Uelewa wa Lissu kwenye uchumi ni mdogo

Uelewa wa Lissu kwenye uchumi ni mdogo

Hata kemia ya maganda ya korosho Tundu Lissu hakusoma. Lakini sicho kinachompeleka mtu Ikulu. Ikulu ya Tanzania imekaliwa na walimu wa Kiingereza na Kiswahili, mkemia, mwandishi wa habari.

Walikuwa na uelewa gani wa uchumi hawa? You cannot be everything. Kazi ya Rais ni kuwatumia wataalam wake vizuri. It is not about the president but the presidency.
Hongera, kamahaja kuelewa Basi ana matatizo.
 
Mkuu General Salary Increment hufanyika uchumi unapokuwa umedorora ili kupunguza makali ya maisha, uchumi unapokuwa imara maana yake kuna unafuu kwenye maisha hatuongezi mishahara ili kuepuka multiplier effects
Mwambieni msemaji wa serikali alitangaze hilo rasmi ili aeleweke. Matamshi yako sio matamshi ya serikali.
Maana serikali bafo haijakubali uchumi wake kuteteleka ni huenda unaisingizia.

Tutaiamini serikali sio wewe
 
Hatafanya salary increment kwa pesa za michango, huyu ni mtu aliyekuwa akililia alipwe mshahara na posho wakati anazunguka ulaya, wakati huo alishatibiwa
 
Nimefuatilia kauli za Lissu akiwa Morogoro mjini, kasema serikali ya JPM haijaongeza mishahara (General salary increment) na yeye akiingia madarakani ataongeza mishahara kulingana na hali ya uchumi ili kupunguza ukali wa maisha...
Magufuli anajua uchumi? Hizo blunders zote anazozifanya na kuharibu uchumi wewe huzioni hizo, acha kuwa hypocrite.
 
Hata kemia ya maganda ya korosho Tundu Lissu hakusoma. Lakini sicho kinachompeleka mtu Ikulu. Ikulu ya Tanzania imekaliwa na walimu wa Kiingereza na Kiswahili, mkemia, mwandishi wa habari.

Walikuwa na uelewa gani wa uchumi hawa? You cannot be everything. Kazi ya Rais ni kuwatumia wataalam wake vizuri. It is not about the president but the presidency.
Umemaliza Kila kitu ......uko sahih 99%
 
Nimefuatilia kauli za Lissu akiwa Morogoro mjini, kasema serikali ya JPM haijaongeza mishahara (General salary increment) na yeye akiingia madarakani ataongeza mishahara kulingana na hali ya uchumi ili kupunguza ukali wa maisha....
Unapingana na boss wako aliyesema nchi hii ina hela nyingi saana??kwa hiyo unataka kusema sisi hatuwezi kuwa 'dona kantre'? Kama hela zipo nyingi kama boss wako anavyosema,basi ningeshangaa waalimu kutolipwa salary kipindi cha corona na pia bado haimzuii kulala salary increment kwa kuwa hela ipo na inatosha kutufanya tuwe kama ulaya in the next 5yrs(according to your boss).

Unaweza ukaona tofauti ya Lissu unaesema hajui uchumi na huyo mwenye utaalamu anaesema kuna hela za kuifanya tz iwe kama ulaya ndani ya miaka 5 hayo.
 
Kama huo uchumi unaousema hapa uliusomea darasani nakushauri nenda kadai ada yako uliitupa bure aseee!

Salary increment ipo kisheria haijalishi hali Ni nzuri au ni mbaya kiasi gani. Unapoongelea suala la petrol na dizel kushuka bei ila haijatokea kwa sababu ya Sera za jpm na serikali yake ile ilitokea kipindi kile cha corona pandemic kama unakumbuka hata marekani ilishuka ikawa -$ so ile ilitokea worldwide.

Pia umesema Bei ya gunia la mahindi kushuka Bei ile pia huwa inatokana na hali ya hewa kwa mfano mwaka Jana gunia la mahindi la kg 100 liliuzwa hadi tsh125,000.

Je huo mwaka Ni lissu ndo alikua madarakani? Mchele Bei ukifika hadi 2500 @kg kwahy kushuka Bei ni kwa sababu msimu huu mvua zilinyesha nyingi so hili halitegemei Sera za Ccm.

Tukihamia kwenye inflation sio 3% unavosema wewe toka utawala wa mkapa mpaka utawala wa magufuli Ni awamu hii ndo inflation imekua kubwa kuliko awamu mbili zilizopita.

