Takribani mwezi mmoja tangu matokeo ya muhula wa pili kutangazwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma, zaidi ya wanafunzi 2,000 bado wanakabiliwa na changamoto ya matokeo yao kuonesha ujumbe wa “Result Withheld” wanapoingia kwenye akaunti zao.
Hali hii inazua hofu zaidi kwa kuwa mitihani ya marudio ilianza Oktoba 12, 2026. Wanafunzi wana wasiwasi kwamba huenda wakakosa kufanya mitihani hiyo na kuishia kufukuzwa chuo (disco).
Kila siku kumekuwa na matangazo kwamba suala hilo linafanyiwa kazi, lakini hadi sasa hakuna muafaka unaoonekana. Wanafunzi wanaendelea kuwa na wasiwasi huku muda wa kufanya mitihani ukiendelea kuyoyoma.