UDSM: Tunaomba msaada wenu JF!

UDSM: Tunaomba msaada wenu JF!

kama ni wengi na hawawezi kujibu hoja za msingi basi kizazi hiki ni cha vilaza vitupu. kitu gani kimeharibu UD ninayoifahamu?

ni makala ngapi hawajajibu.

msomi anapoomba msaada huwa anasema yeye kafikia wapi kimaandalizi, ila kwa hili tumewaomba hoja walizonazo ili tuwasaidie kuedit na wameshindwa kufanya vile. kinachofanyika ni kulia lia, hoo mkandala ni bata aliyeacha vifaranga nyuma etc.

wameshindwa kuturidhisha wale vijana waliofukuzwa kama sio wavuta bangi, au sio wote wavuta bangi, au wote ni wavuta bangi.

wameshindwa kuturidhisha kuwa yule mganda hakuonewa, maana kama hakuja na certificate ya form six, muda uliotolewa unatosha kuwa ametumiwa cheti chake halali. tangu february mpaka leo, jamani ems is a reasonable period for a serious person to have submitted his documents concerned.

tunasema hivi kulingana na hoja zinazoweza kutolewa kuwakandamiza wanafunzi pindi kunapotokea chuo kikafail a suit to the court of law.

wameshindwa kuconvince the majority of the population pale chuoni mpaka kutumia fimbo na fujo.

WAMESHINDWA WAMESHINDWA WAMESHIMDWA...

Wameshindwa kukuridhisha wewe na nani?
 
Angalia post zetu wote ni wapya, mmekuja kama mmeelekezwa kuwa JF watamaliza matatizo yenu, jitahidini kufuta sheria hata kama ni haki yenu, itachelewa lakini mtaipata, mwaka wa mwisho wanagoma ili iweje wamebakiza nearly two weeks kumaliza shule then wakipigwa mwaka mwingine inakuwaje. Je walikamatwa na bangi nao mnawatetea, wanaofanya ufusika mbele ya macho ya watu nao wanatetewa, tunajenga jamii gani ya wasomi wasio heshimu utamaduni wa mtanzania, hawa ndo wanaanza kujifunza ufisadi hukuhuku maana wanakua wanajua kuwa msomi anafanya anachotaka.

Swala la msingi hapa ni uongozi wa chuo kuingilia uchaguzi huru wa wanafunzi wa vyuo vikuu. Hii reflection ya kile kinachofanyika zanzibar na sehemu nyingi za Tanzania kila baada ya miaka mitano toka mwaka 1995.

Hizi kesi za kubambikiwa kila sehemu zipo na ushahidi upo hapa JF. WanaChadema waliopigwa na wanaccm kule Kiteto kwa amri ya Msekwa waliitwa kuwa ni majambazi.

Wapemba waliouwawa na CCM kule zanzibar waliitwa kuwa ni magaidi na wengine hata wakapandikiziwa mabomu nyumbani kwao. Huu mchezo wa Mkandara wa kutaka kupandikizia hawa watoto kesi ni upuuzi mkubwa na hautafaanikiwa katika dunia ya leo.
 
Usilitumie vibaya jina la Mwanamapinduzi na kamanda Chachage kwa upeo wenu mdogo wa kutafakari mambo! Kabla hujamhukumu Mzee Shivji ebu pitia historia yake enzi zake miaka ya 60 na 70 hata kipindi chote cha ujana wake hapo Chuoni utaipata vyema unataka aungane na upuuzi mlioufanya wa kutawaliwa na emotions badala ya rationality? mnaaibisha sana. Hata hivyo ni kweli kwamba chuoni kuna matatizo makubwa sana na sheria na kanuni zifuatwe kwa pande zote,wale wanaozembea na kusababisha matatizo kwa upande wa utawala nao wawajibishwe. Kwa wale tuliopita hapo tunafahamu vyema maana yake nini maji yanapokosekana Chuoni na hilo linaweza kutatuliwa bila hata ya VC kufahamu kama watendaji ngazi ya chini wanawajibika ipasavyo,

Sheria za chuo zianze kufutwa na fisadi, muuaji na dikiteta VC wa chuo - Mkandara ambaye amesababisha haya matatizo yote kwa kuingilia uhuru wa wanafunzi wa kutaka kuchagua viongozi wao.

Kuhusu bangi na madawa Mabibo hakuna uongo hapo,nimeishi miaka mitatu mabibo kule uwanjani usiku ni bangi tupu kiasi kwamba wengi wetu tukijiuliza hawa mameneja na madaktari na wanasheria aina gani watatoka kama sio mafisadi na kituo cha polisi kipo jirani tu na walinzi wanaolandalanda. Ebu tumieni busara katika namna mnavyowasilisha madai yenu.

