KERO UDSM main campus kuwanyima haki wanafunzi wanaovaa kofia za cap kutumia baadhi ya huduma

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Uzi wa kijinga kabisa... kila sehemu kuna utaratibu.
Subiri uwe na familia yako utaanzia hapo kuset standards zako then kuwa na biashara binafsi uishi utakavyo.

Nonsense
 
Wasomi wakubwa mnashindwaje kujua ni wapi uvae mavazi stahili na hapo? Si kila mahali unaweza kuvaa tu mavazi uyatakayo, kuna coding za mavazi yake, vinginevyo utaonekana ni muhuni au mshamba fulani asiyejua kuvaa mavazi yanayostahili mahali hapo
 
Imekuwa ni kawaida kwa walinzi kuwalazimisha wanafunzi kuvua kofia za cap wanapoingia library au sehemu za maofisi, huu ni unyanyasaji dhahiri kwa watanzania ambao wanatumia uhuru wao wa kuvaa kunyimwa haki ya kutumia maeneo muhimu ya kujifunza na kujifunzia. Sababu ya msingi kwanini wanazuiliwa kuingia maeneo hayo zinakuwa hazieleweki.

Je, kuna tatizo gani mtu akiingia library au kwenye ofisi akiwa amevaa kofia ya cap? Je, kuna hatari gani ya kiusalama itatokea kama huyu mtu atakuwa amevaa kofia ya cap.

Kuna watu wana matatizo mbalimbali yanayopelekea kuvaa kofia lakini unakuta hata mtu wa namna hiyo analazimishwa kuvua kofia.

Muda sasa umefika kwa Uongozi wa UDSM kuachana na fikra za kizamani na kuendana na mabadiliko ya dunia na kuruhusu vitu visivyo na madhara sio kwa usalama wa chuo na usaidizi wa kujisomea kuendelea.
Mtarajiwa wa kuwa Graduate unavaa Cap??
Nenda tume ya Ajira ukiwa umevaa cap,ili ufaulu mtihami upangiwe kazi.
 
Unapoenda sehemu inabidi ufate utaratibu tu kama hauwezani nao basi , wewe ndio mwenye shida Wala hapo ulipoenda hapana uhitaji na wewe , kwà sababu wewe una uhitaji na hyo sehemu uliyoenda basi inabidi ufate utaratibu tu
 
Universities should be multicultural. Kama unataka kudhibitisha sura kagua kitambulishi na sura yake kama vinaendana muache avae kofia yake.
 
Kuffi hats, Hijabs, Wigs, Veils, Turban and Sandals with Kanzu aren't a problem, but wearing a cap is a problem.

UDSM is conclave of madness.​
 
Tujifunze kufuata utaratibu na kuzingatia muktadha wa eneo husika. Hii kupuuza puuza vitu ndo maana tunakosa fursa hata kwenye mashirika na taasisi kubwa za kigeni ama hata kwenda/ kufanya kazi nchi zilizoendelea. Watu wamekwambia vua cap we unakuja kulalamika huku tena?! Babako tu huwezi kuongea nae huku unamchungulia kwa hilo licap lako afu unakuja kuzungumzia sehemu ambayo inakuandaa kuja kuitumikia jamii na taifa kwa ujumla!
 
Vijana ujuaji mwingi ndio maana wanaoajirika wachache kuwa presentable kunamtambulisha mtu pia kunakupa confidence, kama hutaki endelea kuvaa jeans na kofia maeneo formal.
 
Library Kuna tatizo gani kwenda na Cap ?
Tii mamlaka na ufuate Sheria
Usipovaa cap utazimia?
Au Kuna jua kali humo ndani kwamba litakubabua kichwa.

Taasisi nyingi za kiserikali hata zisizo za kiserikali kuna dress code.
Cap ni informal.
Hutaki kufuata taratibu basi jifungulie tu library yako binafsi ambayo unaweza kujiwekea utaratibu wa kuvaa cap au chochote unachotaka.
 
Mnalilia kuvaa kofia darasani ? hivi hiyo UDSM ya sasa ikoje?
 
