Uchunguzi wangu katika shule za msingi za serikali umebaini zipo tabia mbaya kwa baadhi ya walimu

Kulazimisha watoto kwa nguvu wakope vipipi huoni kuwa ni shida.. Kama unaona ni sawa basi taifa linasafar ndefu sana
Kama mwanao alikopa mwenyewe kwa njaa yake ..? Unadhan atasema alikopa kwa hiari yake
 
Nimefanya uchunguzi wangu katika shule za msingi za serikali nimebaini mambo ya ajabu sana yanafanywa na baadhi ya walimu kwa watoto!

Kuna tabia za ajabu ajabu kutoka kwa baadhi ya walimu ambao wabadhamana ya kulea watoto wetu kielimu!
Miongoni mwa mambo niliyobaini

1. Walimu hawafuati ratiba ya masomo! Mfano ratiba ya siku ya watoto somo A, anaingia mwalimu wa somo E n.k hii inawafanya watoto wabebe mizigo mikubwa jambo linalowaathili kiafya ukubwani

2. Baadhi ya walimu wanafanya vibiashara kwa lazima kwa watoto mfano! Mwalimu anakuwa na biskuti zile za azam za miatano! Anazibanua kipande kimoja kimoja anawauzia watoto kila kipante cha biskuti tsh 100! Ambae hana anakopesha kwa nguvu kesho alete hela.

3. Baadhi ya walimu wanaingia kwenye darasa wanawagawia visheti, viubuyu watoto kwa lazima na kuwadai pesa jambo linalowafundisha watoto tabia mbaya ikiwemo wizi kwa kuhofia kuchapwa na walimu hao

4. Wanawapanga watoto cha kusema maafisa elimu wanapopanga kuja kutembelea shule! Huwa wanawatishia kuwa atakayesema atafukuzwa shule n.k

Kwa mifano michache ya tabia hizi hawa walimu wanatufundishia tabia mbaya sana kwa watoto!

Tunaomba waziri wa elimu ukalitazame hili, maafisa elimu wako hawatumii mbinu kuwahoji watoto hata kushtukiza,

Walimu wakuu wanakula a kugawana migao ya michango mbalimbali ya watoto..

Ni tabia mbaya sana kuwafanya watoto dili badala kuwafundisha maadili mema!

Tunaandaa watekaji wa baadae pasipo kujua wanaoligharimu taifa!
Ndugu twende kwenye shule binafsi za msingi huko wanafundishwa jinsi kusaidiana kwenye mitihani ya moko na ya kitaifa....
Hili nimelishuhudia kwenye shule nyingi za msingi za binafsi jijini Dar es salaam,mwaka juzi niliandika mchezo mzima wa wizi na udanganyifu wa mitihani kwa ushahidi.
Nilitaka niwatumie NECTA,TAMISEMI,wizara husika ya elimu, ofisi ya waziri mkuu,afisa elimu mkoa na wilaya lakini Kuna watu walinitisha sana eti nitarogwa au nitajiingiza kwenye matatizo makubwa sababu nchi yetu haieleweki na haiwezi kukulinda mtoa taarifa.
 
Broo twende kwenye shule binafsi za msingi huko wanafundishwa jinsi kusaidiana kwenye mitihani ya kitaifa....
Hili nimelishuhudia kwenye shule nyingi za msingi za Dar es salaam,mwaka juzi niliandika mchezo mzima wa wizi na udanganyifu wa mitihani kwa ushahidi.
Nilitaka niwatumie NECTA,TAMISEMI,wizara husika ya elimu, ofisi ya waziri mkuu,afisa elimu mkoa na wilaya lakini Kuna watu walinitisha sana eti nitarogwa au nitajiingiza kwenye matatizo makubwa sababu nchi yetu haieleweki na haiwezi kukulinda mtoa taarifa.
Mwambie huyo maana hajui lolote
 
Walimu wanatembea na vipipi mifukoni vya kuwakopesha wanafunzi kwa lazima ! Unategemea mtoto anajifunza nn kama siyo kuanza kuwa mdokoz ili akalipe madeni kwa hofu ya viboko,
Wengine ndo kabisa ni rahisi kulawitiwa ili wapate pesa ya kulipa
Atajifunza ujasiriamali.....

