Ng'wanamangilingili
JF-Expert Member
- Aug 22, 2015
- 5,778
- 4,859
Ni Tanzania tu mojawapo ambapo polisi huwa inajichunguza, hakunaga tume maalumu huru.Hii issue ya huyu jamaa nimeona kuna vitu viwili vilivyotumiwa na wengi kumhukumu kuwa ni gaidi.
- Kofia aliyokuwa amevaa; hii inatumiwa na dini ya Hamza, ni kielelezo cha kuwa muumini wa dini fulani, kwasababu hii naamini polisi na uchunguzi wao wakamaliza huyu alikuwa gaidi.
- Kutaja jina la "Allah"; pia jina hilo hutumiwa na dini ya Hamza kumuwakilisha Mungu wao, hapa pia jamaa zangu wakaunganisha matukio wakapata jibu walilotaka.
Mwishowe, jamaa zangu walipounganisha matukio ndio wakaja na jibu walilokuja nalo, ukiunganisha na silaha aliyoitumia Hamza kuwashambulia polisi ndio neno gaidi likazaliwa.
Lakini kiuhalisia, nikitazama mlolongo wa matukio uliotufikisha hapo, naona "inawezekana" Hamza alikuwa na tatizo lake binafsi na polisi, kipo alichofanyiwa, na kwa mtazamo wake akaona hawa polisi wananifanyia/tufanyia hivi kwasababu ya dini yetu, ndio maana akatamka yale maneno kwenye ile video, ndio matokeo yake kikatokea kilichotokea.
Dawa ya kumaliza hii issue, Tume Huru ije kuchunguza itoe majibu mjadala ufungwe.
Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app