Imekuwa ni kawaida kwa walinzi kuwalazimisha wanafunzi kuvua kofia za cap wanapoingia library au sehemu za maofisi, huu ni unyanyasaji dhahiri kwa watanzania ambao wanatumia uhuru wao wa kuvaa kunyimwa haki ya kutumia maeneo muhimu ya kujifunza na kujifunzia. Sababu ya msingi kwanini wanazuiliwa kuingia maeneo hayo zinakuwa hazieleweki.

Je, kuna tatizo gani mtu akiingia library au kwenye ofisi akiwa amevaa kofia ya cap? Je, kuna hatari gani ya kiusalama itatokea kama huyu mtu atakuwa amevaa kofia ya cap.

Kuna watu wana matatizo mbalimbali yanayopelekea kuvaa kofia lakini unakuta hata mtu wa namna hiyo analazimishwa kuvua kofia.

Muda sasa umefika kwa Uongozi wa UDSM kuachana na fikra za kizamani na kuendana na mabadiliko ya dunia na kuruhusu vitu visivyo na madhara sio kwa usalama wa chuo na usaidizi wa kujisomea kuendelea.
Umeenda kusoma ay kuvaa kofia?
 
Ongea vizuri mjomba, cap ndio nini? Sema kofia ya kijembe
Msomi mzima mleta mada anaandika mada ndefu kuhusu kofia badala ya kuandika mada za kitaalamu za kutatua changamoto ya nchi

Huyu atakuwa nayesoma digrii za Arts hao ndio huwa na mambo ya kijinga jinga
 
Principal Mitano tena(Codes of conduct),halafu kuvua haitoshi,wahenga tunasema "uhuru ukizidi ni utumwa"
 
Huyu mtoa mada anadhalilisha kwa kuthibitisha umma kwamba hata hiyo elimu anayopata inatia mashaka! Unapata muda wa kuzungumzia kofia ili utetee uhuni sehemu zenye itifaki? Elewa kwamba hata kuvaa cap au miwani nyeusi sehemu yeyote yenye itifaki au kuongea na mtu umevaaa miwani ya Aina hiyo ni ishara kubwa ya dharau, kuna vijana frani walipata nafasi sehemu x usahili kilichowachomoa kukosa kazi ni kisasa Bila tahadhari, miwani nyeusi na kofia. Kulialia mitandaoni ili mtafute uhuruma,za kutetea ujinga huo ni mama!
 
Imekuwa ni kawaida kwa walinzi kuwalazimisha wanafunzi kuvua kofia za cap wanapoingia library au sehemu za maofisi, huu ni unyanyasaji dhahiri kwa watanzania ambao wanatumia uhuru wao wa kuvaa kunyimwa haki ya kutumia maeneo muhimu ya kujifunza na kujifunzia. Sababu ya msingi kwanini wanazuiliwa kuingia maeneo hayo zinakuwa hazieleweki.

Je, kuna tatizo gani mtu akiingia library au kwenye ofisi akiwa amevaa kofia ya cap? Je, kuna hatari gani ya kiusalama itatokea kama huyu mtu atakuwa amevaa kofia ya cap.

Kuna watu wana matatizo mbalimbali yanayopelekea kuvaa kofia lakini unakuta hata mtu wa namna hiyo analazimishwa kuvua kofia.

Muda sasa umefika kwa Uongozi wa UDSM kuachana na fikra za kizamani na kuendana na mabadiliko ya dunia na kuruhusu vitu visivyo na madhara sio kwa usalama wa chuo na usaidizi wa kujisomea kuendelea.
Eti hizi ndio brains🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮
Maliza uende veta.
 
Kijana tii taratibu acha kuja kudekea humu JF,
suala la kofia ni suala dogo sana,

Hata ATM hupaswi kwenda kutoa hela ukiwa umevaa Cap kwa taratibu za kiusalama,

Kwahyo kama huwez kufata hizo taratibu sii lazima usomee library, utasoma zako magetoni tu au venue kwa taratibu unazozitaka wewe.
 
Back
Top Bottom