Na lipo sio moja, kuna mengi. Lakini duara ni kubwa sana ukitaka tu-breakdown matatizo ya nchi hii kulingana
na Rangi, Dini, Kabila na eneo hutakosa la kukuunga mkono.
Tuseme hivi:
Hakika Wahindi na Waarabu katika nchi wana afueni sana, lakini Wamatumbi kama sisi wengi wetu dhoofu hali.
Walioko jela wengi weusi, wanaokula mlo mmoja tu kwa siku wengi weusi n.k n.k.
Waislam wengi tu (Ismailia, Bohora) wana afueni na mambo yao Alhamdulillah yamewanyookea kwenye Elimu na hali. Lakini Waislam wa Kilwa, Rufiji, Kisarawe hali si hali. Halafu rudi kwa Waislam wa Machame mambo yao si mabaya kulinganisha na hao wengine ingawa si mazuri sana kama Ismailia/Bohora!
Njoo kwenye kanda, Kusini si bora sana Kielimu na Kiuchumi kuliko Kaskazini na Nyanda za juu kusini. Lakini hapohapo Kaskazini Manyara wako nyuma kuliko Arusha na Kilimanjaro. Hata mkoa wa Kilimanjaro, Moshi iko mbele kuliko Same.
Unataka na makabila?
Wanyakyusa wako vizuri kielimu kuliko Wagogo. Lakini Wanyakyusa wa Rungwe wako vizuri zaidi ya wale wa Chunya!
Sasa Humo kwa Weusi utakuta Wakristo, Waislam, Wachaga, Wanyakyusa, Wasukuma n.k.
Kwa Kanda utakuta Weusi, Weupe, Wakristo ,Waislam, Wasukuma, Wadengereko n.k
Kwenye dini utakuta kuna Weupe, Weusi, Wasukuma, Wachaga , Wadengereko nk n.k
Na kwenye kabila Hao woote juu pia wamo.
Ndio maana nakushauri toka kwenye hiyo level nenda level ya juu zaidi. Hata miongoni mwa watoto wa familia moja kuna tofauti itakuwa Taifa?
Yatazame matatizo ya Nchi hii kwa upana wake utagundua mengi na hapana shaka tutatoka hapa tulipo kama Taifa.