Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Gwalihenzi,

Sisi hatujapata kuwa na mfadhili.
Chunguza utamuona nani ana wafadhili.

Unajua kuwa kila mfadhili aliyejaribu kuwasaidia
Waislam wa Tanzania alifurushwa?

Tuanze na Chuo Kikuu Cha EAMWS kilichotaka kujengwa
mwaka 1968.

Unamjua aliyekihujumu?

Miaka ya 1980 OIC ilitaka kujenga Chuo Kikuu Tanzania
serikali ikakataa kutoa kibali.

Chuo hicho kikajengwa Mbale Uganda.

Darul Iman walitaka kujenga chuo cha ufundi Kibaha na ardhi
wakanunua na fidia kulipwa.

Ikaja kampeni ya magazeti maarufu tuliipa jina ''Waarabu Wapora
Ardhi.''

Darul Iman wakakunja virago wakaondoka na fedha zao.

Ukitaka mifano zaidi Insha Allah nitakupatia.

Maslahi yangu binafsi ni yapi hayo?
Nifahamishe.
Taja yote unayoweza Mohamed Saidi, lakini uchochezi wako utakapo zaa matunda na watanzania wtakapoanza kuchinjana kama ilivyokuwa Rwanda wewe utapanda ndege kwenda Ulaya na Marekani kwenda kutoa mihadhara ya kujisifu mafanikio ya uchochezi wako!kama unavyojisifu sasa unapoona vijana wakiislam wakitoa laani kwa Nyerere miskitini sasa hivi.
 
Tupo pamoja jamaa yangu, tuungane mkono kuwakataa watu kama Mohamed Saidi wanaohatarisha umoja wetu kama taifa na kutishia amani yetu.

Mohamed Said ajahatarisha amani hizo ni fikra zako.

Alichofanya kaandika kitabu kuwataja wazee wazalendo waliokuwa wametupwa na historia sasa hapo amehatarisha amani gani.
 
Tupo pamoja jamaa yangu, tuungane mkono kuwakataa watu kama Mohamed Saidi wanaohatarisha umoja wetu kama taifa na kutishia amani yetu.

G,

Huo umoja utapatikana kwenye haki na usawa.
Kama kukataliwa ningeshakataliwa siku nyingi.

Nilichokiandika katika kitabu changu kimesimama
kwenye ukweli.

Dawa si kukwepa ukweli.

Dawa ni kukaa kitako na kuangalia tunaondokaje
katika hali hii.

Hizo slogans za ''umoja wetu'' hazisimami penye
dhulma.

Niamini ndugu yangu.
 
Hiyo dhulma mbona huioneshi? nani anadhulum na ninani anadhulumiwa ?
 
Taja yote unayoweza Mohamed Saidi, lakini uchochezi wako utakapo zaa matunda na watanzania wtakapoanza kuchinjana kama ilivyokuwa Rwanda wewe utapanda ndege kwenda Ulaya na Marekani kwenda kutoa mihadhara ya kujisifu mafanikio ya uchochezi wako!kama unavyojisifu sasa unapoona vijana wakiislam wakitoa laani kwa Nyerere miskitini sasa hivi.

G,

Hili ndilo jibu la hayo niliyokuandikia hapo kukueleza
vyuo vilivyohujumiwa visijengwe kwa kuhofia Waislam
watanufaika.

Wala huna haja ya kutaka kujua zaidi ili tupate ufunguo
wa matatizo yetu.

Kama kuna watu serikalini kwa ubaya wao tu wanaamua
kuwabagua Waislam basi tuwaaandame tuwakomeshe.

Haya hayakushughulishi.

Kinachokuwasha ni ''uchochezi wa Mohamed Said'' sio
kujua ukweli.
 
G,

Huo umoja utapatikana kwenye haki na usawa.
Kama kukataliwa ningeshakataliwa siku nyingi.

Nilichokiandika katika kitabu changu kimesimama
kwenye ukweli.

Dawa si kukwepa ukweli.

Dawa ni kukaa kitako na kuangalia tunaondokaje
katika hali hii.

Hizo slogans za ''umoja wetu'' hazisimami penye
dhulma.

Niamini ndugu yangu.
hivi mkuu unajua dhulma inafanywa na serikali na sio ukristo?
 
Mohamed Said ajahatarisha amani hizo ni fikra zako.