Kama ulijua kuna bangi mabibo je ulifanya hatua yoyote kuitaarifu polisi? ohhh nimekumbuka kuwa wewe nawe ulikuwa miongoni mwa wavuta bangi hao!

Huyo bwana mdogo wa Uganda nae ana matatizo kama alifahamu kwamba kugombea nafasi kama Upresida wa UDSM huwa kuna zengwe kwanini hakujiandaa asiwapatie mwanya wa kumkamata!arudie kumsoma Machiavel asipoteze muda na ma law reports kama hamu yake ni siasa ona sasa kapoteza muda wa wafuasi wake watiifu!Hata kama lengo ilikuwa kumfanya asigombee lazima ufahamu mapungufu ya adui yako ili umumalize ebu waulizeni ndugu zenu wa Political science ama wote siku hizi mnasoma madesa hakuna wachambuzi tena?

Inaonekana wewe ndio unahitaji kurudi shule na kusoma vizuri hiyo political sayansi maana inaonekana madesa yamekuponza

Haki hupiganiwa kwa busara na hekima hapa si maanishi kwamba ili kuandamana kwa amani kwamba musubilie mpaka afande Tiba aseme yes kama SHY anavyoshauri maana huyu naye ana matatizo yake,bali nina maanisha kuhakikisha kwamba watawala hawapati kisingizio cha kushusha hadhi yenu machoni pa jamii,

Na hiki ndicho wanafunzi walichofanya hapa, kukataa kupandikiziwa viongozi wasiowapenda.

kwasasa mnaonekana kama wahuni kwa vitendo mlivyofanya! Jisafisheni ombeni radhi kwa jamii kisha leteni hayo madai yenu yachambuliwe!
ALUTA CONTINUA

Wale mnaotetea ufisadi ndio mnaonekana wahuni na ndio inabidi muombe radhi.
 
Once again wanafunzi wamegoma kuingia madarasani na kuna uvumi kuwa kuna mwanafunzi mmoja ambaye alikuwa mjamzito amefariki dunia.

Note:-
Ni uvumi uliotapakaa miongoni mwa wanafunzi ambapo habari hizi bado hazijathibitishwa na UTAWALA, ila baadhi ya wanafunzi wameandamana wakiimba MBINGUNI KUNA MAKAO MAZURI SANA.
Tungojee tusikie kama ni kweli haya wanayoyasema
.

Waga,

nijulishe tena hali ya huyo mwanafunzi anayesemekana kufariki imefikia wapi. Nitumie kwenye PM jina lake na course anayosoma.

Wakati sasa umefika wa kuongeza title nyingine kwenye jina la Mkandara - Muuaji
 
Tatizo ni wao Mkandara Ajiuzuru?kwa sababu gani ajiuzuru??mie nakwambia hakuna haja ya kuwasaidia hawa watoto waache wanende nyumbani then watarudi tena hapo tena kwa kuomba kurudi.

wanawatesa wenzao ambao hawana ndugu hapa Dar es salaam...

Hiki ndicho mafisadi mnapenda, kutesa ndugu zenu huku mkiwapigia magoti wakoloni kina Rostam Azizi, Manji na kichaka.

Unafurahia wenzako wakirudishwa nyumbani na kupata shida wakati wewe na wenzako mkiuza nchi? Hii serikali ya ccm kweli mmefika the lowest point you can get.
 
Hizi ni bangi tupu hapa na wanafunzi wa chuo wana akili na uwezo mkubwa wa kuona huu upuuzi unaotolewa na huyu anayejiita Lawyer
mwafrika wa kike inaonekana kuna information unakosa kuhusu masuala yanayoendelea UDSM, Sidhani kama unadata za kutosha kuhusu huo uchaguzi wa DARUSO na maamuzi yaliyofikiwa, ungekubaliana nami kwamba hawana hoja ya msingi kama nilivyoeleza awali.
 
Wewe bado hujatoa maelezo mbadala ya kwanini dikiteta na fisadi (ambaye soon ataitwa muuaji kama kifo cha mwanafunzi kikithibitishwa) Mkandara anaamua kuingilia uhuru wa wanafunzi kujichagulia viongozi wao.

Siwezi kuungana nawe ambaye unashauri wanafunzi kufanya fujo na kuvunja majengo huku ukiwabeza.
 
Look here Mwafrika wa kike,
Usijitie presha kwa kutetea vijana ambao hawaelewi ni kwa nini wanagoma. wanafunzi wengi waliopo chuoni pale kwa sasa na wao pia hawaelewi kwa nini kuna huo mgomo.

