Mkuu mbona unaonekana anajua mambo mengi kuhusu uhusiano wa jamaa zetu hawa Waislaam na Nyerere kabla ya uhuru, hii ndio mara yangu ya kwanza kuona unayahanisha vizuri tu. Kama sikosei M.S anazungumzia mahusiano ya Serikali ya awamu ya kwanza na Waislaam miezi michache baada ya kupata uhuru - ni kitu gani kilitokea mpaka wakafikia hatua ya kufarakana na baadhi ya Waislaam wanzilishi wa chama ambao wewe unasema na hapa nakunukuu "Wazee wa Kitanganyika ambao walipendana kweli na udugu wa kweli na ndugu zao Wakristu; hawa ambao hawakutaka kumdhuru Nyerere - sababu ya Ukatoliki wake - akikaa katikati yao" Mimi sina utaalamu wa kisaikolojia wa kumfikia Sigmund Freud lakini reading between the lines sina uhakika kama unayo yasema hapo juu huko sincere!! Ulikuwa na nia ya kuvuta wasomaji kwanza alafu baadae ndio uzungumzie uliyo kusudia, napata wakati mgumu kukuelewa kwa nini kila mtu anayezungumzia/kutoa mchango kuhusu historia ya kweli kuhusu Taifa letu wewe unamuona anamchukia Mh.Nyerere (R.I.P) nani Mtanzania mwenye akili timamu ambaye anaweza kuwa na ubavu wa kubeza beza mchango wa Kambarage au kumkosea heshima, hata Mohammed hakuna popote alipo mtukana/kumkosea heshima Baba wa Taifa.
Juzi hapa nilizungumzia kuhusu mzee wangu kutoa Landrover, Public Addressing System na kumpatia Kambarage kuhutubia wananchi, mzee wangu alivunja sheria za kikoloni bila woga; nilizungumzia vile vile kukutana kwangu na Mzee wa kikoloni aliyewahi kuwa PC Tanganyika na kitu gani alinieleza - lakini cha ajabu wewe ukaja na maswali ya kushangaza kidogo eti kwani Nyerere aliwachukia wazazi wangu au jamaa zangu!! Yaani unatumia tactics za ku-steer watu wazungumzie mambo ambayo yako biased na hayana ukweli wowote.
Hivi kwa nini baadhi yetu tumepania ku-derail mada!! Kinacho zungumziwa humu ni Historia ya Taifa letu kuanzia miaka ya 1920s mpaka tunapata uhuru sio DINI, kwa nini tunakazania mambo ya DINI tu? Kuna maswali yangu nayatayalisha kumuhuliza ndugu Mohammed Said, nina hakika atayajibu bila ya kuficha kitu kwamanufaa ya Wananchi wote specifically WAKRISTO.