KERO UDSM main campus kuwanyima haki wanafunzi wanaovaa kofia za cap kutumia baadhi ya huduma

KERO UDSM main campus kuwanyima haki wanafunzi wanaovaa kofia za cap kutumia baadhi ya huduma

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Imekuwa ni kawaida kwa walinzi kuwalazimisha wanafunzi kuvua kofia za cap wanapoingia library au sehemu za maofisi, huu ni unyanyasaji dhahiri kwa watanzania ambao wanatumia uhuru wao wa kuvaa kunyimwa haki ya kutumia maeneo muhimu ya kujifunza na kujifunzia. Sababu ya msingi kwanini wanazuiliwa kuingia maeneo hayo zinakuwa hazieleweki.

Je, kuna tatizo gani mtu akiingia library au kwenye ofisi akiwa amevaa kofia ya cap? Je, kuna hatari gani ya kiusalama itatokea kama huyu mtu atakuwa amevaa kofia ya cap.

Kuna watu wana matatizo mbalimbali yanayopelekea kuvaa kofia lakini unakuta hata mtu wa namna hiyo analazimishwa kuvua kofia.

Muda sasa umefika kwa Uongozi wa UDSM kuachana na fikra za kizamani na kuendana na mabadiliko ya dunia na kuruhusu vitu visivyo na madhara sio kwa usalama wa chuo na usaidizi wa kujisomea kuendelea.
 
Unsposoma degree unaweza kuajiriwa sehemu yoyote na nafasi yoyote. Sasa vijana wa Leo ukiwa boss Kuna namna ya kuishia tofauti na zamani na suala la etiquette and protocol wanatakiwa kuanza kulijifunza wakiwa hapo hapo
 
Unatakiwa kuzingatia utaratibu wa mavazi ktk sehemu mbalimbali, cap sio vazi rasmi la ofisini. Ukienda ktk ofisi yeyote ya serikali vua cap Yako ukitoka ndio uvae. Hao askari wapo sahihi
Imekuwa ni kawaida kwa walinzi kuwalazimisha wanafunzi kuvua kofia za cap wanapoingia library au sehemu za maofisi, huu ni unyanyasaji dhahiri kwa watanzania ambao wanatumia uhuru wao wa kuvaa kunyimwa haki ya kutumia maeneo muhimu ya kujifunza na kujifunzia. Sababu ya msingi kwanini wanazuiliwa kuingia maeneo hayo zinakuwa hazieleweki.

Je, kuna tatizo gani mtu akiingia library au kwenye ofisi akiwa amevaa kofia ya cap? Je, kuna hatari gani ya kiusalama itatokea kama huyu mtu atakuwa amevaa kofia ya cap.

Kuna watu wana matatizo mbalimbali yanayopelekea kuvaa kofia lakini unakuta hata mtu wa namna hiyo analazimishwa kuvua kofia.

Muda sasa umefika kwa Uongozi wa UDSM kuachana na fikra za kizamani na kuendana na mabadiliko ya dunia na kuruhusu vitu visivyo na madhara sio kwa usalama wa chuo na usaidizi wa kujisomea kuendelea
 
Wasomi wa ovyooo kabisa,hujui hata secirity issue ndogo ndogo kama,hizo ni rahisi kwa mualifu kufichaa muonekano wa sura na cap.ulizaliwa na cap wewe
Wewe ULIZALIWA na nguo wewe?? mbona unavaa Nguo unaficha nn, Kwan ulizaliwa na Nguo?? Tuacheni kukariti Maisha usomi hauuusiani na kuvaa, swala la uvaaji ni destuti ya mtu wala sio usomi, Msifikir mtu kusoma ndo kutachange utaratibu wake mzima jinsi anavopenda kuishi na kuonekana, Ukitaka Rasta fuga rasta rasta hazimfanyi mtu aache kuwa na akili. Ni kukariri tu vitu visivyo na Tijaa
 
images (33).jpeg
 
Huo sio utaratibu wa UDSM tu . Hauwezi kwenda pia kwenye ofisi za uma na kofia au pensi au viatu vya wazi. Huo ni utaratibu .
Tafuta tu pesa viatu vya wazi tunaingia navyo adi ofsi ya waziri
Kiatu cha wazi kinaunzwa elf65 ad lk3
 
Ongea vizuri mjomba, cap ndio nini? Sema kofia ya kijembe
 
Back
Top Bottom