Sitaki kuongelea Bei ya vitu kama sukari, bati, Nondo, Saruji Bei imepanda Mara dufu hayo ndo matokeo ya Sera mbovu za jpm
Mwisho Lissu Ni mtaalam wa sheria yeye kutokujua uchumi sio tatizo akiwa rais atatumia wataalam wa uchumi na mambo yatakwenda
#Ni yeye 2020
 
Hata kemia ya maganda ya korosho Tundu Lissu hakusoma. Lakini sicho kinachompeleka mtu Ikulu. Ikulu ya Tanzania imekaliwa na walimu wa Kiingereza na Kiswahili, mkemia, mwandishi wa habari.

Walikuwa na uelewa gani wa uchumi hawa? You cannot be everything. Kazi ya Rais ni kuwatumia wataalam wake vizuri. It is not about the president but the presidency.
Mbona sasa anatoa mipango yake bila wataalamu? Maamuzi kama ya kuongeza mshahara ni ya rais na ameonyesha na kuthibitisha hana elimu ya kuongoza nchi wala busara.
 
Kama unamponda, unakubaliana na mimi. Watu wengine mkijieleza mnaeleweka kwa wazazi wenu tu.
Mbona sasa anatoa mipango yake bila wataalamu? Maamuzi kama ya kuongeza mshahara ni ya rais na ameonyesha na kuthibitisha hana elimu ya kuongoza nchi wala busara.
 
Mkuu trickle down effects ya mishahara haiwezi chochea economic growth, Ni Investments ndio huzalisha trickle down yenye tija, pia uboreshaji wa mnyororo wa thamani huchangia hizo trickle down effects.

Hapa tunaongelea positive effects, lakini Kuna negative effects Kama ufisadi biashara haramu nazo Zina trickle down effects,
Mkuu factor moja ya kukuza investment ni uwepo wa disposable income. WaTz wenye bima tu ni wachache sababu savings zinaendana na disposable income. Ikimaanisha mshahara ni mmoja wapo wa kuchochea uwekezaji sababu inaongeza disposable income.

Pia investment sio lazima zifanywe na mpokea mshahara ila mfano mpokea mshahara anapolipia saluni,nguo,kodi ya fremu yulo mpokeaji anaweza kwenda kuwekeza kwenye shughuli zingine za kiuchumi kwahiyo mshahara unakua kichocheo cha uwekezaji kwa formula hiyo.

Hata ukiangalia tu sera ya fedha kichocheo cha uchumi moja wapo ni kuongeza pesa kwa mzunguko ikimaanisha njia kma hizo za kupandisha mshahara ni suluhu pia kwenye kuongeza mzunguko.
 
Causes of Inflation
The Money Supply. Inflation is primarily caused by an increase in the money supply that outpaces economic growth. ...
The National Debt. ...
Demand-Pull Effect. ...
Cost-Push Effect. ...
Exchange Rates

Na ukizungumzia exchange rate e.g. ya dollar imekuwa stable at tshs 2,300.00 selling , yaani bei Bank watakayo kuuzia.
Na interest rates zimekuwa at most 17%
And below wakati wa inflation ilikuwa 25% to 27%.
Ukiacha hayo mambo mengine ya demand na prices ya essential items za matumizi ya kibanadamu
You might be right lakini hapo kumbuka umeangalia kwa kikundi tu cha watumishi lakini hujaangalia mzunguko wa pesa kwa ujumla na jinsi inaweza kushusha inflation.

Tuwe wakweli tu Currency in circulation + Demand deposits ni ndogo kulinganisha na namba ya watu kwahiyo ni lazima tu inflation cjui interest rate zishuke sababu zitapandaje na demand hamna.

Kwahiyo nadhani kwa upande mwingine hyo inflation sio indicator kwamba uchumi upo vizuri sana bali ni kwamba watu hawana hela sababu ya sera ya fedha ya sasa.

Ndio maana nimeuliza hapo je umeangalia issue ya mzunguko wa fedha kwanza? Ni sawa na marekani wao wananunua nje kuliko wanavyouza? Yaani imports zinazidi exports? Kwa Tz ingeonekana ni uzalishaji kupungua ila kwa US inaonyesha wananchi wana pesa ndio maana wanaimport sana ama issue ya opportunity cost and so on.

Tukijua chanzo cha hiyo inflation ndio utaona umuhimu wa mishahara kupanda.
 
Mkuu factor moja ya kukuza investment ni uwepo wa disposable income. WaTz wenye bima tu ni wachache sababu savings zinaendana na disposable income. Ikimaanisha mshahara ni mmoja wapo wa kuchochea uwekezaji sababu inaongeza disposable income.

Pia investment sio lazima zifanywe na mpokea mshahara ila mfano mpokea mshahara anapolipia saluni,nguo,kodi ya fremu yulo mpokeaji anaweza kwenda kuwekeza kwenye shughuli zingine za kiuchumi kwahiyo mshahara unakua kichocheo cha uwekezaji kwa formula hiyo.

