Uchunguzi ulilenga kumkuta Hamza Mohammed Gaidi

Uchunguzi ulilenga kumkuta Hamza Mohammed Gaidi

Hii issue ya huyu jamaa nimeona kuna vitu viwili vilivyotumiwa na wengi kumhukumu kuwa ni gaidi.

- Kofia aliyokuwa amevaa; hii inatumiwa na dini ya Hamza, ni kielelezo cha kuwa muumini wa dini fulani, kwasababu hii naamini polisi na uchunguzi wao wakamaliza huyu alikuwa gaidi.

- Kutaja jina la "Allah"; pia jina hilo hutumiwa na dini ya Hamza kumuwakilisha Mungu wao, hapa pia jamaa zangu wakaunganisha matukio wakapata jibu walilotaka.

Mwishowe, jamaa zangu walipounganisha matukio ndio wakaja na jibu walilokuja nalo, ukiunganisha na silaha aliyoitumia Hamza kuwashambulia polisi ndio neno gaidi likazaliwa.

Lakini kiuhalisia, nikitazama mlolongo wa matukio uliotufikisha hapo, naona "inawezekana" Hamza alikuwa na tatizo lake binafsi na polisi, kipo alichofanyiwa, na kwa mtazamo wake akaona hawa polisi wananifanyia/tufanyia hivi kwasababu ya dini yetu, ndio maana akatamka yale maneno kwenye ile video, ndio matokeo yake kikatokea kilichotokea.

Dawa ya kumaliza hii issue, Tume Huru ije kuchunguza itoe majibu mjadala ufungwe.
Ni Tanzania tu mojawapo ambapo polisi huwa inajichunguza, hakunaga tume maalumu huru.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Mnatumia nguvu nyingi sana kumtetea huyu gaidi. Huyu ni gaidi mfia dini.

NB: Mtu wa dini yeyote anaweza kuwa gaidi mfia dini.
 
Wambura na Sirro wenyewe wapo kwenye udini ndio maana walijielekeza kwenye dini kwani Sirro alianza kutoa hukumu kabla ya huo walioita uchunguzi,je Wambura anaweza kutuambia ni dini gani mafundisho yake hayo aliyoyaita ni ufia dini inafundisha kufia dini ni kuua polisi.
kumbuka sirro anapewa taarifa za uchunguzi mapema kabla hajazitoa hadharani.

ukiona namhukumu mtu kabla ujue kuna kitu anakijua vizuri.
 
Matukio kama la yule jamaa hufanyika sana huko Marekani wangesema nao wayatambue kama ugaidi basi huko Marekani kungekuwa na magaidi ya kutosha.
kwamba marekani ndio wa kukwambia gaidi yukoje!!!
 
Ila mkuu linapokuja suala la Dini Mimi sioni kama Tanzania Kuna udini kiasi hicho manaake hata hao maaskari wengi wao ni waislam sidhani kama serikali imeajiri wakrito pekeake
mpumbavu huyo,hawezi kutumia akili hata siku moja.
 
Hamza alikuwa ni mwana CCM, kada kindakindaki / mkeleketwa. Sasa unamtenganishaje Hamza na CCM ?

1630671743174.png


Kama kweli Police ni waungwana na wanatenda kazi kwa weredi basi wangeanza Upelelezi hapa kuwa kuwahoji hawa watu wawili ambao wamekaa na GAIDI meza moja.
 
Duuuh 🤣🤣

Hivi mkuu hatuwezi tukawa objective tu? Yaani tukawa kama waungwana tu?

Hamza aliweza kuwa yeyote kati yetu.

Nani hajawahi kukwazwa kwa kuonewa tu na polisi hawa?

Hivi si kweli kuwa kila mtu ana namna yake ya ku react kwenye manyanyaso, ikizingatiwa kuwa temporary insanity nayo ni sehemu ya maisha?
 
Hivi mkuu hatuwezi tukawa objective tu? Yaani tukawa kama waungwana tu?

Hamza aliweza kuwa yeyote kati yetu.

Nani hajawahi kukwazwa kwa kuonewa tu na polisi hawa?

Hivi si kweli kuwa kila mtu ana namna yake ya ku react kwenye manyanyaso, ikizingatiwa kuwa temporary insanity nayo ni sehemu ya maisha?
Marehemu hawezi kujitetea......

Kila jambo litokealo huwa ni FUNZO kwa anayehitaji KUJIFUNZA.....

#SiempreJMT
 
Lady Macbeth...

Here's the smell of the blood still:
All the perfumes of Arabia will not sweeten this little
Hand. Oh, oh, oh!

Out, damned spot! out, I say!—One: two: why,
Then, 'tis time to do't.—Hell is murky!—Fie, my
Lord, fie! a soldier, and afeard? What need we
Fear who knows it, when none can call our power to
Account?—Yet who would have thought the old man
To have had so much blood in him.

