathiriwa kwa kiasi kikubwa na background yake hiyo.
Last edited by a moderator: