Nimefanya uchunguzi wangu katika shule za msingi za serikali nimebaini mambo ya ajabu sana yanafanywa na baadhi ya walimu kwa watoto!
Kuna tabia za ajabu ajabu kutoka kwa baadhi ya walimu ambao wabadhamana ya kulea watoto wetu kielimu!
Miongoni mwa mambo niliyobaini
1. Walimu hawafuati ratiba ya masomo! Mfano ratiba ya siku ya watoto somo A, anaingia mwalimu wa somo E n.k hii inawafanya watoto wabebe mizigo mikubwa jambo linalowaathili kiafya ukubwani
2. Baadhi ya walimu wanafanya vibiashara kwa lazima kwa watoto mfano! Mwalimu anakuwa na biskuti zile za azam za miatano! Anazibanua kipande kimoja kimoja anawauzia watoto kila kipante cha biskuti tsh 100! Ambae hana anakopesha kwa nguvu kesho alete hela.
3. Baadhi ya walimu wanaingia kwenye darasa wanawagawia visheti, viubuyu watoto kwa lazima na kuwadai pesa jambo linalowafundisha watoto tabia mbaya ikiwemo wizi kwa kuhofia kuchapwa na walimu hao
4. Wanawapanga watoto cha kusema maafisa elimu wanapopanga kuja kutembelea shule! Huwa wanawatishia kuwa atakayesema atafukuzwa shule n.k
Kwa mifano michache ya tabia hizi hawa walimu wanatufundishia tabia mbaya sana kwa watoto!
Tunaomba waziri wa elimu ukalitazame hili, maafisa elimu wako hawatumii mbinu kuwahoji watoto hata kushtukiza,
Walimu wakuu wanakula a kugawana migao ya michango mbalimbali ya watoto..
Ni tabia mbaya sana kuwafanya watoto dili badala kuwafundisha maadili mema!
Tunaandaa watekaji wa baadae pasipo kujua wanaoligharimu taifa!