The thane of Fife had a wife: where is she now?—
What, will these hands ne'er be clean?—No more o'
That, my lord, no more o' that: you mar all with
This starting.


By courtesy of William Shakespeare

Kada mtiifu wa CCM...alizaliwa, akalelewa, akakua na akakomaa ndani ya CCM, mara ghafla kawa gaidi. Swali ni je wako wangapi? Je mpaka wote kugundulika watakuwa wametenda mangapi?

Even all the perfumes of Arabia will not cleanse CCM's bloody hands! Adui namba wani wa taifa hili ni CCM!
 
Lady Macbeth...

Here's the smell of the blood still:
All the perfumes of Arabia will not sweeten this little
Hand. Oh, oh, oh!

Out, damned spot! out, I say!—One: two: why,
Then, 'tis time to do't.—Hell is murky!—Fie, my
Lord, fie! a soldier, and afeard? What need we
Fear who knows it, when none can call our power to
Account?—Yet who would have thought the old man
To have had so much blood in him.

The thane of Fife had a wife: where is she now?—
What, will these hands ne'er be clean?—No more o'
That, my lord, no more o' that: you mar all with
This starting.


By courtesy of William Shakespeare

Kada mtiifu wa CCM...alizaliwa, akalelewa, akakua na akakomaa ndani ya CCM, mara ghafla kawa gaidi. Swali ni je wako wangapi? Je mpaka wote kugundulika watakuwa wametenda mangapi?

Even all the perfumes of Arabia will not cleanse CCM's bloody hands! Adui namba wani wa taifa hili ni CCM!

Wako wangapi? Ni swali la msingi sana.

Amini nakwambia Sirro na Wambura na polisi nzima kwa ujumla wake wa najua hayupo mwingine!

Sababu ni kuwa wanajua pia kuwa Hamza hakuwa!
 
Kamanda Wambura ametoa taarifa yake kuhusiana na uchunguzi wa kadhia ya Hamza kuwa alikuwa ni gaidi.

Halipo jipya kwenye taarifa hiyo kwani ni wazi kuwa kilichofanyika ni kuhalalisha tu ambacho polisi kama sehemu ya kadhia wangekitaka.

View attachment 1921631

Ikumbukwe pia kamanda Sirro alishahoji hata uhalali wa wazazi wa Hamza kumzaa tu kama binadamu!

Kwanini walioshambuliwa na Hamza walikuwa ni polisi peke yao? Kwanini Hamza hakuonekana kujaribu kujificha ili kuendelea na mapambano kwa siku au hata masaa zaidi?

Kama Hamza alikuwa ni gaidi hakuwa na washirika wowote hapa nchini? Hakuwa na mawasiliano yoyote na washirika hao?

Kama Hamza alikuwa na washirika nje tu, ushahidi uko wapi?

Waliomfahamu Hamza hawakubaliani na ripoti hii ya polisi. Bila shaka CCM alikokuwa kiongozi na kada mtiifu hawakubaliani na ripoti kuwa Hamza alikuwa msiri au mtu wa kujitenga, achilia mbali kuwa gaidi.

Vipi bastola aliyokuwa nayo, ilimilikiwa kihalali? Hivi Hamza alipigwa risasi ngapi? Naye alifyatua risasi ngapi? Ziko wapi taarifa hizi?

Kulisikika pesa kiasi cha 400,000,000/= kuhusiana na kadhia ya Hamza kupotea. Kumesikika kupotea kwa madini ya Hamza na polisi wakihusishwa moja kwa moja kwenye kadhia hiyo.

Kumesikika uwepo wa kikaratasi (suicide note) chenye maelezo yote ya kwanini Hamza alichukua hatua hii.

Polisi ambaye ni mtuhumiwa anakuwa na uhalali upi kutojipendelea kwenye kadhia hii?

My take:

Ilikuwa ni kwa maslahi ya polisi na serikali kwa ujumla kuhakikisha uchunguzi huru, wa haki na unaoaminika unafanyika kwenye kadhia hii.
kinachonisikitisha ni hasara aliyoipata Wambura , weledi wote aliokuwa nao umezikwa rasmi
 
Marehemu hawezi kujitetea......

Kila jambo litokealo huwa ni FUNZO kwa anayehitaji KUJIFUNZA.....

#SiempreJMT

Ni bahati mbaya kuwa hata kunako mafunzo lengo limekuwa ni kutanguliza siasa na ubinafsi mbele.

Siku tukifanikiwa kuweka siasa na ubinafsi pembeni tukalala mbele na yanayotusibu kama taifa tutafika mbali sana.
 
Kama kweli Hamza alikuwa ni mtu wa kujitoa muhanga - hawa abilia wote leo wangekuwa makaburini

Hamza aliwataka wabaya wake - polisi pekee!

Palihitaji kutanzuliwa hapo. Kwanini polisi peke yao?
 
Back
Top Bottom