It is simple math, unaenda chuo kikuu kusoma basi soma. Tunakubali kuwa chuo ni agent of change katika society na mchango wake kuthaminiwa katika nyanja mbalimbali za ujenzi wa taifa ikiwemo demokrasia. Sidhani chuo kikuu ni mahala pa kwenda kupigania demokrasia maana hakina autonomy kama wilaya au mkoa yenye centres of authority. Chuo kinabaki kuwa provider of social services among other things.
Mimi na wewe tuko mbali na nyumbani,let us wait and see how things unfold. Maana si haki kutetea mtu aliyekutwa na makosa na akapewa adhabu stahili. Hutakuwa tofauti na yule atakayemtetea Lowassa au Chenge kuwa wameonewa na hali hukuwepo kuwasaidia kuiba hizo fedha.
La mwisho, una ushahidi ya kuwa Mukandala ni fisadi, dikteta na muuaji? huyo mwanafunzi marehemu alikuwepo katika kundi lililoenda nyumbani kwa Mukandala na wakafanya vurugu kiasi cha kuvunja geti la kuingilia nyumbani kwake bahati nzuri familia ya Mukandala haikuwepo alikuwepo msaidizi wa kazi za nyumbani na ndugu mmoja. wakaondoka kwa hasira zao na kwenda Swimming pool wakavunja fridge lililokuwa na vinywaji baridi wakazimnywa zote na wakaanza kusheherekea kwa kuogelea ndipo huyo marehemu akarukia kwenye maji na kukumbana na kifo chake.
a. Huoni kuwa walikuwa wanahatarisha maisha ya familia ya mwalimu wao? Je ni sawa kitendo walichofanya?
b. Put yourself in Mukandala's shoes what would you have done?
c. Kuvunja kwa fridge, sio wizi among other things? Do you think they did the right thing.

Nimesoma UDSM na katika kusoma kwangu kulikuwepo na migomo miwili ambayo kwa bahati nzuri they were for sound reasons na utawala ukatuelewa na wala hatukufanya fujo hizo. Why now? Naomba ukubali kuwa we now have a new crop of students ambao ni matokeo ya dhambi nyingi ktk society. Hawa vijana walichokifanya hakina sound reasons up to now. They are just burning my P.A.Y.E. for no reasons at all.
 
Wewe bado hujatoa maelezo mbadala ya kwanini dikiteta na fisadi (ambaye soon ataitwa muuaji kama kifo cha mwanafunzi kikithibitishwa) Mkandara anaamua kuingilia uhuru wa wanafunzi kujichagulia viongozi wao.

Siwezi kuungana nawe ambaye unashauri wanafunzi kufanya fujo na kuvunja majengo huku ukiwabeza.
Naona nawe unahitajika kutoa maelezo ya ziada na uthibitisho wa maelezo yako unayosema Makandala ni fisadi na dikteta labda naweza kukubaliana nawe kama utakuwa na hoja za msingi.
mimi sijashauri wanafunzi wafanye fujo na kuvinja majengo bali sioni kama hiyo ndo njia ya kudai yale wanayoyaona ya msingi.
mwafrika naona umekurupuka na kusimama katika mada ambayo naona bado hujaipata vizuri. naungana na ushauri aliokupa BIMKUBWA ufuate tafadhali.
 
Look here Mwafrika wa kike,
Usijitie presha kwa kutetea vijana ambao hawaelewi ni kwa nini wanagoma. wanafunzi wengi waliopo chuoni pale kwa sasa na wao pia hawaelewi kwa nini kuna huo mgomo.

Bi mkubwa,

Heshima mbele mama.
Nilipokwenda Tanzania december mwaka jana, nilipitia Kahama kwa Uncle yangu. Nikiwa kwenye duka moja ya kuuza soda, kuna vijana walikuwa wakiongea namna ya kushinikiza wakazi wa Shinyanga yote kugomea mikataba bubu ya kuanzia Mwadui hadi Buzwagi.

Cha kushangaza, kuna baadhi ya watu walisema kuwa hakuna sababu ya kugombana na serikali au wazungu kwa ajili ya madini. Waacheni wachukue tu na waondoke watuachie nchi yetu - alisema mzee mmoja kwa uchungu.

It is simple math, unaenda chuo kikuu kusoma basi soma. Tunakubali kuwa chuo ni agent of change katika society na mchango wake kuthaminiwa katika nyanja mbalimbali za ujenzi wa taifa ikiwemo demokrasia. Sidhani chuo kikuu ni mahala pa kwenda kupigania demokrasia maana hakina autonomy kama wilaya au mkoa yenye centres of authority. Chuo kinabaki kuwa provider of social services among other things.

