Ndiyo maana hataki kujibu.
Anafaham kuwa ni delusion na majibu yataodoa dhana nzima kutokana na kukinzana na ukweli au ushahidi.
Nimepitia maandiko yake yote nakuhakikishia hakuna mahali palipoeleza nini maaana ya mfumokristo.
Siku zote zitaanza hadithi na katkati ndipo msomaji anapochomekewa mfumo kristo kwa sana bila kuwa na ufahama wa definition ya mada halisi. Soma hii hapa chini uone mfumo kristo ulivyozuka from no where na kuwa centre of the whole discussion Hapa anamfanya msomaji ajihisi kuwa ni raia wa daraja la tatu. Alichokificha ni kueleza daraja la kwanza na la pili ni akina nani! Halafu akachomeka neno religious animosity. Hakujawahi kuwa na animosity anayoisema, alichokifanya ni kujenga mazingira ya daraja la tatu kuhisi kuwa tayari daraja hilo lilishakuwa imara kupingana na kitu ambacho hajakiweka wazi. Wasoma hadithi hadi hapa ni jazba tu! Psychologically anaelewa kuwa hakutaja raia daraja la kwanza, sasa taratibu baada ya kumfanya raia daraja la tatu ajihisi dhalili na kumtia ushujaa kuwa tayari alishaanza kupambana na ''adui'' ndipo anaweka wazi hiyo Christian dominated. Bado hajatengua kitendawili cha raia daraja la pili ni nani.Kafanikiwa ku-insinuate hoja yake na sasa anaweka wazi kile alichokificha kiuandishi hapo mwanzoni. Kwa vile watu wameshajawa na jazba, kwake ni mteremeko kutumbukiza hoja akijua hakuna nafasi ya kufikiri tena.Keshafanikiwa kuzunguka na sasa ameweka wazi kuhusu Church. Hapo keshamvuta mtu aliyesoma tu bila ufikiri kuingia katika hoja yake ya mfumokristo, si tayari keshataja kanisa na Christians.!Mohamed anaonyesha kuwa Nyerere alishindwa kumuondoa Mwinyi. Akamweka Joseph Warioba mtu ambaye ni sura iliyokuwa haijulikani katika baraza la mawaziri.
Na kwamba hakuwa na sifa zozote ndani ya CCM ili awe makamu wa rais na waziri mkuu.
Apparently unaweza kuona kama ni kweli.
Tukienda kwenye ukweli Mohamed ni mpotoshaji mzuri sana kwa kujua kuwa tayari ameshapandikiza fikra zake za mfumo na madaraja ya uraia hivyo mtu hawezi kufikiri nje ya hapo (out of box)
Ukweli kuhusu warioba ni huu hapa:
Warioba alihitimu UDSM mwaka 1966. Kwa kumbu kumbu tu, yeye ni mmoja wa wale vijana waliompa Nyerere Ultimatum.
1966-1968 alikuwa wakili wa serikali, na mwaka 1968-1970 alikuwa solicitor wa jiji.
Mwaka 1976-1983 alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali wakati huo ya Nyerere.
Kuanzia mwaka 1983 hadi alipochaguliwa na Mwinyi Warioba alikuwa Waziri wa sheria.
Ikumbukwe kuwa alipokuwa mwanasheria mkuu wa serikali, Warioba alikuwa anaingia bungeni kwa wadhifa huo.
Alipokuwa waziri wa sheria tayari alishakuwa mbunge.
Hadi hapo unaona kuwa si kweli kuwa warioba alikuwa ''unknown new face katika cabinet'' wala credential ndani ya CCM.
Hapa panatosha sana kumuonyesha Mohamed kuwa kila mara amekuwa anaongopa, narudia anaongopa
(kama si kweli aje akanushe habari hii).
Anafanya hivyo akijua kuwa katika hasira na chuki ni ngumu mtu kufikiri tofauti.Ni kosa alilofanya kwasababu ameingia chumba cha mkutano B badala ya A na kwa miaka 15 amekuwa anaaminisha watu hivyo Si kweli !
Kawawa alishakuwa waziri mkuu na makamu wa pili wa rais, Msuya alishawahi kuwa waziri mkuu na Daudi Mwakawago alishapewa nyadhifa za ubalozi.
Katika kipindi cha Mwinyi ilikuwa ni muhimu kuwa na damu tofauti na sioni kwanini Mohamed alidhani experience ya watu hao ilidharauliwa. Hapa ni kutaka kumdunisha Nyerere kama alivyowahi kufanya huko nyuma, unfortunate the history denies him unequivocally Mo anataka watu waamini kuwa nafasi ya waziri katika ofisi ya rais ilikuwa nyeti sana kuliko ile ya waziri fedha na waziri wa biashara na viwanda alizokuwa nazo hadi anajiuzulu.
Mo anamtaja Nyerere kama mtu aliyepiga vita serikali ya Mwinyi na Kighoma Malima.
Mo anasahau kuwa Malima alisema kuwa aliyemrithi katika nafasi hiyo Jakaya Kikwete ndiye alikuwa anafanya character assassination dhidi yake.
Mohamed ameficha ukweli kuhusu JK na jinsi alivyobana pesa za Malima pengine jambo lilopelekea stroke.