Alichofanya kaandika kitabu kuwataja wazee wazalendo waliokuwa wametupwa na historia sasa hapo amehatarisha amani gani.
Usijifanye hufahamu uozo anaofanya miskitini kwa kutumia kitabu hicho. Wewe mwenyewe umekiri kwa maandisha yako hapa kuwa sasa hivi kuna misikiti hapa nchini ukitaja jina la Nyerere utazomewa au waumini watashusha laana juu ya jina hilo! Umesha sahau?
 
Nguruvi,

Nimekuambia hapakuwa na hiyo hotuba katika karatasi.
Waikela alinieleza nini alisema katika hiyo hotuba.

Ndugu yangu hebu tuache hivi vitu vidogo vidogo mie
napenda kukupa majibu lakini kwa staili hii itafika nitakuwa
nakusoma napita.

Na hii habari ya kutaka ushahidi nishakueleza kwani mimi na
wewe tuko mahakamani kuwa nikupe ushahidi?

Nishasema mimi siko hapa kushinda hoja niko hapa kuwapa
hawa wasikizaji 80, 000 ambao hawajapatapo kusikia historia
hii.

Kwangu wewe ni njia tu ya kuwafikia hao wasikilizaji wangu.
Kwahiyo hilo ni simulizi na wala si kitu ambacho 80,000 wanachoweza kukitia akilini. Nami naweza kusema Waikela baada ya hotuba ile aliitwa na Nyerere akamuomba radhi kutokana na source zangu na bado 80,000 wakatusoma.

Mohamed hawa 8K baadhi yao walikuwa wanatatizika sana na maandishi yako na mara zote wanapofuatilia ni pale wanapoona yale yaliyo katikati ya mistari na nia yako yanapoowekwa hadarani.

Hiwezekani 8K wakakuelewa kwa kusema k.Sykes ndiye alikuwa kinara wa AA wakijua kuwa alikua katibu mkuu.
Wanajiuliza Rais alikuwa nani na makamu alikuwa nani? Na kwanini uongozi utoke kwa Sykes kwenda kwa Sykes kana kwamba ilikuwa urithi. Ndio, walikuwepo na walifanya walichofanya tunashukuru lakini inakuwa misrepresented kwa exaggeration, twists and fabrications

Leo 8K wanajua kuwa kumbe Cameron akiwa mkuu wa nchi na mwakilishi wa King hakuwachukia Waislam kama ilivyoandikwa na kuaminishwa na kwamba uhusiano wa Tanzania na commonwelath ni wa jadi na si mfumokristo

Leo 8K wanahangaika kutafuta ubaya wa Nyerere kwa waislam maana umetajwa lakini hakuna evidence, ironically kuna ushahidi wa Nyerere kuwa kipenzi chao.

Leo 8K wanajiuliza vipi serikali iliendeshwa na kanisa wakati Kawawa na wazee wa TANU walikuwepo?

Leo 8K wanajiuliza ilikuwaje Alhaji Mwinyi akabeba mikoba ya kanisa kama alivyobeba JK

Leo 8K wanajiuliza kama Nyerere na CCM kwa kupitia kanisa ndio walizuia jitihada za waislam kujiokomboa kieliem iweje basi waislam hao hao wanong'onezane kuichagua CCM ile ile iliyowadhulumu.

Kwa kupitia maandishi yako tunaifikia 8K katika uwazi, ukweli na kuchimbua yaliyojificha katika kitabu na nafsi.
Leo wangewezaje kujua hii ni ngano kama si kupitia wewe na ngano nzima?
 
Usijifanye hufahamu uozo anaofanya miskitini kwa kutumia kitabu hicho. Wewe mwenyewe umekiri kwa maandisha yako hapa kuwa sasa hivi kuna misikiti hapa nchini ukitaja jina la Nyerere utazomewa au waumini watashusha laana juu ya jina hilo! Umesha sahau?

G,

''Uozo?''
Hebu fafanua.

Sijakuelewa unaposema ''nakiri'' sijui una maana gani.

Mimi ninasema kila mahali kuwa Nyerere akitajwa kweli
analaaniwa na si siri muulize Muislam yeyote hili atakuambia.

Jumapili iliyopita nilialikwa kwenye semina Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
mada yangu ilikuwa ''Jinsi Umoja wa Watanganyika Ulivyoshinda Njama za
Wakoloni.''

Hili jambo la kulaaniwa kwa Nyerere nimelieleza.
Wewe unashtuka kwa kuwa ni kitu kigeni kwako.

