KERO Udidimizaji wa Haki za Wahandisi wanaofundisha Shule za Sekondari za Ufundi ni changamoto inayohitaji utatuzi wa haraka

KERO Udidimizaji wa Haki za Wahandisi wanaofundisha Shule za Sekondari za Ufundi ni changamoto inayohitaji utatuzi wa haraka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari,

Mimi ni mhandisi ambaye niliajiriwa ajira za waalimu kwa tangazo la mwaka 2020 kwa niaba ya wenzangu wahandisi kutoka shule za ufundi tunapenda kutoa masikitiko yetu juu haki zetu kama watumishi wa umma.

Ikumbukwe serikali ilituajiri tukiwa wahandisi lakini mambo yalibadilika tulivyoripoti vituoni ambapo walitupa baadhi ya stahiki za ki-ualimu ili hali sisi si waalimu hivyo kupelekea kukosa baadhi ya stahiki muhimu ikiwemo kuthibitishwa kazini na kupanda madaraja na zingine nyingi, badala yake serikali kupitia katibu mkuu TAMISEMI inatutaka tukasomee POSTGRADUATE DIPLOMA YA UALIMU ili tuwe waalimu 100%.

Suala la kusoma ni jambo la hiyari, matokeo yake wametuacha huku wakijua kuwa hawatupi stahiki zetu na wakati huo huo tunaendelea kutekeleza majukumu ya kuwafundisha watoto, kibaya zaidi tukijaribu kuomba kuhamia kwenye taasisi zenye muundo wa kihandisi wakurugenzi wa Wilaya na Manispaa zilipo shule hizo hawaruhusu hata kutoa maoni yao kwenye barua za kuomba uhamisho.

Hii ni kinyume cha utaratibu wa kanuni za kudumu za Utumishi wa Umma na Utawala Bora zinazomtaka mwajiri ambaye ni Mkurugenzi atoe maoni yake kwenye barua na si kukataa kupitisha barua.

Naomba serikali imalize hii changamoto kwa maslahi mapana ya elimu ya amali, vinginevyo wanufaika wa elimu ya amali ambao ni wanafunzi, wapo kwenye wakati mgumu sana maana wahandisi wanaowafundisha wanafunzi wa shule hizo wanafanya 'bora liende' tu kwakuwa tumetelekezwa, hakuna anayejali kuhusu sisi.

Screenshot 2024-07-26 at 07.03.34.png
Screenshot 2024-07-26 at 07.04.50.png
Screenshot 2024-07-26 at 07.05.03.png
 
Umeweka hoja nzuri Sana.
Itawasaidia watu wengi.
Poleni wahandisi.
Waalimu wetu wa "nyunga". Hapa watu wa technical school watanielewa.
 
Watanzania vichwa venu ni vigumu,mashariti ya ajira yalisema utaajiriwa kama Mwl. Daraja la IIIB na C-na hili ndio kigezo kikubwa.Ni vizuri ukiwa Roma ishi kama Waroma waishivyo-kasome update uhalali wa kuwa Mwl.
 
Mimi nadhan ungetuwekea mkataba wa ajira ili tuone mkataba ulikua unasema nini, maana inawezekana mwajiri ana shida au inawezekana shida ipo kwako maana watanzania hatusomagi vipengele vya mkataba, tunaangalia maeneo ya kusaini tu
 
Back
Top Bottom