UDOM yatoa ufafanuzi wa madai ya Wanafunzi 400 kuondolewa masomoni, wasema walidukua mfumo na kuchezea matokeo ya mitihani

UDOM yatoa ufafanuzi wa madai ya Wanafunzi 400 kuondolewa masomoni, wasema walidukua mfumo na kuchezea matokeo ya mitihani

Za kukariri.., kama suala ni kutengeneza motor, mtu apewe vifaa aanza kufanya assembly.., mambo ya Faradays law na Ohms law akae nayo kichwani kwake, si ameshasoma? Sisi tunataka motor izunguke na pump ipandishe maji, hapo ndio mwalimu ataoe maksi…
Mwl mwenyewe ukute hawezi kufanya hivyo, badala yake ni mtaalamu tu wa Theory.
 
Mwl mwenyewe ukute hawezi kufanya hivyo, badala yake ni mtaalamu tu wa Theory.
Ndio maana inabidi tutoke kwenye huu mfumo wa elimu usio na tija. Mtu asome law zote anazotaka yeye, ila kwenye mtihani tunataka adanye assembly na Radio iwake na ishike frequency zote za F.M na A.M, hapo ndio unapewa maksi.., sio hii elimu ya kipimbi.., mtu anafanya titration hata haelewi ina faida gani…
 
Nadhani chuo kingefanya uchunguzi kujua kama wadukuzi ni wanafunzi wao au ni walinunua experts nje ya chuo na pengine nje ya nchi.
Kama wadukuzi ni wanafunzi wao,walitakiwa wawatunuku shahada zao hata kama ni first year
 
TAARIFA SAHIHI KUHUSU TUHUMA ZA WANAFUNZI 400 WANAODAIWA KUONDOLEWA MASOMONI

Kusoma taarifa ya awali, bofya hapa ~ Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Kuna Nini? Wanafunzi zaidi ya 400 wame disqualify

Chuo Kikuu cha Dodoma kimepitia taarifa zinazosambazwa mitandaoni za madai zenye madai ya wanafunzi 400 kufutwa masomo kwa tuhuma za kudukua mfumo. Ukweli ni huu;

Jumla ya wanafunzi 170 walituhumiwa kuchezea Mfumo wa matokeo (SR2) Mwaka 2023/2024. Serikali iliunda Kikosi Kazi kilichohusisha wataaalamu wa Mifumo ya Komputa kuchunguza tuhuma hizo na kuwasilisha ripoti yao Chuo Kikuu cha Dodoma. Baada ya Chuo kupokea ripoti hiyo hatua za ndani zilianza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwapa wito watuhumiwa kuja kusikilizwa kabla ya kutoa maamuzi kwa mujibu wa Kanuni zilizopo.

Jumla ya wanafunzi 148 walisikilizwa, wanafunzi 32 hawakufika kusikilizwa. Katika wanafunzi waliosikilizwa, wanafunzi 121 walipatikana na hatia ya kuhusika kuchezea matokeo ya mitihani na kikao cha Seneti ya Chuo kupitisha kuondolewa masomoni (Discontinue). Kesi za wanafunzi 15 zinaendelea na uchunguzi zaidi. Wanafunzi wawili hawakukutwa na hatia.

Kwa mujibu wa taratibu za Chuo Kikuu cha Dodoma, mwanafunzi ambae hajaridhika na maamuzi ya Seneti anapewa nafasi ya kukata rufaa. Hivyo wanafunzi ambao hawajaridhika taratibu ziko wazi, wana fursa ya kukata rufaa kupitia mifumo iliyowekwa na Chuo.

Dirisha la rufaa hufunguliwa wiki mbili baada ya matokeo ya mitihani kutoka na kufungwa baada ya wiki mbili. Mwanafunzi ambae yupo nje ya muda, anaruhusiwa wakati wowote kuomba kukata rufaa nje ya muda

Chuo kitaendelea kusimamia taratibu, Kanuni na Sheria za kimitihani ili kulinda ubora wa taaluma na hadhi ya Chuo, pasipo kumuonena mtu yeyote.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Masoko (UDOM)
22/2/2025
Siku hizi ni mwendo wa kutoa UFAFANUZI kila mahali....
 
Back
Top Bottom