Kuhusu swali lako
Abdulwahid Sykes, kulingana na maelezo ya
Mohamed Said, alikuja kujulikana tu baada ya kuvamia ofisi za TAA na kufanya mapinduzi kwa kutumia uwezo wake mkubwa katika masumbwi. Cha ajabu ni kwamba hata baada ya mapinduzi hayo hakuweza kuchaguliwa kuiongoza TAA na badala yake akachaguliwa msomi Dr. Kyaruzi. Hakuna popote ambapo Kleist Sykes na mwanawe Abdulwahid Sykes waliwahi kuchaguliwa kuongoza vyama vya AA, TAA wala TANU kama inavyohadithiwa na
Mohamed Said, hapana, huo ni uongo.
Zali la Mentali, jitahidi umpe haya maswali Mwalimu wako wa darsa
Mohamed Said,
- Je, Mwalimu akiwa bado yuko Tabora mwaka 1945, Abdulwahid Sykes alikuwa na wadhifa gani ndani ya AA?
- Je, Mwalimu alipofika mara ya kwanza Dar es Salaam kabla ya safari yake masomoni Uingereza, Abdulwahid Sykes alikuwa na wadhifa gani ndani ya AA?
- Je, kabla ya Abdulwahid kuivamia ofisi ya TAA kwa masumbwi, alikuwa na wadhifa gani ndani ya TAA?
Ukiweza kupewa majibu ya haya maswali, uwe tayari kukiri kwamba hujui lolote kuhusu mambo yanayojadiliwa humu na ingekuwa heri sana ukae kimya, ubaki mtazamaji tu. Nitakuwa naingia humu kuweka tu mambo sawa nitakapoona kuna uongo na upotoshwaji unafanyika...umbea, mipasho na ngojera za mitaani sitazijibu, wengine hatukulelewa katika mazingira hayo.