Ufafanuzi kuhusu kanisa Katoliki kutokuwafanyia maziko ya kikanisa baadhi ya waamini wake

Kijana acha kuropoka ovyo,unaoneka uko shallow sana kwenye maandiko(Biblia),apo kwenye hilo LA nguruwe umeonesha ni jinsi gani ulivyo shallow.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo Mussa, Jacob,Joseph, joshua au na Yesu alikula Nguruwe? Katika bible tunasoma ilikuwa story nabii aliadithia kuwa alilala juu ya nyumba sumit akaota ndoto kuwa ananjaa na akatelemshiwa wanyama ili achinje ale na yeye kwakuwa alikuwa anatalemshiwa wanyama najisi kama torati ilivyoandikwa akakataa kuwala ndotoni akaambiwa kitokacho mwilini ndio najisi bali kiingiacho sio najisi.. so wengi wakachukulia hapo hapo advantage ya kula nguruwe.. ile ndtoo has nothing to do kuchange torati ya Mussa.. even Jesus alisema hakuja kuitengua torati bali kuitimiliza so kama waniona nipo Shallow endelezeni tu libeneke la kuvunja torati mwisho ndio mtakuja kufahamu kuwa kupotoshwa ni kujitakia Soma biblia uwe huru minyororo uliyofungwa ni mikubwa sana...STUKA. .

Achana na Roma mfuate Yesu... Roman are not Christian kuna wimbi kubwa sana haswa ulaya wa Roman catholic wakihamia ukristo tizama news utaelewa...

Waeza pia wewe yakakukuta kama ya mrema
 
it seem huna uelewa wowote wa mada husika kuwa Roma catholic wamemkataa Mkatoliki Mwenzao kumzika hadi Wakristo wametokea na kumzika hujaona kama ni hukumu tena kwa mtu ambaye ndio Tamati yake...
 
Ndg biblia haijakataza nguruwe ni usomaji hafifu wa biblia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndg biblia haijakataza nguruwe ni usomaji hafifu wa biblia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo Maneno na torati ya Mussa unaipinga na kukataa kwani ndio iliyoandika even Noah aliambiwa awapakie Wanyama wa kila aina wasafi saba na wachafu wawili tu. Wewe uneisoma biblia tofauti. Uzuri wa bible wame Mantion kabisa
 
Asante.

Naomba twende taratibu...

Nabaki kwenye katazo,biblia kupitia kupitia agano la kale ilikataza aina nyingi ya viumbe wasiliwe kwa kuwa ni najisi mfn,Sungura,Ngamia,Nguruwe nk pia baadhi ya samaki wasio na magamba kama Kambale nk na ndege wa angani kama Tai nk,kwa ufafanuzi pitia Walawi 11:1-14

Swali;Ninyi mnaokataa kula nyama ya Nguruwe kwa mujibu wa biblia,Je Sungura,Ngamia pia mnawakataa...???Vp samaki wasio na magamba(Kambale)..????

Naomba tubaki kwenye Katazo(Torati) kwanza alafu tuendelee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa naona mnagombania fito. Jibuni basi maswali yangu.
 
it seem huna uelewa wowote wa mada husika kuwa Roma catholic wamemkataa Mkatoliki Mwenzao kumzika hadi Wakristo wametokea na kumzika hujaona kama ni hukumu tena kwa mtu ambaye ndio Tamati yake...
Ok,may be huenda ikawa sina uelewa...

Swali;Kanisa Katoliki lilimkataa marehemu au marehemu alilikataa Kanisa akiwa hai...????

Ndg naomba usiandike kwa mihemko ya kidini,hebu tenda haki ktk uandishi wako na Mungu atakubariki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ona anavyojibu tuhuma kwa staili ya ACACIA ili kuzuia shares kwenye stock market zisishuke.., biashara zingine hizi..
 
Lazima Kanisa Katoliki liwe na msimamo maana lisipokuwa na msimamo watu tutabweteka sana, inabidi tujifunze kupitia wengine.
 
Exactly!
 
Mkuu kuwa mlengo wa kushoto hakukupi Uhuru wa kubeza kulia.
Nadhani umetoa Uzito wa Mantiki za maswali uliyouzia, Ungeishia kwenye kuuliza tu ila Lugha uliyomalizia haivutii, haipendezi na si ya kiuungwana.
 
Taratibu kidini: Waroma wanataratibu zao. Muslims wanazao ( wanawake hawashiriki maziko, wala hawaagi mwili ni taratibu.) Maiti hatiwi kwenye sanduku ( jeneza)
Budha wanataratibu zao, Hindu hali kadhalika.
Taratibu kimila: Kila kabila linazo zake. Wahehe tuna zetu,wakurya wahaya wajaluo wanazo zao.
Tusiwahukumu warumi.
 

Mkuu nimeyaona,

Swali la no1 na no 4 its almost the same,naomba niyajibu kwa umoja wake,
Kwanza naomba ieleweke Kanisa alikuhukumu ila lilitoa msimamo kuwa alitaweza kushiri kwenye safari ya mwisho ya marehemu kwa kuwa marehemu katka safari yake hapa duniani hakuwa na ushirika na Kanisa,nafikiri kama umemsoma vzuri Ben Makasa amejaribu pia kunukuhu vifungu vya biblia ili kuweza kuifahamisha hadhira hii ya jf,na kuhusu matendo yake kuwa na uchaji wa Mungu sidhani kama Kanisa linaweza kupambanua hayo wkt marehemu alikuwa mbali na Kanisa,nafikiri tumuachie Mungu mwenyewe.

Swali no 2,Kuhusu kujitoa kwa maskini hilo ni jambo gumu kdgo kwa Kanisa kwani majitoleo huwa ni siri ya mtoaji na mpokeaji,na hata kama alijitoa kwa masikini wewe au mimi tungeshayasikia,mfn Mengi huwa anajitoa sana na lzm utayasikia kama sio kwake na vyombo vyake basi utayasikia toka wasaidiwa,mfn mwengine jana tumeona Billionaire Bill Gates akitoa msaada mkubwa sana ktk nchi yetu,hilo tusiliongee kwani hakuna ajuae ila Mungu.

Swali no 3,Kuhusu Askofu Eliud wa I.E.C,unajua ndugu kuna misemo ya kiswahili unasema hivi
Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchuzi.
Kwenye msafara wa mamba kenge wapo.

Fafanuzi,kukata kwa Kanisa(PAKACHA) kumsindikiza marehemu ktk safari yake ya mwisho kumekuwa nafuu kwa I.E.C(MCHUKUZI),Nafikiri siku hiyo huyo Askofu aliinadi I.E.C vividly,na msafara huo sio kila mmoja anakuja kuzika,siku hiyo kuna mtu alichukua dem/msela au aliiba aidha simu/sahani/chupa ya kinywaji,kwahyo Askofu Eliud siku hiyo ulikuwa ni sehemu ya mavuno aidha kwa kukandia/kutokandia upande mwingine.

Mkuu nafikiri nimekujibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je, hao mapadri na makardinali wenye hizo kashfa kanisa litakataa kuwazika au kwa sababu wanashiriki kanisani hayo madhambi hayawezi kuwatenga na kanisa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…