Kama wanafunzi wa vyuo vikuu vya marekani wangekaa na usemi wako huu miaka ya sitini wakati wa civil rights movements, leo hii bado america ingekuwa vietnam, blacks wasingekuwa wanapiga kura, na labda wanawake wangenyanganywa haki yao ya kupiga kura.

Kilichotokea kwenye campus za vyuo maarufu kama Columbia na UCLA miaka ya 60, kulibadilisha sera za marekani forever.

Mimi na wewe tuko mbali na nyumbani,let us wait and see how things unfold.

Kwa usemi wako, sioni pia sababu ya kuongelea mambo ya Buzwagi na Kiwira maana niko mbali pia.

Maana si haki kutetea mtu aliyekutwa na makosa na akapewa adhabu stahili. Hutakuwa tofauti na yule atakayemtetea Lowassa au Chenge kuwa wameonewa na hali hukuwepo kuwasaidia kuiba hizo fedha.

Unaongelea mambo tofauti kabisa hapa.

La mwisho, una ushahidi ya kuwa Mukandala ni fisadi, dikteta na muuaji? huyo mwanafunzi marehemu alikuwepo katika kundi lililoenda nyumbani kwa Mukandala na wakafanya vurugu kiasi cha kuvunja geti la kuingilia nyumbani kwake bahati nzuri familia ya Mukandala haikuwepo alikuwepo msaidizi wa kazi za nyumbani na ndugu mmoja. wakaondoka kwa hasira zao na kwenda Swimming pool wakavunja fridge lililokuwa na vinywaji baridi wakazimnywa zote na wakaanza kusheherekea kwa kuogelea ndipo huyo marehemu akarukia kwenye maji na kukumbana na kifo chake.

Naona wewe unaongelea mwanafunzi tofauti. Kuna habari ambazo bado hazijathibitishwa kuwa kuna mwanafunzi mjamzito amekufa kwa kupigwa na mabomu ya FFU jana mlimani. Kama hii ikithibitika kuwa ni kweli, Mkandara atajulikana kama Muuaji hapa JF mpaka siku nikipotea na mimi.

a. Huoni kuwa walikuwa wanahatarisha maisha ya familia ya mwalimu wao? Je ni sawa kitendo walichofanya?
b. Put yourself in Mukandala's shoes what would you have done?
c. Kuvunja kwa fridge, sio wizi among other things? Do you think they did the right thing.

Ningekuwa Mkandara nisingeingilia uchaguzi huru kabisa wa wanafunzi wangu.

Nimesoma UDSM na katika kusoma kwangu kulikuwepo na migomo miwili ambayo kwa bahati nzuri they were for sound reasons na utawala ukatuelewa na wala hatukufanya fujo hizo. Why now? Naomba ukubali kuwa we now have a new crop of students ambao ni matokeo ya dhambi nyingi ktk society. Hawa vijana walichokifanya hakina sound reasons up to now. They are just burning my P.A.Y.E. for no reasons at all.

Sidhani kama wakati umesoma mlimani uongozi wa chuo uliingilia uhuru wa wanafunzi wa kuchagua viongozi wao.
 
Naona nawe unahitajika kutoa maelezo ya ziada na uthibitisho wa maelezo yako unayosema Makandala ni fisadi na dikteta labda naweza kukubaliana nawe kama utakuwa na hoja za msingi.
mimi sijashauri wanafunzi wafanye fujo na kuvinja majengo bali sioni kama hiyo ndo njia ya kudai yale wanayoyaona ya msingi.
mwafrika naona umekurupuka na kusimama katika mada ambayo naona bado hujaipata vizuri. naungana na ushauri aliokupa BIMKUBWA ufuate tafadhali.

Kuingilia uchaguzi huru wa wanafunzi ni udikiteta. Kuwa mshauri wa raisi ambaye kila siku inathibitisha kuwa serikali yake imejaa mafisadi ni ufisadi. Kusababisha kifo cha mwanafunzi mjamzito kutokana na agizo kwa FFU kupiga wanafunzi wasio na hatia ni uuaji.
 
mwafrica wa kike why are you misleadind our young brothers? umepandikizwa kufanya hivyo? please please i have started doubting.

kwa nini hupendi vijana wetu kutulia na kufikia lengo lao?

ninaomba unijibu maswali haya.
1. je wewe ulimaliza UD mwaka gani?
2. je kwenye kipindi chako kulitokea mgomo?
3. ulishiriki kiasi gani? au ulikuwa kama remot control ukitumia internet wakati wenzako wanapigwa mabom.
4. kama huko Ud sasa hivi je unashiriki kiasi gani? au huko tu kwako unatumia propaganda za internet?

nimekudoubt sana. sababu unaongelea democracy lakini huongelei uvunjaji wa democracy ya wale waliotolewa maktaba na madarasani bila kuzingatia kama wao ni postgraduates or the opposite.

