Mzee MS; Shukran kwa maneno mazuri juu ya viewers. Pia nahisi umefanya vizuri kukaa pembeni na maswali yaliyokuja. Nadhani wakati umefika kwa vijana wako machachari kujibu huku na wewe unatafuna kashata na kusikiliza the Beatles (Sergent Pepper???). Tutajuaje wameiva?Stay well.
Wickama,
Umejuaje kama mie ni mpenzi wa Beatles?
Ngoja nikupe kitu.
Udogoni nikipiga guitar na band na kuna nyimbo moja ya Beatles ''Things We Say Today''
nikiipiga huku nikitumia lyrics za Kiswahili...''Umenitoroka nyumbani kwangu...''
Hizi lyrics aliandika Cuthbert Sabuni wa Flaming Stars moja ya band za vijana katika 1960s
hapa Dar.
Iko siku niko na mwenyeji wangu tunapita Dakota Appartments pembeni mwa Central Park,
New York.
Sasa jamaa ananieleza kuwa hiyo nyumba akiishi John Lenon na jana yake kabla hajapigwa
risasi yeye alimtembelea pale lakini John alikuwa kalala kwa hiyo akazungumza na mkewe Yoko...
Nakipunguza kisa.
Sasa mimi nikamwimbia nyimbo nzima ya Beatles ''...how could I dance with another when I saw her
standing there...''
Jamaa kapigwa na butwaa maana hakutegemea haya.
Jamaa leftist ajabu na ndiyo maana akaelewana na Lennon.
Kufika kwake New Jersey yeye na mkewe wakanambia kuwa kesho kuna maandamano makubwa na
mimi wananialika maana hii serikali ya kishenzi lazima tuiangushe.
Waamerika hao tena walimu wa chuo kikuu Ivy League.
Nina picha nimepiga Central Park nimesimama Strawberry Hill hapo ndipo ilipo kumbukumbu ya Lennon.
Wickama,
Sikuwezi.
Mara unaniudhi mara unanifurahisha.
Hahahahahahahahahahahahahahha!
Ahsante sana.