UDSM mnakosa hata Solar power karne hii?

UDSM mnakosa hata Solar power karne hii?

Andrew123

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2012
Posts
8,358
Reaction score
10,976
Mna vitivo vya Uhandisi, sayansi, ICT sheria ila mpaka zama hizi mnakosa Solar power project kusaidia wakati wa mgao? Mbona mnanunua V8/VX kila uchwao?

Mnakwama wapi?
**Kipi ninajivunia miaka 60 ya kuanzishwa kwenu?
 
Nilidhani ungeshangaa mgao wa umeme karne hii wakati kila uchwao serikali inanunua magari mapya ila kwenye vitu vya msingi vinatumika vya karne ya 19! Sasa kwa akili yako, mpaka leo hii kuna haja ya kutumia TypeWritter zile za zama za giza!?
 
Unashindwa kushangaa mgao wa umeme hadi kipindi cha mvua kubwa kama hizi alafu unaongelea taasisi ambayo ipo chini ya wizara nyingine?

Tanesco kwenye wizara ya nishati unaweza kusema inajitegemea hata kwenye bajeti inatengewa bajeti yake lakini bado kuna mgao.
 
Nilidhani ungeshangaa mgao wa umeme karne hii wakati kila uchwao serikali inanunua magari mapya ila kwenye vitu vya msingi vinatumika vya karne ya 19! Sasa kwa akili yako, mpaka leo hii kuna haja ya kutumia TypeWritter zile za zama za giza!?
Kuna watu watakuambia wanatumia typewriters kwa sababu ya usalama ili wasijue siri za nchi 😄 🤣
Wanapowazaga haya ndio huwa natamani kufa 😄
Yaani wanajifananisha na Russia au Korea na us
 
Mnapenda kuwaza mambo madogo madogo, badala ya kushangaa nchi kuwa na mgao wa umeme miaka 60 baada ya uhuru, wewe unawashangaa UDSM kukosa solar power!
Taasisi inayozalisha wasomi ilitakiwa kuwa na mbadala wa umeme wa uhakika ili hata wasomi wake wakitoka hapo waone kuwa ni aibu nchi kuwa gizani waweze kutatua.
 
Huo ni mfano halisi tu ila nchi kama nchi kusema kweli kabisa tuna shida sana.

Nikuhakikishie tatizo la kweli la nchi yetu wala sio hayo ya mgao sijui V8 siju ila ni mindset za watu. Kubali kataa bado tunasafari ndefu sana ili kufanana na binadamu wengine. Nitakupa mifano michache sana hapa chini

1. Polisi na wanajeshi ndio wasimamizi wakuu wa sheria lakini

a. Hawalipi nauli hata kama wanaenda mizunguko yao binafsi
b. Hawasimami kwenye foleni au kwenye traffic lights hata kama hawana emergency yoyote anatoka kazini au anaenda kazini
c. Polisi na usalama wa Taifa badala wasimamie sheria kwa haki wakati wa uchaguzi wanakuwa washirika namba moja kuiba kura na kukibakiza madarakani chama fulani hata kwa gharama za kuuwa watu

2. Tazama uendeshaji wa boda boda au daladala. Haijalishi kuna nini yeye lazima anataka kuwa mbele kabisa. Kwenye taa nyekundu hawasimami hata kama traffic yuko hapo au ndio anaongoza magari.

3. Utakuta mtu ana li V8 asubuhi anaenda kazini kavaa tai na suti ila barabarani anatanua hataki kukaa foleni hata kama hana emergency yoyote na huyu eiza ni mfanyabiashara au ofisa wa serekali ila kachelewa kutoka kwake sasa anapita barabarani kwa kutanua hataki kufata foleni

4. Wabunge, mawaziri na Rais hawalipi kadi kwenye mishahara yao na kila siku wako majukwaani wanaongelea umuhimu wa kadi na wanatunga sheria kukamata raia wasiolipa kadi

Ni mind set zetu tu tukiweza kuziweka sawa nchi hii maendeleo ndani ya miezi 6 tu mbona tunapata
 
Back
Top Bottom