UEFA Champions League: Droo ya Robo & Nusu Fainal Ijumaa Saa 9:00 Alasiri

Bayern ni wazuri hata kama wanapitia kipindi kigumu. Kuna timu experience zinawabeba kwenye michuaono hii mikubwa mfano Real madrid.
Experience haina uzito huo... huwezi kutana na wale watoto wa Arsenal wanakimbia muda wote halafu useme wewe utawafunga kwa experience wakati form yako mbovu, hili halipo.

Hao R. Madrid unaosema wana experience mbona last season walikalishwa na Man City?!

Form ndio kila kitu kwenye mpira.
 
Hapa unazungumzia UEFA. Hauzungumzii ligi mkuu.

Misimu miwili nyuma Liverpool,Psg , Manchester city, walikuwa kwenye ubora wa Hali juu lkn hawa wote walipigwa na Real Madrid aliyekuwa si tishio na akabeba ndoo.

Msimu 2021/2022 Manchester City alikuwa ubora wa Hali juu lkn alipigwa nje ndani na Chelsea kuanzia kwenye ligi, FA na UEFA Chelsea akabeba ndoo.

Liverpool Kawa kwenye ubora wa hali ya juu kwenye Misimu kadhaa iliyopita ya UEFA mpaka hatua ya kuingia fainali mara tatu lkn mara mbili nzima alipoteza mbele ya Real Madrid. Ambapo mara ya mwisho Liverpool aliingia fainali na Madrid dhaifu kabisa.

Vipi Psg aliyekuwa kwenye ubora wa Hali ya juu msimu wa 2020/2021 mbele Mbappe, Neymar na Hakim lkn akapoteza mbele ya Bayern ambayo haikuwa tishio.

Na bado mifano ipo mingi kwenye timu ambazo hazikuwa zinafanya vizuri katika ligi na mashindano mengine lkn katika UEFA walifanya maajabu.

Kwahiyo Arsenal anaweza akawa vizuri lkn Bayern Munich uzoefu ukawabeba na wakaishia kupigwa nje ndani kwenye hii robo fainali. Na kumbuka kocha ni Thomas Tuchel. Usimu underrate.
 
masheikh kama nyiny mnahitajika muwe wengi muwape vijana somo la soka maana wengine huwa wanazani hichi ni kijiwe cha kahawa au kila mtu kaaza kutazama mpira wakati yupo chuo
 
Hawalielewi hilo mkuu, umeelezea vyema kabisa.
 
Kwahiyo unategemea upepo sio form ya timu kwa wakati husika, unaponiambia timu inaweza kuwa na form mbovu nyumbani lakini UEFA wakafanya vizuri.

Hao Bayern game yao ya kwanza last 16 walipigwa na Lazio, kibonde kabisa kwenye ligi ya Italy, sasa kwanini Bayern asingetumia historia yake UEFA kumfunga Lazio away kama mnaamini kwenye historia kuamua matokeo?

Ndio maana nawaambia na bado nitaendelea kuwaambia, Bayern Munich ya sasa haina maajabu, labda utokee upepo tu wa kimpira, lakini kama ni kuweka kabumbu chini, nampa Arsenal nafasi kubwa kumtoa Bayern M.

Kama Arsenal akiutumia vizuri uwanja wa nyumbani, namuona Bayern M akila tano au sita wala sitashangaa, zikipungua sana tatu. Tuchel ameishiwa mbinu kwenye ligi hizo za UEFA atazipata wapi? yule anatembea na upepo tu, Bayern hawana chemistry.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