Uelewa wa Lissu kwenye uchumi ni mdogo

Uelewa wa Lissu kwenye uchumi ni mdogo

eddy

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2007
Posts
17,079
Reaction score
12,312
Nimefuatilia kauli za Lissu akiwa Morogoro mjini, kasema serikali ya JPM haijaongeza mishahara (General salary increment) na yeye akiingia madarakani ataongeza mishahara kulingana na hali ya uchumi ili kupunguza ukali wa maisha. Ni kweli "General increment" kwenye salary adjustment hufanyika pale mfumuko wa bei unapokuwa 7.8 na kuendelea hizo ndio hesabu za macro economic perspective. Kwa sasa mfumuko wa bei wa ujumla upo chini ya 3.4 hivyo kwa mahesabu ya kiuchumi huwezi kufanya "salary adjustment". Hizi ni kanuni za kiuchumi sio common sense tu.

Hebu tuangalie ukali wa maisha anaozungumzia Lissu; Mwaka 2015 bei ya mchele ilikuwa 2700 kwa kilo sasa hivi ni 1100, bei ya nyama ilikuwa 8500 sasa hivi 3500, bei ya diesel ilikuwa 2700 sasa hivi 1650, gunia la mahindi lilikuwa 135,000/= sasa hivi 48,000/=, bei ya saruji ilikuwa 27,000/= leo hii 16,500/=, nauli ya daladala 400 na sasa ni hiyohiyo 400. Huo ukali wa maisha anaupima vipi? Au ukali wa maisha uko nyumbani kwake tu? Kimsingi maisha kwa mwananchi wa kawaida yamekuwa nafuu zaidi kuliko 2015 niko tayari kusahihishwa. Lissu akumbuke tumeshaanza kupiga hatua kutoka kwenye umasikini, sasa hivi tuko uchumi wa kati na tunazidi kusonga mbele.

Lissu akumbuke muda sio mrefu tumehangaika na janga la corona, walimu wamekaa majumbani miezi sita na bado wamelipwa mishahara kama kawaida, leo kuna malori yameegeshwa uganda kwa kuzuiliwa karantini, madereva wanalipwa mishahara posho na wanalipia maegesho na yanapigwa girisi kila siku tuongeze mishahara kutoka wapi? Leo hii bus linatoka Dar Mwanza na abiria sita na linarudi na abiria wanne tuongeze mishahara kutoka wapi, namshauri aangalie uhalisia wa yale anayoyaongea asijepotosha watu.

Lissu akumbuke uchumi wetu ni mdogo, ndio juzi tumeingia uchumi wa kati, viwanda vyetu ni "labor intensive" ukiongeza mishahara maana yake gharama za uzalishaji ziongezeke na final product ipande bei, vitu vikipanda bei maana yake mfumuko wa bei umepanda, hiyo inaitwa "multiplier effect" kwa sasa kinachofanyika ni ku stabilize life style ili fedha kidogo tunayopata ipangike inaitwa "household budget efficiency"

Lissu atueleze huko Ubelgiji kakaa miaka mitatu wabelgiji wamepandishiwa mishahara mara ngapi? au wao hawana ukali wa maisha? Lissu nimkumbushe, kumefanyika salary adjustment nyingi amuulize mnyika, kuna vigogo walijilipa hadi 40m kwa mwezi kama mishahara, vikao vya wakurugenzi vilivyokuwa vikifanyika Dubai na Hongkong havipo tena, ziara za wabunge kwenda kuangalia mitaa Dubai hazipo tena labda ndio huo ukali wa maisha anao uzungumzia.
 
Hata kemia ya maganda ya korosho Tundu Lissu hakusoma. Lakini sicho kinachompeleka mtu Ikulu. Ikulu ya Tanzania imekaliwa na walimu wa Kiingereza na Kiswahili, mkemia, mwandishi wa habari.

Walikuwa na uelewa gani wa uchumi hawa? You cannot be everything. Kazi ya Rais ni kuwatumia wataalam wake vizuri. It is not about the president but the presidency.
 
Unakata kutwambia sheria ya nchi inayoelekeza annual increment imekosewa? Je nayo ilitungwa na Lissu? Acheni kutapatapa... Hata Rungwe, Muttamwega, Lipumba ni wagombea nao. Wanastahili kuongelewa na kuletewa post hapa pia.
Nimefuatilia kauli za Lissu akiwa morogoro mjini, kasema serikali ya JPM haijaongeza mishahara (General salary increment) na yeye akiingia madarakani ataongeza mishahara kulingana na hali ya uchumi ili kupunguza ukali wa maisha..
 
