KERO UDSM main campus kuwanyima haki wanafunzi wanaovaa kofia za cap kutumia baadhi ya huduma

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mvumilieni mleta mada. Huenda ana komwe kubwa au uso mpana hivyo anajisikia confortable akiwa na hiyo cap au mzula.
 
Sisi hili nalo ni kero?? Kila ofisi na utaratibu wake, kikwetu hata salam huku umevaa kofia si uungwana, cap ktk ofisi nyingi inaonekana kama uhuni. Fuata maelekezo hakuna kero hapo. Unaenda kuswali mskitini unaingia na viatu si sahihi, unaenda kanisani umevaa bukta si sahihi, vivyo hivyo mwanachuo kwenda ofsini unazungumza na kiongozi wake huku umeweka kofia lako.
 
Library ni ofisini ?
LIbrary kwa sehemu zilizoendelea kuna camera kwa ishu ya usalama sasa ww na cap lako unaficha nini?? Hata library ni ofsi ya mkutubi anayewapa wateja huduma.
 
Ishu kubwa ni usalama kama unatatizo la kiafya vaa kibaragashia inatakiwa uso wako uonekane kwenye camera
 
Mei mosi utawakuta hao wanaosema cap uhuni wametinga macap, hata waliokaa kivulini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…