Hata ukiangalia tu sera ya fedha kichocheo cha uchumi moja wapo ni kuongeza pesa kwa mzunguko ikimaanisha njia kma hizo za kupandisha mshahara ni suluhu pia kwenye kuongeza mzunguko.
Mkuu huwezi ku float money into economy Kama inflation Ni 3.4 unafanya hivyo iwapo inflation Ni -1, ili inflation ifike angalau +2.5, pia zoo lazima upandishe mishahara ya public sector, unaweza punguza interest kwenye Treasury Bill na kuongeza interest rates kwenye bank loans,
 
Nimefuatilia kauli za Lissu akiwa Morogoro mjini, kasema serikali ya JPM haijaongeza mishahara (General salary increment) na yeye akiingia madarakani ataongeza mishahara kulingana na hali ya uchumi ili kupunguza ukali wa maisha. Ni kweli "General increment" kwenye salary adjustment hufanyika pale mfumuko wa bei unapokuwa 7.8 na kuendelea hizo ndio hesabu za macro economic perspective. Kwa sasa mfumuko wa bei wa ujumla upo chini ya 3.4 hivyo kwa mahesabu ya kiuchumi huwezi kufanya "salary adjustment". Hizi ni kanuni za kiuchumi sio common sense tu.

Hebu tuangalie ukali wa maisha anaozungumzia Lissu; Mwaka 2015 bei ya mchele ilikuwa 2700 kwa kilo sasa hivi ni 1100, bei ya nyama ilikuwa 8500 sasa hivi 3500, bei ya diesel ilikuwa 2700 sasa hivi 1650, gunia la mahindi lilikuwa 135,000/= sasa hivi 48,000/=, bei ya saruji ilikuwa 27,000/= leo hii 16,500/=, nauli ya daladala 400 na sasa ni hiyohiyo 400. Huo ukali wa maisha anaupima vipi? Au ukali wa maisha uko nyumbani kwake tu? Kimsingi maisha kwa mwananchi wa kawaida yamekuwa nafuu zaidi kuliko 2015 niko tayari kusahihishwa. Lissu akumbuke tumeshaanza kupiga hatua kutoka kwenye umasikini, sasa hivi tuko uchumi wa kati na tunazidi kusonga mbele.

Lissu akumbuke muda sio mrefu tumehangaika na janga la corona, walimu wamekaa majumbani miezi sita na bado wamelipwa mishahara kama kawaida, leo kuna malori yameegeshwa uganda kwa kuzuiliwa karantini, madereva wanalipwa mishahara posho na wanalipia maegesho na yanapigwa girisi kila siku tuongeze mishahara kutoka wapi? Leo hii bus linatoka Dar Mwanza na abiria sita na linarudi na abiria wanne tuongeze mishahara kutoka wapi, namshauri aangalie uhalisia wa yale anayoyaongea asijepotosha watu.

Lissu akumbuke uchumi wetu ni mdogo, ndio juzi tumeingia uchumi wa kati, viwanda vyetu ni "labor intensive" ukiongeza mishahara maana yake gharama za uzalishaji ziongezeke na final product ipande bei, vitu vikipanda bei maana yake mfumuko wa bei umepanda, hiyo inaitwa "multiplier effect" kwa sasa kinachofanyika ni ku stabilize life style ili fedha kidogo tunayopata ipangike inaitwa "household budget efficiency"

Lissu atueleze huko Ubelgiji kakaa miaka mitatu wabelgiji wamepandishiwa mishahara mara ngapi? au wao hawana ukali wa maisha? Lissu nimkumbushe, kumefanyika salary adjustment nyingi amuulize mnyika, kuna vigogo walijilipa hadi 40m kwa mwezi kama mishahara, vikao vya wakurugenzi vilivyokuwa vikifanyika Dubai na Hongkong havipo tena, ziara za wabunge kwenda kuangalia mitaa Dubai hazipo tena labda ndio huo ukali wa maisha anao uzungumzia.
Sasa mkuu hao wabeligiji wanatuhusu nini na maisha yetu!umeanza vizuri umemaliza vibaya
 
Yupi afadhali? yule ambaye hashauriki hata na wataalamu wa uchumi au ambaye anashaurika?
 
Tatizo ni kwamba ili topic yako ipate mvuto lazima kumtaja Lissu 😂 kwanini usiweke topic yenye jina la Magufuli kuhusu kujua uchumi 😂😂 hii inaonyesha nguvu ya mtu
 
Sijamzungumzia JPM kwani sijamsikia, mie naeleza niliyoyasikia kwa lissu
 
Back
Top Bottom