Uchumi wa Frame Tanzania

Uchumi wa Frame Tanzania

Hivi ushirikiano ungekuapo apo awali situngegoma wapangaji ili haki zetu zilindwe sasa walivyokua waoga ukipewa notice mtu hajui kuisimamia haki yake sasa cjajua pale lugalo maana hawanaga masiala mwendo wa Sheria tu[emoji23][emoji23][emoji23]
Sasa hata hapo lugalo utafanya biashara Gani ili upate faida maana ukitembea kidogo unafika kawe kule Kuna Kila biashara na maduka. I think tuna ubunifu ni zero
 
Uchumi wa Frame unashika kasi sana Tanzania, ni Frame juu ya Frame, ni frame ukikata kona ni frame ukinyosha ni frame.

Hii nchi na hisi uwezo wa wetu wa kufikiria nahisi usha fikia tamati yake, nchi kwa sasa iko kwenye uchumia wa frame, si Jeshi la Police, Si Jeshi la Wananchi, Si makanisa yaani wote wanawaza Frame, Frame zinaoteshwa kama uyoga, miji imejaaa frame. Halimshauri, ni frame, Majiji ni Frema, Manisapaa zinawaza Frame.

Sasa wameona mjini hakutoshi, Frame zimehamia hadi kwenye makambi ya jeshi, Vituo vya Police, Mitaani maeneo ambayo ni kwa ajili ya Makazi kumejaaa Frame.

Tunako elekea Frame zitakuwa nyingi kuliko watu kama speed itakuwa ni hii hii ya sasa.

Je, hatuna Idea zingine nje ya Uchumi wa Frame?

Tunaandaa frame za kusapoti uchumi wa China make asilimia 99 ya hizo frame lazima ukutane na products za China.
Frame zinapunguza biashara barabarani.
 
Tuiite Framenomics...

Hii ni hatua ya mwisho ya taifa kuwa la madali wa bidhaa za kigeni.

Unaweza kushangaa Profesa wa Chuo kikuu anakomaa kujenga frame na kuli wa bandarini naye anajenga frame. Vivyo hivyo mawaziri na wabunge nao wanapambana kukamilisha frame kabla ya 2025. Hamna mwenye mawazo tofauti wote sawa kana kwamba akili zao zipo controlled na robot.

Uchumi wa kweli, uchumi utakaotuweka huru tumewaachia Wahindi, Waarabu na kwa kasi Wachina. Wao ndiyo wamiliki wa kweli wa njia kuu za uchumi kwa maana ya kilimo cha kisasa, viwanda na usafirishaji.

Kuna kila sababu ya kufanya uasi wa fikra miongoni mwa wazawa wa Tanzania wajue framenomics haiwezi peleka nchi uchumi wa kati bali kwa kufanya uwekezaji kwenye njia kuu za uzalishaji mali.

CCM nao hawajambo wana frame nchi nzima kuanzia kwenye viwanja vya mpira hadi kwenye ofisi zao. Huenda CCM wameambukiza wananchi mahaba ya frame na hivyo kuchochea uchumi wa frame!
Tuite franomics🤣
 
Bongo sijui hata nianzie wapi ngazi za juu zinazotakiwa kuhamasisha uzalishaji na kuongeza thamani za bidhaa zetu zinapinga jitihada zozote watu wanazozionesha mfano mtu akikutwa anazalisha pombe ya kienyeji anafungiwa badala ya kuendelezwa ili aboreshe viwe viwango kama ya Gin ya scotland. Kuna tatizo kubwa la ajira linakuja badala ya kufikiria kuwekeza kwenye vyanzo vya kukuza ajira wanafikiria kubana middle income earners kwa kupitia kodi muda si mrefu hawa middle income earners hawatakuwepo tena.
 
Tatizo lenu ni ujuaji.
Lile eneo kwa sehemu kubwa liko kwenye makazi ya wanajeshi.

Hadi uone limefanyika vile lazima walipata baraka zote kutokea Ikulu.

Hakuna kinachojificha zama hizi za tech.

Inaonesha wengi mmekosa frame pale ndo maana mwapiga kelele
 
Tatizo lenu ni ujuaji.
Lile eneo kwa sehemu kubwa liko kwenye makazi ya wanajeshi.

Hadi uone limefanyika vile lazima walipata baraka zote kutokea Ikulu.

Hakuna kinachojificha zama hizi za tech.

Inaonesha wengi mmekosa frame pale ndo maana mwapiga kelele
Ni sawa sasa kwanini hazikujengwa katika mpangilio mzuri?

Nyingine zimekaa kama zile nyumba za Tembe, nyingine zimebomoka...Hapana aisee

AU ndiyo kila Mwanajeshi alikuwa anajenga Frame yake akimaliza apangishe au auze mwenyewe?
 
Katika kitu nimekataa Nyumbani kwangu ni kuweka flemu, kwanza napenda shape ya nyumba yangu ionekane kama ilivyo na iko mtaani kabisa tena mtaa mkubwa kabisa, lakini habari ya fremu kwangu marufuku.

Wife ndio ana plot yake binafsi somewhere huko ndio Kajenga maflemu yake kawapangisha watu apate kodi, ila Nyumbani sitaki kabisa kusikia habari ya fremu.
Wife ana plot yake binafsi? Ila plot yako ni ya wote? Vijana kataeni ndoa ni utapeli
 
Back
Top Bottom