Usijifanye hufahamu uozo anaofanya miskitini kwa kutumia kitabu hicho. Wewe mwenyewe umekiri kwa maandisha yako hapa kuwa sasa hivi kuna misikiti hapa nchini ukitaja jina la Nyerere utazomewa au waumini watashusha laana juu ya jina hilo! Umesha sahau?
G,
''Uozo?''
Hebu fafanua.
Sijakuelewa unaposema ''nakiri'' sijui una maana gani.
Mimi ninasema kila mahali kuwa Nyerere akitajwa kweli
analaaniwa na si siri muulize Muislam yeyote hili atakuambia.
Jumapili iliyopita nilialikwa kwenye semina Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
mada yangu ilikuwa ''Jinsi Umoja wa Watanganyika Ulivyoshinda Njama za
Wakoloni.''
Hili jambo la kulaaniwa kwa Nyerere nimelieleza.
Wewe unashtuka kwa kuwa ni kitu kigeni kwako.
Mimi kwa mara ya kwanza nilisikia laana hiyo Mnazi Mmoja 1995 katika
muhadhara wa Muzdalifa ambao mimi nilikuwa nahadhir na mada yangu
ilikuwa ''Uislam na Siasa Tanzania.''
Binafsi mimi nasikitishwa kuwa hadi tumefika hali hii serikali yetu haitaki
kukubali kuwa tuna tatizo.
Gwalihenzi,
Kuwa unanisoma vizuri.
Nadhani hayo niliyoandika yamekudhihirishia kuwa nasimama katika kile
nilichokisema.
Usiniletee lugha za ''kukiri'' mimi nikiri kwa lipi.
Kukiri ndiyo nini na nakiri kwa nani?
Mimi naaandika, nasema na maneno yangu yapo katika maandishi na katika
sauti yangu.
Narudia sijasahau kitu chochote katika yale nilosema.
Ukipenda rudia kusoma hii post upya.
Tutafahamiana.