Uelewa wa Ulimwengu unatisha Maajabu ya Jua (Sun) nilichoona 5-march-2018 huenda kuna mabadiliko makubwa kila uchao.

Uelewa wa Ulimwengu unatisha Maajabu ya Jua (Sun) nilichoona 5-march-2018 huenda kuna mabadiliko makubwa kila uchao.

Hali iliyotokea juzi tarehe 5.03.2018 ilinitisha na kuniogofya nisijue nini cha kufanya wala sikujua ni kitu gani kimesababisha Jua kubadirika na kutengeneza hali yenye utisho mpaka sasa nimejaribu kupitia makala mbalimbali kwa siku tatu lakini sijapata majibu hikii.

Kilichotokea.
Ilikuwa mda wa saa 6:45 mchana nikiwa mashambani huku nikipiga picha kutumia camera ndogo ya kisasa Jua lilikuwa kali sana likichoma lakini cha kushangaza Jua lilipunguza mngao ghafla nilianza kuona kitu kama rangi rangi za kila namna zikiangaza pale chini ktk ardhi.

Nilishituka hali iliyonipelekea kutazama angani nilichokiona kilinishitua sana Jua lilionyesha kukosa ung'aavu ingawa lilichoma sana na lilitengeneza duara mawinguni iliyoweka weusi flani kupunguza mng'ao wa Jua na wingu lililokuwa la duara lilitengeneza rangi za kila namna ktk mzunguko wake.


Nilivaa miwani ya Jua ambayo siku zote kama mtafiti huwa siiachi ili nilitazame vema Jua niliona kidoti kikubwa kama nusu ya Jua lote nilijita hidi kuangaza vizuri ili nigundue Jua limepataje kidoti kikubwa namna ile.


Nilipochunguza vyema maana ilinibidi nilale chali nilichokiona lilikuwa ni kama tundu kubwa ambalo kwa mwonekano wa Jua tukiwa hapa duniani ungeweza kuingiza mpira wa miguu wa namba 6.


Nilichukua camera na kuanza kupiga picha ili nipate ushahidi kwa ambao nitawaelezea na niendelee na utafiti kutafta majibu kwa wenye uelewa zaidi.


Ghafla Jua lilirudisha mng'ao wake halisi na kidoti kile kilifutika na mviringo ktk mawingu ulitoweka na zile rangi rangi zote nilianza kuchukua video haraka lakini cha kushangaza camera ilizima ghafla,.

Nilipofika nyumbani nilitoa memory card kuweka kwenye PC haikuonyesha chochote kila kitu kimefutika, na nilijaribu kuchaji camera ikakataa na nimepeleka camera kwa fundi anasema imeungua haitawezekana kutengeneza.

Jee hii hali kuna yeyote amewahi kuishuhudia naomba mchango wa mawazo.

Hasa ni kitu gani hiki

Maana ktk Jua sioni kidoti wala tundu!
Siwezi kuthibitisha maneno yako moja kwa moja lakini Nina LA kuongeza juu ya hili ingawa Mimi sikushuhudia.
Siku moja sikumbuki ni lini lakini ilikuwa Around mid February niliporudi nyumbani kutoka katika mizunguko yangu ya kawaida kijana wangu Wa kazi aliniuliza hivi:
" aisee, hivi uliliona jua LA Leo LA mida ya SAA sits nusu?" Nikamjibu hapana kwani ilikuwaje? Akajibu
" kwanza lilibadilika rangi ilikuwa kama limepoteza mng'ao wake Fulani mpaka nikashangaa. Nilipotoka kivulini kuingia juani lilikuwa linachoma kupita kawaida kiasi unaweza kuhisi huwezi kuvumilia. Nilihisi nimeona Mimi peke yangu lakini nikasikia pia wamama Wa nyumba ya jirani wakiulizana kuhusu mwanga huu Wa jua kubadilika ila wakaishia kusema hii ni kazi ya Mungu.. Nilishangaa sana"

Mwisho Wa kunukuu..
Sikushuhudia lakini pia sikuwauliza majirani hao.. Ila inawezekana kuna kitu hakipo sawa
 
Yaani JF ina watu wa maajabu sana unaandika ukweli wa ulichoona unajibiwa comedy

Hapana. Sijasema kwamba umeandika comedy. Nimesoma nikakuelewa sana. Lakini jambo hili sina utaalamu nalo. Sikuona sababu ya ku comment kwako kwa jambo ambalo silifahamu. Nilianza kusoma michango ya wachangiaji nikitegemea lablda kuna mwenye uelewa wa hicho kitu ulichozungumzia. Lakini kabla sijafika mwisho, nikakutana na hiyo comment ya jamaa akiUliza kwamba "PICHA NDIYO HIZO".