Unakata kutwambia sheria ya nchi inayoelekeza annual increment imekosewa? Je nayo ilitungwa na Lissu? Acheni kutapatapa... Hata Rungwe, Muttamwega, Lipumba ni wagombea nao. Wanastahili kuongelewa pia.
Sheria inasema salary increment itafanywa kulingana na hali ya uchumi
 
Anaongea Kiingereza zaidi ya ku phont phage, atapata washauri wa uchumi. Mawasiliano ndiyo muhimu hata akienda Zimbabwe watamuelewa.
Nakujua wewe kindakindaki Manka. Nakubali Urais ni taasisi, sasa akubali pia Lisu kutosema vitu ambavyo havielewi, ajikite kwenye sheria
 
Haiitaji ujuzi wa Uchumi au Utaalamu kuona ugumu wa maisha kama ni bora kwa sasa kuliko hapo nyuma..., Hilo unahitaji macho tu..., unahitaji ufahamu wa ziada ili uweze kutetea vitu ndivyo sivyo ili vioneka ndivyo (justification...)

Let get back to basics..., haya mambo ya kumwambia mtu Uchumi umekuwa maradufu hence maisha yako ni better off..., its just Propaganda...
 
Kama uelewa wa Lissu ni mdogo, uelewa wa Magufuli aliyesababisha bei ya sukari ipande kutoka 1800 hadi 2800/3000 sasaivi kw matamko yake ya ajabu ya kupiga marufuku uagizwaji wa Sukari huyu utasema uelewa wake ukoje?

Na bado!!! Huyo ndo Lisu, CCM lazima mrukwe na kichaa mwaka huu!!!
 
Aah sana! Yeye ni mwanaharakati wa haki za binadamu kwenye migodi.

Uchumi wapi na wapi!

Baada ya uchaguzi aunge juhudi atafaa sana kuwa Waziri wa Habari, utamaduni na michezo, au Wizara ya wanawake na watoto.

Ikishindikana kabisa kwenye uwaziri basi ukuu wa mkoa wa Dar utamfaa sana apambane na D. Bashit.
 
Nimefuatilia kauli za Lissu akiwa morogoro mjini, kasema serikali ya JPM haijaongeza mishahara (General salary increment) na yeye akiingia madarakani ataongeza mishahara kulingana na hali ya uchumi ili kupunguza ukali wa maisha...
Successful societies depend on the government run-systems. Business success rely on the government-run business tools that enhance efficiency and effectivenes of public and private sector, in return for, they will be business growth and an increase of an employment rate, hence more revenue and economic growth. I have writen this in my Entrepreneurship book. stay tuned to be ready in november 2020. Nimeandika hivyo kwenye kitabu changu cha ujasiriamali kitakuwa tayari mwezi novemba 2020.
 
Hebu tuangalie ukali wa maisha anaozungumzia Lissu; Mwaka 2015 bei ya mchele ilikuwa 2700 kwa kilo sasa hivi ni 1100, bei ya nyama ilikuwa 8500 sasa hivi 3500, bei ya diesel ilikuwa 2700 sasa hivi 1650, gunia la mahindi lilikuwa 135,000/= sasa hivi 48,000/=, bei ya saruji ilikuwa 27,000/= leo hii 16,500/=, nauli ya daladala 400 na sasa ni hiyohiyo 400...
Mchele wa 1100 ..unaongelea mkoa gani?

Nyama ya 3500...mkoa gani?

cement kwa Dar ni 14,500....13,000 na 13,500 mikoa mingine inafika 20,000.. hapa imeshuka sana kwa Dar japo tunalilia na hako ka jero katoke irudi 14,000

Daladala hutofautiana na umbali lakini 400 ni ya awali..mfano kigamboni 450.

Dar-Mwanza basi zinajaza kama kawaida abiria sita sio kweli.

Diesel na petrol zimeshuka mwaka huu tu nadhan.

pia kafanye research ya bei ya unga...mafuta ya kupikia...vitu vingi vimepanda
 
Nimefuatilia kauli za Lissu akiwa morogoro mjini, kasema serikali ya JPM haijaongeza mishahara (General salary increment) na yeye akiingia madarakani ataongeza mishahara kulingana na hali ya uchumi ili kupunguza ukali wa maisha...

Angekuwa na uelewa MDOGO ungehemuka kwa kiasi KIKUBWA namna hiyo? Nyie vichwapanzi mnajitekenya na kucheka wenyewe.
 
Back
Top Bottom