Mimi kwa mara ya kwanza nilisikia laana hiyo Mnazi Mmoja 1995 katika
muhadhara wa Muzdalifa ambao mimi nilikuwa nahadhir na mada yangu
ilikuwa ''Uislam na Siasa Tanzania.''

Binafsi mimi nasikitishwa kuwa hadi tumefika hali hii serikali yetu haitaki
kukubali kuwa tuna tatizo.

Gwalihenzi,

Kuwa unanisoma vizuri.

Nadhani hayo niliyoandika yamekudhihirishia kuwa nasimama katika kile
nilichokisema.

Usiniletee lugha za ''kukiri'' mimi nikiri kwa lipi.
Kukiri ndiyo nini na nakiri kwa nani?

Mimi naaandika, nasema na maneno yangu yapo katika maandishi na katika
sauti yangu.

Narudia sijasahau kitu chochote katika yale nilosema.
Ukipenda rudia kusoma hii post upya.

Tutafahamiana.
 
Usijifanye hufahamu uozo anaofanya miskitini kwa kutumia kitabu hicho. Wewe mwenyewe umekiri kwa maandisha yako hapa kuwa sasa hivi kuna misikiti hapa nchini ukitaja jina la Nyerere utazomewa au waumini watashusha laana juu ya jina hilo! Umesha sahau?

Hayo ni kweli kabisa kwanza unatakiwa hujue Waislam kumpiga Nyerere hawajaanza kupitia kitabu cha Mohamed Said, wameanza kumpinga toka alipowakamata Masheikh na kuwaweka ndani baada ya uhuru.
 
Una uhakika gani hiyo hotuba ilitolewa?

MM,

Hii hotuba haikutolewa kabisa mie naona Mzee Waikela alikuwa anastawisha barza.
Wala Waikela hakuwa mwasisi wa TANU Tabora.

Wala Waikela hakuwa katibu wa EAMWS Western Province.

Wala Sheikh Hassan bin Amir hakuwa mwanachama wa TANU.
Watu tu bwana wanapenda kuandika ngano na nini hakuna chochote.

Jipumzikie Mwanakijiji achana na huu uzushi.
 
Hayo ni kweli kabisa kwanza unatakiwa hujue Waislam kumpiga Nyerere hawajaanza kupitia kitabu cha Mohamed Said, wameanza kumpinga toka alipowakamata Masheikh na kuwaweka ndani baada ya uhuru.

Ritz
Hebu tusaidie kidogo.
Nikisema kwa mfano: "waislam wanawachukia wakristo" au "waislam ni matajiri" hii itakuwa ni over-generalization. Si waislam wote wanawachukia wakristo na wala si wote ni matajiri.

Sasa unaposema "Waislam walianza kumchukia Nyerere wakati Masheikh walipotiwa kizuizuini", sidhani kama unamaanaisha waislam wote.

Kwa sababu hiyo basi naomba kujua aina za waislam tulionao hapa Tanzania. Je kuna watu tunaofikiri ni waislam (kwa mfano walioko Bakwata, surah ya maimam) kumbe sio? Je kuna madhehebu (kwa mfano: ibadhi, sunni, shia, ismailia nk) ambayo si waislam wa kweli? Ni nani anayeamua na kwa vigezo gani kuwa Abdukarim ni muislam na Jaffary sio muislam iwapo hawa wote wanafuata na kutimiza nguzo za uislam?
 
Last edited by a moderator:
MM,

Hii hotuba haikutolewa kabisa mie naona Mzee Waikela alikuwa anastawisha barza.
Wala Waikela hakuwa mwasisi wa TANU Tabora.

Wala Waikela hakuwa katibu wa EAMWS Western Province.

Wala Sheikh Hassan bin Amir hakuwa mwanachama wa TANU.
Watu tu bwana wanapenda kuandika ngano na nini hakuna chochote.

Jipumzikie Mwanakijiji achana na huu uzushi.
kumbe habari yenyewe ya waikela ni uzushi.
 
MM,

Hii hotuba haikutolewa kabisa mie naona Mzee Waikela alikuwa anastawisha barza.
Wala Waikela hakuwa mwasisi wa TANU Tabora.

Wala Waikela hakuwa katibu wa EAMWS Western Province.

Wala Sheikh Hassan bin Amir hakuwa mwanachama wa TANU.
Watu tu bwana wanapenda kuandika ngano na nini hakuna chochote.

Jipumzikie Mwanakijiji achana na huu uzushi.

mzee kwenye sarcasm you are not very good at it... nice try though
 
Back
Top Bottom