Habari, mimi ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Matokeo ya mwaka huu yametoka, lakini kwa baadhi yetu yamewekwa kwenye mfumo kama “withheld”, licha ya kuwa tumekamilisha malipo yote ya ada na hatuna deni lolote la chuo.
Chuo kimetoa namba ya Bursar ambayo wanafunzi wenye changamoto hizi wanatakiwa kuwasiliana nayo kwa ajili ya kupata ufafanuzi. Hata hivyo, unapopiga simu kwenye namba hiyo, mara nyingi inakuwa busy na baadaye inakuelekeza kwenye namba nyingine ambayo haipokelewi.
Kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba mitihani ya marudio (supplementary examinations) inaanza Jumatatu, lakini hadi sasa baadhi yetu bado hatujaweza kuona matokeo yetu kwa sababu yamewekwa “withheld”.
Tunaomba UDOM itoe ufafanuzi kuhusu sababu ya matokeo hayo kuzuiwa kwa wanafunzi ambao wameshakamilisha malipo yao, pamoja na kuweka utaratibu wa haraka wa kushughulikia changamoto hii kabla ya kuanza kwa mitihani ya marudio.
Mwanafunzi anapaswa kujua matokeo yake kwa wakati ili aweze kujipanga ipasavyo kwa hatua inayofuata ya masomo. Tunaomba suala hili lishughulikiwe haraka.