Majanga ya kiangazi hayana uvivu wala nini, yakija yamekuja, tungekua wavivu kama mlivyo aisei nchi yetu hii tungejikufia zamani, haupewi vyote, yaani nyie hapo mumepewa liinchi likubwa lenye rotuba nzuri kila sehemu, madini ya kumwaga, vivutio bora kuzidi vyote Afrika yaani kila kitu kizuri ila mkanyimwa uwezo wa kujituma na utumiaji wa akili.
Sisi tukanyimwa vyote hivyo tukapewa kainchi kadogo na zaidi ya nusu yake ni kame tupu, lakini tukapewa uwezo wa kujituma na kutumia ubongo, hadi hapa sasa uchumi wetu unakaribia kuwa mara mbili ya wa kwenu.
Nahisi tatizo lenu ni kubwa sana zaidi ya mnavyo onekana, kuna huu uzi nimeupitia hadi huruma, kuna Watanzania wanatambua hilo tatizo lenu lakini wamebaki hoi hawana namna ya kuwanusuru maana mlishajichimbia, hebu soma ndugu zako wanavyohuzunika
Tanzania inaweza kuwa Taifa la Watu Wajinga zaidi Duniani!