Sidhani kama ninatakiwa kuwa nimesoma UD ili kuwatetea wanafunzi wa UD. Mwanakijiji alianzisha kampeni hapa ya kutetea wanafunzi wa Ukraine na sidhani ni kwa sababu alikuwa amesoma Ukraine.

Juzi hapa tulianzisha kampeni ya kutetea wanafunzi wa China na sio kwamba tuko China tunasoma. Kukiwa na uvunjifu wa haki kama unaofanywa na fisadi na dikiteta Mkandara chuoni leo hii, basi ni jukumu la wapenda haki kutetea haki kwa nguvu zote.

Nina hakika kuwa kama chuo kingewaacha wanafunzi wakachagua hao viongozi wao haya yote yasingetokea. Mimi hapa napigana na root cause ya hili tatizo - dikiteta na fisadi (ambaye soon ataitwa muuaji) Mkandara.
 
Once again wanafunzi wamegoma kuingia madarasani na kuna uvumi kuwa kuna mwanafunzi mmoja ambaye alikuwa mjamzito amefariki dunia.

Note:-
Ni uvumi uliotapakaa miongoni mwa wanafunzi ambapo habari hizi bado hazijathibitishwa na UTAWALA, ila baadhi ya wanafunzi wameandamana wakiimba MBINGUNI KUNA MAKAO MAZURI SANA.
Tungojee tusikie kama ni kweli haya wanayoyasema
.

Waga,

Mawasiliano na jamaa wa utawala yamekuwa magumu. Wote wamekataa kuthibitisha kifo hiki ambacho kama kimetokea ni cha kusikitisha sana. Hata hivyo hakuna anayekana ingawa niliyoongea naye ana panic ya ajabu na hakutaka kuongea sana na mimi.

Nipatie ile namba nyingine kwani ndio mwanzo nafuatilia hii habari kujua undani wake.
 
Inaelekea wengi wenu hamjui kilicho wapele hapo au njaa na tamaa ndizo zimewazidi hamkumbuki mlipo valishwa t-shirt + juice na madiko diko mengine mkimsifu bwana mkubwa, mliwakumbuka wazazi wenu walio vijijini ambao hawa juice juice ni nini... msisubili vitu vinavyo wahusu nyie zaidi ndiyo ngome..na siasa nyie ndiyo mmeiendekeza
 
Wasipogomea vitu vinavyowahusu wao, then watagomea nini? Hawa wanafunzi siku za karibuni wamekuwa very active na wametoa matamko mara kwa mara wakikekemea ufisadi wa serikali ya ccm.

Katika hili, Mkandara aache udikiteta na ufisadi na awaachie wanafunzi wachague viongozi wao wanaowataka wao.
 
Waga,

Mawasiliano na jamaa wa utawala yamekuwa magumu. Wote wamekataa kuthibitisha kifo hiki ambacho kama kimetokea ni cha kusikitisha sana. Hata hivyo hakuna anayekana ingawa niliyoongea naye ana panic ya ajabu na hakutaka kuongea sana na mimi.

Nipatie ile namba nyingine kwani ndio mwanzo nafuatilia hii habari kujua undani wake.

Am right here at Utawala wandugu .Hakuna wa kutaka kusema lolote ila wanasema niende polisi.Natafuta wanafunzi kama kuna mwenye details zaidi .
 
Am right here at Utawala wandugu .Hakuna wa kutaka kusema lolote ila wanasema niende polisi.Natafuta wanafunzi kama kuna mwenye details zaidi .

'Tuhongidze mtwa' (Asante Mkuu), i love JF ipo kila mahali tena live.
 
Am right here at Utawala wandugu .Hakuna wa kutaka kusema lolote ila wanasema niende polisi.Natafuta wanafunzi kama kuna mwenye details zaidi .

Lunyungu nakuaminia mkuu!

Fuatilia hili jambo kwa undani kabisa ujue kama fisadi na dikiteta Mkandara amefikia this down.
 
Hawa vijana wanatakiwa kukua vyuo vingine havina matatizo haya. Muda wa kedekezwa umekwisha na huu ni wakati wa elimu.
 
Back
Top Bottom