Kwa vile jicho lake lipo katika mfumokristo hayo mengine yapo chini ya kapeti.Je, umuhimu wa nafasi hiyo umefikia kikomo lini? JK naye ame lock out kama Nyerere. Hapa ndipo sasa anakomelea msumaria alioukusudia wa mfumokristo kitu asichojua maana yake lakini anajua kinafanyaje kazi.
Geeky kwa mtazamo huo hapo juu ambao umejaa upotoshaji na spinning za kiwango cha kimataifa ni ngumu sana kupata definition ya mfumokristo.
Jambo ambalo ni la hatari sana ni kuwa wapo wanaoongelea mfumo huo bila kujua maana yake na hawa ndio tunawaalika hapa wajue kuwa wanaongelea dude lisilo na miguu au kichwa lakini linatisha sana. Lazima uogope tu!
Wengine wanshindwa kujua walisema nini kama mwenzetu aliyetuambia ''Jumbe kasemakama serikali haina dini kwanini ina mashirikiano na Vatican'' alipoulizwa afafanue hoja hiyo, hana jibu.
Amemeza tu kwasababu amesikia mahali mfumokristo.Kila anayejisikia basi neno mfumokristo linatangulia ulimini, sasa wajiulize kama mwasisi hajui maana ya hilo neno wao wanalitumia kwa mantiki ipi?
Mohamed, wasaidie waislam si kuwapotosha, haiendi hivyo na wala hiyo si suluhu ya matatizo.Ulisema uislam ni ukweli, sijui kama unasimama katika hilo kila mara watu wanapokuja hapa na kukuonyesha ''kisicho cha kweli''.
I have to admit this is a turning out to be a very interesting debate but much is to be attributed to the ignorance of some of us in the thread especially when it comes to the history of this beautiful country. Ila tutafika. Thanks to "shule za kata" I hope tume ya Mh Pinda itakuja na mitaala rasmi ili tusijeingiza sumu katika historia na vichwa vya kizazi kijacho.
I know that there is a throng of people that just dont like Nyerere for all kinds of reasons:
Some people will criticize Nyerere for limiting freedom to information eg. the alleged ban on tv imports and Mtikila [a christian]was a voiced and an outspoken critic of this then on his own unlicensed radio station.
yet some have questioned Nyerere's leadership tactics but never in the context of religious intolerance. Things like the culture he left behind : the handling of critics like the alleged assasination of Horace Kolimba note that tanzania is not special in this regard nchi nyingi za kikomunist zina silence critics yet it was a sign that tz was still a 'police state' post single party rule. Labda swali la msingi hapo kolimba ni dini gani?
Yet some will question Nyerere's economic policies and the utopia that we were sunk into but never in the context of religious intolerance. 'kaptula la Max' is a good example and we know what happened to kezilahabi's book hapa ilikua udini au policing the critics wa sera za kikomunisti ? Mkapa (mkristo) alishindana na Mch Munisi (mkristo) kwa sababu hizo hizo, alifunga hakielimu kwa sababu kama hizo hizo za kukosolewa serikali :
ninachotaka kusema ni kwamba tanzania ni police state na imekua hivyo tangu mwanzo kama kawaida ya sera tulizoamua kuzifuata na Nyerere hakutunga communism- thats too much credit - na serikali yetu sio unique katika hilo serikali nyingi sana zilizopo/zilizotokea ktk sera za kikomunist zinafanya hivyo kwa justification ya national interest.
So whatever Nyerere reasons were we can understand he had bigger fishes to fry than squabbling with religion. In fact mie huwa napata shida kuona ni vipi Nyerere was a devout catholic kwa kiwango anachokuwa potrayed na hapohapo akawa statesman wa hadhi aliyokuwa nayo in one person, he must have been agnostic lying to us or rather a political genius kama Julio Caesar wa kitabu chake (shakespeare's caesar). Ukimjua Nyerere vizuri you will believe the later. and yet and he himself admitted that he and his gov were not a company of angels.
No one in his right mind can ever ever question the unyielding love this one man had for this beautiful country. Kama Mwanakijiji alivyotangululia kusema Nyerere aliwahi mkingia kifua Mwinyi kwa jeshi though it was not favourable towards Mwinyi. Ni Nyerere huyohuyo aliyetumia veto kumpitisha mkapa na kumfanya Kikwete atulie na bila shaka tunaona alikua na point kiwete alikua bado. You need a level of nobility and moral authority to pull that before the whole ccm congress. Nyerere aliwahi kuwa na nguvu kuliko bunge lote wakati fulani na alionesha hilo. Pia wapo kina Oscar Kambona, Mzee Mtei na wengine wengi tu wali cross path na Mzee mzima wakaishia pabaya. Sasa nao wakristo wakiamua kuchukua mifano hiyo na kuifanya mitaji ya kihistoria wakasema Nyerere alidanganywa na wazee wa kiislamu akafanya 1, 2, 3 akitumika. hapo kila mtu akamuhadithia mtoto wake kwa context ya dini yake. je kwa hali hiyo anayosema Mohamed kwamba "mie nimeandika ya kwangu na nyie andikeni ya kwenu" kutakalika?
it never occured to me that anybody would level any religious accusations against mwalimu at this scale- je kuna mtu amekemea udini, ukabila na ubara-visiwani kama mwalimu? Guys its not yet 20 years na bado tuliomuona na kumsikia tupo hai Stop it!!