Mnapigiaga kelele vitu ambavyo wala havina ishu sasa mwalimu kuuza pipi nayo ishu? Watu wanajichotea tu mahela kimyaaaa sh 100 ya mwalimu yowe. Mzazi mpe mwanao hela mwalimu ainjoi 😹
 
Ujue kuna tabia ndogo tunazichukulia poa ila zinaligharim sana taifa!
Kufundisha watoto uongo, kufundisha watoto wizi ndiyo maana kuna vitoto vya shule huko mtaani vinaranda randa kuomba mia kumbe vinaogopa shuleni vinadaiwa na walimu mia mia za pipi vilikopeshwa kwa lazima!

Ujue mtoto mdogo anapokuwa stressed na videni kama hivyo ni rahisi hata kulawitiwa ili apate pesa ya kumpa mwalimu shuleni ili asizomewe na watoto wengine kuwa anadaiwa
haaa umekazia kwel
 
Mpeleke mtoto shule za maana, ushasikia st what mwalimu anauza visheti? Au Ilboru huko mwalimu anauza vipande vya biscuit??

Ukimleta chaurembo shule ya msingi, tutamuuzia tu 😹
😂😂😂😂
 
Hata olympio na diamond pirika hzo zimejaaa hasa darasa la kwanza na la pil vile vile wanandaa home package kila likizo mtoto lazima anunue na mzazi hapew report bila ya kununua sasa report wenyew shallow to extent hazieditiwi na kuhaririwa kwa usahihi halafu wakirudi likizo hawaulizwi hata wanafunzi kama wakuja nazo ili wazisahihishe na zinazoenda shule wanazirundika na kuyatup in bulk mbali na kulazimisha visafar vya nke ya shule bt mifumo hii wamepangana kuanzia the big boss
 
Nimefanya uchunguzi wangu katika shule za msingi za serikali nimebaini mambo ya ajabu sana yanafanywa na baadhi ya walimu kwa watoto!

Kuna tabia za ajabu ajabu kutoka kwa baadhi ya walimu ambao wabadhamana ya kulea watoto wetu kielimu!
Miongoni mwa mambo niliyobaini

1. Walimu hawafuati ratiba ya masomo! Mfano ratiba ya siku ya watoto somo A, anaingia mwalimu wa somo E n.k hii inawafanya watoto wabebe mizigo mikubwa jambo linalowaathili kiafya ukubwani

2. Baadhi ya walimu wanafanya vibiashara kwa lazima kwa watoto mfano! Mwalimu anakuwa na biskuti zile za azam za miatano! Anazibanua kipande kimoja kimoja anawauzia watoto kila kipante cha biskuti tsh 100! Ambae hana anakopesha kwa nguvu kesho alete hela.

3. Baadhi ya walimu wanaingia kwenye darasa wanawagawia visheti, viubuyu watoto kwa lazima na kuwadai pesa jambo linalowafundisha watoto tabia mbaya ikiwemo wizi kwa kuhofia kuchapwa na walimu hao

4. Wanawapanga watoto cha kusema maafisa elimu wanapopanga kuja kutembelea shule! Huwa wanawatishia kuwa atakayesema atafukuzwa shule n.k

Kwa mifano michache ya tabia hizi hawa walimu wanatufundishia tabia mbaya sana kwa watoto!

Tunaomba waziri wa elimu ukalitazame hili, maafisa elimu wako hawatumii mbinu kuwahoji watoto hata kushtukiza,

Walimu wakuu wanakula a kugawana migao ya michango mbalimbali ya watoto..

Ni tabia mbaya sana kuwafanya watoto dili badala kuwafundisha maadili mema!

Tunaandaa watekaji wa baadae pasipo kujua wanaoligharimu taifa!
Mwalimu Mpwayungu Village njoo huku mnasemwa!!
 
Back
Top Bottom