Hicho ndicho kilinifanya nicheke. Kwa sababu umeadika kwamba camera yako ilizimika na haiku display kitu na ulipofuatilia kwa wataalam ukaambiwa imeungua na hvivyo hapakua na uwzekano wa kupata hizo picha.
Swali la jamaa yangu ndilo nililiona kama intertainment. Ninadhani hata yeye alikuwa anatania. Vinginevyo, endelea kutafiti ukipata jibu, tushirikishe.
 
Wewe unafanya utafiti huo kwa ajili ya nani na unamanufaa gani kwa taifa hili ambalo halina taasisi yoyote inayojishughulisha na Sayasi ya Anga za juu?
 
Naona mmeanza mambo ya alfu lela ulela.. Kwa hilo acha nibaki tomaso tu
 
Jinsi ilivyoundwa kamera ya digitali sio kama zile za analojia.
Za digital toka inapokusanya taswira ktk mwanga na kuitengeneza kitu ktk mfumo wa 'binary object' ni hatua ndefu na hakuna muunganiko wa moja kwa moja toka kwenye 'aperture' ya kamera hadi kwenye kihifadhi kumbukumbu (memory card) kama ilivyo ktk kamera ya analojia itumiayo mkanda (camera film).

Unachojaribu kusema ni kwamba huo mwanga uligeuka umeme mkubwa kiasi cha kuunguza memory kadi, kitu ambacho kamera yote ingeungua na kama vile vinapoungua vifaa vya umeme na kuzalisha joto na moshi. kama iliungua hivyo tuwekee picha ya kamera yako iliyoungua na bila shaka wewe pia ungekuwa umeumia mkononi.

Kamera ya analojia ni rahisi kuungua picha ktk mkanda kwa vile kwa namna fulani mwanga unaenda moja kwa moja kutengeneza taswira ktk mkanda.

Haya madai yako sio sahihi labda kama umeandika kazi fulani ya fasihi. Ambayo hata mimi umenishika vizuri maana bado sijapata maudhui yake.
 
Asant mkuu ila hiki ninachosema siyo hadithi pia sikuwa peke yangu watu ziadi ya 10 walikuwepo na walitazama angani kuona tatizo lilikuwa ni mng'ao mkali wa Jua walishindwa kutazama kwa ufasaha kama nilivyofanya Mimi niliye kuwa nimevaa miwani ya Jua asante sana

HABARI,
"impongo,
Sawa nimekuelewa uko mkoa gani na eneo gani hapo lilipotokea.

LUMUMBA
 
Siwezi sema kwel hayo uliyashuhudia lkn mi nilishawahi kusimuliwa kitu kama hicho kitambo huo uzi wako ni mara ya pili kuongelea jambo kama hilo na mie kila nikisimuliaga watu hunitoa akili kama wanavyokufanyia ww coz sina ushahid so bro mie binafsi yangu naamin inaeezekana we hayo umeyaona
 
Kuna muda unaweza kuonekana mpuuzi/mwongo wakati unaloongea ni muhim sana na ni la ukweli,mtu anasema alikuwa na camera lakini picha anayoambatisha kachukua mtandaoni!
 
Ki ukweli hiki kitu nishakisikia na kuona picha yake, ambaye dada angu alikua geita alipiga simu na kuniambia ameona kitu kama hicho lakini cha ajabu mimi huku sikuona kitu kama hicho. Na picha alinitumia.
 
Hahaha ila we mtunzi mzuri nmekumbuka ile hadithi yko ya kuchungulia kuzimu
 
memory ukatoa na haikusoma hapo hapo camera haikuwaka so nimekuelewa mkuu
 
Ni kweli mkuu hata mm niliona hivohivo unavosema. ....amin usiamin mtoa mada!!
 
Iwe umetoa sehemu au umetunga haijalishi,kule kuchochea fikra inatosha kuthamini.

Ulichosema si kigeni,kipo na bado kina mkanganyiko.

Na kwa kuwa ni ngumu kuthibitisha inakuwa ngumu kuelewa na kuamini.

Na si kwa jua Tu, hata na dunia ina kitu kama hicho.

Hata mimi nina imani ya kuwa Magimba ya angani ikiwemo Dunia yetu ni milango (portal),Kuwezesha kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Ila kuna wahuni fulani duniani wanaficha ukweli, Ila nikiri tu sijafahamu kama ni kwa nia Mbaya au Njema.

Ila usitegemee watoto wachanga wakakuelewa.ubarikiwe
 
Back
Top Bottom