UDSM, MUHAS & UDOM Vinashika Nafasi Tatu za juu kwa Vyuo Vikuu Kumi Bora Tanzania

Wote mnaosoma ranking za vyuo huwa mnakosea kitu kimoja muhimu sana tena sana. Wanaopanga hivyo vyuo huzingatia hasa ukubwa wa chuo na wingi wa vitivo na kozi za hapo. Chuo chenye vitivo 10 kitaonekana kikubwa kuliko chuo chenye vitivo 4 specialized.

Mfano DIT inaonekana ni ya chini kwa SAUT kutokana na SAUT ina kozi nyingi na majengo mengi. XXX ukianzisha chuo ukafundisha degree za kulea watoto na kufua nguo na design hiyo zikawa nyingi, mwingine YYY akaanzisha Institute inafundisha aircraft engineering na aeronautics pekee basi XXX unaonekana una chuo bora.

Marekani pale kuna vyuo kama Yale na Harvard vinatoa kozi nyingi sana na ni vikubwa, huwa vinaonekana ni vya juu kwenye ranks kuliko MIT ambayo kama huna akili kwanza hukanyagi pale, na ukikanyaga 'hutoboi' hata ulale juu ya mawe. Bado kuna chuo kimejikita kwenye afya tu cha John Hopkins University pale Maryland, private ila hakanyagi kilaza pale. Ile hata top 5 huikuti ila imetoa chanjo kibao na wanafunzi wake na maprof wake wanatibu magonjwa makubwa vibaya mno.

Hata pale UK haya mambo ndio yalifanya Cambridge University ijitenge na Oxford University pale Uingereza. Oxford ni pana na inapenda sanaa, Cambridge inafundisha sayansi zaidi na ni ndogo. Kwenye ranks utakuta Oxford ni kubwa.

Binafsi napendelea nchi iwe na specialization kwenye vyuo, Universities ziwe hata tatu pekee na vingine viwe institutes zenye specialization, tuwe na DIT, NIT na MUST nyingi sio unakuta Degree za HR kila chuo sasa HR ni nusu ya chuo wanaenda kupanga rasiliamali watu wapi?

Architecture ya Ardhi inakubalika sana ila UDSM nayo ina level za dunia (from someone ambaye amesoma nje).
Electrical Engineering ya MUST ilionekana ni bora kuliko ya chuo chochote bongo kwa wastani wakati tunaulizia vyuo tukiwa A level na hiyo ndio imani ya watu walio kwenye field hiyo. Civil ya UDSM nzuri zaidi, niliona hili nilipokuwa CCECC Wachina wanaikubali Civil ya UDSM, hata Yappi Merkezi ni hivyo. Hesabu yoyote ya Mzumbe inakubalika mno, TIA wanafaulisha GPA za 4+ ila tia maji, mitihani yao inavuja sana kwa kuwa wanatunga kwa kuzunguka branches. Hata CPA zao huwa ni ufaulu, ila actual performance ni tofauti kabisa. Wanaojua accounting wataleta ushahidi ni wangapi maofisi ni CPA ila kupanga hesabu anashindwa hadi na mwenye Diploma, hasa pisi kali zina CPA sijui wanatoa wapi wale
 
Nenda ukasome sua mwez mmoja tu,,, uje urudie kucomment hiv [emoji23]
SUA napajua vizuri sana,kuhusu SUA huna la kuniambia.

Umewahi kuona chuo wanaweka wastani wa kufaulu mkubwa,halafu wanafunzi wakifeli wanaanza kusumbuana kuongeza chochote ili kufaulisha?,

Kuna vyuo bora ila SUA sikioni hapo labda kwa baadhi ya kozi ndio bado wako serious mfano VET pale.

Watu wanadhani ubora aa chuo ni kufelisha,nenda SUA hata leo ndio utajua kwanini wanafeli,nenda udsm angalia kwanini hakuna huu msemo bali SUA tu.
 
Utopolo Kama utopolo mwingine chuo Cha kata kinaingiaje 3 Bora
 
Mleta mada sijui umetumia criteria zipi ila nadhani inawezekana criteria ulizotumia zimepitwa na wakati!
Kwa taarifa yako SUA is the best University in Tz. Moja ya criteria ni hii ya kuwa na Publications nyingi kuliko chuo chochote.
Nimeambatanisha hapa MTAFITI namba moja Tz as of June 2022.
 
UDOM chuo cha kata ambacho hakitambuliki kimataifa kinachotoa phd kwa wanasiasa wa bongolala wakiwemo kina jafu, msukuma na biteko na chenyewe kinakipiku chuo nguli kama SUA, unaijua reputation ya Nelson Mandela University Internationally, au hizi ndo tafiti zinazofanyika kwenye vijiwe vya gahawa...
 
nimeona hilo bango mwanae masters udsm amempost mshua.
 
Bwana Kudasai Hiyo no moja ni kwa citation tu, na hapo reference yako ni AD index tu, ndiyo maana mimi katika kufanya utafiti wangu huu mdogo sikutumia reference moja, mfano mdogo tu ni Udom kwenye UniversityGru(UK) kimetajwa kama chuo namba 2 kwa ubora Tanzania. Hili kupata huwiano mzuri imenibidi nitumie criteria na references of ranking zaidi ya moja.
 
Tanzania hakuna chuo kikuu bora. Tuna bora vyuo.

Shukuru Mungu tu ana BET na Africa hata hawa Madaktari wetu hawajaiva kufa ni 50% Theatre!!
 
Bwana Nyumisa usiwe kama mwamba ngoma,Wewe ndiyo hukitambui, Udom kinatambulika kila sehemu duniani, tafuta references zako zote za vyuo bora Tanzania Udom utakikuta.
 
Tanzania hakuna chuo kikuu bora. Tuna bora vyuo.

Shukru Mungu tu ana BET na Africa hata hawa Madaktari wetu hawajaiva kufa ni 50 Theatre!!
Bwana WAZO2010 ina maana hata leo hujaona kazi kubwa walichokifanya madaktari MUHIMBILI kutenganisha mapacha walioungana?
 
Bwana T14 Armata naheshimu mawazo yako, lakini pia umeeleweka vizuri.
 
Bwana Alfred vipi ulisoma Mkuu Sekondari?
Hapana Mkuu, sikusoma huko Maeneo ya Rombo. Nilisoma Shule Moja Kongwe ipo maeneo ya Moshi mjini.. Ni Maarufu kama Shule ya sekondari ufundi Moshi Kabla ya kwenda kusoma High school pale Moshi School Miaka hiyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…