Look here Mwafrika wa kike,
Usijitie presha kwa kutetea vijana ambao hawaelewi ni kwa nini wanagoma. wanafunzi wengi waliopo chuoni pale kwa sasa na wao pia hawaelewi kwa nini kuna huo mgomo.
Bi mkubwa,
Heshima mbele mama.
Nilipokwenda Tanzania december mwaka jana, nilipitia Kahama kwa Uncle yangu. Nikiwa kwenye duka moja ya kuuza soda, kuna vijana walikuwa wakiongea namna ya kushinikiza wakazi wa Shinyanga yote kugomea mikataba bubu ya kuanzia Mwadui hadi Buzwagi.
Cha kushangaza, kuna baadhi ya watu walisema kuwa hakuna sababu ya kugombana na serikali au wazungu kwa ajili ya madini. Waacheni wachukue tu na waondoke watuachie nchi yetu - alisema mzee mmoja kwa uchungu.
It is simple math, unaenda chuo kikuu kusoma basi soma. Tunakubali kuwa chuo ni agent of change katika society na mchango wake kuthaminiwa katika nyanja mbalimbali za ujenzi wa taifa ikiwemo demokrasia. Sidhani chuo kikuu ni mahala pa kwenda kupigania demokrasia maana hakina autonomy kama wilaya au mkoa yenye centres of authority. Chuo kinabaki kuwa provider of social services among other things.
Kama wanafunzi wa vyuo vikuu vya marekani wangekaa na usemi wako huu miaka ya sitini wakati wa civil rights movements, leo hii bado america ingekuwa vietnam, blacks wasingekuwa wanapiga kura, na labda wanawake wangenyanganywa haki yao ya kupiga kura.
Kilichotokea kwenye campus za vyuo maarufu kama Columbia na UCLA miaka ya 60, kulibadilisha sera za marekani forever.
Mimi na wewe tuko mbali na nyumbani,let us wait and see how things unfold.
Kwa usemi wako, sioni pia sababu ya kuongelea mambo ya Buzwagi na Kiwira maana niko mbali pia.
Maana si haki kutetea mtu aliyekutwa na makosa na akapewa adhabu stahili. Hutakuwa tofauti na yule atakayemtetea Lowassa au Chenge kuwa wameonewa na hali hukuwepo kuwasaidia kuiba hizo fedha.
Unaongelea mambo tofauti kabisa hapa.
La mwisho, una ushahidi ya kuwa Mukandala ni fisadi, dikteta na muuaji? huyo mwanafunzi marehemu alikuwepo katika kundi lililoenda nyumbani kwa Mukandala na wakafanya vurugu kiasi cha kuvunja geti la kuingilia nyumbani kwake bahati nzuri familia ya Mukandala haikuwepo alikuwepo msaidizi wa kazi za nyumbani na ndugu mmoja. wakaondoka kwa hasira zao na kwenda Swimming pool wakavunja fridge lililokuwa na vinywaji baridi wakazimnywa zote na wakaanza kusheherekea kwa kuogelea ndipo huyo marehemu akarukia kwenye maji na kukumbana na kifo chake.
Naona wewe unaongelea mwanafunzi tofauti. Kuna habari ambazo bado hazijathibitishwa kuwa kuna mwanafunzi mjamzito amekufa kwa kupigwa na mabomu ya FFU jana mlimani. Kama hii ikithibitika kuwa ni kweli, Mkandara atajulikana kama Muuaji hapa JF mpaka siku nikipotea na mimi.
a. Huoni kuwa walikuwa wanahatarisha maisha ya familia ya mwalimu wao? Je ni sawa kitendo walichofanya?
b. Put yourself in Mukandala's shoes what would you have done?
c. Kuvunja kwa fridge, sio wizi among other things? Do you think they did the right thing.
Ningekuwa Mkandara nisingeingilia uchaguzi huru kabisa wa wanafunzi wangu.
Nimesoma UDSM na katika kusoma kwangu kulikuwepo na migomo miwili ambayo kwa bahati nzuri they were for sound reasons na utawala ukatuelewa na wala hatukufanya fujo hizo. Why now? Naomba ukubali kuwa we now have a new crop of students ambao ni matokeo ya dhambi nyingi ktk society. Hawa vijana walichokifanya hakina sound reasons up to now. They are just burning my P.A.Y.E. for no reasons at all.
Sidhani kama wakati umesoma mlimani uongozi wa chuo uliingilia uhuru wa wanafunzi wa kuchagua viongozi wao.